Innocent Ngaoh
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha. Ni podcast ya kipekee ambayo utajifunza mambo mengi ambayo yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku, kila kitu kinachozungumzwa hapa kina uhalisia na siyo nadharia ya kusadikika. Kuwa sehemu ya familia hii na uhakika hautakuwa kama ulivyokuwa mwanzo, podcast ambayo itaboresha na kuongeza thamani ya maisha yako mara 10X au zaidi. Hakikisha unafollow ili uwe wa kwanza kupata episode mpya kila wiki.
Author
Innocent Ngaoh
Category
Podcast website
Latest episode
Apr 18, 2026
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Ujenge Nidhamu Ya Fedha Kwenye Maisha Yako. 28.10.2022 16:44
Safari ya kuelekea uhuru wa kifedha unahitaji kuwa na msingi wa nidhamu fedha; Je unataka kuwa na nidhamu ya fedha Ili uongeze kiwango cha kufanikiwa kwa maana ya mafanikio ya eneo la fedha. Sikiliza kisha fanyia kazi ambayo utapata kwenye episode hii utaona matokeo baada ya muda kwenye maisha yako.
Hatua Nne (04) Ambazo Maono Yako Yatapita Hadi Kukupa Mafanikio. 21.10.2022 16:51
Maisha yako yapo ndani ya dakika tano ambazo unazo, swali la kujiuliza unaishi kwa maono au ilimradi tu unavuta pumzi? Maisha mahali popote yanaongozwa na maono hata mafanikio yako yanategemea sana maono yako. Unajua hatua ambazo maono yako itapitia kabla ya kukupa mafanikio basi hii ni episode muhimu sana kwako sikiliza mpaka mwisho.
Jinsi Ya Kuacha Tabia Ya Kuwahukumu Watu Wengine. 04.10.2022 21:13
Tabia ya Kuwahukumu watu wengine ni tabia ya kiumaskini kwa sababu wewe siyo Mungu mpaka uwe unatoa hukumu kwa mabaya ya wengine, inaweza kuwa ni madhaifu, mapungufu, kasoro, makosa yao n.k lakini tambua kusikiliza episode hii utaweza Kuacha tabia ya hukumu watu wengine kwenye Maisha yako.
Sababu Saba (07) Za Kwanini Unaweza Kukabiliana Na Msongo Wa Mawazo Kwenye Maisha Yako. Part 02 26.09.2022 22:19
Njia pekee ya kutatua tatizo ni kutafuta suluhu ya tatizo si ndiyo? Hata msongo wa mawazo ni lazima ujue namna gani unaweza kukabiliana ili uwe mtu mwenye furaha, kujiamini, afya nzuri ya akili na mwili. Episode hii itakupa maarifa na taarifa za kina ni kwa namna gani unaweza kukabiliana na msongo wa mawazo kwa kupitia uzoefu, takwimu na ushauri kutoka kwa watu wenye maarifa ya kutosha na wataalam...
Tambua Dalili Nane (08) Za Mtu Anayesumbuliwa Na Msongo Wa Mawazo Na Athari Zake. Part 01 18.09.2022 21:57
Tafiti za shirika la American Psychology la Marekani inaonyesha mwaka 2020 zaidi ya watu milioni 190 wanasumbuliwa na msongo wa mawazo mkubwa sana duniani kote na zaidi ya watu milioni 284 wanasumbuliwa na hofu kubwa. Msongo wa mawazo unaiba furaha kwa kujua au kutokujua. Je unajua visababishi, dalili na athari za kuwa na msongo wa mawazo? Basi sikiliza episode hii upate kujifunza na kuwa balozi k...
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unapaswa Kuacha Tabia Ya Kulalamika Kwenye Maisha Yao. 08.09.2022 18:45
Je una tabia ya kulalamika kwenye maisha yako? Inawezekana unalalamikia wazazi, walezi, ndugu, marafiki, mpenzi, serikali, mfumo wa elimu, majirani zako n.k kuwa sababu ya wewe kuwa hapo. Lakini kumbuka hakuna faida ya wewe kulalamika kwa maana hiyo hii episode ni sahihi kwako na kuwa daraja kwa watu wenye tabia ya kulalamika kuacha na kuanza kuwajibika. Sikiliza na ujifunze...
Tumia Kanuni Ya 60/30/10 Kwenye Mgawanyo Wa Watu Kuambatana Nao. 30.08.2022 12:25
Watu ambao unaambatana nao wana nafasi kubwa ya wewe kufanikiwa au kutofanikiwa. Je unajua kanuni ya 60/30/10 itakusiadia Kuambatana na watu wa faida? Majibu yote utapata kwa Kusikiliza episode hii. Usishau kushare link kwa marafiki wajifunze na subscribe kupitia app ya castbox, Apple podcast, audiomack, afripod, google podcast, spotify, anchor fm n.k.
