radiorahma
RadioRahma
Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Wahudumu wa afya nyanjani waelimisha jamii kuhusu taratibu stahiki za ulaji wa dawa/Part 2. 16.03.2022 7:58
Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani. Bila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu. Hatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, k...
Wahudumu wa afya nyanjani waelimisha jamii kuhusu taratibu stahiki za ulaji wa dawa/Part 1 16.03.2022 8:25
Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani. Bila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu. Hatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, k...
Ukulima Wa Unyunyiziaji Maji Kwale. 14.03.2022 10:07
Nchi nyingi za Afrika zinazopatikana Kusini mwa jangwa la Sahara hazina chakula cha kutosha. Hali hii hutokana na sababu nyingi ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambapo wakulima wanaotegemea mvua mara nyingi huishia kutopata mavuno mvua inapokosa kunyesha. Mhariri wetu Ruth Keah ametembelea wakulima wa Unyunyiziaji Maji huko Kinango kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo.
Sumu Ya Plastiki 01.03.2022 11:11
By:Nasra Mkali
Watu Wenye Ulemavu Wanavyotunza Mazingira Mombasa 24.02.2022 7:54
Kufuati kukithiri kwa mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira duniani,Hapa jijini Mombasa watu wenye ulemavu wamejitosa katika utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira. Watu hao wenye ulemavu chini ya shirika la 'Tunaweza Women With Disability' wameanzisha mradi wa kutengeneza bidhaa za urembo kama vile bangili,vipuli na shangaa kwa kutum...
Changamoto wanazopitia wanawake wanaojifungua watoto Walemavu 16.02.2022 16:52
Idadi kubwa ya wanawake wanaojiufungua watoto wenye ulemavuhujikuta wamepewa talaka au kutengwa na waume zao hatua inayowafanya kuishi maisha magumu. Hata hivyo yapo mashirika yaliyojizatiti katika masuala ya kusaidia watoto walemavu ili kuyaboresha maisha yao ya baadae. Mashirika haya yamewapa wanawake hawa matumaini katika maisha. Mwandishi: Mwanaharusi Rashid
Munga Aupuuza ulemavu na kung’aa kimataifa kwenye mchezo wa Soka 14.02.2022 11:59
Mchezo wa Mpira wa miguu maarufu zaidi kama kandanda au soka, ni mchezo unaopendwa na wengi. Katika Makala haya, mhariri wetu Ruth Keah anamuangazi kijana kwa jina Mohammed Munga aliye na ulemavu wa mguu lakini akapuuza ulemavu huo na kwa sasa anang’aa katika ulingo wa soka kimataifa.
Programu ya rununu inavyosaidia watu wenye ulemavu kupata ajira. 31.01.2022 10:56
Watu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukutana na miundo msingi isiyo rafiki na kunyimwa ajira. Hatua, iliyosababisha shirika moja la kibinafsi kuzindua programu ya simu ya rununu inayowawezesha watu wenye ulemavu kupata kazi bila kubaguliwa. Kama anavyosimulia Mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala- programu ya rununu inavyosaidia watu wenye ulemavu kupata ajira.
Makala Habari Za Urongo Zaathiri Utoaji wa HPV 24.01.2022 11:34
Raisi Uhuru Kenyatta alizindua rasmi zoezi la wasichana walio na umri wa miaka 10 kupewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi ya Human Papilloma Virus yaani HPV. Lakini zoezi hilo limekumbwa na pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali. Mhariri wetu Ruth Keah ameandaa Makala maalum ya jinsi habari za urongo mitandaoni pia zimechangia jamii kutokumbatia utoaji huo wa chanjo. By:Ruth K...
Uvuvi wa kamba mwani wapigwa jeki Lamu 31.12.2021 15:53
Uvuvi wa Kamba mwani kwa kimombo Lobsters ni maarufu katika kaunti ya Lamu haswa katika eneo la Kizingitini kisiwa cha Pate. Wavuvi wa Kamba mwani katika kaunti ya Lamu kwa ushirikiano na washikadau mbalimbli wanaendeleza mikakati ya kupata kibali cha kimataifa ili kulifikia soko kubwa, mikakati hii iliyoanza mwaka wa 2011 ni kutokana na uhutaji wa lobsters ulioyopo katika soko. Kibali hiki kikita...
Unyanyasaji wa wanawake walio na matatizo ya akili. 30.12.2021 13:48
Huku maradhi ya matatizo ya akili yakiendelea kushuhudiwa nchini na ulimwengu kwa jumla, wanawake walio na matatizo haya wamekua wakinyanyaswa kimapenzi, hasa wanaorandaranda mitaani na barabarani kutokana na kukosa wakuwahifadhi. By: Nuru Mwalimu.
Kupigania Haki za Wanawake Wenye Ulemavu Waliodulumiwa Kingono 27.12.2021 13:28
Idadi kubwa ya wanawake wenye ulemavu wa akili,ulemavu kutosikia na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii, wengi wa wanaobakwa usalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria. Jijini Mombasa Pwani ya Kenya shirika la “Tunaweza Women With Disability” limeanza kutoa usaidizi wa kisheria na mafunzo mbali mbali kwa wanawake...
Uchunguzi wa habari kuwa vyandarua vya mbu vyaleta kunguni nchini Kenya. 21.12.2021 12:46
Licha ya shirika la afya duniani WHO,kuidhinisha matumizi ya vyandarua vya mbu vilivyotibiwa,hapa nchini Kenya mkakati huu unakabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu kuna taarifa za uongo zinazosambaa kwamba vyandarua hivyo husababisha uvamizi wa kunguni majumbani pindi tu vinapotumika. By:Mwanaharusi Rashid.
