Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Matukio ndani ya UDA yanaonyesha upungufu wa sera. 01.08.2024

Matukio yanayoendelea ndani ya chama cha UDA ni dhihirisho tosha la umbali wa safari yetu kuwa na vyama vya kisiasa vyenye sera na msimamo. Vyetu ni vyama vinavyotumiwa tu kuwa daraja la kuingia mamlakani na baada ya uchaguzi, kudondoshwa kama kaa moto.

Bunge la Kitaifa Laanza Msasa wa Mawaziri Walioteuliwa 31.07.2024

Bunge la Kitaifa linaanza kuwapiga msasa Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto, katika Baraza jipya alilotangaza. Hii ni fursa adimu kwa Bunge kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba na kuonesha kuwa ni taasisi huru na inayojisimamia bila kushurutishwa na Serikali tendaji. Hii ni fursa ya Bunge kusafisha jina lake ambalo limekuwa si lolote la kujivunia.

Kumbukumbu ya Hatua za Kinidhamu na Maswali ya Hatima 30.07.2024

Chama cha ODM kimeendelea kutoa msimamo kinzani kuhusu hatua ya viongozi wake wakuu kujumuishwa serikalini, na kuibua kumbukumbu ya hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Wabunge wake waliotangaza msimamo wao wa kushirikiana na serikali baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Je, viongozi hawa wakuu wa chama hiki watachukuliwa hatua zozote. Kama sivyo, basi tusihadaiwe zaidi. 

Heshimu Wanahabari na Taaluma ya Uanahabari 25.07.2024

Maandamano yaliyofanywa na wanahabari nchini hayashinikizi lolote nje ya Katiba ya nchi. Yanashinikiza tu taaluma ya uanahabari kuheshimiwa na haki za wanahabari kulindwa kama ilivyo katika sheria za nchi. Wanahabari sio wahalifu, wao ni mwito wa kuitumikia nchi na wananchi wake.

Rais Ruto Askilize Vijana Kwa Matendo, Sio Vitisho: Sepetuko 24.07.2024

Maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali yanamaanisha kuwa Rais William Ruto atastahili kuwasikiliza zaidi vijana wanaoandamana. Kusikiliza huku hakuwezekani katika mazingiraya kujipiga kifua na vitisho. Kusikiliza huku ni zaidi kupitia kwa matendo.

Bustani ya Demokrasia 22.07.2024

Harakati ambayo imekuwa ikiendelezwa dhidi ya serikali lazima ikuze taifa linalosikiliza. Linalosikiliza kwa lengo la kuelewa, na kukumbuka kuwa serikali ni raia na sio vinginevyo. Government by the people, for the people...

Kamwe tusiruhusu wahuni kurejea katika mitaa yetu, na siasa zetu. 19.07.2024

Maandamano dhidi ya serikali yameingiliwa na wahuni ambao nia yao ni kupora, kujeruhi na hata kuua na kuharibu. Jumatano wiki hii, wahuni pia wametatiza mkutano wa Azimio, wakisababisha purukushani na majeraha kwa wanahabari. Ni wakati wahuni hawa na wafadhili wao wakabiliwe vilivyo.

Kuendeleza Uhuru wa Vyombo vya Habari ni Kudumisha Demokrasia ya Kenya 18.07.2024

Kukamatwa kwa mwanahabari mtajika Macharia Gaitho katika mazingira ya kudhalilisha na kuhujumu haki za mtu, siku moja tu baada ya mwanahabari wa Kameme kufyatuliwa risasi na polisi huko Nakuru alipokuwa akiangazia maandamano dhidi ya serikali kunaonesha kuchipuka tena kwa majaribio ya kudunisha uhuru wa vyombo vya habari unaolindwa Kikatiba. Kamwe tusikubali hilo kufanyika, uhuru wa wanahabari na...

Dhuluma Dhidi ya Uhuru wa Habari 17.07.2024

Tukio la kufyatuliwa risasi mwanahabari wa Kituo cha Kameme Nakuru Wanjeri wa Kariuki katika maandamano dhidi ya serikali ni mfano hai wa majaribio ya serikali kuwalenga wanahabari, kwa lengo la kuwanyamazisha wasitekeleze wajibu wao ambao unalindwa na Katiba ya Kenya. Kamwe hatuko tayari kurudisha nyuma hatua kubwa zilizopigwa katika kukuza demokrasia na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.

