radiorahma

RadioRahma

Society SW ↓ 186 episodes

Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana

Author

radiorahma

Category

Society

Podcast website

www.radiorahma.co.ke

Latest episode

Nov 27, 2023

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 1 25.09.2022

Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya. Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa. Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea. Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Nafasi za kisiasa kwa watu wenye ulemavu zayumbayumba. 25.09.2022

Watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi ya jamii zilizotengwa. Na ili kuimarisha uwakilishi wao katika ulingo wa siasa,Kumekuwa na kila juhudi kuhakikisha kuwa makundi yaliyotengwa yamepata nafasi sawa za uwakilishi. Hata hivyo kulingana na matokeo yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 humu nchini Kenya, hayakuwapendeza watu wenye ulemavu. Kama anavyoarifu mhariri wetu Ruth Keah kw...

Simulizi za kutafuta uhuru mikononi mwa maafisa wa usalama 25.09.2022

Kutokana na ajali nyingi za barabarani zinazoshuhudiwa humu nchini hasa kwa watu wanaotembea, Serikali iliweka mikakati ya kupunguza ajali hizo kwa kujenga madaraja ya juu ili mwananchi atumie kwa usalama wake mwenyewe. Lakini licha ya hatua hiyo ya serikali, bado kuna baadhi ya watu wanaopuuza kutumia daraja hizo,mwishowe huishia kutiwa nguvuni na polisi ama askari wa kaunti kwa kukiuka sheria. M...

Gharama ya maisha inawadumaza wanawake wenye ulemavu 18.09.2022

Kupanda kwa gharama ya maisha kumeathiri wanawake wenye ulemavu wengi wao wakiwa walezi ambao hawana kazi na wengine wakitegemea kuomba omba mitaani. Mfumko huo wa bei za vyakula umewafanya wengi wao kulala njaa kwa kukosa namna ya kukidhi mahitaji ya familia zao. Mwandishi:Nuru Mwalimu

Umuhimu Wakunyonyesha Watoto 15.09.2022

Licha ya wanawake waliojifungua kusisitizwa kunyonyesha watoto wao,bado kunao ambao hawanyonyeshi watoto. Kulingana na shirika la afya duniani WHO, karibu watoto 2 kati ya 3 hawanyonyeshwi maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 iliyopendekezwa—kiwango ambacho hakijaimarika katika miongo 2. Mwandishi:Zahra Nakaya Akosa.

Juhudi za kupungunza mkurupuko wa homa ya Dengue Mombasa /Part 2 05.09.2022

Kaunti ya Mombasa imekuwa ikishuhudia mkurupuko wa homa zinazosababishwa na mbu ikiwemo homa ya Dengue, Chikungunya na Malaria. Magonjwa ambayo yanasababishwa na aina Fulani ya mbu. Mhariri wetu Ruth Keah katika Makala yafuatayo,ameeleza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau wa afya kuhakikisha kuwa inatokomeza magonjwa hayo.

Juhudi za kupungunza mkurupuko wa homa ya Dengue Mombasa/ Part 1 05.09.2022

Kaunti ya Mombasa imekuwa ikishuhudia mkurupuko wa homa zinazosababishwa na mbu ikiwemo homa ya Dengue, Chikungunya na Malaria. Magonjwa ambayo yanasababishwa na aina Fulani ya mbu. Mhariri wetu Ruth Keah katika Makala yafuatayo,ameeleza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau wa afya kuhakikisha kuwa inatokomeza magonjwa hayo.

Ahudumia jamii kwa kujitolea licha ya kuwa Mlemavu. 26.08.2022

Katika miji mingi kumeshuhudiwa ombaomba wa aina tofauti tofauti. Katika kundi la ombaomba kuna makundi makuu matatu ambao ni watoto, walemavu na wazee. Kundi kumbwa ambalo lina wahusika wengi katika kuomba ni kundi la watu wenye ulemavu. Lakini kwa Naima Omar Ali, amekataa kuwa katika kundi hilo la kuomba na badala yake kujitolea kufanya kazi za kusaidia jamii bila malipo. Naima alifanya mahojian...

