Nukta Habari
Nukta the Podcast
Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
ELIMU YA SAIKOLOJIA INAVYOWABEBA WATU WENYE UALBINO TANZANIA 21.03.2023 9:15
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao. Abdushakur Mrisho ametuandalia...
Ifahamu zahanati iliyoanzishwa kwa mkopo wa halmashauri 01.10.2022 8:20
Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.
Mradi wa umemejua unavyowafaidisha wanavijiji Tanzania 03.06.2022 7:30
Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi shuleni Pangani 22.04.2022 6:34
Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.
Zaidi ya Watanzania 500,000 kukumbukwa na uhaba wa chakula 25.03.2022 3:29
Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini. Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na...
“Show” ya kibabe iliyowakutanisha mastaa wa Afrika 25.03.2022 5:48
‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika. Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo. Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika. Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, mu...
Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu 25.03.2022 1:40
Utunzaji wa mazingira yanayotuzunguka ni njia mojawapo ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mafuriko na ongezeko la joto.
Ukame ulivyowarudisha wafugaji kwenye umaskini Tanzania 24.03.2022 6:00
Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini. Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni...
Mbinu zitakazosaidia kudhibiti taka za baharini 23.03.2022 5:53
Kudhibiti uchafuzi wa bahari Serikali na wadau wanasema taasisi za utafiti na viwanda zinahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuimarisha mifumo ya ulejerezaji taka. Pia kupiga marufuku kabisa matumizi ya chupa za plastiki na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira ya bahari kama anavyoripoti Suleman Mwiru.
Gharama kubwa zinavyorudisha nyuma jitihada za kuokoa mazingira Wilaya ya Kibaha 22.03.2022 5:48
Baada ya kubaini faida na urahisi wa kutumia nishati ya gesi kupikia, mwalimu wa moja ya shule za sekondari wilayani Kibaha aliamua kuchukua hatua. Alianza jitihada za kutumia gesi kuongeza ufanisi katika mapishi shuleni kwao na kupunguza kiasi cha kuni zinazotumika kupikia ili kuokoa mazingira. Hata hivyo, changamoto iliyobaki ni gharama kubwa za kupata nishati hiyo. Herimina Mkude anatujuza zaid...
Changamoto zinapokuletea fursa 18.03.2022 7:55
Ni filamu ya "Fine Wine", inayomuhusu mwanadada Kaima anayepitia changamoto katika mahusiano. Licha ya uzuri na ‘usmati’ alionao binti huyu, mahusiano yake na kijana Tunji ni pasua kichwa kuliko hata majukumu yake ya kazi. Maisha ya Kaima yanabadilika siku ambayo wanakubaliana kukutana na Tunji katika mgahawa fulani, lakini kaka huyo anamwambia mpenziwe kuwa amsubiri kwani kuna jambo la ghafla lim...
Taka za kielektroniki zinavyotafuna mazingira ya Tanzania 14.03.2022 4:21
Hakuna mifumo mizuri ya kutupa taka za kielektroniki nchini Tanzania kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea hivyo suluhu kubwa iliyopo ni kuzitupa kama taka nyingine.
The Last Royal Treasure: Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako 11.03.2022 6:47
Filamu ya ‘The Last Royal Treasure’, inahusu kundi moja la maharamia au kwa Kiingereza wanafahamika kama pirates. Meli yao imebeba watu ambao wana historia tofauti za kimaisha. Wengine walikuwa majenerali wa vita, watoto wa manahodha, huku wengine wakiwa ni wezi walioshindikana.
Changamoto zinazorudisha nyuma urejelezaji taka Tanzania 10.03.2022 7:02
Ukosefu wa elimu ya udhibiti wa taka hasa plastiki, sera na sheria zinazosimamia mazingira zimetajwa na wadau wa mazingira kuwa zinaweza zikachelewesha safari ya kupunguza uharibifu wa mazingira hasa unaosababishwa na taka za plastiki.
