radiorahma

RadioRahma

Society SW ↓ 186 episodes

Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana

Author

radiorahma

Category

Society

Podcast website

www.radiorahma.co.ke

Latest episode

Nov 27, 2023

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Dosari Ya Shilingi katika kaunti ya Mombasa 29.12.2022

Makala ya Dosari Ya Shilingi yalioandaliwa na Oscar Ochieng yanahusu madeni katika kaunti ya Mombasa. Makala haya yanazamia sababu zinazopelekea kaunti hii kushuhudia madeni ya kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ya kifedha iliyopita wakati ambapo utawala wa sasa umeunda jopo kung'amua ukweli kuhusu madeni hayo.

Wanawake wakumbatia kilimo cha agrivoltaics kukabili mabadiliko ya tabia nchi. 25.12.2022

Hali ya kiangazi na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kukumba sehemu mbali mbali humu nchini, hivyo basi inasababisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mazao ya chakula. Hali hii imeathiri mapato na kupanda kwa bei za vyakula. Katika kutafuta suluhu zinazowezekana kukabili hali hii, kikundi cha wanawake wakulima kutoka eneo la Lunga Lunga,walianzisha mradi unaoitwa "agrivoltaics,"yaani kutumia panel...

Malkia wa Gasi 22.12.2022

Kwa mara nyingi sekta ya usambazaji wa gasi safi imechukuliwa kama kazi inayofanywa na wanaume. Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake kutoka kaunti ya Mombasa waliojiingiza katika sekta hiyo na kujipatia kipato na kuimarisha maisha yao. Mtayarishi wa makala haya ni Ruth Keah.

Changamoto za mimba za utotoni kwa wasichana wenye matatizo ya akili 05.12.2022

Wizara ya afya nchini Kenya ilirekodi visa 45,724 vya mimba za utotoni mnamo Januari na Februari mwaka 2022.Visa hivyo ni vya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19 wakiwemo watoto wenye ulemavu wa akili. Watoto hao wenye ulemavu wengi ubakwa na kupachikwa mimba na kuachwa wakiangaika pasi usaidizi. Mwandishil:Rose Tawa

Mwelekeo Kwa wajane waliodhulumiwa 25.11.2022

Licha ya kuwa na haki ya urithi pindi mwanawake anapofiliwa na mumewe, jamii imekua tishio kubwa kwa kina mama pindi wanapofiliwa kutona na mila na desturi potofu katika jamii huku takwimu nchini zikionesha kuwa takriban wajane milioni 8 nchini wametelekezwa kutokana na mila potofu na umaskini. Mwandish:  Nuru Mwalim.

Kaa La Wanawake 22.11.2022

Makala haya yanahusu wanawake wanaopata mafunzo ya kujikimu kimaisha wakati ambapo suala la ajira limekuwa changamoto nchini. Kando na kujikimu ki maisha, mafunzo wanayopata vile vile yanalenga kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kilimo Baharini/Part 2 10.11.2022

Wakazi wengi ukanda wa pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.

Kilimo Baharini/Part 1 10.11.2022

Wakazi wengi ukanda wa Pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah   kwenye makala ifuatayo.

Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 2 08.11.2022

Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo, Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi. Kama anavyoeleza Ru...

Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 1 08.11.2022

Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo, Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi. Kama anavyoeleza Ru...

Ahudumia jamii licha ya changamoto ya kuona 31.10.2022

Kila mwaka Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ni maalumu kwa kuelimisha jamii kuhusu ulemavu wa kuona, athari zake na njia za kuzuia matatizo ya macho. Mwaka huu,siku hiyo iliadhimishwa tarehe 13 mwezi wa Oktoba. Makala haya ambayo yametayarishwa na Ruth Keah, yanazungumzia kuhusu mwanamke ambaye ana changamoto ya kuona lakini amepuuza changamoto hiyo na anahudumia jamii kwa njia mbalimbali.

Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part Two 21.10.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part One 21.10.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Mradi wa Skills Mtaani waboresha elimu kwa Vijana Mombasa 21.10.2022

Tangu ya kuanzishwa kwa Mradi wa Skills Mtaani eneo bunge la Mvita zaidi ya Vijana 11,000 wamenufaika na mradi huo na sasa wengine wameajiriwa na wengine wamefungua biashra zao. Mwanahabari wetu Athuman Luchi ametuandalia makala,kuhusu mradi huo.

Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two 21.10.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part One 21.10.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni.  Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Uhifadhi wa Mikoko kupitia ufugaji wa Nyuki 21.10.2022

Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini. Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu. Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Kijana anayesakata soka ya kimataifa licha ya ulemavu wake 13.10.2022

Makala haya yanaangazia juhudi za kijana kutoka kaunti ya Kilifi-Kenya anayeng'aa katika soka ya kimataifa licha ya kuwa mlemavu. Licha ya kukatazwa kucheza na wazazi wake, hakufa moyo na kuendeleza kipaji chake na kwasasa anategemewa na familia yake kutokana na kipato anachopata kutokana na kucheza soka.

Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part Two 10.10.2022

Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo. Lakini kuna matumaini ya tatizo h...

Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part One. 10.10.2022

Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo. Lakini kuna matumaini ya tatizo h...

Chupa zageuzwa kuwa mazalia ya Samaki baharini. 10.10.2022

Mirundiko ya takataka sio tu katika nchi kavu bali pia baharini kwa miaka mingi imekuwa shida kubwa kuthibiti, taka za baharini zikichangia kuharibika kwa miamba ya matumbawe. Lakini katika Kijiji cha Mkwiro kaunti ya Kwale Ukanda wa pwani, baadhi ya taka za baharini na zile za nchi kavu zimegeuzwa kuwa thamani kwa kutumia mchakato mbadala wa kutengeneza chupa za matumbawe. Kama anavyoeleza mharir...

Kukomesha Unyanyapaa na Ubaguzi kwa wanaokabiliwa na tatizo la Afya ya Akili 10.10.2022

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu nchini Kenya asilimia 0.3% ya watu wanaugua ulemavu wa akili jijini Mombasa. Wengi wa wenye ulemavu wa akili ukumbwa na unyanyapa,msongo wa mawazo na utengwa katika jamii,hivyo wanajipata wakirandaranda mitaani. Juma Ali ni kijana mwenye umri wa miaka 30, aliyepona matatizo ya akili yaliyomsumbua kwa muda wa miaka 5. Anasema alianza kurukwa na ak...

Kilio cha mtoto mwenye ulemavu wa akili aliyebakwa na kupachikwa mimba 27.09.2022

Watoto wengi wenye matatizo ya akili upitia unyanyasaji wa kingono,kupachikwa ujauzito na wengi wa wanao bakwa usalia kimya wasijue wapi pa kuripoti kisa hicho,Mariam mwenye umri wa miaka 16 ni kati ya watoto wenye ulemavu wa akili walionajisiwa na kupachikwa mimba. Mariam ambalo si jina lake kamili alibakwa na kusalia kimya bila hata kumjulisha mamake. Kwa Sasa Mariam analea mtoto mvulana mwenye...

Changamoto za usalama wa barabarani kwa watu wenye Ulemavu 25.09.2022

Bara la afrika limemulikwa sana katika ukuaji wa miundo msingi yake katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi na upanuzi wa barabara. Licha ya miradi hiyo kurahisisha usafiri kwa mwananchi,bado kuna changamoto kubwa kwa jamii ya watu wenye ulemavu kutokana na ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwao. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 2 25.09.2022

Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya. Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa. Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea. Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Listen to the RadioRahma podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.