Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Sepetuko Podcast; Uteketezaji shule- je walimu wakuu huwasikiza wanafunzi? 10.11.2021

Shule kadhaa zimeripotiwa kuwatoza wanafunzi wote faini kufuatia visa vya kuteketezwa shule. Mbona kuwabebesha mzigo wanafunzi wote na hali makosa yamefanywa na wachache? Hatua kama hizo zinaashiria kwamba wakuu wa shule bila shaka hawawasikizi wanafunzi!

Sepetuko Podcast; Wanafunzi kuteketeza shule kunaashiria tatizo kuu zaidi katika jamii! 09.11.2021

Kenya imekuwa ikijenga desturi ya haki za kimsingi; haki za watoto, haki za wanawake, haki za wazee lakini imeshindwa kujenga mwenendo wa kuwajibikia makosa! Wanafunzi wanaoteketeza shule wanafikiria kwamba wanapigania haki, hawajui kwamba haki huanza kwa kuwajibikia makosa.

Sepetuko Podcast; Kuwafuta kazi wafanyakazi KEMSA ni kukosa busara ya kifalme 08.11.2021

Nchi nzima imefahamu tangu mwaka jana (2020) kwamba wakosaji katika shirika la KEMSA wamekuwa wasimamizi-mameneja. Lakini sasa wanaobebeshwa mzigo ni wafanyakazi wadogo wasio na mamlaka katika taasisi ile; huo unaitwa ukosefu wa ufalme!

Sepetuko Podcast; Suala la kisomo cha Oscar Sudi laibua maswali kadhaa! 04.11.2021

Mbona mbunge wa Kapseret ameshinda uchaguzi wa eneo bunge kwa mihula miwili na hali kiwango chake cha masomo kinatiliwa shaka- amewezaje kuifanya kazi ya ubunge bila elimu ifaayo. Sudi ana kipi bora kinachowafanya wapiga kura wa Kapseret kumpenda?

Sepetuko Podcast; Unafiki wa kutaka mawaziri wahusikao siasa wajiuzulu 01.11.2021

Tangu ije serikali ya Jubilee mwaka 2013 baadhi ya mawaziri wametekeleza maagizo ya kisiasa kutoka kwa wakubwa wao wa kisiasa. Mbona wanasiasa wanaolalamika leo hawakulalamika? Tumesema yamekuwapo makosa tangu mwanzo- ni unafiki kuanza kulalamika leo.

Sepetuko Podcast; Ndoa ya kisiasa ya Anne Waiguru na Mwalimu Ruto PhD 29.10.2021

Muungano wa Gavana wa Kirinyagah na mwalimu Ruto PhD ni sawa na ushirika wa sungura wawili. Ni watu wawili wanaojua namna ya kujitafutia nafasi ya kujikuza hivi kwamba mioyoni mwao mawazo ya kuihudumia jamii huja baadaye.

Sepetuko Podcast; Fedheha za Anwar Loitiptip- Seneta wa Lamu. 26.10.2021

Wakenya wamekuwa wakiskia habari za kufedhehesha kumhusu Seneta wa Lamu; mara amefyatua risasi, mara amefyatuliwa risasi, mara binti amedai kupigwa naye. Visa hivi vingi vinaripotiwa kufanyika usiku wa manane. Tunautaja huo kuwa ukiukaji wa sura ya katiba inayohusu uongozi na maadili.

Sepetuko Podcast; Sarakasi za Ugavana Nairobi- Jiji yafaa liondolewe miongoni mwa kaunti 25.10.2021

Kwa kuwa jiji la Nairobi huwakilisha Kenya nzima likiwa jiji kuu, yafaa lisimamiwe na idara maalum ya serikali ya taifa wala sio kwa njia za kisiasa. NMS imefanya kazi nzuri kuliko wanasiasa wawili ambao wamekuwa magavana tangu mwaka 2013.

Sepetuko Podcast; BABA na Mwalimu Ruto wabembeleza kura Kirinyagah 21.10.2021

Wanasiasa wawili maarufu zaidi nchini wametumia kilele cha mashujaa dei kule Kirinyagah kubembeleza kura za Mt Kenya. Mwalimu Ruto, PhD, na BABA wametumia ndimi laini kutaka wakubalike Mt Kenya, wala hawakufika Wang’uru Stadium kuhudhuria mashujaa dei!

Sepetuko Podcast; Ahadi kwa mjane wa Dedan Kimathi na Mau Mau 19.10.2021

BABA amecheza mchezo wa siasa kwa kupiga magoti mbele ya mjane wa shujaa Dedan Kimathi kupokea baraka. Ametoa ahadi ya kuwafadhili kwa namna wakereketwa wa Mau Mau. Ahadi kwa wakereketwa hao zisiwe ahadi za kawaida za wanasiasa kama ilivyokuwa ahadi za viwanja vya michezo ambazo Jubilee ilizotoa 2013.

Sepetuko Podcast; Siasa ni mchezo wa kibinadamu wala hamna Mungu mle 18.10.2021

Imekuwa ikidaiwa kwamba William Ruto ana watu na Mungu. Raila Odinga huenda ndiye mgombeaji wa THE SYSTEM. Ukweli ni kwamba siasa hazina Mungu, siasa ni sarakasi za kibinadamu ambapo kila kitu hufanywa na watu wala hamna suala la kiroho mle.

Sepetuko Podcast; Hofu ya kusalitiwa yachelewesha miungano ya siasa kwa ajili ya 2022 14.10.2021

Ukiukaji wa makubaliano ya Rainbow 2003 na mgongano ulioibuka kwenye Jubilee umewafanya wanasiasa wakuu msimu huu kuingiwa na woga wa kushirikiana na wenzao kwa sababu wanahofia ile roho ya kumalizana ambayo ni kama wimbo unaorejelewa kwenye siasa za Kenya.

