United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ 100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Author

United Nations

Category

News

Podcast website

news.un.org

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

19 JUNI 2026 19.06.2026

Hii leo jaridani tunaangazia wito wa UN wa kulinda mamilioni wa wakimbizi kote duniani, masuala ya kijinsia Zanzibar nchini Tanzania, na ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani. Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi kesho Juni 20, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na hatua za...

UN yataka dhamira mpya wakati takriban wakimbizi milioni 42 duniani wakiendelea kuhitaji ulinzi 19.06.2026

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi kesho Juni 20, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na hatua za kimataifa za kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao kote duniani kutokana na vita, vurugu na mateso. Anold Kayanda amefuatilia na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Mauaji na majeraha ya watoto yafikia kiwango cha kutisha duniani - UN 19.06.2026

Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani. Takribani watoto 24,174 waliuawa, kujeruhiwa, kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha, kubakwa au kuathiriwa kwa namna nyingine na ukiukwaji mkubwa wa haki katika maeneo yenye mizozo mwaka 2025. Leah Mushi amemsikiliza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa...

UN Women na EU waleta matumaini kwa wanawake waathirika wa ukatili viziwani Zanzibar 19.06.2026

Je, maisha yangekuwaje kama kila manusura wa ukatili wa kijinsia angejua mahali pa kupata msaada kwa wakati? Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linaimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, h...

18 JUNI 2026 18.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Katika mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliomalizika wiki iliyopita baadhi ya wahudhuriaji walikuja na wakalimani wao, kutoka Tanzania Mbunge Nassriya Nassir Ali mwenye ulemavu wa kusikia au Kiziwi aliambatana na mkalimani wake Tusajigwe Ernest. Baada ya mkutano huo Leah Mushi aliketi na Tusajigwe na hapa anaa...

Vijana wanahitaji ajira, stadi na matumaini bila hivyo, ni rahisi kutumbukia kwenye uhalifu - Monica Juma 17.06.2026

Wakati dunia ikikabiliwa na ongezeko la uhalifu wa kupangwa, biashara haramu ya binadamu na matumizi ya dawa za kulevya, mwanamke kutoka Afrika Mashariki amepewa jukumu kubwa la kusaidia kuongoza mapambano ya kimataifa dhidi ya changamoto hizo. Monica Juma, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), anavunja rek...

Watoto 9 waliotumikishwa kijeshi na waasi waachiwa na kuanza maisha mapya nchini Sudan Kusini 17.06.2026

Watoto tisa waliokuwa wakihusishwa na vikosi vya ulinzi katika Jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wameanza safari mpya ya maisha baada ya kutambuliwa, kuachiliwa na kukabidhiwa kwa ajili ya kurejeshwa katika familia na jamii zao.

Mashirika ya UN FAO na WFP waonya kuongezeka kwa njaa kali kwenye maeneo 13 duniani 17.06.2026

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na Mpango wa Chakula Duniani, WFP, yametoa onyo kali kuwa hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kwa mamilioni ya watu katika nchi 13 zilizotajwa kuwa maeneo hatari ya njaa kati ya mwezi Juni na Novemba mwaka huu wa 2026. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo.

17 JUNI 2026 17.06.2026

Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula barani Afrika, utumikishaji wa watoto jeshini Sudan Kusini, na ujumbe wa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia nchini Zimbabwe. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na Mpango wa Chakula Duniani, WFP, yametoa onyo kali kuwa hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula in...

Hata kama ulipata mimba ukiwa na umri wa miaka 14 huo sio mwisho wa maisha yako - Mary Chigumira 17.06.2026

Leo tunakupeleka Zimbabwe kwa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia ya “Unlimited Hope Alliance”. Kandoni mwa moja ya mikutano ya Zama Zijazo ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani alipata fursa ya kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akipaza sauti kwa viongozi wa dunia kuhakikisha wanawake na wasichana wa vijijini hawapewi kisogo katika ajenda za m...

