SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 930 episodes

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Author

SBS

Category

News

Podcast website

www.sbs.com.au

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Taarifa ya Habari:Polisi wamfungulia mashtaka ya ugaidi, mwanamke aliyerudi Australia kutoka Syria 28.05.2026

Jeshi la Polisi la Shirikisho la Australia limemkamata mwanamke mmoja, kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea chini ya Operesheni Kurrajong.

How does political grief affect social cohesion? - SBS Examines: Huzuni yakisiasa inawezaje athiri mshikamano wa kijamii? 27.05.2026

When we're exposed to events or ideologies that go against our own beliefs, we can feel what experts call 'political grief'. Some say it's playing a role in the growing polarisation of our society. - Tunapokabiliwa na matukio au itikadi zinazo enda kinyume na imani zetu binafsi, tunaweza hisi ambacho wataalam wanaita 'huzuni yakisiasa'. Baadhi wanasema inacheza nafasi katika ongezeko la mgawanyiko...

Australia Yafafanuliwa: Bendera yawa Aboriginal: Alama ya Utambulisho na Kuwa Sehemu ya Jamii 26.05.2026

Je, umewahi ona bendera ya rangi nyekundu, nyeusi na njano ikiwa pamoja na bendera ya Australia? Hii ni bendera yawa Aboriginal.

Yaliyojiri Afrika: Idadi ya watu wanaoshukiwa kuambukizwa Ebola nchini DRC yafika 900 26.05.2026

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema zaidi ya watu 900 wanashukiwa kuwa wameambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taarifa ya Habari:Waziri Mkuu atuliza hofu kuhusu sheria inayo tarajiwa kwa upunguzaji wa kodi ya mtaji 26.05.2026

Waziri Mkuu Anthony Albanese anasema upunguzaji wa kodi ya faida ya mtaji, hautajumuishwa katika sehemu ya kwanza ya sheria inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni katika siku zijazo.

SBS Learn Eng Ep 110 Jinsi yaku tafuta viatu vinavyo kufaa 26.05.2026

Je, unajua jinsi yakuomba msaada kwa Kiingereza, kupata viatu vinavyo kufaa.

Makala leo: Joto kali lawakaribisha mahujaji Macca kwa Hijja ya mwaka huu 26.05.2026

Ma milioni wame jumuika mjini Mecca Saudi Arabia, kwa hija ya mwaka huu.

Taarifa ya Habari: Kasi yaongezwa kuajiri wauguzi waku kabiliana na mlipuko wa Diphtheria 22.05.2026

Mipango inafanywa kupeleka wauguzi zaidi katika Wilaya ya Kaskazini kujibu mlipuko mbaya zaidi wa diphtheria nchini kwa zaidi ya miaka 30. Kesi 230 za maambukizo zimeripotiwa mwaka huu, kesi nyingi zikiwa katika Wilaya ya Kaskazini, lakini pia katika majimbo ya Magharibi Australia, Kusini Australia na Queensland. Nchini Uganda, zaidi ya watu 100 wamewekwa karantini, baada ya kushukiwa kuambukizwa...

Makala Leo: WHO yatangaza dharura ya afya duniani baada ya mlipuko wa Ebola DR Congo na Uganda 22.05.2026

Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ni dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi kimataifa. WHO inasema mlipuko huo hauja fikia vigezo vya dharura ya janga, lakini nchi zinazo changia mipaka ya ardhi na DRC ziko katika hatari kubwa ya usambaaji zaidi. Kwa wakazi wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekuwa na mambo men...

SBS Learn Eng Ep111 Jinsi yakupata huduma bomba zako nyumbani zikiwa na tatizo 22.05.2026

Je, unajua jinsi yakuomba msaada kwa Kiingereza bomba zako nyumbani zikipata tatizo? Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa Bonyeza hapo juu kwa mafunzo ya Kiingereza chepesi, kuhusu namna ya kuzungumza kuhusu bomba ambazo zina matatizo nyumbani kwako.

Taarifa ya Habari:Serikali ya Shirikisho ya tetea jibu lake kwa mlipuko wa Diphtheria 22.05.2026

Waziri wa Afya Mark Butler ametetea utoaji wa kifurushi cha dola milioni 7 kutoka kwa serikali kusaidia kujibu mlipuko wa ugonjwa wa diphtheria ambayo ni maambukizi makubwa ya bakteria yanayoambukiza sana na huathiri njia zakupumua na inaweza sababisha vidonda kwenye mwili pia. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Australia kimepanda hadi asilimia 4.5, huku kazi 19,000 zikiaondoka katika uchumi mna...

What can be done to stop price gouging during the fuel crisis? - SBS Examines:Nini inaweza fanywa kusimamisha kupandisha bei ya mafuta kwa njia ya unyonyaji? 21.05.2026

Fuel prices have spiked, and so have concerns and complaints about alleged price gouging. Are retailers cashing in on the crisis? - Bei za mafuta zimepanda, na wasiwasi pamoja na malalamiko kuhusu madai ya kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji nao pia ume ongezeka. Je, wauzaji wa rejareja wanafaidika kupitia mgogoro huu?

