Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Sepetuko Podcast; Sakata ya Rio-Utumbili unaoathiri ushujaa michezoni 18.09.2021

Adhabu yaja baada ya miaka mitano ya kutokea ufisadi uliovuruga ushujaa wa wanamichezo wa Kenya Rio De Janeiro. Sakata nyingine zinazovuruga maisha ya wakenya zasubiri kusuluhishwa, kuu zaidi ikiwa NYS!

Sepetuko Podcast; Ughali wa mafuta-Serikali isiyomjali raia 16.09.2021

Mafuta yakiwa ghali, gharama ya maisha hupanda maana mafuta ndio kawi ya kuendesha maisha. Serikali inafahamu hilo lakini inakosa roho ya kulegeza gharama hizo kumpunguzia mkenya mzigo.

Sepetuko Podcast; Ahadi za Raila Odinga kwa Wamaasai 15.09.2021

Mkataba wa Anglo-Maasai treaty -1904, uliifanya jamii ya Maasai kuwa iliyoathirika zaidi kwa ukoloni kuliko jamii nyingine za Kenya. Kwa hivyo ahadi za wanasiasa zisiwe za kimatamshi tu. Ziwe ahadi za kurekebisha athari za ukoloni.

Sepetuko Podcast; Kuwarekebisha viongozi ni jukumu la kanisa 14.09.2021

Nathan Mtume alifika mbele ya Daudi Mfalme na kumwambia ukweli kwamba alikuwa amefanya makosa. Akasema pia kwamba Mungu atamwadhibu! Kuwaambia viongozi ukweli ni jukumu la viongozi wa dini.

Sepetuko Podcast; Mkasa wa Laikipia una mizizi kwenye siasa 13.09.2021

Idara za usalama zafaa kuangalia kwa umakini chanzo cha mavamizi ya Laikipia; kichocheo ni ushindani wa 2022.

Sepetuko Podcast; Kuwashirikisha wazazi kwenye masomo ya wanao hufanywa tofauti 09.09.2021

Tangu elimu iliyoletwa na wakoloni kuanzishwa barani Afrika, mzazi ameshiriki kwa njia ya ushauri na ufadhili sio kushirikiana na mwanawe kufanya mitihani jioni.

Sepetuko Podcast: CBC mtihani mkubwa kwa wazazi 08.09.2021

Mfumo wa CBC ni wazo zuri lakini utekelezaji wake unafanywa kwa njia inayomlimbikizia mzazi mzigo mkubwa.

Sepetuko Podcast: Jubilee Imeshindwa Kumkabili Ruto; Inajiaibisha! 07.09.2021

Hatua ya Chama cha Jubilee kuendeleza shutuma dhidi ya Naibu wa Rais, William Ruto ni ishara kwamba kimekosa mwelekeo na kimekosa njia za kumkabili. Jubilee inaendelea kujipaka tope...

Sepetuko Podcast; ODM, Wacha Vita na IEBC; Tumia 'System' Kuwafidia Waliodhulumiwa -ndiyo kazi muhimu 18.08.2021

Chama cha ODM kinafaa kujisafishia jina kwa kuacha tabia za kulalamika kuhusu kila kitu. Wakati huu ambapo Raila anashirikiana na Uhuru Kenyatta, kelele za ODM za kupanga kumwondoa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati hazina maana. ODM itumie 'system' kuhakikisha kuwa wafuasi wake waliodhulumiwa na polisi huko Nyanza wakati wa uchaguzi wanafidiwa. Kulialia kila mara hakufai.

Sepetuko Podcast; Museveni Anawajali Wanariadha Kuliko Uhuru; Aibu ya Kuwatuza Siku 10 Baadaye 18.08.2021

Wanariadha wa Kenya walioshiriki Olimpiki jijini Tokyo Japan wameliletea taifa sifa kedekede kwa kuibuka la kwanza barani Afrika. Hata hivyo, hawakupokelewa kishujaa walipowasili JKIA. Aidha, Rais Kenyatta aliwaalika katika hafla ya kutuzwa siku 10 baada ya kuwasili nchini. Rais Museveni kwa upande wake aliwatuza wanariadha wa nchi yake punde walipowasili. Ni wazi kuwa Kenya haiwajali wanaspoti wa...

