Standard Media

Sepetuko

News SW ↓ 142 episodes

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.

Author

Standard Media

Category

News

Podcast website

www.standardmedia.co.ke

Latest episode

Aug 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Wito kwa Rais Ruto Kuzuia Maziko ya Vyombo vya Habari: Sepetuko 18.03.2024

Vyombo vya habari vilivyo dhabiti na huru ni msingi mojawapo wa demokrasia. Kwa demokrasia kuendelea kudumu nchini Kenya, ni muhimu kwa serikali kutolemaza vyombo vya habari vya kibinafsi vilivyopo. Sepetuko inamrai Rais William Ruto kutoruhusu maziko ya vyombo vya habari kufanyika wakati wa hatamu yake.

Mgomo wa Madaktari: Serikali Yalaumiwa Kwa Kupuuza Afya ya Wananchi 15.03.2024

Mgomo wa madaktari unaoendelea nchini unaionesha serikali kuwa isiyomjali raia. Afya ni kiungo muhimu katika uhai wa binadamu, hivyo serikali lazima ifanye kipaumbele suala la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za matibabu. Ni muhimu kwa serikali kufanya mazungumzo na vyama vya madaktari ili kuhakikisha mwananchi hataabiki kupata huduma za matibabu.

Siasa za Urithi ODM: Nani Afaa Kuvaa Kiatu cha Odinga?- SEPETUKO 13.03.2024

Hatua ya Kiongozi wa ODM kutangaza kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC imeibua mjadala mkubwa kuhusu nani anafaa kuvaa kiatu chake kuongoza chama hicho? Sepetuko inakariri kauli ya muigizaji wa Marekani William Powell kuwa ''power must be taken. It is not given." Yeyote asiketi hapo na kusubiri kukabidhiwa usukani wa ODM.

Kenya Kusaidia Haiti- Je, Ni Kafara au Ushujaa?: Sepetuko 11.03.2024

Marekani imeanza kuwaondoa nchini Haiti raia wake wanaofanya kazi kwenye Ubalozi wake nchini humo. Wakati uo huo, serikali ya nchi inaiomba Kenya kuharakisha mchakato wa kuwatuma maafisa wake wa polisi kuenda kudumisha usalama katika taifa hilo la eneo la Karibea. Hayo yanajiri huku magenge ya uhalifu yakiendeleza uhalifu katika nchi hiyo ya jumla ya watu milioni 11. Sepetuko inakariri kuwa kuwatu...

Miaka 30 ya Kusubiri-Mwanajeshi Mstaafu Ahangaika Kupata Pensheni 07.03.2024

Isaiah Ochanda, Afisa wa Jeshi aliyestaafu alifika mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Seneti akiwa kwenye kitanda cha hospitalini. Ochanda alistaafu kutoka Jeshini miaka ya 1990s na kwa miaka hiyo yote juhudi zake za kupata pesa zake za baada ya kustaafu zimegonga mwamba. Kulikoni? Mbona wafanyakazi wa serikali waliostaafu hutaabishwa mno kupata malipo ya uzeeni? Iko wapi serikali kuangazia suala hili?

Namwamba; kuna mwamba kuboresha spoti | Sepetuko Podcast 14.10.2022

Kuna changamoto nyingi katika sekta ya michezo nchini Kenya. Waziri wa Michezo, Ababu Namwamba ana kibarua na mwamba mkubwa kurejesha Kenya katika hadhi nzuri kispoti.

Baa la njaa; tupande mimea aina-aina | Sepetuko Podcast 14.10.2022

Baa la njaa limekuwa likizua kero kwa miaka mingi nchini Kenya. Ipo haja ya kutegemea mimea mbalimbali ya chakula - si mahindi pekee.