Miili Tisa Kware Yazua Maswali Kuhusu Ufanisi wa Usalama 16.07.2024

Tukio la kupatikana miili zaidi ya tisa eneo la Kware, Embakasi ni dhihirisho tosha la nchi ambayo taasisi zake za kiusalama hazifanyi kazi, zimefeli pakubwa. Iweje watu wauliwe na miili yao kutupwa bila NIS, DCI au Idara ya Polisi kuwa na ufahamu ya tukio hilo la kihalifu? Tunataka uwajibishwaji wa ofisi husika.

Kupunguzwa kwa Washauri Serikalini 11.07.2024

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amewaandikia Mawaziri wote kuwataka kupunguza idadi ya washauri kutoka wawili hadi mmoja kwa kila Waziri ili kupunguza matumizi ya pesa za serikali. Hatua hii imeibua swali la hivi hawa washauri wamekuwa wakifanya kazi gani ikiwa kwa kipindi cha miaka miwili serikali hii imekuwa ikifanya baadhi ya maamuzi mabovu mno, kiasi cha kugeuka na kuwa shubiri kiasi hik...

Kenya Baada ya Miaka Sitini: Mabadiliko Makubwa Yaja! 10.07.2024

Miaka sitini tangu kupata uhuru uongozi wa nchi ya Kenya umekuwa ukiendeshwa na wanasiasa wabinafsi wasiomjali yeyote ila maslahi yao tu. Hali inaonekana inabadilika na sasa wananchi wataanza kujiamulia wanavyotaka kuongozwa. Hilo lifanyikapo, basi ole wao hawa wanasiasa. Interesting times ahead!

Mgomo wa Maafisa wa Kliniki Wamalizika Baada ya Siku 99 09.07.2024

Maafisa wa Kliniki wametamatisha mgomo wao ambao umedumu siku 99 baada ya mapatano kati yao na Baraza la Magavana COG. Hii ni nafuu kubwa kwa Wakenya ambao hutegemea huduma katika hospitali za umma, japo inatoa changamoto kwa serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa migomo hii ya mara kwa mara katika sekta ya afya.

Hongera kwa Serikali kwa Kubadili Mwenendo na Kuwasikiliza Raia 08.07.2024

Sepetuko leo inahongera serikali kwa hatua yake ya kubadili mwenendo na kuanza kuwasikiliza raia. Ni katika kuwasikiliza raia ndipo serikali itaweza kuafiki mengi, na sio katika kuwapuuza wananchi ambao ndio wenye serikali.

Unyenyekevu wa Wanasiasa Baada ya Maandamano ya Vijana 04.07.2024

Viwango vya unyenyekevu miongoni mwa wanasiasa wetu, ambavyo vinashuhudiwa baada ya maandamano na harakati za vijana wa kizazi cha Gen Zs na wengine ni mfano hai wa uwezo wa watu. Yaani hadi wanasiasa wetu wenyewe wanakataa nyongeza ya mishahara waliyokuwa wameongezewa na Tume ya Utathmini wa Mishahara na Marupurupu SRC! Huu unafaa kusalia kuwa mkondo. Wanasiasa kujua kuwa kuipuuza sauti ya mwanan...

Maandamano Yafanyike Kwa Amani 03.07.2024

Maandamano yanayoendelezwa nchini dhidi ya serikali yanalindwa na Katiba ya Kenya, bora tu yafanywe kwa amani. Inasikitisha kuwaona wahuni wakihitilafiana na maandamano haya, kuwapora Wakenya mali yao waliyoitafuta kwa jasho lao. Wacha watuhumiwa hawa wasakwe na kukabiliwa na mkono wa sheria kutokana na shughuli zao za kihalifu. Hawa sio sehemu ya waandamanaji na kamwe hawafai kuchukuliwa hivyo.