Sepetuko Podcast; Nani yu tayari kuiga njia aliyofuata Dkt John Pombe Magufuli? 13.10.2021

Viongozi wa One Kenya Alliance waashiria kutaka kujenga uadilifu kwenye siasa za nchi na kwenye utumishi wa umma. Kwenye kampeni zao Makueni wamezungumzia uaminifu. Je watafanikiwa katika nchi inayoathirika kwa utumbili usungura na ufisi?

Sepetuko Podcast; Ondoa utumbili kwanza, jenga uadilifu nchini Kenya 12.10.2021

Ni msimu wa wanasiasa wakuu kutangaza ajenda zao kwa taifa ili kuwavutia wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Mwaka 2022. Lakini ni vigumu ahadi hizo kutekelezwa kwa sababu ya ukosefu wa uadilifu kwenye daraja mbalimbali za kisiasa na kwenye utumishi wa umma.

Sepetuko Podcast; Hofu yachochea mikutano ya Mt Kenya Foundation. 08.10.2021

Vikao vinavyofanywa na Mt Kenya Foundation vinachochewa na hali ambapo msimu huu eneo litalazimika kumpigia kura mgombeaji urais asiye mwenyeji wa eneo la Mt Kenya. Historia imeonyesha kwamba eneo hilo halijawahi kumpigia kura mgombeaji urais asiye mwenyeji wa eneo.

Sepetuko Podcast; Ufichuzi wa Pandora 07.10.2021

Rais Kenyatta achukua hatua ya haraka kuzima makisio kufuatia 'ufichuzi wa Pandora'. Lakini hatua ya rais iliacha maswali badala ya majibu. Wakenya sasa wasubiri kuona iwapo kutakuwa na majibu kwenye taarifa yake akisharejea nchini kutoka Amerika

Sepetuko Podcast; IEBC yagharamika zaidi kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu nchini. 05.10.2021

IEBC imekuwa ikilalamikia uchache wa pesa za kufadhili shughuli zake ikiwemo usajili wa wapiga kura wapya kwa sababu Kenya inaathirika kwa watu kukosa kuaminiana. Kukiwa na mwenendo wa kuaminiana, IEBC haitahitaji teknolojia ya gharama za juu kuendesha shughuli zake.

Sepetuko Podcast;Kizungumkuti cha Mt Kenya kumpigia kura mtu asiye asili wa eneo 01.10.2021

Historia ya uchaguzi wa urais nchini Kenya inaonyesha kwamba Mt Kenya haijawahi kumpigia kura mwanasiasa asiye asili wa eneo hilo tangu 1963. Iwapo Raila Odinga au William Ruto watapata kura za urais kwenye eneo hilo, basi itakuwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini.

Sepetuko Podcast;Kizungumkuti cha Mt Kenya kumpigia kura mtu asiye asili wa eneo 01.10.2021

Historia ya uchaguzi wa urais nchini Kenya inaonyesha kwamba Mt Kenya haijawahi kumpigia kura mwanasiasa asiye asili wa eneo hilo tangu 1963. Iwapo Raila Odinga au William Ruto watapata kura za urais kwenye eneo hilo, basi itakuwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini.

Sepetuko Podcast; Athari za Uchina ni ajenda muhimu 2022 29.09.2021

Mwanasiasa atakayeshinda urais 2022 atakuwa na jukumu la kukomesha uingizaji vifaa na bidhaa za kutoka Uchina nchini Kenya ambazo zinaweza kutengenezwa humu nchini. Kenya inunue Uchina kile haiwezi kukiunda.

Sepetuko Podcast; Ukienda kwa wakwe kupeleka posa, andamana na vijana wa sura nzuri! 28.09.2021

BABA atafuta kura za Mt Kenya lakini aandamana na vijana wasiojua kuzungumza, Je wazee wa jamii watakubali kumwoza binti aitwaye ‘kura za Mt Kenya?’ William Ruto akielekea kule huandamana na wale wanaojua kuzungumza.

Sepetuko Podcast; Raila abadilisha mbinu za kutafuta kura 27.09.2021

Awali shujaa wa mikutano ya hadhara, mwanasiasa wa mvuto mbele ya umati alikuwa BABA. Siku hizi shujaa wa umati na kampeni za mikutano anaibuka kuwa Dkt William Ruto. Je mbinu hizi zitamfaa nani zimlemee nani?

Sepetuko Podcast; Ughali wa mafuta; Bunge latoa kauli za ndumakuwili 23.09.2021

Mawaziri na wabunge wana uwezo wa kurekebisha bei ya mafuta; wabunge kulia machozi ya kwikwi sasa ni kuwachezea wakenya mchezo wa shere- ni sherehe za tumbili!

Sepetuko Podcast; Kejeli za wanasiasa wa Mt Kenya 21.09.2021

Eneo la Mt Kenya linachangia 23% ya idadi nzima ya watu nchini Kenya, kudai 40% ya nyadhifa serikalini ni kuwafanyia wakenya stihizai na kejeli. Yafaa wanasiasa hao wafanye utafiti waelewe ukweli wa mambo!

Sepetuko Podcast; Kuelimika ni kutohusika ufisadi na wizi 20.09.2021

Kuhusika ufisadi ni kutoelimika. Elimu ya vyuoni yafaa ifunze Filosofia. Filosofia hufunza maadili; nidhamu, tabia na mienendo. Anayedai kuwa na elimu ya chuo kikuu lakini anahusika ufisadi hajaelimika!

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.