Mateso ya Wakenya Saudia; serikali iingilie | Sepetuko 15.09.2022

Kwa miaka mingi, Wakenya wanaokwenda Uarabuni, hasa Saudi Arabia kwa kazi za nyumbani wamekuwa wakiteswa, kunyimwa chakula, dawa na wengine kuuliwa. Serikali ya Kenya inafaa kutafuta suluhu ya tatizo hili. Dalmus Sakali anasimulia katika Sepetuko.

Uchaguzi wa amani Kenya | Sepetuko 15.09.2022

Wakenya walishiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka wa 2022 kwa amani. Ni mfano wa kuigwa kote Afrika. Dalmus Sakali anakupa uhondo katika makala ya Sepetuko.

Ruto alishinda, yasema Mahakama; kazi yamsubiri | Sepetuko 15.09.2022

Baada ya Mahakama ya Upeo kutupilia mbali kesi za kupinga ushindi wa William Ruto, sasa anacho kibarua cha kuiongoza Kenya, kuwaunganisha wote na kutekeleza ahadi alizotoa. Dalmus Sakali anasimulia.

Sepetuko Podcast; Kwa kutegemea kura za Mt Kenya Ruto ateleza! 13.02.2022

Baada ya rais Kenyatta kutangaza mwanzo wa siasa kali, joto litapanda huku mlengwa akiwa mwalimu William Ruto PhD. Itaibuka karibuni kwamba kosa kuu ambalo Ruto amelifanya ni kutegemea kura za eneo la Mt Kenya ambalo halijawahi kumpigia kura mwanasiasa asiyekuwa mwenyeji!

Sepetuko Podcast; Mbona hamkumtaja BABA kuwa msaliti, mbona akawa Mudavadi? 28.01.2022

Tangazo la Mudavadi Jan 23 kushirikiana na mwalimu Ruto (PhD) limechukuliwa vibaya kuliko tangazo la Raila Machi 9 2018 kushirikiana na rais Kenyatta- ajabu ni kwamba wote wamewasaliti wenzao

Sepetuko Podcast; Uanasiasa wa mwanasiasa Dkt Matiangi 17.12.2021

Katiba ya sasa ilipoandikwa ilifikirika kwamba mawaziri wakiteuliwa kutoka miongoni mwa wataalamu, watu wasio wanasiasa, huduma za baraza la mawaziri hazitaathirika kwa siasa. Lakini namna ambavyo Dkt Fred Matiangi amehusika siasa yaelekea njia hiyo sio suluhu ya kuondoa siasa kwenye huduma za mawaziri.

Sepetuko Podcast; Ukweli wa jina BABA ni safari ndefu ajabu! 13.12.2021

Mwaka 1988 kama mkenya angetamka jina Raila katika mazingira rasmi au ya umma, angejipata pabaya mbele ya vyombo vya serikali. Leo hii jamaa wa jina hilo (Raila) anaitwa BABA! Ni ishara ya Kenya kubadilika.

Sepetuko Podcast; Raila bado kupanda mlima- angali na kazi nzito mbele yake! 09.12.2021

Hata baada ya Mt Kenya Foundation kutangaza kumuunga mkono Raila Odinga, historia ya uhusiano inaathirika kwa propaganda dhalimu za miaka mingi zilizoliharibu jina la Odinga miongoni mwa watu wa Mt Kenya.

Sepetuko Podcast; Uchumi wa Fuliza sio utajiri! 03.12.2021

Rais katangaza kwamba Kenya sasa ni namba 6 kwa utajiri barani Afrika, Je utajiri huo uko wapi? Je upo miongoni mwa wakenya wanaotegemea mikopo ya Fuliza? Mbona magazeti yamejaa matangazo ya madalali kuuza mali ya watu wanaoshindwa kulipa mikopo ya benki?

Sepetuko Podcast; Iwapo uchumi umekua mbona vijana hawapati kazi? 02.12.2021

Rais amedai uchumi umekua ajabu hivi kwamba sasa Kenya ni namba 6 kwa utajiri barani Afrika, lakini mbona uchumi huo umeshindwa kubuni nafasi za kazi. Mojawapo ya dalili za ukuaji wa uchumi ni biashara za watu kupata faida huku watu wa umri wa kufanya kazi wakipata hizo kazi!

