Nukta Habari

Nukta the Podcast

News SW ↓ 89 episodes

Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.

Be sure to visit the podcast's website and support the creator: nukta.co.tz

Author

Nukta Habari

Category

News

Podcast website

nukta.co.tz

Latest episode

Sep 26, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android almost 10M downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Mashaka ya maumbile yanavyozuia penzi la kweli 18.02.2022

Kwa maringo na mikogo ya Roxanne, unaweza kuhisi ni wa kishua au ana kila kitu lakini huwezi amini, na urembo wake wote alionao, anadaiwa kodi ya pango na kila siku anakimbizana na mwenye nyumba.

Filamu ya Brazen: Maandishi yanayomuwinda mwandishi wa vitabu 11.02.2022

Filamu ya “Brazen” inamuhusu mwanamama Grace Miller ambaye ni nyota maarufu wa vitabu vya simulizi nchini Marekani ambaye maandishi yake yanaanza kugeuka uhaisiana kumuwinda.

Kifahamu kisa cha kuumiza kinachoihusu kampuni ya Gucci 04.02.2022

Patrizia anavutiwa na kijana mmoja anaekutana naye kwenye party hiyo. Unaweza kuelezea hisia alizo nazo kama mtu kupata msamaha wa deni la timiza au kuwa zamu katika kupokea hela ya kikoba. Bila shaka unajua hisia hizo.

Filamu: Dunia inampatia mwanamfalme nafasi ya kuchagua kati ya nchi yake na huba. 28.01.2022

Izzy anajikuta akivunja kibubu chake alichojitunzia kwa muda mrefu kwa ajili ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani.

Utafanya nini pale ndoto yako inapokuingiza matatani? 21.01.2022

Siku moja Bom akiwa katika shughuli za kikazi, anaona wafanyakazi wenzie wawili  wanapigana, lakini anaposogea kwa karibu anakutana na kitu tofauti. Mfanyakazi mmoja ametapakaa damu usoni na anapomtazama kwa karibu anagundua kuwa mtu huyo amebadilika na kuwa kama ‘Zombie’.

Ifahamu filamu ‘inayotrend’ kwenye mitandao ya Kijamii Tanzania 14.01.2022

Changamoto za mahusiano, malezi, umaskini na mategemeo zote zimeelezewa kupitia wahusika wanne: Tumaini, Angel, Stella pamoja na Rose.

Safari ya ndugu waliopotezana kutafuta ukweli wa wazazi wao 07.01.2022

Filamu hii inawahusu mabinti watano ambao kwa mara ya kwanza wanakutana katika moja ya hoteli iliyopo Cancun mjini Mexico.

Kumpoteza mtu umpendaye ni mwanzo wa safari mpya 31.12.2021

Filamu hii inamleta tena Buster Moon, mdau wa sanaa za maonyesho ambaye kutengeneza show ya muziki inayoweza kukusanya sayari zote ni kitu kidogo sana.

A Naija christmas : Filamu ya kuchangamsha siku kuu yako. 24.12.2021

Filamu hii inahusu familia ya Madam Agatha, singo mother mwenye vijana wa kiume watatu Chike, Obi, na Ugo.

Filamu ya king’s affection: Majukumu yanavyobadilisha jinsia 17.12.2021

Filamu hii inaturudisha nyuma enzi hizo wakati nchi ya Joeson haijaitwa Korea. Katika kipindi hicho, Mwana mfalme mteule au “crown prince” Anatarajia mtoto ambaye atakuja kurithi kiti cha enzi kama mfalme wa Joeson.

Itakuwaje ikiwepo sayari ya wanaume peke yao? 10.12.2021

Ni filamu inayomhusu mwanadada ambaye anajikuta katika sayari iliyo na wanaume tu baada ya kupata ajali.

Huyu ndiye mwanamke shujaa wa Afrika 29.11.2021

Historia ya malkia huyu inatufanya turudi nyuma miaka 500 iliyopita, ambapo Amina akiwa ni ‘princess’ mdogo mwenye ujasiri na kipenzi cha baba yake.