Tishio kwa Amani na Utawala wa Sheria 02.07.2024

Visa vinavyoendelezwa na serikali vya kuwateka nyara vijana na wanasiasa wanaohusishwa na maandamano dhidi ya serikali yanatia shubiri uwezekano wa kufumbua fumbo hili. Zaidi ni uhuni ambao ni kinyume kabisa na sheria za nchi. Amani haipatikana kwa kiganja kilichofumbatwa.

Matatizo ya serikali yanatokana na Rais asiyeaminika 01.07.2024

Sehemu kubwa ya matatizo yanayokumba serikali hii ni Wakenya kukosa imani kwake kutokana na kuwapo Rais asiyependa ukweli. Rais ambaye hadi leo amekwama katika uongo wa kuwatetea maafisa wa usalama waliohusika katika ukatili dhidi ya waandamanaji. Rais anayesema hili, kisha naye anafanya jingine. Ni hadi Rais Ruto amaanishe ayasemayo, afanye anayosema na ajifundishe kusema ukweli ndipo hali hii ya...

Uwezo wa Vijana Katika Maandamano ya Demokrasia 28.06.2024

Vijana wa Gen Zs na vijana wengine ambao wamekuwa wakiendeleza maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 wametukumbusha uwezo tulio nao kama wananchi wapigakura. Uwezo wa kupiga kura kuwachagua viongozi wetu, lakini zaidi kuwawajibisha wanapokuwa ofisini. Harakati hii haifai kukoma. Huu unafaa kuwa mwanzo tu wa kutetea Katiba yetu na kudai uongozi bora ambao tunastahili.

Aibu Kwa Bunge la Kitaifa! 27.06.2024

Hatua ya serikali kuwatuma wanajeshi kusaidia polisi kuwakabili waandamanaji ni ukiukaji mkubwa wa sheria za nchi. Inasikitisha kuwa Bunge la Kitaifa limetumiwa kutia muhuri uhayani huu! So unfortunate!

Ulinzi wa Amani au Uvunjaji wa Haki za Binadamu? 26.06.2024

Tukio la vijana waliokuwa wakiandamana kuingia katika majengo ya Bunge kamwe sio la kushabikiwa. Hata hivyo, tukio hilo na mengine ya waandamanaji kuharibu mali ya umma na kibinafsi hayatoi sababu tosha kwa maafisa wa usalama kuwafyatulia risasi na kuwaua waandamanaji. Hayatoi sababu kwa Rais kuwaita Wakenya kuwa wahalifu na wahaini.

Sauti ya Vijana Haipuuzwi Tena 25.06.2024

Maandamano yanayoendelezwa dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 ni ukumbusho kwa serikali kuhusu jinsi sauti ya vijana imekuwa ikipuuzwa. Vijana wanakumbwa na changamoto mbalimbali, kuu miongoni mwazo, ikiwa ni ukosefu wa ajira nchini. Serikali haina budi kutafakari mbinu mahsusi ya kutatua hili na changamoto nyingine zinazowakumba vijana.

Serikali Yalazimika Kukubali Ukweli wa Maandamano ya Vijana 24.06.2024

Serikali sasa imegundua kuwa haiwezekani kupuuza maandamano yanayoendelezwa na kizazi cha vijana dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024. Rais mwenyewe amekiri kuwa ipo haja ya kufanyika mazungumzo kati yake na vijana hawa. Kiukweli, hakuwa na budi. Kuanzia mwanzo haingewezekana tu kuwapuuza vijana hawa kutokana na sababu kadhaa.

Maandamano ya Amani: Kulinda Haki za Wananchi wa Kenya na Katiba 21.06.2024

Kuandamana ni haki ya wananchi wa Kenya, na inalinda na Katiba ya sasa ya nchi. Bora tu maandamano haya yafanywe kwa amani bila kuvuruga usalama. Hatua ya maafisa wa usalama kuwakabili waandamanaji wanaoandamana kwa amani ni uvunjaji wa sheria.

Maandamano ya Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha wa 2024 20.06.2024

Maandamano yanayoendelezwa na Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 ni zaidi ya Mswada wa Fedha. Ni dhihirisho la kutaabika kwa muda mrefu ambako Mkenya amekuwa akipitia mikononi mwa serikali isiyojali na inayowadharau, kwa miaka. Hii ni sababu tosha ya serikali kuwa na wasiwasi.

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.