Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Hatari Zinazokumba Jamii: Athari za Mafuriko kwa Makazi karibu na Mito 07.05.2024

Wakenya wanaoishi kwenye maeneo ya mito na mabwawa ya maji wameendelea kuhamishwa kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini. Sepetuko inauliza noani waliidhinisha ujenzi wa makazi ya watu kwenye maeneo haya. Je, wapo maafisa wa serikali waliotepetea na kuzuru ujenzi huu, na ikiwa ndiyo, ni haki wawajibishwe kisheria. 

Kutenga Fedha kwa Ajili ya Waathiriwa wa Mafuriko: Wito wa Uwajibikaji 06.05.2024

Serikali ya Kitaifa na za Kaunti zimeendelea kutangaza kutengwa kwa mabilioni ya pesa kwa ajili ya waathiriwa wa mafuriko nchini na mikakati ya kukabili mafuriko. Wacha fedha hizo zitumiwe ifaavyo na maafisa wanaohusika wawajibishwe kwa matumizi yake. 

Kilio cha Mfanyakazi Mkenya 02.05.2024

Kenya inaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi. Sepetuko inakariri kuwa mfanyakazi Mkenya hana lolote la kusherehekea. Mishahara ni duni, ushuru anaotozwa ni maradufu, mazingira anamofanyia kazi ni duni na masaibu mengine mengi anayokumbana nayo.

Janga la Mafuriko: Msaada wa Dharura Unahitajika! 30.04.2024

Janga linaloendelea nchini la mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 150 linahitaji juhudi za pamoja na dharura kutoka kwa serikali na washikadau wengine. Sepetuko inairai serikali kuweka kando mipango mwingine yoyote isiyokuwa ya dharura na ya lazima, na kulifanya janga hili kuwa kipaumbele.

Nini cha Kufanya Wakati wa Mafuriko 29.04.2024

Mafuriko yanayoendelea nchini yameendelea kusababisha mauti na uharibifu mkubwa. Ndiyo, tuilaumu serikali kwa kukosa kujiandalia majanga kama haya, lakini ni muhimu pia uchukue tahadhari. Usalama wako wakati huu unaanza na mimi na wewe.

Mafuriko Yanabainisha Udhaifu wa Serikali na Miundombinu Duni 26.04.2024

Mafuriko yanayoshuhudiwa jijini Nairobi na kote nchini yanaonesha wazi uwezo duni wa serikali kujiandaa kwa ajili ya majanga, na pia kuwepo kwa miundomsingi duni kustahimili majanga yanapotokea. Sepetuko inazirai Serikali za Kaunti na ya Kitaifa kuweka mikakati kabambe ya kujiandalia majanga kama mafuriko ili kuepusha mauti yanayoshuhudiwa.

Huduma za Afya Zimepooza kwa Siku 40: Serikali Inawajali Wakenya Kweli? 24.04.2024

Kwa zaidi ya siku 40, Wakenya wameendelea kukosa huduma za matibabu katika hospitali za umma kufuatia mgomo wa madaktari. Madai ya serikali eti kunao mwafaka unaoelekea kutiwa saini kati yake na madaktari inaonekana ilikuwa njama tu ya kuwashinikiza madaktari kusalimu amri. Hii ni serikali aina gani inayowachezea watu wake kiasi hiki? Mbona idai kuna mwafaka ilhali huo sio ukweli? Nani anamjali Mk...

Kifo cha CDF Ogolla Kimezua Maswali Mengi; Wakenya Wadai Majibu 22.04.2024

Kweli ajali haina kinga. Hata hivyo tukio la Jenerali wa Jeshi la Nchi kufariki kwenye ajali ya ndege, akiwa ndani mwa nchi yake, ni jambo ambalo lazima lichunguzwe. Je, kunao waliolala kazini kiasi cha kuruhusu tukio hili kutokea au ni ajali tu kama ajali nyingine? Lazima pafanyike uchunguzi wa kina kubaini kilichojiri.