Filamu ya ‘Red Notice’: Kikulacho ki nguoni mwako 19.11.2021

Filamu ya “Red Notice”, ipo kutukumbusha kuwa makini na wale wageni wanaogonga kwenye milango ya mioyo yetu na kutufanya tuone kuwa dhamira zao juu yetu ni za dhati.

Filamu ya “No Time To Die”: Mashaka yaliyojaa majuto 12.11.2021

Bahati ya mapenzi siyo ya wote, Wakati Adamu akikutana na Hawa kwa urahisi, wengine ni Samson wanaoishia na Delila. Samson wa leo ni James Bond almaarufu kama Agent 007.

Pesa zilivyoweka rehani maisha ya vijana watano 05.11.2021

Ni katika filamu ya Filamu ya the Army of Thieves inayohusu kikundi cha wezi waliobobea kuibia mabilionea

“My Name” Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako 22.10.2021

Katika filamu hii  ya “My name”, yaani jina langu, tunakutana na binti mrembo Yoo Ji Woo, ambaye katika maisha yake amekuwa akilelelewa na baba yake tu. Kwa jinsi baba yake alivyokuwa akimpenda sana, basi Jiwoo anaweza kujiita “dad’s daughter” kama vile wadada huwa wanajigamba. Maisha ya Jiwoo na baba yake siyo mazuri sana, kwani baba yake hakuwa na kazi rasmi ya kuwaingizia kipato zaidi ya k...

Mfahamu ‘single mother’ mpambanaji wa filamu ya Maid 15.10.2021

Clean Bandit hawakukosea walipoimba kibao Cha Rockabye , ambacho kinaelezea jinsi single mothers wengi wanavyopambana kwa hali na mali ili kuwalea watoto wao.

Wanawake na safari ya ushiriki maendeleo Kigoma 13.10.2021

Ushiriki wa wanawake katika maendeleo ya kata zao umechangia kuwepo kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule.

Wema unaosukuma maendeleo ya elimu Tanzania 13.10.2021

Kutana na watu wanaochangia maendeleo ya elimu Mkoani Kigoma kwa kuwasaidia wanafunzi kuvuka mto ambao umekuwa kikwazo cha elimu Mkoani humo.

Maisha ya ahueni baada ya Teleza 12.10.2021

Teleza ni wahalifu waliokuwa wanajipaka mafuta mwilini au oili na kuwabaka wakina mama mkoani kigoma. 

Matumaini mapya baada ya ujenzi wa shule kukwama Kigoma 12.10.2021

Endapo serikali itachelewa kukamilisha mradi wa shule hii, huenda ikachangia kwa wananchi kukata tamaa ya kujitoa kwenye shughuli za maendeleo.

Utafanya nini iwapo hakuna anayekuamini tena? 08.10.2021

Ni filamu ya “The Last Duel”, inayohusu kufa kwa uaminifu kati ya Marguerite na watu wake wa karibu

Filamu ya The Squid Game: Tamaa mbele mauti nyuma 01.10.2021

Uchambuzi wa filamu ya ‘The Squid Game’ inakukutanisha na watu wanaofanya maamuzi magumu baada ya maisha yao kutokuwa na ahueni kila uchao, huku mmoja wapo akiwa ni Gi-Hun . Hun ni mhusika mkuu katika filamu hii, ambaye maisha yake amekuwa akiyaendesha kwa ‘kuunga unga’ tu, huku kazi yake kubwa ikiwa ni kucheza kamali.

Saa 24 za kummaliza rafiki aliyegeuka kuwa adui 24.09.2021

Filamu ya Kate inamhusu mwanadada ambaye hajawahi kufaidi mapenzi ya baba na mama, kwani waliomleta duniani walifariki akiwa bado ni mtoto.

Wananchi wanaopambana kuokoa maisha Geita 23.09.2021

Ni kupitia ujenzi wa zahanati ambazo zitatumika kufanya matibabu ya wakazi wa mkoa huo.

Listen to the Nukta the Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.