SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 930 episodes

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Author

SBS

Category

News

Podcast website

www.sbs.com.au

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Australia Yafafanuliwa:Je ukotayari kwa msimu wa mafua nchini Australia? 12.05.2026

Kirusi cha Influenza ni aina ya mafua yanayo ambukizwa kwa urahisi mkubwa na huzunguka mwaka mzima, lakini shughuli za mafua huongezeka wakati wa vuli, na maambukizi hufika kilele chake katika miezi ya majira ya baridi.

Taarifa ya Habari: Ugavi wa nyumba utakuwa muhimu katika bajeti ya shirikisho ya kesho serikali ya sema 11.05.2026

Waziri wa Makazi Clare O'Neil, anasema bajeti ya shirikisho itasaidia sana kushughulikia upungufu wa usambazaji wa makazi.

Anne "karibuni tusherehekee utu wa mwanamke, uvumilivu na neema" 09.05.2026

Wanawake wanao ishi katika maeneo ya jiji la Melbourne wame andaliwa tukio maalum Jumapili 10 May, ambayo huadhimishwa kama siku ya kina mama.

Taarifa ya Habari:Wanawake watatu wenye uhusiano na kundi la ISIS kufikishwa mahakamani 08.05.2026

Wanawake watatu wa Australia wenye uhusiano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (ISIS) wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya utumwa, uhalifu dhidi ya binadamu, na mashtaka ya ugaidi, baada ya kurejea nyumbani kutoka miaka kadhaa ya kuzuiliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Syria.

Yaliyojiri Afrika:Rais Tshisekedi adokeza uwezekano wa kuwania muhula wa tatu 08.05.2026

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amedokeza juu ya uwezekano wa kuwania muhula wa tatu, na kuchelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa katika muda wa miaka miwili ijayo.

Makala leo:Akiba dhidi ya matumizi: Chalmers anasema bajeti ijayo ni 'yenye uwajibikaji zaidi' 06.05.2026

Mweka Hazina wa Shirikisho Jim Chalmers ameahidi kutoa bajeti inayowajibika zaidi, lakini akiba inayotarajiwa katika kila wizara.

Taarifa ya Habari: Serikali yakana shutuma kwamba inawalenga wawekezaji wa "mama na baba" katika bajeti mpya 05.05.2026

Jim Chalmers amepuuza mapendekezo kwamba mabadiliko yanayowezekana kwa matumizi hasi ya vifaa au kodi ya faida ya mtaji yatakuwa ni kuvunja ahadi na wapiga kura.

Yaliyojiri Afrika: Viongozi wa Tanzania na Rwanda kuimarisha ushirikiano wa kikanda 05.05.2026

Viongozi wa Tanzania na Rwanda wamekubaliana kuchukua jukumu la kuhakikisha ushirikiano ndani ya Jumuiya ya afrika mashariki unaimarika kwa ajili ya manufaa ya kanda hiyo na watu wake.

Makala leo: Jinsi uchaguzi mdogo wa vijijini unavyoweza ashiria matatizo kwa upinzani wa Australia 05.05.2026

Uchaguzi mdogo ujao wa Mei 9 katika eneo bunge la Farrer jimboni New South Wales, unaweza kuwa na athari kubwa kwa siasa za kitaifa.

Taarifa ya Habari: Akiba itazidi matumizi na kodi katika bajeti ijayo Mweka Hazina aeleza taifa 04.05.2026

Mweka Hazina Jim Chalmers amesema bajeti ya shirikisho ya wiki ijayo itakuwa na kikomo chake kikubwa zaidi, wakati akiba ikitarajiwa kuzidi mabadiliko ya matumizi na kodi.

Australia Yafafanuliwa: Mbinu zakupunguza gharama ya mafuta 01.05.2026

Kuongezeka kwa bei za mafuta kunaweka shinikizo kwenye bajeti za familia kote nchini Australia—na kwa watu wengi, kunabadilisha jinsi wanavyosafiri.

Taarifa ya Habari: Upinzani waikosoa Serikali ya Madola kwa kuto fanya yakutosha kuimarisha usalama wa taifa 01.05.2026

Mbunge wa Upinzani Jonathon Duniam amesema Serikali ya shirikisho lazima iende mbali zaidi ili kuimarisha usalama wa taifa, kufuatia kutolewa kwa ripoti ya muda iliyotolewa na Tume ya Kifalme inayochunguza maswala ya chuki dhidi ya wayahudi na Uwiano wa Kijamii.