Jinsi Ya Kujenga Ujasiri Wa Kuzungumza Mbele Ya Watu. 23.08.2022 15:14
Ujuzi wa kungumza mbele ya watu ni muhimu sana kuwa nao pasipo kujali upo wapi na unafanya nini, Unajiuliza ni kwa namna gani si ndiyo eeh! Hebu jiulize hapo ulipo si umezungukwa na watu pia kitu unachofanya kinahusisha watu? Ikiwa jibu lako ni NDIYO! Basi hakikisha unasikiliza hii Podcast ili na ujuzi na ujasiri wa kuongea mbele ya watu.
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unaweza Kujenga Uwezo Wa Kujiamini Kwa Kushinda Hofu/Uoga. 15.08.2022 15:05
Unaweza Kujiamini kwa kiwango cha juu maishani ikiwa utasikiliza episode hii yenye dakika 15 za mabadiliko na kuweza kuwa mtu wa kujiamini, chukua hatua sasa.
Nguzo Sita (06) Za Ukweli Ambazo Zitabadili Maisha Yako..! 14.08.2022 11:30
Ukweli ambao watu wengi hawapendi kusikia, Sikiliza ukweli ambao utabadili mtazamo wako pamoja na maisha yako; Sikiliza kisha ufanyie kazi ambayo umejifunza kwenye episode hii Kisha utaweza kuona unapiga hatua kwenye maisha yako.
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unapaswa Kujipenda Pasipo Kujichukia. 27.06.2022 14:54
Je unajipenda kwa kiwango gani? Lakini tambua kujipenda ni wajibu wako was asilimia 100% tofauti na hivyo tambua hujipendi.
Mambo Manne (04) Ya Kufanya Unapo Pitia Hali Ya Kukataliwa Kwenye Maisha Yako. 18.05.2022 10:05
Moja ya changamoto iliyokatisha ndoto za watu wengi, ni ile ya kukataliwa ama kupingwa. Watu wengi wamekutana na hali hii, kuna ambao wameweza kuishinda, pia kuna ambao imekuwa kikwazo kwao. Jambo moja muhimu la kufahamu ni kwamba kukataliwa ni suala la kawaida, hata uwe bora kwa namna gani sio kila mtu atakubaliana wewe. Watu watakukataa kwa sababu zao wenyewe, wapo ambao watakukataa kwa sababu y...
Kanuni Tatu (03) Za Kuzingatia Ili Uwe Msomaji Mzuri Wa Vitabu 07.05.2022 8:24
Je unataka kufaidika na usomaji wa vitabu? Basi Sikiliza episode hii ujifunze mambo muhimu ambayo yatafanya uwe msomaji mzuri zaidi wa vitabu na kupata matokeo chanya kwenye kusoma vitabu. Hakikisha una subscribe Castbox na Apple Podcast na turn on notifications Ili uwe kwanza kusikiliza.
Mambo Manne (04) Ya Kufanya Ili Kurudisha Hamasa Iliyopotea...! 07.04.2022 12:01
Sikiliza episode hii ujue nini ufanye kurudisha hamasa iliyopotea na kuwa na morali ya kuendelea kupambania malengo, ndoto na maono yako.
Makosa Matano (05) Ambayo Unapaswa Kuepuka Ili Usipoteze Fedha Zako...! 26.03.2022 14:15
Je umekuwa unapoteza fedha zako kirahisi? Umekuwa unataka kufanikiwa kwenye eneo la fedha lakini huoni hatua yoyote unapiga. Kupitia episode hii utaweza kujua makosa gani ambayo unapaswa kuepuka ili ufanikiwe kwenye eneo la fedha. Sikiliza episode hii kisha fanyia kazi ambayo utajifunza baada ya muda kupita utanipa ushuhuda kuwa hii episode imekupa matokeo chanya kwenye eneo la fedha
Siri Tatu (03) Za Kuzingatia Ili Uwe Mwekaji Mzuri Wa Akiba Ya Fedha Zako. 19.03.2022 8:53
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha inategemea sana na maarifa ambayo unayo juu ya fedha kwa maana hiyo ukiwa unataka kupiga hatua zaidi basi unapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba ya fedha zako (Saving). Je unajua ufanye nini ili uweze kuweka akiba fedha zako? Basi Sikiliza episode hii upate kujua siri 3 ambazo zitakusaidia kujua namna gani uwe mwekaji mzuri wa akiba ya fedha zako
Sababu Saba (07) Za Kwanini Unapaswa Kujua Nguvu Ya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako. 10.03.2022 16:19
Je Unataka kubadili mfumo mzima wa maisha yako, mtazamo wako, aina ya marafiki, namna unavyofanya, mahusiano yako, biashara yako, Huduma yako n.k? Basi episode hii itakupa ufahamu wa nguvu wa mabadiliko kwenye maisha yako na kuweza kuchukua hatua Ili upate mabadiliko . Sikiliza mpaka mwisho upata kujua kwanini unaweza kupata mabadiliko kwenye eneo lolote ambalo upo
Mambo Matatu (03) Ambayo Hupaswi Kumshirikisha Kila Mtu Kwenye Maisha Yako 22.02.2022 8:37
Muda mwengine unashindwa kupiga hatua kwenye maisha yako Kwa sababu ya kushirikiana watu baadhi ya mambo ambayo hayapaswi kabisa kuwashirikisha lakini kwa kuchukulia poa imekuwa inagharimu sana watu wengi, hivyo unapaswa kuwa makini kujua mambo gani unapaswa kutoshirikisha kabisa watu na mambo gani ambayo unaweza kushirikisha watu kwa maana hiyo maisha ni kuwa na kiasi kujua nini ufanye na nini us...