Serikali Inajitahidi Kweli Kupunguza Matumizi? 18.04.2024

Juma hili kumefanyika Kongamano la Kutathmini Viwango vya Mishahara na Marupurupu wanayopata wafanyakazi wa serikali. Rais amekariri kuwa serikali yake inajizatiti kupunguza mianya ya ufujaji serikalini. Sepetuko inasema kuwa kongamano hili na juhudi hizi ni kazi bure ikiwa serikali bado inaendelea kupanua viwango vya mishahara kwa kuwaajiri Mawaziri Wasaidizi CAS.

Mgogoro wa Madaktari Unahatarisha Maisha ya Wengi 17.04.2024

Mgomo wa madaktari umetimiza sasa siku 35, naam majuma matano. Hakuna mwafaka wowote wa aina yoyote, na mwananchi anayetegemea huduma za afya katika hospitali za umma ndiye anaumia. Nani atamjali raia huyu?

Nairobi Yazamishwa na Mafuriko: Serikali Iko Wapi? 16.04.2024

Mvua inayonyesha nchini inaanika wazi upungufu wa serikali katika kujiandaa kwa ajili ya msimu wa mvua ambao hutabiriwa mapema. Sepetuko inatoa changamoto kwa serikali kutafuta mbinu ya kuimarisha mfumo wa uzoaji majitaka, na kuvuna maji ya mvua kusaidia siku za usoni.

Mbolea Ghushi: Serikali Yajichanganya 12.04.2024

Serikali imeendelea kujikanganya kuhusu taarifa za kuwapo mbolea ghushi nchini. Waziri wa Kilimo sasa anadai kuwa iliyokuwapo sio mbolea ghushi ila mbolea isiyokuwa na madini hitajika. Who's fooling who?

Mgomo wa Madaktari: Uhai wa Wakenya Uko Hatarini 11.04.2024

Mgomo wa madaktari unaoendelea sasa unatishia haki ya binadamu kwa uhai. Sepetuko inatoa wito kwa serikali na vyama vya madaktari kulegeza misimamo na kufumbua fumbo hili kwa faida ya raia.

Iweje Serikali Ikose Pesa Kulipa Madaktari, Lakini Iwe na za MaCAS na Ziara za Viongozi? 09.04.2024

Mgomo wa madaktari unapoendelea, Rais William Ruto amewarai madaktari kurejea kazini, akisema serikali haina pesa na kuwa hali ni ngumu. Sepetuko inashangaa ni vipi serikali haina pesa za kuwaajiri madaktari wanagenzi lakini ina hela za kuwaajiri maCAS na kufadhili ziara za hapa na pale za Rais na Mawaziri serikalini.

Usalama Barabarani: Kila Mtu Akiwajibika Kupunguza Ajali 08.04.2024

Description - Maelfu ya Wakenya wanaendelea kuaga dunia nchini kutokana na ajali barabarani. Familia zinaendelea kupoteza wapendwa wao kwa mnyama huyu anayeweza kuepukika. Ni wakati sasa sote tuwajibikie usalama barabarani -madereva, watumiaji wa miguu, wahudumu wa bodaboda na raia wengine. Jukumu la usalama barabarani sasa lazima liwe letu sote.

Uchaguzi wa UDA: Uingiliaji wa Serikali Kupitia Wenyeviti wa KRA na KPLC? 04.04.2024

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Ushuru Nchini KRA na mwenzake wa Kampuni ya Nguvu za Umeme KPLC kusimamia uchaguzi wa viongozi wa chama cha UDA haufai kabisa. Sepetuko inasema wacha uongozi wa chama utenganishwe na uongozi wa nchi na mashirika yake. Mambo haya mawili kamwe yasichanganywe.

Masomo kwa Kenya Kutoka kwa Ufanisi wa Diomaye Faye, Rais Mpya Wa Senegal 03.04.2024

Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ameapishwa rasmi kuiongoza nchi hiyo. Faye, mwenye umri wa miaka 44 anakuwa Rais wa tano wa taifa hilo na Rais mchanga zaidi kuongoza taifa hilo la Afrika Magharibi. Ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliopita ni wa kihistoria kutokana na kuwa yeye si mtu maarufu mno katika siasa nchini humo, na aliondoka jela siku tisa tu kuelekea Uchaguzi Mkuu. Tunajifun...

