Luphurise Lema
Uplifting Moment with Luphurise Mawere
Hongera sana kwa kuchukua nafasi kusikiliza masomo haya ambayo yanaletwa kwako kila Jumatatu. Masomo haya yatakupa maarifa na hekima kutoka kwa Mungu itakayakusaidia uwe na Wiki yenye mafanikio na ushindi. Watumie wengine link hii ili waweze kujifunza.
Author
Luphurise Lema
Category
Podcast website
Latest episode
Feb 5, 2026
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Je unapitia changamoto basi Omba 07.09.2021 1:27:59
Neno lililofundishwa kwenye Fellowship ya Wanawake iliyofanyika leo Jumanne tarehe 7 September 2021
Nguvu ya Neno la Mungu by Luphurise Mawere 01.09.2021 1:47:40
Power in the Word of God, Neno lililofundishwa kwenye Fellowship ya Wanawake inayofanyika Kila Jumanne. Tarehe 31 August 2021.
Mtazame Mungu Sahau Unayoyapitia by Luphurise Mawere 25.08.2021 1:48:09
Mafundisho yaliyofundishwa kwenye Women Fellowship ya Jumanne tarehe 24 August 2021
Mwanamke Mwenye Ushawishi, Bathsheba by Luphurise Mawere 17.08.2021 2:00:19
The influential Woman, Somo lililofindishwa Women Fellowship tarehe 17 August 2021
Usiogope Bwana atakupigania na Luphurise Mawere 10.08.2021 2:01:29
Women Fellowship ya tarehe 10 August 2021.
Namna ya kupokea Muujiza kutoka kwa Mungu na Luphurise Mawere 03.08.2021 1:29:17
Mafundisho yaliyofundishwa kwenye Women Fellowship ya Jumanne tarehe 03 August 2021. Karibu ujumuike nasi kwenye Fellowship na Maombi Kila Jumanne saa 11: 30 Jioni. Kwa maelezo zaidi wasiliana na +255 628 704 781
Nguvu ya Jina la Yesu by Luphurise Mawere at Women Fellowship 27.07.2021 1:12:52
Power in the Name of Jesus
Karama za Roho Mtakatifu by Luphurise Mawere 01.07.2021 1:04:17
Somo lililofundishwa kwenye Fellowship ya Wanawake inayofanyika kila Siku ya Jumanne
JIEPUSHE NA KUJIINUA By Luphurise Mawere 28.06.2021 10:28
Jiepushe na Kujiinua
SIFA ZA BINTI WA VIWANGO/ THE ATTRIBUTES OF A SINGLE LADY OF CLASSY By Luphurise Mawere 03.05.2021 2:05:29
Karibu katika mtiririko wa somo hili kwa ajili ya mabinti/single ladies nilifundisha kwenye Semina ya Mabinti, Ngome Holdings, Sinza Africasana, Jumamosi 1 May 2021_ *1. Kuweka vitu vya kwanza kuwa vya kwanza, Kuhakikisha Mungu ni kwanza kwenye ubinti wako* _Mathayo 22: 37-38_ _Mathayo 6: 33_ Yatupasa kumpenda Mungu kwanza na kumuweka wa kwanza kwenye maisha yetu. Usiweke wazazi, walezi, ma-sponso...
Apandacho mtu ndicho atakachovuna By Luphurise Mawere 12.04.2021 22:10
Wagalatia 6: 7-9_ _6 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna._ _8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele._ _9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho._ _2 Wakoritho 9: 6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba...
Jiepushe na Ubinafsi by Luphurise Mawere 15.03.2021 16:26
Wafilipi 2: 4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. *Ubinafsi* ni ile hali ya kujali mambo yako kwa kiasi kikubwa sana na kuyapa mambo ya wengine nafasi ndogo mno. Kujali mambo yako zaidi na kutoangalia mambo ya wengine kabisa. Dunia tunayoishi imejaa watu wengi wenye ubinafsi, maendeleo na changamoto zilizoko ulimwenguni zinazidi kufanya watu kuwa wabin...
Ukipita katika Shida mtumaini Mungu atakuokoa By Luphurise Mawere 24.02.2021 38:22
Zaburi 138: 7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa._ Soma pia _2 Mambo ya Nyakati 20: 1-30_ Tunaishi katika Ulimwengu uliojaa shida na taabu nyingi. Tuko kwenye Majira ambayo dunia imegubikwa na hofu na huzuni kubwa kwasababu ya shida ya janga la Corona, changamoto za upumuaji na tauni vinavyomaliza watu. Watu wengi w...
Ondoa macho yako kwenye upepo, Mtazame Yesu by Luphurise Mawere 26.01.2021 43:52
Somo lililofundishwa leo Jumanne tarehe 26/01/2021 katika Fellowship ya Wanawake inayofanyika kila Jumanne, saa 11: 30 Jioni, Makumbusho, Dar es Salaam
Ukimruhusu Mungu atunze kazi za mikono yako, HAUTATAABIKA By Luphurise Mawere 25.01.2021 14:13
*Ukimruhusu Mungu atunze kazi za mikono yako, HAUTATAABIKA!* _Kumbukumbu la Torati 11: 10-12 _10 Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinywesheleza kwa mguu wako, kama shamba la mboga;_ _11 lakini nchi mwivukiayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyweshwa maji ya mvua ya mbinguni;_ _12 nayo ni nchi itunzwayo na...