Maswali Matano (05) Ambayo Yatakusaidia Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako. 15.02.2022 17:39
Je unataka kujua kwanini umezaliwa? Kabla ya kujua umezaliwa kufanya nini basi tambua kuwa wewe hujazaliwa kwa bahati mbaya, hujazaliwa kwa bahati nasibu, hujazaliwa kwa miujiza, hujazaliwa kwa kuwa wazazi wako walitaka mtoto. Lakini tambua kwamba wewe umezaliwa kwa kusudi hivyo haupo duniani kwa bahati mbaya. Ili maisha yako yawe yenye maana ni kujua kusudi la kuzaliwa kwako. Sikiliza Episode hii...
Onyo! Hata Usifikirie Kushinda Tabia Ya Kughairisha Malengo Yako Mpaka usikilize Hii... 06.02.2022 13:41
Sababu kuu tano (05) za kwanini unapaswa kushinda tabia ya kughairisha malengo yako kwenye maisha yako...! Sikiliza mpaka mwisho utajifunza mengi
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uboreshe Mahusiano Yako 30.01.2022 11:42
Je unajua jinsi ya kuboresha mahusiano yako yadumu kwa muda mrefu? Mahusiano ni zaidi ya kupendana kwa maana upendo hautoshi kufanya mahusiano yadumu, ni mahusiano mangapi yamevunjika japokuwa watu bado wanapendana? Ni kwa sababu ya kutojua namna gani wanaweza kuboresha mahusiano yako Basi Podcast hii Itakusaidia kujua namna gani unaweza kuboresha mahusiano yako na kuweza kudumu kwa muda mrefu. Su...
Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Yako. 22.01.2022 11:13
Je unataka kutimiza malengo yako kwa asilimia ngapi? Unajua kwamba kutimiza malengo yako inategemea sana namna ya kupanga malengo yako kwa bahati mbaya changamoto kubwa watu wengi hawajui namna gani wanapanga malengo vizuri na kwa ufanisi. Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga maalengo yako, Kutimiza malengo ipo ndani ya uwezo wako ni wewe kujua h...
Jinsi Ya Kubadili Mtazamo Hasi Na Kuwa Na Mtazamo Chanya. 15.01.2022 13:13
Mtazamo Chanya ndio kila kitu maishani, bahati mbaya mtazamo hasi ndio hutawala akili zaidi kutokana na sababu mbalimbali kama vile jinsi unavyojitazama, sehemu ambazo unashinda, aina ya marafiki ambao unao, maneno ambayo unajiambia, tabi zako n.k. lakini Podcast hii itakusaidia mbinu sita rahisi za kuwa na mtazamo chanya kwenye maisha yako. Sikiliza Podcast hii kisha Subscribe kwenye platform amb...
Gundua Maajabu Ya Kutumia Kioo Kubadili Maisha Yako. 09.01.2022 13:53
Je unajua kioo kinaweza kubadili maisha yako? Kioo ni zaidi ya kujitazama kwa maana kwamba Kioo kina faida na matumizi mengi zaidi unavyojitazama. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue maajabu ya kutumia kioo.
Jinsi Ya Kupanga Bajeti Ya Fedha Zako Kupitia Kanuni Ya 40/30/10/10/10. 02.01.2022 10:26
Hii ni kwa watu wanaotaka kujua Kupanga bajeti ya fedha zao kwa usahihi lakini hawajaanza bado, Sikiliza mpaka mwisho utaweza kupanga bajeti ya fedha zako na Kanuni ya 40/30/10/10/10 ambayo ni rahisi sana. Kazi kwako kusikiliza madini haya kisha fanyia kazi ili mwaka 2022 uwe mwaka wa kufanikiwa wewe kwenye eneo la fedha
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.