radiorahma

RadioRahma

Society SW ↓ 186 episodes

Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana

Author

radiorahma

Category

Society

Podcast website

www.radiorahma.co.ke

Latest episode

Nov 27, 2023

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Wanafunzi waliopachikwa mimba warudi shuleni Kwale 18.11.2021

Simulizi zifuatazo ni za waschana kati ya umri wa miaka 13-14 kutoka shule za msingi tofauti tofauti hapa Kwale. Watoto hawa chini ya umri wa miaka 14 wamedhulumiwa kwa kupachikwa mimba na sasa ni walezi wa watoto. Ila watoto hawa ambao pia ni wanafunzi wameziweka nia za kuendeleza masomo yao ima kwa mimba au baada ya kujifungua. By: Mwanaharusi Rashid

Mazingira na Ajira part 2 28.10.2021

Huku changamoto za taka zikiendelea kulikumba jiji hili la mwambao wa Bahari Hindi, makundi ya kujitegemea yamechipuka kama uyoga kuisaidia serikali ya kaunti ya Mombasa kukabiliana na jinamizi hili. By: Majani Rashid

Mazingira na Ajira part 1 28.10.2021

Vijana wabuni ajira kupitia kuboresha usafi wa mazingira mitaani Likoni, Mombasa. Huku changamoto za taka zikiendelea kulikumba jiji hili la mwambao wa Bahari Hindi, makundi ya kujitegemea yamechipuka kama uyoga kuisaidia serikali ya kaunti ya Mombasa kukabiliana na jinamizi hili.  By: Majani Rashid

Tumaini ya Kina Mama 21.10.2021

Ulemavu ni swala ambalo hadi sasa baadhi ya jamii nchini wanalichukulia kama laana na mzigo katika jamii huku jamii ya kiume ikionekana kuchukua usukani katika dhana hiyo.   By:Nuru Mwalimu

Mashindano ya Maboti Kilifi 18.10.2021

Mashindano ya Maboti ufanyika kila mwaka kaunti ya Kilifi bonyeza usikikilize. By:Baya Kitsao

Biashara ya Manamba Mombasa 10.10.2021

Licha ya wengi uidharau kazi ya Manamba na kuihusisha na wezi kwa jina maarufu la mitaani mateja, biashara hii imeonekana kuvutia wengi katika kaunti ya Mombasa bila kigezo cha mri. Mwanahabari wetu Nuru Mwalimu ametuandalia makala kuhusu Biashara ya Manamba Mombasa. By:Nuru Mwalimu

Biashara ya njuguu kwa Walemavu Kwale 07.10.2021

Licha ya kuwa jamii inawatenga kutokana na maumbile yao, idadi kubwa ya walemavu eneo la Pwani wamejikita katika biashara ndogo ndogo ili kujikimu kimaisha. Katika kaunti ya Kwale baadhi ya walemavu wamejikita katika uuzaji wa njuguu. By:Athuman Luchi

Wanawake Waliojitokeza Kuwania Viti Vya Kisiasa 06.10.2021

Wanawake ulimwenguni wanaendelea kujitokeza kwa hali na mali kupigania usawa wa kijinsia kwa kujiunga katika ulingo wa siasa. Katika makala haya Mhariri wetu Ruth Keah amezungumza na wanawake ambao wamejitokeza kuwania nafasi za uongozi katika siasa mwaka 2022. By:Ruth Keah

Mradi wa ‘Elimu Ni Sasa Initiative' Wasaidia Wanafunzi Kwale 29.09.2021

Tangu kuanzishwa kwa mradi wa ‘Elimu Ni Sasa Initiative’kaunti ya Kwake idadi kubwa ya wanafunzi katika kaunti hio wanaofanya vyema wanajiunga na shule za upili na vyuo vikuu ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo wanafunzi wengi hasa kutoka familia maskini walikuwa wanakwama kuendeleza masomo yao. Mfumo wa Elimu Ni Sasa ulianzishwa mwaka 2013 na lengo kuu ni kuimarisha viwango vya elimu katika k...

Dhana kuwa chanjo ya corona sio salama kwa wagonjwa wa sickle Cell 16.09.2021

Licha ya kuwa ugonjwa wa selimundu yaani Sickle Cell kuwa hatari na usiokuwa na tiba cha kushangaza ni kuwa kuna baadhi ya watu wanaougua ugonjwa huo wanaamini kuwa chanjo ya corona sio salama kwao,hivo kususia kudungwa chanjo hio. By:Athuman Luchi

TASWIRA MPYA YA MAJAA MOMBASA 30.08.2021

Suala la takataka kujaaa katika majaa pamoja na mitaani huenda likawa linachukua mkondo mwengine baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa, mashirika binafsi pamoja na vijana kuongeza juhudi za kusafisha mazingira. Jaa la Kibarani ambalo limekuwa kero kwa wengi kwa miaka mingi kwa sasa ni bustani nzuri ya wananchi kupata upepo mwanana. Je ni vipi jaa hilo lilibadilishwa hadi kuwa bustani ? By Ali Nar...

