Innocent Ngaoh
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha. Ni podcast ya kipekee ambayo utajifunza mambo mengi ambayo yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku, kila kitu kinachozungumzwa hapa kina uhalisia na siyo nadharia ya kusadikika. Kuwa sehemu ya familia hii na uhakika hautakuwa kama ulivyokuwa mwanzo, podcast ambayo itaboresha na kuongeza thamani ya maisha yako mara 10X au zaidi. Hakikisha unafollow ili uwe wa kwanza kupata episode mpya kila wiki.
Author
Innocent Ngaoh
Category
Podcast website
Latest episode
Apr 18, 2026
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Jinsi Ya Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2022 Kwa Kishindo... 26.12.2021 15:25
Je unataka kutimiza malengo yako? Je unajua namna gani unaweza kutimiza malengo yako...? Usijali Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua ufanye nini Ili utimize malengo yako kwa kishindo mwaka 2022
Kanuni Mbili (02) Za Kupangilia Muda Wako Vizuri (Time Management.) 19.12.2021 11:19
Muda ndio rasimali ya pekee ambayo haina mbadala, masaa 24 ambayo unayo unapaswa kuyatumia vizuri kwa kufanya mambo ya Muhimu na kuacha kufanya mambo yasiyo na umuhimu na ambayo yanakupotezea Muda wako, Hivyo kutumia Muda wako vizuri ni lazima ujue Kupangilia Muda wako vizuri kwa maana hiyo podcast hii ni Maalumu kwa ajili ya kukusaidia wewe kuwa na matumizi mazuri ya muda wako. Sikiliza Podcast h...
Mambo Sita (06) Ambayo Unapaswa Kufanya Ili Upate Kibali Machoni Pa Watu. 12.12.2021 14:21
Nguvu ya Kibali imebeba Mafanikio yako na mtaji wa mtu ni watu, ili watu wewe mtaji wako ni lazima uwe na nguvu ya Kibali Ili uweze kukubalika zaidi; Sikiliza episode hii mpaka mwisho baada ya kusikiliza utagundua jinsi gani ulikuwa unakosea na kushindwa kupata Kibali kwa watu. Karibu sana kusiliza episode kwenye channel hii ya “Maisha Ni Kuthubutu”
Usikate Tamaa Kama Kweli Unataka Kupiga Hatua Kwenye Maisha Yako. 05.12.2021 10:41
Usikate tamaa sababu umezaliwa kufaniwa kwa maana hiyo Sikiliza episode hii mpaka mwisho itakupa nguvu ya kupambania malengo yako na ndoto zako pasipo kukata tamaa na kuweza kusonga mbele kwenye maisha yako
Makosa Matano (05) Ambayo Unafanya Na Kupelekea Kupoteza Fedha Zako. 28.11.2021 15:04
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha unahitaji sana kuwa na maarifa sahihi juu ya fedha, kupitia podcast hii kuwa na uhakika utaweza kusahihisha makosa haya ambayo hupelekea kupoteza fedha zako ikiwa tu utaweka utekelezaji kwenye maarifa haya kazi kupitia Podcast hii na kuweza kupiga hatua kwenye eneo la fedha
Mambo Sita (06) Ya Kufanya Ili Uwe Msomaji Mzuri Wa Vitabu 21.11.2021 14:17
Kusoma vitabu ni tabia, maarifa ni nguzo ya mafanikio kwenye maisha yako kama utafanyia kazi kwa maarifa ambayo unajifunza; maarifa mengi yapo kwenye vitabu kwa maana hiyo kupitia episode hii utaenda kuwa msomaji mzuri wa vitabu.
Lugha Tano (05) Za Upendo Kwenye Mahusiano (The 5 Language Of Love) 14.11.2021 12:28
Mahusiano yanajengwa na mawasiliano, bahati mbaya mahusiano mengi wana wasiliana kwa namna ambayo sio sahihi kwa sababu kila mtu mtu kwenye mahusiano ana lugha yake ya upendo ambayo akionyeshwa lugha hiyo anaona anapendwa, anathaminiwa na kujaliwa kwa maana hiyo ni vema sana kujua lugha ya upendo ya mpenzi wako, mchumba wako, mume wako au mke wake na uweze kuwasiliana nae kupitia lugha ya upendo a...
Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako. 06.11.2021 12:51
Utajiri mkubwa haupo kwenye machimbo ya almasi na dhahabu, utajiri mkubwa upo makaburini kwa maana hiyo usikubali kufa na kusudi ndani yako na nafasi pekee ya kuanza kuliishi na kutimiza kusudi lako ni sasa; kupitia episode hii utaweza kugundua kusudi la kuzaliwa kwako hapa duniani na unapaswa kufanya nini (Your Purpose). Sikiliza episode hii mpaka Mwisho pia usisahau ku-subscribe na kuandika comm...