ATHARI YA KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE WAKATI WA KUJIFUNGUA 04.12.2021 11:33
ATHARI YA KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE WAKATI WA KUJIFUNGUA.
Changamoto za watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kwa jina albinism 01.12.2021 10:02
Kulingana na wataalamu wa afya ni kwamba miale ya jua ni kiungo muhimu kwa afya ya binadamu, ila kuna jamii ya watu ambao jua ni hatari kwao na huchukuliwa kama adui mkubwa kwenye ngozi zao. Kwenye Makala haya ya afya tunaangazia changamoto za watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kwa jina albinism. Mtayarishi ni Ibrahim Juma Mudibo.
WAJIPATIA RIZIKI KUPITIA KILIMO CHA MBUYU 29.11.2021 12:38
Wengi hufahamu jina mabuyu yaliyozoeleka kuliwa kwa kumumunya utamu wake ambapo hupikwa kwa kuchanganya na sukari, rangi iwe ya kijani nyekundu au hata njano pamoja na viungo vyengine ambapo badae huuzwa katika paketi kati ya shilingi 5-50 Lakini je unapomumunya utamu wake unafahamu pale yanapotokaa?.Yanatoka kwa mti wa m'buyu kwa kimombo baobab tree. Ni mti mkubwa wa ukanda wa tropiki na ma...
Chanjo za Corona haziathiri nguvu za kiume 28.11.2021 5:33
Chanjo za Corona haziathiri nguvu za kiume kama inavyodhaniwa na wengi. Mwanahabari wetu alifanya mazungumzo na wanaume waliodungwa chanjo hio na wametibithisha kuwa hawajaathirika,nguvu zao za kiume bado ziko imara. By:Athuman Luchi
Vyama vya pesa mashinani wakati wa Corona 26.11.2021 9:54
Ujio wa virusi vya Corona humu nchini ulivuruga shughuli nyingi ikiwemo za kiuchumi. Kina mama wengi wamelazimika kujiunga na vyama vya mashinani ambapo wanapata mikopo bila riba na kujiendeleza na bisahara zao ndogo ndogo. Ruth Keah amezungumza na baadhi ya wanawake waliojiunga na vikundi hivyo na kutuandalia makala haya. By:Ruth Keah
Juhudi za kunasua familia kimawazo dhidi ya makovu ya mauaji ya kiholela 26.11.2021 11:06
Familia nyingi hupata msongo wa mawazo wanapopoteza wapendwa wao kutokana na mauaji ya kiholela. Katika makala haya Ruth Keah amezungumza na baadhi ya waathiriwa ambao wamepoteza jamaa zao mikononi mwa maafisa wa usalama. Wengi kwa sasa wamejiunga na vikundi vya kubadilishana mawazo ili kupunguza msongo wa mawazo wanaopitia. By:Ruth Keah.
Ukumbatiaji wa Bayoteknolojia kwa usalama wa chakula 25.11.2021 11:27
Mhogo ni chakula kinachoenziwa na wengi na zao ambalo limewapa wakulima mapato humu nchini. Chakula chake ni maarufu katika baadhi ya mataifa ya bara la Afrika, Asia na Amerika Kusini. Kulingana na shirika la utafiti wa kilimo na mifugo humu nchini KALRO, mihogo inapandwa katika hekari laki moja na elfu sabini na mbili nchini ambapo asilimia 60 hupandwa kutoka eneo la Magharibi, Pwani asilimia 30...
MAKALA YA JINSI SEKTA YA AFYA ILIVYOIMARIKA BAADA YA UGATUZI KWALE 24.11.2021 9:20
Makala by Ali Nariri
Tamu Tamu ya asali yapotea kwa ukame 21.11.2021 14:56
Mbali na kuwa mdudu mkali wapo waliozama katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uzalishaji wa asali kwa matumizi mbalimbali ikiwemo dawa. Ikumbukwe kuwa si wengi wenye ujasiri na ukakamavu wa kufuga nyuki kutokana na dhana na kasumba kuwa ni wadudu hatari kufuga licha ya kuwa na manufaa tele. Ufugaji wa nyuki hauna mahitaji mengi ikilinganishwa na ufugaji mwengine wowote cha msingi ni mf...
Uongozi wa wanawake Wapigiwa upatu Pwani. 20.11.2021 9:20
Wanawake wengi wameshindwa kuafiki katika maswala ya uongozi kutokana na kasumba inayoendelezwa na baadhi yao kwamba mwanamke hawezi kuwajibikia majuku yake ipasavyo. Kulingana na takwimu za shirika la kimataifa la wanawake UN Women, duniani kuna nchi 27 ambapo wanawake wanachangia chini ya asilimia 10 ya wabunge. By:Nuru Mwalim
Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale-Part 2 18.11.2021 8:30
Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa humu nchini. Lakini licha ya hivyo watu wengi hawajaukumbatia sana ukulima wa mmea huo. Mhariri wetu Ruth Keah aliwatembelea baadhi ya wakulima wanaoendeleza ukulima wa pamba ya kisasa katika kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo awamu ya pili- Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale. By:Ruth Keah
Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale-Part 1 18.11.2021 8:05
Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa humu nchini. Lakini licha ya hivyo watu wengi hawajaukumbatia sana ukulima wa mmea huo. Mhariri wetu Ruth Keah aliwatembelea baadhi ya wakulima wanaoendeleza ukulima wa pamba ya kisasa katika kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo- Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale. BY:Ruth Keah
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.