4. Amini kwamba Mungu atakufanikisha By Luphurise Mawere 04.01.2021 26:58
2 Wafalme 4: 1-7 Hesabu 27: 1-11 _Nehemia 2: 20 Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu._ Mistari hiyo hapo juu inaonyesha namna ambavyo Mwanamke mjane na mabinti za Selofehadi walikuwa kwenye changamoto kubwa. Walikuwa kwenye mazingira ambay...
Interview TBC Taifa FM: Kujipanga kwa matumizi ya fedha kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka 22.12.2020 23:21
By Luphurise Mawere
SIFA ZA MWANAMKE ALIYE-STRETCH YAANI ALIYEFANYA ZAIDI - PART 3 By Luphurise Mawere 21.12.2020 23:40
2 Wafalme 4: 1-7 Hesabu 27: 1-11 3. Amezungukwa na watu sahihi Umezungukwa na watu wa namna gani? Watu waliokuzunguka wanakusadia kufikia hatma yako au ndio wanakwamisha usifikie hatma yako? Watu waliokuzunguka wanaweza kubeba maono makubwa uliyonayo? Ukisoma hiyo mistari hapo juu utaona Mwanamke mjane ambaye alikuwa kwenye madeni yaani changamoto ngumu ya kifedha alikuwa amezungukwa na watu sahih...
SIFA ZA MWANAMKE ALIYE-STRETCH, ALIYEFANYA ZAIDI-PART 2 By Luphurise Mawere 07.12.2020 23:13
2 Wafalme 4: 1-7 Hesabu 27: 1-11 *2. Anaamini kwamba ndani yake kuna kitu cha kuleta mabadiliko anayoyataka* Ukisoma habari za Wanawake hao hapo juu ilifika mahali wakaamini kitu cha kubadilisha maisha yao kiko ndani yao na kwa kufanya hivyo changamoto walizokuwa wanapitia ziliondoka. Mwanamke aliye-Stretch anaamini anaweza, Ameondoka kwenye mazoea, Anajua yeye sio mtupu, Anajua ana uwezo, mkubwa...
Unaweza kusimama kwenye kusudi lako hata kama hujulikani by Luphurise Mawere 09.11.2020 14:20
2 Samweli 20: 16-22 Ukisoma kitabu cha 2 Samuel 20 utaona habari za mtu asiyefaa Sheba ambaye alitaka kuhatarisha amani ya Israel kwa kuwafanya watu kumfuata yeye badala ya kumfuata mfalme Daudi. Katika mistari inayotuongoza leo tunasoma habari za Mwanamke mmoja ambaye hata jina lake halijulikani lakini aliweza kusimama kwenye kusudi na kusaidia kuwepo kwa Amani Israeli na kuukomesha mpango wa She...
Ondoka kwenye Mazoea au kwenye Comfort Zone 02.11.2020 15:30
Naomba usome pamoja nami *2 Wafalme 7: 3-16* Watu wengi hawapigi hatua maishani kwasababu ya kukaa sana kwenye mazoea. Wengi wanatamani kufanikiwa ila hali za kukaa kwenye mazoea zinawazuia kabisa kupiga hatua katika maisha yao. Mazoea au Comfort zone ni ile hali ya kuwa mahali ambapo panakupa faraja na panakufanya ujisikie amani, usalama na nafuu. Katika habari tuliyosoma kwenye *2 Wafalme 7: 3-1...
Usifiche Talanta yako By Luphurise Mawere 26.10.2020 17:50
USIFICHE TALANTA YAKO _By Luphurise Mawere_ Mathayo 25: 14-18 _Mathayo 5: 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani._ Habari tuliyosoma kwenye Kitabu cha Mathayo 25: 14-18 inafananishwa na maisha yetu hapa duniani. Mungu amewekeza ndani yetu talanta, yaani ameweka karama, vipawa, ujuzi na maarifa. Kila mtu amepewa kadri uwezo wa...
Fanya zaidi, Stretch, Panua mahali pa hema zako By Luphurise Mawere 19.10.2020 16:07
_Isaya 54: 2 Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako._ Pia soma _2 Wafalme 4: 1-7_ Huduma ya Soaring Women International tumeandaa Summit ya Wanawake na tunasimama na neno STRETCH sawasawa na _2 Wafalme 4: 1-7_. STRETCH ina maana nyingi zinazolenga kumsukuma mtu afanye zaidi. Kwa Kiswahili tunaweza kuw...
Usiweke moyo wako kwenye vitu au mali ulizonazo _By Luphurise Mawere_ 12.10.2020 22:33
Luka 12: 15-21 _Zaburi 62: 10b Mali izidipo msiiangalie sana moyoni._ Kwa kiingereza huu mstari unasema _"If your riches increase, don't set your heart upon them"_ Mistari hiyo hapo juu kutoka kitabu cha Luka tunaona habari za mtu tajiri aliyekuwa na shamba lililokuwa limezaa sana, kwa lugha nyepesi mtu huyu alikuwa amefanikiwa sana na mali kumzidi. Tunaona hadi anaweka mikakati namna ambavyo ataw...
Jiepushe na Kiburi usije ukashushwa By Luphurise Mawere 05.10.2020 15:27
Jiepushe na Kiburi usije ukashushwa _By Luphurise Mawere_ _Mithali 29: 23 Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa._ Kiburi ni nini? Yeremia 9: 23-24 inatupa maana nzuri ya Kiburi _23 BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;_ _24 bali a...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.