Jinsi Ya Kujitofautisha Na Watu Wengine Bila Kupoteza Uhalisia Wako 25.10.2021 11:48
Wewe umezaliwa na upekee ndani yako na upekee wako ndio utambulisho wako kwa maana hiyo wewe ni wa kitofauti sana hivyo anza kuishi uhalisia wa maisha yako Ili uweze kujitofautisha na watu wengine kwenye maeneo tofauti tofauti ambayo upo kwa sababu ndani yako umebeba kusudi maalumu ambalo halifanani na mtu yeyote hapa duniani
Aina Tano (05) Za Nguvu Zinaleta Mafanikio Kwenye Maisha Yako... 14.10.2021 24:09
Je unajua umebeba nguvu na uwezo mkubwa ndani yako? Lakini kwa bahati mbaya unatumia sehemu ndogo ya uwezo wako na kupelekea kushindwa kufanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye malengo yako, maono yako, ndoto zako n.k kwa maana hiyo unahitaji sana kujenga nguvu hizi Ili uweze kupiga hatua kwenye maisha yako na kufanikiwa kwa sababu Unastahili kufanikiwa na Inawezekana. Usisiahau kuniandikia maoni yako...
Jitambue Wewe Ni Nani? 02.10.2021 17:43
Elimu ya kujitambua haifundishwi shuleni na vyuo vikuu na kupeleka watu wengi kujitambua kwa kiwango kidogo, ili uishi Maisha yenye furaha msingi wa kwanza ni kujitambua wewe ni nani kwa maana hiyo episode hii inakupa uwezo wa kujitambua kwa kiwango cha juu baada ya kusikiliza mpaka mwisho episode hii...! Usisahau ku subscribe kwenye Apple Podcast pia niandike maoni yako muhimu sana ✍🏾. Kauli Mbi...
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uweze Kutimiza Malengo Yako 22.09.2021 16:00
Hii ni kwa watu wanaotaka kutimiza malengo yao pasipo kujali umeanza au bado hujaanza, unaweza kutimiza malengo yako ukijua sifa za malengo sahihi na kujua siri muhimu za kutambua Ili uweze kutimiza malengo yako; kinachohitajika ni uteyari wako pamoja na uthubutu wa kufanyia kazi ambayo utajifunza kupitia episode hii. Usisahau ku subscribe na kuanndika comment yako umejifunza nini kupitia episode...
Sababu Tano (05) Za Kwanini Za Kwanini Unapaswa Kuepuka Majuto Kwenye Maisha Yako 15.09.2021 10:43
Je unajua kwamba majuto ni adui wa maisha yako? Ndio adui ni adui mkubwa sana furaha yako, mahusiano yako, malengo yako, ndoto zako n.k hivyo ukichelewa kuchukua hatua kuyaepuka majuto kwenye maisha yako tegemea kupata msongo mkubwa wa mawazo (stress) na kutopiga hatua sababu majuto mara zote hupoteza hamasa pamoja na kutokuwa mwenye ufanisi kwenye kitu unachofanya hivyo njia sahihi ya kuepuka na...
TABIA TANO (05) ZA KUEPUKA ILI UFANIKIWE KWENYE MAISHA YAKO 05.09.2021 15:28
Kiwango cha mafanikio yako inategemea sana na muenendo wa tabia zako za kila siku, tabia ina nafasi kubwa ya kufanya ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha yako hivyo unahitaji maarifa haya ambayo yatakusaidia kuepuka tabia zuizi ili ufanikiwe kutimiza malengo yako, ndoto zako pamoja na maono yako. Kumbuka unastahili kufanikiwa ndio maana umezaliwa......! Sikiliza mpaka mwisho podcast hii Usisahau...
Sifa Sita (06) Za Mtu Anayetaka Mafanikio. 07.08.2021 20:21
Kiwango cha mafanikio kinategemea sana kiwango chako cha kujitambua, unatamani kufanikiwa kwenye kitu unachofanya lakini hujui nini ufanye Ili ufanikiwe kwenye kitu unachofanya kwa maana kutimiza malengo yako, ndoto zako pamoja na maono yako; Lakini tafiti zimefanyika kuna sifa sita ambazo mtu akizijenga anavuta mafanikio kwenye maisha yake, kupitia podcast jiandaee kuwa mtu mwenye mafanikio makub...
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uongeze Uwezo Wa Kujiamini 31.07.2021 13:06
Hofu na uoga imekuwa kizuizi cha kushindwa kutimiza malengo yako pamoja na ndoto zako? Kupitia Podcast hii utakuwa mtu mwenye kujiamini kwa kujua nini ufanye ili uweze kushinda na Kutawala hofu na uoga kwenye maisha yako; kujiamini ni matokeo ya kushinda hofu na uoga ili upate matokeo makubwa hakikisha unafanyia kazi uliyojifunza kupitia Podcast hii na uanze kuwa mtu mwenye kujiamini inawezekana s...
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Kabla Ya Kutumia Fedha Yako 22.07.2021 20:04
Elimu ya fedha haifundishwi shuleni na vyuo vikuu na kupeleka watu wengi kupoteza fedha zao kirahisi kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi ya fedha; Leo nimekuandalia mambo matano ya kufanya kabla ya kutumia fedha au pesa yako Ili uweze kufanikiwa kwenye eneo la fedha kwa kupata maarifa sahihi ambayo shuleni wala vyuo vikuu hukufundishwa. Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
Mambo (07) Ya Kuzingatia Ili Uongeze Thamani Ya Maisha Yako Leo. 18.06.2021 15:13
Jifunze kupitia Lolo Facts Podcast kila wiki podcast za maisha na maendeleo binafsi
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.