Ukakamavu Wangu 25.08.2022

Licha ya jamii na baadhi ya familia kuonekana kuwakejeli watu wenye ulemavu,hali ilikuwa tofauti kwa familia ya Lucy Chesi na dadazake wawili ambao wote walizaliwa na ulemavu wa viungo. Wazazi wake walijizatiti na kuwalea vyama na kuwapa elimu ya kutosha. Katika msururu huo wa maisha,Lucy na wenzake walipitia unyanyasaji lakini,waliupuzilia mbali na kusonga mbele kimaisha na kutibithishia umma kuw...

Wanawake wenye ulemavu wanaowania viti vya siasa kama wagombea huru wakumbwa na changamoto za usafri wa kufanyia kampeni 08.08.2022

Licha ya wanawake wenye ulemavu kujitosa kwenye siasa,bado wanakumbwa na changamoto ya usafiri kufuatia maumbile yao,hasa kwa walemavu wenye matatizo ya viungo vya miguu na wale wasioona. Wanasiasa hawa ambao wanawania kama wawaniaji huru jijini Mombasa,hawana gari za kufanyia kampeni mashinani,hatua inayowafanya kulemaza kampeni zao. Mwanahabari wetu Athuman Luchi ametusimulia.

Ubaguzi wa Wanawake wenye ulemavu wanaowania viti vya kisiasa Mombasa 07.08.2022

Wanasiasa wanawake wenye ulemavu ubaguliwa ,hukejeliwa na kutengwa katika harakati za kisiasa kufuatia maumbile yao,ubaguzi huo unawaathiri wanasiasa hao wenye ulemavu,hatua inayowafanya kushindwa kuendeleza azima yao ya kuwania viti vya kisiasa. Mwandishi:Athuman Luchi

Kura isiyosiri 04.08.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu changamoto ambazo jamii ya watu walio na changamoto ya kuona wanapitia wakati wa upigaji kura uchaguzini. Mwandishi:Ruth Keah

Ugonjwa wa upungufu wa akili watibiwa Mombasa 15.07.2022

Takwimu zilizowasilishwa kwa kamati ya Seneti ya Afya mwezi Machi na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe zinaonyesha ugonjwa wa mfadhaiko ndio aina ya ugonjwa wa akili unaoenea zaidi nchini. Amina Abdalla ni Mwanzilishi wa kituo cha Women Empowerment for Mental illiness Treatment and Rehabilitation Centre, anasema aliamua kuanzisha makao hayo baada ya kuona hakuna makao ya kuishi ya watu wenye akili pungu...

Chanjo ya Saratani –Tumaini kwa vizazi Vya baadaye 04.07.2022

Mwaka wa 2019 raisi Uhuru Kenyatta alizindua rasmi zoezi la wasichana walio na umri wa miaka 10 kupewa chanjo ya saratani yaani HPV, lakini zoezi hilo lilipata pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali nchini. Katika Makala haya,mhariri wetu Ruth Keah ameangazia kuhusu habari za urongo ambazo zilifanya wazazi kupuuza chanjo hiyo na wataalamu ambao wamekosoa habari hizo za urongo.

Uregeshaji Wa Matumbawe Kwale Part 2 27.06.2022

Mabadiliko ya tabia nchi yaani climate change, uvuvi haramu,ongezeko la chupa za plastiki baharini na kuharibiwa kwa matumbawe kumetajwa kuwa moja wapo ya mambo yanayoathiri viumbe wa majini na shughuli za uvuvi. Lakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari ni miongoni mwa mambo yanayotishia ustawi wa bahari ambayo ni tegemeo kwa Maisha ya binadamu. Mhariri wetu Ruth Keah alizuru eneo la...

Uregeshaji Wa Matumbawe Baharini Part 1 27.06.2022

Mabadiliko ya tabia nchi yaani climate change, uvuvi haramu,ongezeko la chupa za plastiki baharini na kuharibiwa kwa matumbawe kumetajwa kuwa moja wapo ya mambo yanayoathiri viumbe wa majini na shughuli za uvuvi. Lakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari ni miongoni mwa mambo yanayotishia ustawi wa bahari ambayo ni tegemeo kwa Maisha ya binadamu. Mhariri wetu Ruth Keah alizuru eneo la...