Sepetuko Podcast; George Kinoti ajipeleke jela ahudumie kifungo kwanza! 30.11.2021

Ni vigumu kwa afisa wa serikali ambaye mahakama imemtaja kuwa mfungwa kuendelea kuhudumu katika idara muhimu kwenye utaratibu wa kulinda sheria nchini -DCI. Itakuwa vigumu kwa mahakama kukubali saini zake kwenye rekodi za kesi zinazowasilishwa na idara ya upelelezi wa jinai.

Sepetuko Podcast; Ubaguzi dhidi ya Afrika kufuatia ugunduzi wa virusi vya Omicron 29.11.2021

Wazungu wamekuwa wepesi katika kutoa marufuku kwa ndege za mataifa ya kusini mwa Afrika na hali kile Afrika kusini ilifanya ni kugundua aina mpya ya virusi vya Korona-haikumaanisha kwamba Omicron imeanzia Afrika Kusini au Botswana.

Sepetuko Podcast; Mike Sonko aomboleza ‘mkasa’ wa kupoteza ugavana! 24.11.2021

Kinachomchochea aliyekuwa gavana wa Nairobi kuandaa kanda za video zilizonasa kwa siri watu anaoamini wamemdhulumu kwa namna, ikiwemo kumwondoa mamlakani Nairobi, ni kupoteza kiti cha ugavana. Hata sio suala la kuwakabili wafisadi.

Sepetuko Podcast; JE bodaboda watakataa pesa za abiria ambao hawajachanjwa? 23.11.2021

Hoteli zinatazamia kukusanya faida msimu wa likizo ya krisimasi, magari ya matatu pia yanajiandaa kufaidika zaidi msimu wa likizo hasa kwa kuwa msimu wa Korona uliathiri vibaya shughuli zao. Je serikali itatekeleza vipi maagizo kwamba wakenya ambao hawajachanjwa wanyimwe huduma?

Sepetuko Podcast; Wafanyakazi wadogo kubebeshwa mzigo wa makosa ya wakubwa! 22.11.2021

Kamati inayoongoza shughuli za kufufua Kenya Power yakiuka haki za wafanyakazi kwa kuwaitisha habari za akaunti zao za benki na mpesa. Ni mara nyingine tena ambapo wafanyakazi wadogo wanabebeshwa mzigo wa makosa ya mameneja!

Sepetuko Podcast; Wepesi katika kukabili suala la Kamiti- lakini imekuwapo walakin! 19.11.2021

Kuondolewa kwa mkuu wa magereza Whycliffe Ogallo kulifanywa kana kwamba alikuwa ndiye mfungwa wa Kamiti aliyekuwa ametoroka jela. Kuwaondoa wakubwa afisini kwafaa kuandamana na heshima zinazoendana na daraja la afisi zao.

Sepetuko Podcast; Kumzuia Miguna Miguna kunaipa serikali sifa mbaya 18.11.2021

Suala la raia wa Kenya kila mara kukwama katika viwanja vya ndege barani ulaya, huku ikidaiwa kwamba serikali ya Kenya imemzuia asirejee nchi aliyozaliwa, linaifanya Kenya kuchekwa na mataifa ya wazungu; ni hali inayochangia katika utani dhidi ya waafrika!

Sepetuko Podcast; FKF imekuwa kaburi la kuzika vipawa vya soka 16.11.2021

Vijana wakiwa shuleni ni mashujaa katika kucheza soka. Lakini punde wakishajiunga na sekta ya soka nchini vipawa hufa; sababu ni FKF kutowapa nafasi watu wanaoweza kuongoza soka kwa roho safi ili kuboresha viwango vya mchezo huo nchini.

Listen to the Sepetuko podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.