RFI Kiswahili
Habari RFI-Ki
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
DRC: Muungano wa upinzani wa C64 kutangaza kuendelea na maandamano yake ya amani Julai 22 09.07.2026 10:02
Tangazo hilo limetolewa licha ya kushiriki kwenye mazungumzo ya kisiasa na rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Siku ya Kiswahili duniani Juni 07 2026 07.07.2026 9:58
Dunia hivi leo inaadhimisha siku ya Kiswahili Duniani, kutambua mchango wa lugha ya Kiswahili katika kuunganisha watu, tamaduni na mataifa mbalimbali, kauli mbiu ikiwa Kiswahili Lugha ya kimataifa ya amani, mshikamano na diplomasia ya kiuchumi.” Siku hii inafanyika wakati pia RFI Kiswahili tunatimiza miaka 16 tangu tulipoanza kurusha matangazo yetu, una ujumbe gani kwetu?
Je, serikali ya Afrika Kusini ilichukua hatua za kutosha kulinda usalama wa raia wa kigeni? 06.07.2026 9:58
Wiki iliyopita, maelfu ya raia wa mataifa mbalimbali ya Afrika waliondoka Afrika Kusini kutokana na hofu ya usalama baada ya maandamano yaliyolenga wageni. Baadhi ya nchi zimeikosoa serikali ya Afrika Kusini kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Uganda : Yamfurusha wakili na mwanaharakati Martha Karua 01.07.2026 9:45
Tunaangazia serikali ya Uganda kumfurusha wakili na mwanaharakati wa Kenya, Martha Karua nchini humo, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ambayo yamekuwa yakishuhudiwa hapa Afrika Mashariki. Skiza maoni ya waskilizaji.
Kila Ijumaa unapata nafasi kutoa maoni ndani ya rfi Kiswahili 26.06.2026 9:47
Kila Ijumaa unapata nafasi kuchangia chochote kile, pengine ulikiskia kwenye matangazo yetu au kile kinafanyika hapo uliopo. Skiza maoni ya mskilizaji
Kenya : Miaka miwili baada ya maandamano ya Gen Z 25.06.2026 9:56
Shaba yetu leo inalenga nchini Kenya mbapo raia nchini humo wameadimisha miaka miwili tangu kutokea kwa maandamano ya mwaka 2024 ya vijana waliokuwa wapigigania mageuzi nchini humo. