United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
10 JULAI 2026 10.07.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya m...
Ushirikiano kati ya wahudumu wa afya na wanajamii unavyosaidia kupambana na Ebola DR Congo 09.07.2026 3:05
Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza. Anold Kayanda na ma...
09 JULAI 2026 09.07.2026 9:59
Hii leo jaridani tunaangazia washindi wa Tuzo ya UNFPA, harakati za kutokomeza Ebola nchini DRC, na watoto wenye ulemavu nchini Kenya. Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na k...
Kila mtu anazaliwa na kipaji chake tusiwatenge wenye ulemavu – Jofreshia Family and Community Services 09.07.2026 3:10
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu...
Mshindi wa tuzo ya UNFPA aelezea linalopaswa kufanyika kutokomeza fistula ya uzazi ifikapo 2030 09.07.2026 2:25
Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "KICHAKATA MATINI". 08.07.2026 0:49
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".
08 JULAI 2026 08.07.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho, Julai 9, ni miaka 15 tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake kutoka Sudan. Hata hivyo, matumaini ya amani yalitikiswa miaka miwili baadaye, mwezi Desemba 2013, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya serikali na makundi pinzani, hali iliyoendelea kuwaathiri mamilioni ya wananchi hadi leo. Katika juhudi za kurejesha amani, Ujumbe wa Umoja wa Mat...
07 JULAI 2026 07.07.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili nampisha John Kibego wa redio washirika, Kazi Njema Redio nchini Uganda, kukueleza kuhusu harakati za kukuza lugha hiyo barani Afrika wakati huu ambapo UNESCO imeshaitangaza miaka mitano iliyopita kuwa lugha ya kimataifa. John, anamulika mpango wa ujenzi wa makao makuu ya kamisheni ya Kiswha...
06 JULAI 2026 06.07.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendelo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo limeendesha midahalo ya amani na utatuzi wa migogoro kwa vijana, lengo, ni kuimarisha amani kwa Maendeleo Endelevu. Siku nne tu baada ya shambulio kubwa la Urusi dhidi ya Ukrai...
02 JULAI 2026 02.07.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tunaangazia fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo au kwa lugha ya kiingereza Internship hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Rashid Malekela kutoka Mwanza Tanzania, ambaye aliomba na kupata fursa hiyo anazungumzia na Leah Mushi wa Idhaa hii kueleza ni nini faida yake. Mashirika ya misaada nchini Ukraine leo Alhamisi Julai 2 yameongeza juhudi za kutoa...
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKUNGURU." 01.07.2026 0:33
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGURU."
01 JULAI 2026 01.07.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Ikiwa ni siku chache baada ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wasioona na viziwi inayoadhimishwa tarehe 27 Juni kila mwaka, Rashid Malekela wa Idhaa hii anakupeleka Mashariki ya Kati akimmulika mkazi mwenye ulemavu ambaye anakumbwa na changamoto katikati ya vita. Wakati harakati za uokozi na usaidizi zikiendelea nchini Venezuela baada ya matetem...
30 JUNI 2026 30.06.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia sekta ya ufugaji wa samaki na viumbe vingine na mimea baharini na kwenye maziwa, sekta ambayo inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa duniani, huku uzalishaji wa samaki ukifikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa. Shughuli za uokoaji zinaendelea nchini Venezuela kufuatia athari za matetemeko makubwa ya ardhi yaliyoua maelfu ya watu na kuwaac...
29 JUNI 2026 29.06.2026 9:40
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka mjini Caracas nchini Venezuela, mshikamano na raia wa nchi hiyo wadhihirika wakati huu wakiwa kwenye majonzi baada ya matetemeko ya ardhi kukumba wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo. Nchini Venezuela Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa msaada kufuatia matetemeko mawili ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo wi...
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Lengelenge lako si jipu langu.” 26.06.2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, tunasalia huko huko Nairobi Kenya kwani leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lengelenge lako si jipu langu”.
26 JUNI 2026 26.06.2026 11:02
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka jijini Nairobi nchini Kenya ambako kunafanyika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, IGF, mahususi kwa bara la Afrika pekee, AfIGF. Stella Vuzo, Afisa Habari wa UNIS Nairobi, Kenya amezungumza na mmoja wa vijana washiriki na kukuletea maoni yake. Idadi ya waliokufa kwenye matetemeko mawili makubwa ya ardhi yal...
Tunataka wasichana nchini DRC wasahau machungu ya vita na kuanza maisha mapya: Lydie Mwenge 25.06.2026 7:38
Katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako miongo ya vita imeacha maelfu ya watoto bila familia, elimu au usalama, Lydie Mbusa Mwenge ameweka maisha yake katika mstari wa mbele wa kupigania haki za wasichana walioathiriwa na vita. Mwenge ni mwanzilishi na mratibu wa shirika la Action Intervention des Femmes Entrepreneurs pour le Développement, linalojikita kati...
25 JUNI 2026 25.06.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa kingono. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea na harakati za kutoa msaada wa dharura kwa Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yali...
Papa Leo XIV: Juhudi na mshikamano wa kimataifa ni kiini cha kutokomeza njaa 24.06.2026 2:34
Katika kipindi ambacho idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kiuchumi, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa Kumi na Nne (Leo XIV), ametuma ujumbe wa mshikamano kwa kutembelea makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, mjini Roma nchini Italia wiki hii. Ziara hiy...
UN yathibitsha zaidi ya matukio 500 ya ukatili wa kijinsia nchini Sudan 24.06.2026 2:24
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imetoa ripoti kuhusu ongezeko kubwa la ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo nchini Sudan tangu mapigano yalipoanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Ofisi hiyo imekumbusha jumuiya ya kimataifa umuhimu wa kuhakikisha haki na uwajibikaji vinapewa kipaumbele wakati juhudi za kusitisha mapigano na kutafuta suluhu ya mzozo huo zikiendelea. Tupate...
24 JUNI 2026 24.06.2026 9:55
Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa mabaharia katika Mlango Bahari wa Hormuz, ongezeko kubwa la ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo nchini Sudan, na ujumbe wa Papa Leo wa Kumi na Nne (Leo XIV), kuhusu ongezeko la njaa duniani. Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) limetangaza mpango wa kuwaondoa zaidi ya mabaharia 11,000 waliokwama katika Mlango Bahari wa Hormuz kufuatia...
IMO yatangaza mpango wa kuwaondoa mabaharia waliokwama Hormuz 24.06.2026 3:08
Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) limetangaza mpango wa kuwaondoa zaidi ya mabaharia 11,000 waliokwama katika Mlango Bahari wa Hormuz kufuatia makubaliano ya amani kati ya Iran na Marekani yaliyolenga kurejesha usalama wa usafiri wa baharini katika eneo hilo. Anold Kayanda amefuatilia hatua hiyo. Karibu Anold utufahamishe zaidi.
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "TANUWINI" 23.06.2026 0:59
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "TANUWINI"
23 JUNI 2026 23.06.2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Leah Mushi ameketi chini na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nassriya Nassir Ali akieleza safari yake ya uongozi wa nafasi za umma kupitia mkalimani wake wa lugha ya alama Tusajigwa Ernest. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari na jifunze Kiswahili. Janga la tabianchi linakaribia k...
22 JUNI 2026 22.06.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hivi karibuni Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI, UNAIDS kupitia ripoti yake mpya limeonya kuwa kupungua kwa ufadhili wa kimataifa na uwekezaji mdogo katika huduma za kinga dhidi ya Virusi vya UKIMWI, VVU kunaweza kufuta mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI duniani. Katika hatua za mwitikio wa kitaifa, wiki iliyopita,...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.