Chupa za plastiki za vinywaji vya kuongeza nguvu zinavyochocheo uharibifu wa mazingira 05.03.2022 7:00
Kuzagaa kwa chupa za plastiki za rangi zinazotumika kuhifadhia vinywaji vya kuongeza nguvu katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam kumeibua changamoto mpya ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira. Licha ya chupa za maji kuokotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejelezaji, chupa za rangi zimekuwa zikiachwa zikizagaa mitaani kwa sababu wenye viwanda hawazihitaji katika shughuli zao.&nbs...
Magugu maji yanavyowatesa watumiaji wa Ziwa Victoria 28.02.2022 6:34
Kuendelea kuwepo kwa magugu maji katika Ziwa Victoria kumeibua kadhia mbalimbali kwa watumiaji wa ziwa hilo wakiwemo wavuvi na wamiliki wa boti na meli kwa sababu hutanda katika eneo kubwa na kuzuia shughuli zao. Wanafanya nini kukabiliana nayo? Msikilize mtangazaji Herimina Mkude ambaye anatoa ufafanuzi zaidi.
Simulizi ya Mtaa unaomezwa na maji ya Ziwa Victoria 25.02.2022 6:57
Ni Mtaa wa Ziwa mkoani Mwanza ambao umeharibiwa huku nyumba za wakazi wake zikizama kwenye maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Victoria. Kuongeza kwa kina cha maji cha ziwa hilo ni matokeo ya uchafuzi wa mazingira, mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2020. Wadau wa mazingira washauri watu kuondoka katika mtaa huo huku wakihimiza watu kuacha kujenga au kufanya shughuli za kilimo na uzal...
Mashaka ya maumbile yanavyozuia penzi la kweli 18.02.2022 8:47
Kwa maringo na mikogo ya Roxanne, unaweza kuhisi ni wa kishua au ana kila kitu lakini huwezi amini, na urembo wake wote alionao, anadaiwa kodi ya pango na kila siku anakimbizana na mwenye nyumba.
Filamu ya Brazen: Maandishi yanayomuwinda mwandishi wa vitabu 11.02.2022 7:05
Filamu ya “Brazen” inamuhusu mwanamama Grace Miller ambaye ni nyota maarufu wa vitabu vya simulizi nchini Marekani ambaye maandishi yake yanaanza kugeuka uhaisiana kumuwinda.
Kifahamu kisa cha kuumiza kinachoihusu kampuni ya Gucci 04.02.2022 8:13
Patrizia anavutiwa na kijana mmoja anaekutana naye kwenye party hiyo. Unaweza kuelezea hisia alizo nazo kama mtu kupata msamaha wa deni la timiza au kuwa zamu katika kupokea hela ya kikoba. Bila shaka unajua hisia hizo.
Filamu: Dunia inampatia mwanamfalme nafasi ya kuchagua kati ya nchi yake na huba. 28.01.2022 7:12
Izzy anajikuta akivunja kibubu chake alichojitunzia kwa muda mrefu kwa ajili ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani.
Utafanya nini pale ndoto yako inapokuingiza matatani? 21.01.2022 8:42
Siku moja Bom akiwa katika shughuli za kikazi, anaona wafanyakazi wenzie wawili wanapigana, lakini anaposogea kwa karibu anakutana na kitu tofauti. Mfanyakazi mmoja ametapakaa damu usoni na anapomtazama kwa karibu anagundua kuwa mtu huyo amebadilika na kuwa kama ‘Zombie’.
Ifahamu filamu ‘inayotrend’ kwenye mitandao ya Kijamii Tanzania 14.01.2022 9:25
Changamoto za mahusiano, malezi, umaskini na mategemeo zote zimeelezewa kupitia wahusika wanne: Tumaini, Angel, Stella pamoja na Rose.
Safari ya ndugu waliopotezana kutafuta ukweli wa wazazi wao 07.01.2022 9:16
Filamu hii inawahusu mabinti watano ambao kwa mara ya kwanza wanakutana katika moja ya hoteli iliyopo Cancun mjini Mexico.
Kumpoteza mtu umpendaye ni mwanzo wa safari mpya 31.12.2021 8:13
Filamu hii inamleta tena Buster Moon, mdau wa sanaa za maonyesho ambaye kutengeneza show ya muziki inayoweza kukusanya sayari zote ni kitu kidogo sana.
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.