United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Hifadhi ya Ngorongoro: Ambapo uhifadhi, utamaduni na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu 03.06.2026 9:01
Tukilekea Siku ya Mazingira Duniani hapo Juni 5, Leo tunakupeleka katika moyo wa Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamad...
03 JUNI 2026 03.06.2026 10:33
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na...
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “CHOTORA” 02.06.2026 0:50
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Mtalaam wetu Onni Sigalla kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA anafafanua maana ya neno “CHOTORA”
02 JUNI 2026 02.06.2026 10:47
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu. Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapem...
01 JUNI 2026 01.06.2026 9:34
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo hii leo tutaelekea jijini Kampala nhcini Uganda kuangazia uzunduzi wa awamu ya tatu ya safari ya hija ya “Twende Zetu Butiama”, kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kmabarage Nyerere, rais wa zamani wa Tanzania aliyedumisha amani, msikamano na kupigania maendeleo ambazo ni ajenda zinazopewa kiaumbele cha juu na Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu kati...
29 MEI 2026 29.05.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo tunamwangazia mmoja wa maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya. Mwisho wa wiki hii, Joyce, raia wa Tanzania ambaye pia amewahi kuhudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNEP na pia Benki ya Dunia anahitimisha utumishi wake katika Umoja wa Mataifa akiwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya...
28 MEI 2026 28.05.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Taifa la Tanzania na Balozi Togolani Idriss Mavura mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na Flora Nducha kuhusu suala hili muhimu.“Nataka niwe mkweli; hii ni moja ya changamoto zetu kubwa zaidi. Hatu...
Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE." 22.05.2026 0:42
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."
22 MEI 2026 22.05.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililo...
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.” 21.05.2026 1:06
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”
21 MEI 2026 21.05.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi. Hadi sasa Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewa...
20 MEI 2026 20.05.2026 9:58
Hii leo kwenye Jarida la Habari tuna Muhtasari na Mada kwa Kina. MUHTASARIOngezeko la idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRCUmuhimu wa kushirikisha jamii kwenye udhibiti wa Ebola Mpango wa Tanzania wa kukabiliana na makazi duniMADA KWA KINAInaangazia uchambuzi wa ripoti ya uanishaji wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania ambapo tumezungumza na Afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Cha...
19 MEI 2026 19.05.2026 10:29
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waa...
18 MEI 2026 18.05.2026 11:11
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mlipuko wa Ebola nchini DRC na Uganda na ujumbe wa Profesa Mohamed Yakub Janabi Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika kuhusu hatua WHO inachukua kudhibiti ugonjwa huo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo..Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa 79 wa...
15 MEI 2026 15.05.2026 10:40
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa s...
14 MEI 2026 14.05.2026 12:13
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme ili...
Katibu Mkuu Antonio Guterres aaga Muungano wa Afrika na kutoa tathmni ya ushirikiano wa UN-AU 13.05.2026 2:33
Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.. Assumpta Massoi anafafanua...
13 MEI 2026 13.05.2026 9:59
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar. Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa...
UNDPTanzania yajengea uwezo wasaidizi wa kisheria 126 kisiwani Pemba, ili kutatua migogoro kwa njia mbadala 13.05.2026 2:48
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. Rashid Malekela na taarifa zaidi.
AfroKids International ni tumaini kwa wanawake wakimbizi barani Ulaya - Farina 13.05.2026 3:19
Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nduch...
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “Payapaya.’’ 12.05.2026 1:02
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya.’’
12 MEI 2026 12.05.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Côte d'Ivoire ambako wakulima wameshuhudia kuimarika taratibu kwa uzalishaji wa kakao baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kusaidia wakulima nchini humo kurejesha ardhi katika ubora wake na kuongeza uzalishaji kupitia mbinu endelevu za kilimo mseto cha misitu, mazao na mifugo..Afrika imekuwa mstari wa mb...
Akili Mnemba au AI haiwezi kuchukua nafasi ya kuwa mama 11.05.2026 3:03
Je Akili mnemba AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilit...
Siku ya Kinamama: Mama ni nguzo ya jamii na msingi wa haki za watoto 11.05.2026 2:42
Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa na Redio washirika wetu Domus.
11 MEI 2026 11.05.2026 11:21
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres nchini Kenya, Akili Mnemba katika nafas iza ajira, na nafasi ya mama katika jamii ikiturejesha nchini Kenya kusikiliza simulizi za wamama. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika mak...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.