Yaliyojiri Afrika:Vikosi vya ulinzi vya Uganda vya shtumiwa kwa kuwauwa raia na kuwatesa wafuasi wa upinzani 01.05.2026

Shirika lakutetea hazi za binadam la Amnesty International, limevishtumu vikosi vya usalama vya Uganda kwa kuwauwa raia, kuwakamata kiholela na kuwatesa wafuasi wa upinzani katika kipindi chaku elekea na baada ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Makala leo: Ripoti mpya yataka mkakati wa kitaifa kuhusu Akili Bandia mahali pa kazi 01.05.2026

Ripoti mpya inasema kwamba Australia haina mkakati wa kitaifa wa kudhibiti kuenea kwa akili bandia mahali pa kazi.

Tips to reduce petrol costs | Fuel in Focus - Australia Yafafanuliwa:Mbinu za kupunguza gharama ya petroli | Mafuta Yalengwa 30.04.2026

Rising fuel prices are putting pressure on household budgets across Australia, and for many people, it’s changing the way they travel. So what can you do to reduce your fuel costs without giving up your daily routine? Here are some simple, practical ways to save money on petrol. - Kuongezeka kwa bei za mafuta kunaweka shinikizo kwenye bajeti za familia kote nchini Australia, na kwa watu wengi, kun...

Taarifa ya Habari:Burundi yaanza chanjo dhidi ya saratani ya kizazi 30.04.2026

Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anahimiza China kuanza tena usafirishaji wa mafuta ya ndege yanayo letwa Australia, baada ya mkutano na mwenzake wa China.

Makala leo: Matendo yakuzomea yachafua huduma za alfajiri 28.04.2026

Waaustralia wameadhimisha Siku ya Anzac kote nchini na katika fukwe ya Gallipoli nchini Uturuki kuwakumbuka waliohudumu katika jeshi.

Wiki Hii Barani Afrika: Nchi za Afrika Mashariki kujenga kiwanda chakusafisha mafuta Tanga, Tanzania 28.04.2026

Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki zime anza mazungumzo kuhusu, ujenzi wa kiwanda chakusafisha mafuta katika bandari ya Tanga, nchini Tanzania.

Taarifa ya Habari: Waasi wa Touareg wachukua udhibiti wa mji wa Kidal nchini Mali 28.04.2026

Australia itatumia jumla ya dola bilioni 1.2 kutengeneza mamia ya magari ya kijeshi aina ya Bushmaster, na kuboresha magari yanayo lindwa aina ya Hawkei. Dola milioni 750 zimetengwa kutengeneza karibu magari 300 aina ya Bushmaster, ikiwa ni pamoja na magari yaliyo agizwa na serikali ya Uholanzi.

Makala leo: Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yavunjika tena 28.04.2026

Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yamevunjika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kutangaza Jumapili kwamba anafuta safari ya mjumbe wake kwenda Pakistan.

Wiki Hii barani Afrika: Somaliland tayari kuipa Marekani rasilimali zake kwa ajili yakutambuliwa kama taifa 24.04.2026

Uongozi wa Somalilanda, uko tayari kuipa marekani haki za kuchimba madini nakuweka kambi zaki jeshi, kwa ajili yakutambuliwa kama nchi huru.

SBS Learn Eng Ep 108 Jinsi yakuzungumza kuhusu gharama ya maisha 24.04.2026

Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu gharama ya maisha ukitumia Kiingereza?

Taarifa ya Habari: Hatimae Tume ya Jaji Chande yatoa ripoti ya vurugu za uchaguzi Mkuu Tanzania 24.04.2026

Waziri Mkuu anasema wavu wa usalama wa umma utakuwa tayari kwa wakati, kuwasaidia Waaustralia watakao ondolewa kutoka Mpango wa Bima wa Kitaifa ya Ulemavu (NDIS) yenye thamani ya mabilioni ya dola.

Makala leo: Watetezi waunga mkono uamuzi wa kuoga bure katika huduma ya utunzaji wa wazee nyumbani 24.04.2026

Wiki hii umakini mkubwa umekuwa kwenye Mfumo wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu (NDIS), serikali ya shirikisho ikitangaza makato ambayo yanakadiriwa yata ondoa makumi ya maelfu ya watu kwenye mfumo huo.

The overlooked story: Aboriginal and Torres Strait Islander service on ANZAC Day - Hadithi iliyopuuzwa: Huduma yawa Aboriginal na wana Visiwa wa vya Torres Strait katika siku ya ANZAC 23.04.2026

Each year Australians gather on ANZAC Day to remember those who served in wars, conflicts and peacekeeping missions. But whose stories are we remembering? Are there stories we don’t always hear? In this episode we explore an important part of Australia’s history that has often been overlooked—the service of Aboriginal and Torres Strait Islander peoples. - Kila mwaka Waaustralia hujumuika katika si...

Listen to the SBS Swahili - SBS Swahili podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.