16 JUNI 2026 16.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa Makao Makuu ya UN kusikia mahojiano maalum na ya kina baina ya Flora Nducha wa Idhaa hii na Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC. Pia tunakuletea Muhtasari wa habari. Kumekuwepo na imani kwamba ugonjwa wa Ebola si halisi, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,...

15 JUNI 2026 15.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia ziara ya kihistoria ya Rais wa Baraza Kuu la UN, Annalena Baerbock, kwenye kituo cha kukusanya, kuchakata  na kurejeleza taka cha Korogocho (Korogocho Material Recovery Facility - MRF) kujionea namna vijana wanavyogeuza taka kuwa fursa ya kiuchumi na silaha ya kutokomeza umasikini na uhalifu mitaani. Ku...

12 JUNI 2026 12.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Lililo lujani ni la lusu” 11.06.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lililo lujani ni la lusu”.

11 JUNI 2026 11.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umetamatishwa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Idhaa hii imepata fursa ya kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mkutano huu muhimu, Mtanzania Zuleikha Tambwe. Pia tunakuletea jifunze Kiswahili na muhtasari wa habari kama zifuata...

10 JUNI 2026 10.06.2026

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina maalum ambayo kama nilivyokujuza hapo awali inaangazia mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa chini ya kauli mbiu “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.”Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na ma...

Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "MKWARUZO." 09.06.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."

09 JUNI 2026 09.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho kutwa Alhamisi ya Juni 11, macho na masikio yanaelekezwa Mexico, Canada na hapa Marekani kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu, au soka al maarufu kabumbu. Ingawa hivyo zama za sasa za mchezo huo maarufu zaidi duniani zinakumbwa na madhara ya  athari za mabadiliko ya tabianchi. Ongezeko la joto kali linavuruga mec...

Kevin Wekesa ambaye ni nyota wa raga anaongoza uchechemuzi wa mazingira kupitia michezo 08.06.2026

Nyota wa mchezo wa raga ama rugby, Kevin Wekesa kutoka nchini Kenya ambaye alishiriki Michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa mwaka 2024, ameeleza nia yake ya kufanya vizuri uwanjani huku akitumia umaarufu wake kuhifadhi mazingira na kuhamasisha hatua endelevu kupitia michezo ili kujenga dunia yenye mnepo. Rashid Wekesa na taarifa zaidi.

08 JUNI 2026 08.06.2026

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya baharí duniani na kumulika ni hatua gani Zanziba zinachukua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia tunakwenda nchini Kenya kufuatilia simulizi ya mchezaji wa raga. Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na ku...

Mradi wa UNEP na wadau wake Zanzibar waimarisha uhifadhi wa bahari kupitia upandaji wa mikoko na ufugaji bora wa nyuki 08.06.2026

Jamii katika mkoa wa Kaskazini Unguja huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaadhimisha siku ya bahari hii leo Umoja wa Mataifa ukielezea dhahiri mafanikio ya mradi wa uhifadhi wa mikoko na ufugaji wa nyuki unaochagiza sio tu upatikanaji endelevu wa kipato bali pia uhifadhi wa mazingira na bahari. Assumpta Massoi na maelezo zaidi ya mradi huo.

Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 08.06.2026

Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutoa wito wa hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na hali hiyo. Akizungumza kwa njia ya video katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya Bahari inayoadhimishwa kila mwaka Juni 8, Bwana Guterres amesema bahari ni msingi wa maish...

05 JUNI 2026 05.06.2026

Jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo dunia inaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani huku maadhimisho ya kimataifa yakifanyika jijini Baku nchini Azerbaijan. Maudhui ya mwaka huu ni "Sasa kwa ajili ya Tabianchi", yakiweka msisitizo mkubwa wa kuchukua hatua dhidi ya za uhifadhi wa mifumo ya ikolojia na hatua za kukabili tabianchi. Hivi karibuni, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria pamoja na wad...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu” 04.06.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”

04 JUNI 2026 04.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni  kuboresha zao hilo na kuin...

Listen to the Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.