Mgogoro wa Afya: Maisha ya Wakenya Yapo Hatarini! 02.04.2024

Baada ya wiki kadhaa za mgomo wa madaktari, hali katika hospitali na vituo vya afya vya umma nchini Kenya imechukuwa sura mbaya zaidi kufuatia kujiunga kwa matabibu katika mgomo huo. Mgogoro huu umepelekea athari kubwa kwa mfumo wa afya nchini, na kusababisha ugumu mkubwa kwa wananchi wanaotegemea huduma za matibabu kutoka hospitali za umma. Sharti seriklai ifanye jambo kwa upesi mno kuokoa hali....

Rais Ruto Awe Kiongozi Mwenye Uzalendo, Atatue Mgomo wa Madaktari: SEPETUKO 28.03.2024

Mgomo wa madaktari unaoendelea lazima ufanywe kipaumbele na serikali. Wagonjwa wanaendelea kutaabika kutokana na kushindwa kupatiwa huduma muhimu za matibabu. Sepetuko inasisitiza kuwa ni wakati Rais William Ruto aangazie mbinu za kusitisha mgomo huu ili kuokoa maisha ya Wanjiku.

Wetangula Dhidi Ya Natembeya: Bora Kwa Demokrasia Ila Sio Kwa Vurugu 27.03.2024

Ubabe wa kisiasa kati ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ni dhihirisho la demokrasia ya nchi. Hata hivyo, ubabe huu haufai kuishia kuwa wa vurugu. Sepetuko inakariri kuwa kamwe vurugu hazifai kuwa sehemu ya siasa za taifa hili. Wanaohusika katika kuzua vurugu mazishini, kwenye mikutano ya hadhara au kwingineko kokote kule lazima wawajibishwe kish...

Je, Nairobi Iko Tayari Kukabiliana na Mvua Kubwa? 26.03.2024

Mvua iliyonyesha usiku wa Jumapili imesababisha mauti na uharibifu mkubwa jijini Nairobi. Mvua hiyo imeonesha wazi jinsi miundomsingi iliyopo haina uwezo wa kustahimili mvua kubwa, hivyo kuna haja ya uekezaji wa kumaanisha katika miundomsingi ya ukusanyaji maji taka (drainage) ili kuwaepushia wakazi madhara.

Mgomo wa Madaktari: Wananchi Waathirika, Suluhisho Lahitajika Haraka 25.03.2024

Vitisho vinavyotolewa na Waziri wa Afya Susan Nakhumicha na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja dhidi ya madaktari wanaogoma si sahihi. Havitoi suluhisho kwa mgomo huu ambao umelemaza shughuli katika hospitali za umma nchini. Wanaoumia ni wananchi wanaotegemea huduma hizi na hawana pesa za kutafuta huduma katika hospitali binafsi. Serikali itafute suluhisho la kusitisha mgomo huu mara moja.

Mgomo wa Madaktari, Ukosefu wa Ajira, Ufisadi Vyaongezea Huzuni kwa Wakenya: SEPETUKO 22.03.2024

Umoja wa Mataifa juzi umetoa orodha ya mataifa yenye furaha zaidi duniani. Finland kwa mara nyingine tena imeibuka nafasi ya kwanza, kutokana na huduma bora wananchi wa taifa hilo wanapata kutoka kwa serikali. Kenya iko katika nafasi ya 114 duniani. Sepetuko inakiri kuwa Wakenya wengi hawana furaha kutokana na ugumu wanaopitia, huku serikali ya siku ikionekana kutojali. Wakenya watafurahi vipi wak...

Ni Nani Anayewajibika kwa Mbolea Ghushi?- Sepetuko 21.03.2024

Taarifa za wakulima nchini kuuziwa mbolea ghushi zinaibua swali la Je, Kenya ni nchi ya ughushi? Tulifikaje kiwango hiki cha kuanza kuchezea uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii -Kilimo? Sepetuko inasisitiza kuwa kamwe haiwezekani tuendelee kufanya michezo hii na uzalishaji wa chakula nchini.

Rita Tinina: Mwanamke Jasiri Aliyevunja Vizuizi Katika Sekta ya Habari: Sepetuko 19.03.2024

Sepetuko inaomboleza kifo cha mwanahabari wa NTV Rita Tinina. Yapo mengi ya kujifundisha kutokana na maisha ya Tinina, kuanzia kwa uchapakazi wake, unyenyekevu wake na ukarimu wake.

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.