WENYE AKILI PUNGUANI WAPONA MOMBASA | PART 2 17.08.2021

By Athman Luchi

WENYE AKILI PUNGUANI WAPONA MOMBASA | PART 1 17.08.2021

Nchini Kenya inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya watu 10 anaugua shida ya akili, Huku mtu mmoja kati ya watu wanne wenye ugonjwa wa akili anahudhuria vituo vya afya. Wagonjwa wengi wa akili ujipata wametengwa katika jamii na wanaonekana kama waliolaniwa.  Jijini Mombasa kumefunguliwa makao na kituo maalumu ya kuwahudumia wagonjwa wa akili cha Women Empowerment for Mental illiness Treatment and...

UZAZI NA CHANJO YA CORONA 16.08.2021

Ujio wa chanjo ya kudhibithi virusi vya corona nchini imepokelewa kwa mtazamo tofauti , huku baadhi wakisema kuwa chanjo hiyo inazuwia wanawake kupata uja uzito sambamba  na wanaume kutokuwa na uwezo wa kuzalisha. By: Nuru Mwalimu

CHANJO YA CORONA KWA WANAWAKE 15.08.2021

Wakati huu dunia ikiendelea kuhakikisha chanjo dhidi ya virusi ya corona imesambazwa kwa kila mtu duniani,Asasi za afya zikiongozwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limetoa wito kwa umma kupuuza habari za urongo zinazosambazwa kuhusu chanjo hizo na kudungwa. Miongoni mwa habari hizo za urongo zimeelekezewa wanawake zikidai kuwa wanapopata chanjo hiyo watapoteza afya yao ya kizazi. Katika...

CHANGAMOTO ZA WANAWAKE WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA 13.08.2021

By Ali Nariri

MUI HUA MWEMA 11.08.2021

Dawa kali za kulevya kama heroin almaarufu kwa jina unga ni miongoni mwa mihadarati inayojulikana sana Pwani ya Kenya katika miji ya Mombasa, Kwale, Lamu na Kilifi. Dawa hizi zimewasababishia watumizi walio vijana, watu wazima waume kwa wanawake hasara kubwa za kiafya, kiuchumi na kijamii. Pindi mtu anapoanza ya matumizi ya heroine tabia zake hubadilika pakubwa na sio rahisi kuiacha. Utafiti uliot...

MABADILIKO YA MAJUKUMU KWA WAFUGAJI | PART 2 07.08.2021

By Ruth Keah

MABADILIKO YA MAJUKUMU KWA WAFUGAJI | PART 1 06.08.2021

Mabadiliko ya tabia nchi huathiri shughuli za kibinadamu huku tafiti zikionyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi zaidi ya wanaume. Makala haya yanaangazia jinsi mabadiliko ya tabia nchi yamewaathiri wanawake kutoka familia za wafugaji huko Maungu kaunti ya Taita Taveta kiasi cha kuwa wamebadilisha   majukumu ya familia. Ambapo kwa sasa wanawake...

UVUMI KUWA CHANJO ZA CORONA INAATHIRI NGUVU ZA KIUME 04.08.2021

Kulingana na wizara ya afya nchini Kenya, takribani 2% ya Wakenya wamedungwa chanjo hio, huku kati ya 2% ya watu waliodungwa chanjo ya corona zaidi ni wanaume. Pamoja na hayo, kuna uvumi  unaoendelea kuwa chanjo hiyo husababisha utasa na kupoteza nguvu za kiume.  Licha ya kuweko na uvumi huo, idadi kubwa ya wanaume wanaendelea kudungwa chanjo hio. By Athman Luchi

GENDER KHUNTHA 03.08.2021

Khuntha ni watoto wanauzaliwa na jinsia mbili ambapo wakati mwengine jinsi moja huzidi nyengine, katika makala haya tutazungumzia utekelezaji wa haki kwa watoto wanaozaliwa khuntha By Nuru Mwalimu

SINGENGE YA KASAINI | PART 2 02.08.2021

By Ruth Keah

SINGENGE YA KASAINI | PART 1 02.08.2021

Tatizo la wanyamapori kuingia katika mashamba ya watu katika kaunti ya Taita Taveta limekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kwa miaka mingi. Ili kutatua tatizo hilo, mtafiti wa kisayansi Simon Kasaine, alivumbua singe’nge inayotengenezwa kwa mabati madogo madogo na kupewa jina la KASAINE FENCES. Mhariri wa Radio Rahma Ruth Keah alizuru eneo la Maungu ambapo wakulima wamenufaika na singe’nge hiyo na...

MASAIBU YA WANAWAKE WENYE WATOTO WALEMAVU 30.07.2021

Makala By Mwanaharusi Rashid

UBAKAJI WA MATEJA WA KIKE 26.07.2021

Kaunti ya Mombasa ina idadi kubwa ya waraibu wa kike wa mihadharati, ambao wengi wao hujipata wamebakwa wakiwa maskani mwao. Wengi wa waraibu hao hushindwa kutafuta haki baada ya kubakwa,hivyo kuishia kuishi na makovu ya milele. By Athman Luchi

Listen to the RadioRahma podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.