Anne "kina mama wanawezaje sawazisha kuhudumia naku imarisha mali ya familia zao" 21.05.2026

Kuto simamia mali vizuri, kunaweza weka mahusiano na familia nyingi katika hali mbaya. Anne Mureithi hutoa mafunzo kwa familia na jinsi yaku kuza mali zao. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Bi Anne alichangia mbinu ambazo familia zinaweza tumia kuimarisha familia na mali zao. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.

SBS Examines:Nini inaweza fanywa kusimamisha kupandisha bei ya mafuta kwa njia ya unyonyaji? 21.05.2026

Serikali ya Australia imeanzisha hatua kadhaa za kusaidia kupunguza shinikizo la usambazaji wa mafuta linalo endelea. Hatua hizo zinajumuisha kupunguzwa kwa muda kwa ushuru wa mafuta, na mamlaka zaidi kwa ACCC kupambana na kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji. Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi

Taarifa ya Habari: Chama cha Liberal hakifai fuata mwongozo wa chama cha One Nation Andrew McLachlan asema 19.05.2026

Mbunge wa chama cha Liberal Andrew McLachlan anasema Upinzani wa Mseto haufai kutafuta mwongozo kutoka kwa chama cha One Nation kuhusu maendeleo ya sera zao, huku akiendelea kupinga pendekezo la Angus Taylor la kupunguza malipo ya ustawi wa jamii kwa watu ambao si raia.

Yaliyojiri Afrika: Seriklai ya DRC kufungua vituo vitatu vya matibabu ya virusi vya Ebola 19.05.2026

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema Jumatatu itafungua vituo vitatu vya matibabu, kwa ajili ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika jimbo la Ituri.

Labor yatetea mabadiliko ya kodi ya nyumba katika bajeti licha ya ukosoaji katika kura za maoni 19.05.2026

Mjadala unaendelea kuhusu mustakabali wa mfumo wa kodi wa Australia, baada yakutolewa kwa bajejeti ya Shirikisho wiki iliyopita.

Taarifa ya Habari:Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda afariki 18.05.2026

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC iliyoko mjini The Hague, Uholanzi imesema mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda Felicien Kabuga amefariki dunia.

Taarifa ya Habari:Pendekezo la bajeti la upinzani lashtumiwa kuwa na madeni, upungufu wa kifedha, na utengano 15.05.2026

Waziri wa Fedha Jim Chalmers ame ongeza mashambulizi ya chama cha Labor dhidi ya hotuba ya majibu ya bajeti ya Angus Taylor, akimshtumu kiongozi huyo wa Upinzani kwa kutoa pendekezo lenye madeni, upungufu wa kifedha, na utengano.

Australia Yafafanuliwa: Vidokezo vya kupunguza gharama ya petroli |Mafuta Yalengwa 15.05.2026

Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu. Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu.

Makala leo: Maamuzi magumu kuhusu kupunguzwa kwa NDIS yatawala baada ya kutolewa kwa bajeti ya shirikisho 15.05.2026

Upunguzaji wa fedha katika Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu ndio chanzo kikubwa zaidi cha uokoaji wa fedha katika bajeti ya serikali shirikisho, jambo linalowaacha watu wengi katika jamii ya wenye ulemavu wakiwa na hasira na wasiwasi juu ya kile kinachokuja.

Taarifa ya Habari: Ghana kuwaondoa raia wake 300 wanaoishi Afrika Kusini 14.05.2026

Serikali ya Ghana imetangaza kuwa itawarudisha raia wake 300-wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia ongezeko la visa vya wageni kushambuliwa.

Yaliyojiri Afrika: Dangote kufungua kiwanda chakusafisha mafuta Kenya 14.05.2026

Mmoja wa matajiri wakubwa barani Afrika Aliko Dangote, ameonesha nia yakuanzisha kiwanda chaku safisha mafuta nchini Kenya.

Makala leo:Takwimu mpya zafichua malipo duni ya kimfumo kwa wafanyakazi wahamiaji 12.05.2026

Utafiti mkubwa zaidi nchini Australia kuhusu mazingira ya kazi ya wahamiaji umefichua maelezo ya kutisha ya malipo duni yaliyoenea na ya kimfumo.

Taarifa ya Habari:Mweka Hazina asema bajeti ijayo ina malengo, akiba na mageuzi makubwa kuliko kawaida 12.05.2026

Mweka Hazina wa taifa, Jim Chalmers, ameelezea bajeti inayokuja kama ile yenye malengo makubwa zaidi ya serikali ya Labor kufikia sasa, ikiwa na kile anachokiita akiba na mageuzi makubwa kuliko kawaida.

Listen to the SBS Swahili - SBS Swahili podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.