Sepetuko Podcast; Uhuru ameamua ni Raila - kuondoa chuki za kihistoria 13.08.2021

Uhuru Kenyatta amefanya kikao kilichowaleta pamoja Raila Odinga na viongozi wa One Kenya Alliance, OKA. Uhuru aliwashawishi kumuunga mkono Raila, akisema ndiye wa pekee mwenye ushawishi wa kisiasa. Japo haijasemwa, Uhuru analenga kuondoa siasa za chuki za kihistoria na kuchimbana...za tangu miaka ya 60. Pia analenga kuondoa propaganda dhidi ya familia ya Jaramogi ila kumtenga Ruto au kutotimiza ah...

Sepetuko Podcast: Wakimbiaji wa Uganda wapokewa kishujaa; wa Kenya wapuuzwa 11.08.2021

Serikali ya Kenya ni zuzu. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaandalia wanariadha wa nchi yake makaribisho ya kifahari; wametembezwa mijini kwa magari ya kifahari kuwapungia mikono wananchi, wakapewa kitita cha fedha na zawadi ya magari. Hapa Kenya, serikali imenyamaza kama maji mtungini bila kujivunia nafasi ya kwanza ambayo Kenya ilipata barani Afrika katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo Japa...

Sepetuko Podcast: Rais Uhuru, kumwaibisha Ruto ni kukosa ufalme 05.08.2021

Rais Kenyatta ampe heshima Naibu wake, William Ruto sawa na walivyofanya marais wa awali kwa Makamu wao. Kulumbana na kuaibishana haradhani kunatoa taswira mbaya. Ni ukosefu wa ufalme.

Sepetuko Podcast: Ruto, jifunze kupitia CCM ya TZ na ANC ya Afrika Kusini, si NRM ya Museveni 05.08.2021

Baada ya Naibu wa Rais wa Kenya, William Ruto kuzuiwa kwenda Uganda, maswali mengi yameibuka kuhusu lengo lake la kwenda katika nchi hiyo. Ushauri wa Sepetuko ni kwamba asijifunze siasa za Chama cha NRM cha Yoweri Museveni wa Uganda kwa vile kinahusishwa na dhuluma dhidi ya wapinzani na kukatalia madaraka. Ruto ajifunze siasa kupitia Chama cha CCM cha Tanzania au kile cha ANC cha Afrika Kusini; si...

SEPETUKO PODCAST; Ni Vigumu kwa Odinga Kukubalika Mlima Kenya -Chuki za Kihistoria 30.07.2021

Ni vigumu kwa Raila Odinga kupata ufuasi Mlima Kenya. Mbegu za chuki zilipandwa tangu miaka ya sitini na Jaramogi na Jomo kisha kuendelezwa na Uhuru na Raila. Kubadili si rahisi. Umati mkubwa ambao Raila alikuwa akikusanya awali, Ruto ndiye mwenye uwezo wa kufanya hivyo sasa.

SEPETUKO PODCAST; Uadui Kati ya Jaramogi na Kenyatta; Athari Zingalipo 30.07.2021

Sababu za jamii ya Mlima Kenya kumchukia Raila Odinga kisiasa ni za kihistoria. Ni uhasama ulioanza miaka ya sitini ambapo Tom Mboya alimchochea Jaramogi kutaka apewe kiti cha urais kwa njia zote. Jamii ya Agikuyu ilimwona Jaramogi kuwa adui aliyetaka kumpokonya kiti Mzee Jomo Kenyatta. Ikabidi kafara zifanywe Mlima Kenya ili kukilinda kiti cha urais. Uhasama wa kisiasa baina ya Jaramogi na Jomo u...

SEPETUKO PODCAST: Kutoaminiana na kusalitiana katika NASA; hakuna utu-uzima 23.07.2021

Viongozi wa NASA wanazidi kutapatapa na kuchanganyikiwa kisiasa. Kuaminiana hakupo. Utu-uzima haupo. Kusalitiana na kulumbana kuhusu pesa na nani ni bora nani si bora kumetawala. Huu si ukomavu wa kisiasa.

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.