Changamoto Za Usafiri Zinazowakumba Wanasiasa Wanawake Wenye Ulemavu 22.06.2022

Licha ya wanawake wenye ulemavu kujitosa kwenye siasa,bado wanakumbwa na changamoto ya usafiri kufuatia maumbile yao,hasa kwa walemavu wenye matatizo ya viungo vya miguu na wale wasioona. Wanasiasa hawa ambao wanawania kama wawaniaji huru jijini Mombasa,hawana gari za kufanyia kampeni mashinani,hatua inayowafanya kulemaza kampeni zao. By Rose Tawa

Ubaguzi Wa Kisiasa Kwa Wanawake Wenye Ulemavu Wanao Wania Viti Vya Kisiasa. 17.06.2022

Licha ya Kifungu  81[1c] cha katiba kusisitiza uwakilishi wa usawa na haki kwa watu wenye ulemavu bado wanawake wenye ulemavu waliojitosa kwenye siasa,wanakumbwa na ubaguzi wa kisiasa kutoka kwa wapinzani wao na hata wafuasi wa wapinzani hao. Pia kifungu cha katiba cha 27[5] kinaeleza kuwa Mtu hatabaguliwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja dhidi ya mtu mwingine kwa sababu zozot...

Watu wenye ulemavu wanavyonufaika na utengenezaji wa siagi ya njugu Mombasa 18.05.2022

Licha ya kuwa na ulemavu Wanawake kutoka shirika la Tunaweza Women Living with Disability wamejitosa katika biashara ya kutengeneza siagi ya karanga almaarufu peanut butter walioipa jina la Onja Utamu. Siagi hio inatengenezwa kutumia njugu pekee ambazo husagwa kwa kutumia mashini.

Vifo vya uzazi vyapungua Kwale. 19.04.2022

Tangu serikali ya kaunti ya Kwale kuongeza idadi ya vituo vya afya nyanjani, Idadi ya wanawake  wanaoaga dunia kutokana na changamoto za kujifungua kaunti ya kwale  imepungua kutoka wanawake 560 Kila mwaka Hadi wanawake 35 Kati wanawake laki 1 wanaojifungua kote  nchini. By:Mwanaharusi Rashid

Ulemavu Wangu 09.04.2022

Jamii nyingi uhusisha ulemavu na laana pamoja na ushirikina,huku wengine wakihusisha ulemavu huo na  kasoro zinazotokana kwa mzazi haswa wa kike. Kufuatia madai hayo baadhi ya wanajamii uonekana kuwatenga watoto wanaozaliwa na ulemavu. Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wako sawa tu kama wengine wasio walemavu. Katika Makala haya “Ulemavu Wangu” leo tunaangazia dada watatu waliozaliwa na ule...

Watu wenye ulemavu wanavyonufaika na utengenezaji wa siagi ya njugu Mombasa 04.04.2022

Licha ya kuwa na ulemavu Wanawake kutoka shirika la Tunaweza Women Living with Disability wamejitosa katika biashara ya kutengeneza siagi ya karanga almaarufu peanut butter walioipa jina la Onja Utamu. Siagi hio inatengenezwa kutumia njugu pekee ambazo husagwa kwa kutumia mashini. By:Silvia Maina

Kuwanusuru wanawake na watoto wenye ulemavu waliobakwa Mombasa 30.03.2022

Idadi kubwa ya wanawake na watoto wenye ulemavu  wa akili,ulemavu wa kuskia na wale wanaokabiliwa na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii,wengi wa wanaobakwa hutishiwa maisha na husalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria. Katika eneo la Kisauni ambapo ninakutana na msichana mwenye umri wa miaka 16 na ambaye...

Gharama ya mawasiliano kwa watu wenye changamoto ya matamshi. 28.03.2022

Mawasiliano ni mchakato wa kuhamisha taarifa kutoka chombo kimoja hadi kingine. Mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kama mchakato kati ya wahusika wawili una mwelekeo uliokubaliwa. Lakini kwa jamii ya watu wenye changamoto ya matamshi, utumiaji wa simu hizo za mkononi hasa kwa mazungumzo ni changamoto kwao,kama anayosimulia mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Takataka Za Plastiki Zinavyotumiwa Kuimarisha Mazingira. 21.03.2022

Idadi ya uchafu wa plastiki baharini imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni, Likiwa ni tatizo kubwa linalokabili mazingira duniani. Jambo ambalo limeathiri sana upatikanaji wa Samaki kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya bahari eneo la pwani, Lakini kikundi cha Gazi Women Magrove Boardwalk kimejitolea kulinda msitu wa mikoko katika eneo hilo la Gazi ili mbali na kulinda mazingira, pia wapat...

Listen to the RadioRahma podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.