United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ 100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Author

United Nations

Category

News

Podcast website

news.un.org

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

UN yawekeza dola milioni 340 Nairobi kuimarisha kitovu chake barani Afrika 11.05.2026

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika. Stella Vuzo kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairob...

08 MEI 2026 08.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bad...

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKUNGUNI." 07.05.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI."

07 MEI 2026 07.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki. Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Ha...

Miaka 25 ya Jukwaa la Watu wa Asili Tanzania imepiga hatua kutujumuisha - Ole Kulet Mwarabu 07.05.2026

Haki ya afya kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni haki ya kila mtu bila kujali uko kwenye kundi au jamii gani. Huo ulikuwa ni msisitizo mwaka huu kwenye Jukwaa la jamii za watu wa asili lililokuja jamvi wiki iliyopita hapa New York Marekani. Na kandoni mwa kikao hicho Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Ada...

Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo 06.05.2026

Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo ja...

Abiria mwingine amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa virusi vya Hanta 06.05.2026

Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.  Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

06 MEI 2026 06.05.2026

Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili. Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu walio...

UNICEF Tanzania yaongoza kampeni kukomesha adhabu ya viboko shuleni 06.05.2026

Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadauwa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema." 05.05.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."

05 MEI 2026 05.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus ka...

Kenya tunashirikiana na mataifa jirani kutokomeza ukeketaji_ Hanna Wendot Cheptumo 04.05.2026

Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekan...

WHO Afrika yawatoa hofu wananchi kuhusu Hantavirus 04.05.2026

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika limesemalinafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka kufikia sasa watu watatu wamepoteza maisha. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

04 MEI 2026 04.05.2026

Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio l...

Janga la njaa na mateso vinazidi kutuangamiza, raia nchini Somalia wamweleza Fletcher 04.05.2026

Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi...

30 APRILI 2026 30.04.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili...

Rwanda ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kukabiliana na homa ya ini 29.04.2026

Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C yanaanza kuonesha mafanikio, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, iliyotolewa Aprili 28, 2026. Ripoti hiyo, imezinduliwa wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Homa ya Ini mjini Bangkok, Thailand, mkutano ulioingia leo siku ya pili na unakunya jamvi kesho. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Nimesahau yaliyopita na naganga yajayo baada ya kuuawa kwa baba yangu - Rwibutso 29.04.2026

Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliu...

29 APRILI 2026 29.04.2026

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 unaokunja jamvi leeo, Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C, na maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda. Mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 “World Health Summit 2026” umehitimishwa leo mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja zaidi ya wajumbe el...

Mkutano wa WHO kuhusu mifumo ya afya katika kanda ya Afrika umekunja jamvi Nairobi Kenya 29.04.2026

Mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 “World Health Summit 2026” umehitimishwa leo mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja zaidi ya wajumbe elfu moja kutoka takribani nchi 50 kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na duniani. Anold Kayanda na taarifa zaidi

Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku, Mhandisi NASA 28.04.2026

Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mw...

28 Aprili 2026 28.04.2026
Kenya: Mradi wa majaribio walenga kudhibiti plastiki na kemikali kwenye kilimo 27.04.2026

FAO nchini Kenya inasema mradi huo wa miaka mitano uitwao FARM, unalenga kuimarisha uwekezaji katika mbinu mbadala na usimamizi endelevu wa kemikali hatari na plastiki kwenye sekta ya kilimo barani Afrika na Amerika ya Kusini. Tweet URLUkifadhiliwa na Fuko la Mazingira Duniani, GEF, mradi unafanya kazi na vikundi vya wataalamu wa kitaifa kutoka taasisi mbalimbali, kuangazia vipaumbe...

Balozi Ngoga: Manusura wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Rwanda baada ya mauaji ya kimbari 27.04.2026

Tweet URLSuala hilo la mchango wa manusura katika kuepusha mauaji kama hayo hayajirudii tena, nililimulika wakati wa mazungumzo yangu ya hivi karibuni na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga ambaye bila kumung’unya maneno alinieleza kuwa, “ wanamchango mkubwa sana kwa sababu kwanza wanapambana na hali ambayo katika hali ya kawaida ya ubinadamu ni ngumu. C...

Kila saa moja zaidi ya wanawake na wasichana 100 wanafurushwa nchini Sudan Kusini 27.04.2026

Zaidi ya wanawake na wasichana 100 wanakimbia makazi yao kila saa nchini Sudan Kusini huku kuongezeka kwa mapigano na njaa kukichochea kuongezeka kwa janga la kibinadamu, Anna Mutavati, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women) ameeleza leo baada ya ziara ya siku tano nchini humo. Kupitia taarifa ya UN Women iliyos...

Listen to the Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.