Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Maandamano ya Wakenya Dhidi ya Mswada wa Fedha 19.06.2024

Maandamano ya Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha yahweh onyo kwa serikali. Onyo kuwa wananchi wamejifundisha kujitetea na kutetea haki yao wanapohisi kuhujumiwa. Kinyume na maandamano ya miaka ya nyuma, haya yanaongozwa na Wakenya wenyewe, na sio wanasiasa.

Udhaifu wa Maamuzi ya Bunge 18.06.2024

Mwenendo wa Wabunge wetu wakati wa kufanya maamuzi muhimu yanayomhusu Mkenya wa kawaida ni dhihirisho tosha la maamuzi duni ambayo huwa tunafanya Bungeni. Haimhitaji mpigakura kumtumia arafa Mbunge ama kuandamana ili wafanye maamuzi bora ya kutuwakilisha. Tujifundishe kitu, inatupasa kufanya maamuzi bora debeni siku za usoni.

Junior Starlets Wafuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake Chini ya Miaka 17 18.06.2024

Heko kwa Junior Starlets kwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa wanawake chipukizi chini ya miaka 17. Historia iliyoje! Junior Starlets inakuwa timu ya kwanza kabisa ya Kenya ya kandanda kufuzu kwa Kombe la Dunia. Maandalizi ya kushiriki kombe hilo yaanze sasa.

Pengo Kubwa katika Bajeti ya 2024/2025 14.06.2024

Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Kifedha wa 2024/2025 yalisomwa Bungeni na Waziri wa Fedha Njuguna Ndungu. Katika makadirio hayo ya jumla ya shilingi trilioni 3.99 lipo pengo la shilingi bilioni 600. Pengo hili lazima likutie wasiwasi. Unajua kwa nini?

Kuwajibika kwa Mafao ya Rais Mstaafu: Je, Jopo ni Lazima? 13.06.2024

Suala la mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta halistahili jopo, ni suala ambalo sheria za nchi zinatosha katika kulitatua. Kenyatta anauliza kipi kilifanyika kwa mgao wake wa bajeti kwa miaka miwili, kwa mfano, haihitaji jopo kujibu swali hilo.

Heko Rais Ruto Kwa Kushughulikia Malalamishi ya Kenyatta 12.06.2024

Suala la mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta halistahili jopo, ni suala ambalo sheria za nchi zinatosha katika kulitatua. Kenyatta anauliza kipi kilifanyika kwa mgao wake wa bajeti kwa miaka miwili, kwa mfano, haihitaji jopo kujibu swali hilo.

Hujuma kwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. Ni Aibu kwa Taifa. 11.06.2024

Hujuma anayopitishiwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na ofisi yake ni aibu kubwa kwa taifa hili. Rais William Ruto anamkosea heshima Kenyatta na Wakenya wote kijumla kwa kupuuza maslahi ya Kiongozi wa nchi ambaye aliihudumia nchi hii kwa miaka kumi. Ikiwa hujuma hii inatokana na uhasama wa kisiasa wa uchaguzi mkuu uliopita, basi shame on this Government.

Sharti rais Ruto na Gachagua wakomeshe ukabila 10.06.2024

Ukabila bado ni sumu hatari inayokumba Kenya na Wakenya. Wacha Rais na Naibu wake waoneshe mfano bora katika kutokomeza jinamizi hili na sio kuanzisha siasa za kimaeneo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatishia kuigawanya nchi.

Uongozi wa Wanawake: Kutimiza Ndoto za Uongozi wa Kike Kenya 04.06.2024

Kuchaguliwa kwa mwanamke kuwa Rais wa Mexico ni dhihirisho tosha la jinsi mtazamo wa watu unaweza kubadilika na wakaukumbatia uongozi wa wanawake. Naamini ipo siku Kenya itakuja kutimizwa ndoto hii ya wanawake wengi kuchaguliwa katika nyadhfa za uongozi. Ipo siku.

KIONGOZI WA KITAIFA AU MSIMAMIZI WA ENEO? 03.06.2024

Juhudi zinazoendelezwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua kusukuma ajenda za eneo la Mlima Kenya zinahujumu azma ya tiketi ya Urais kuwa nembo ya umoja wa nchi nzima na sio eneo moja. Naibu Rais anafaa kuhudumia nchi nzima na sio kujikita tu katika eneo anakotoka.

Ruto Alifadhiliwa na Nani Kuenda Marekani? 31.05.2024

Madai ya Rais William Ruto kuwa sehemu ya ziara yake kuenda nchini Marekani ilifadhiliwa na marafiki zake ni kinyume na Katiba ya Nchi. Waliomfadhili Rais ni kina nani na walifanya hivyo kwa nia gani?

Serikali Ilenge Kupanua Idadi Ya Walipa Ushuru 30.05.2024

Kuendelea kwa serikali kuongeza ushuru wanaotozwa wafanyabiashara kunatishia kuwatorosha waekezaji hadi mataifa mengine. Serikali ilenge kupanua idadi ya walipaushuru, sio kuwatoza walipaushuru waliopo ushuru zaidi ya uwezo wao.

Serikali Izingatie Maoni ya Wananchi Kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024 29.05.2024

Vikao vinavyoendelea vya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 visiwe tu kwa nia ya kujifanya kuheshimu Katiba. Wacha maoni ya Wakenya yatiliwe maanani na kuheshimiwa.

Athari za Kutuma Maafisa wa Polisi Haiti 28.05.2024

Hatua ya kuwatuma maafisa wa Polisi Haiti ni uamuzi usiokuwa wa hekima. Ni uamuzi ambao hauwezi kuelezwa kwa njia nyingine yoyote ile, isipokuwa kuonesha ubaraka kwa taifa la Marekani na washirika wake. Na hilo litakuja na athari zake mbovu kwa nchi.

Ruto Aambia Dunia KQ ni Ghali Kuliko Ndege Binafsi 27.05.2024

Rais William Ruto amejitetea kuhusiana na hatua yake kutumia ndege ya kibinafsi kusafiri hadi nchini Marekani, akidai kuwa kufanya hivyo kulikuwa kwa gharama ya chini kuliko kutumia ndege za Shirika la Ndege la Kenya Airways. Kujitetea huku kuionesha serikali hii kuwa isiyojali kuhusu utunzaji wa Mali ya umma na pia maafisa wakuu wa serikali hawana Imani na huduma zinazotolewa katika mashirika ya...

Safari ya Haki: Balozi wa Uingereza Azuru Kenya Kutafuta Ukweli kwa Agnes Wanjiru 24.05.2024

Ziara ya Balozi wa Uingereza Nchini Kenya kwa familia ya Mkenya Agnes Wanjiru aliyetuhumiwa kuuliwa na mwanajeshi wa Uingereza kwenye kambi ya Jeshi ya Uingereza iliyoko Nanyuki uwe mwanzo wa kupatikana kwa haki kwa Wanjiru na waathiriwa wengine wa hujuma mikononi mwa wanajeshi wa Uingereza waliomo nchini.

Serikali Itatue Mgomo wa Walimu wa JSS Kuokoa Elimu 23.05.2024

Jinsi serikali inashughulikia mgomo wa walimu wa JSS kunaonesha serikali isiyojali. Mbona tunachezea elimu ya watoto wetu? Mbona suala hili halifanywi kipaumbele?

Mgao wa Fedha za Serikali Kwa Idadi ya Watu Unahatarisha Umoja Wetu 21.05.2024

Gumzo la mgao wa fedha za serikali na maendeleo kutolewa kwa msingi wa idadi ya watu, linatishia kurejesha nyuma hatua ambazo zimepigwa kuhakikisha ujenzi wa Kenya moja. Jamii zote zinazoishi Kenya zinastahili kujihisi kuwa nyumbani, bila kujalisha idadi yao.

Okoa Mpango wa Lishe Shuleni 20.05.2024

Pendekezo la serikali kufutilia mbali mpango wa lishe shuleni sio la hekima. Linatishia kurejesha nyuma hatua zilizopigwa katika kuhakikisha wanafunzi kutoka maeneo kame, mitaa ya mabanda na maeneo mengine yaliyosalia nyuma kimaendeleo wanapata elimu.

Mswada wa Fedha 2024/2025: Je, Kenya Kwanza Inakujali Wewe? 17.05.2024

Mapendekezo yaliyomo kwenye Mswada wa Fedha wa mwaka wa kifedha ujao yanaonesha wazi kuwa serikali ya Kenya Kwanza haina ufahamu wa hali halisi ya Mkenya. Haijali kuhusu vipaumbele vya Mkenya. Lakini, nani aliiweka serikali hii mamlakani kama sio Mkenya yuyu huyu. Huwa tunauliza maswali kuhusu nani atafadhili ahadi chungu nzima zinazotolewa na wanasiasa wakati wa kampeini?

Ruto na Ushuru: Kutatua Deni au Kutatua Ufisadi? 16.05.2024

Rais William Ruto amekariri kuwa analenga kupandisha hata zaidi ushuru anaotozwa Mkenya, eti ili kupunguza deni la taifa. Sepetuko inamkumbusha Rais kuwa tatizo la Kenya sio la kimapato, ila ni mianya iliyopo ya uporaji wa mali ya umma.

Mswada wa Fedha wa Mwaka wa 2024/2025: Je, Ni mzigo Mpya Kwa Wananchi? 15.05.2024

Mswada wa Fedha wa Mwaka wa 2024/2025 una baadhi ya mapendekezo ambayo kimsingi yatamuongezea Mkenya mzigo wa ushuru ambao tayari ni mzito. Sepetuko inakariri kuwa kamwe haiwezekani kwa nchi kujiendeleza kupitia kuwatoza wananchi wake kodi nyingi! Haiwezekani.

Fedha za Elimu: Hatari kwa Maendeleo ya Elimu ya JSS 13.05.2024

Shule zinapofunguliwa kwa masomo ya muhula wa pili, Sepetuko inairai serikali kuangazia masuala kadhaa kwenye sekta ya elimu. Miongoni mwa masuala hayo ni kucheleweshwa kwa fedha za serikali za kufadhili elimu, na changamoto zinazokumba elimu ya JSS. 

Mipango ya Kupambana na Ufisadi Kutoka Fiji hadi Kenya: Kesi ya Frank Bainimarama 10.05.2024

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama amefungwa jela kwa kuzuia uchunguzi wa ufisadi. Hapa Kenya, vita dhidi ya ufisadi havijazaa matunda aina hii, na kuibua swali la inawezekanaje kwa mwanasiasa wa haiba hii kufungwa jela. Sepetuko inakariri kuwa vita dhidi ya ufisadi haviwezekani ikiwa yetu ni kuwatetea na hata kuwachagua kwa nyadhfa za juu wanasiasa mafisadi. 

Sakata ya mbolea ghushi: Kesi ya Waziri Mithika Linturi 09.05.2024

Wabunge wana nafasi ya kuwadhihirishia Wakenya kuwa yao ni taasisi huru katika hoja ya kumbandua Waziri wa Kilimo Mithika Linturi iliyoko mbele yake. Hii ni fursa ya kuubaini ukweli na kutoa uamuzi wa haki kwa Linturi, lakini zaidi kwa Wakenya ambao huenda wakadhurika kutokana na wakulima kuuziwa mbolea ghushi. 

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.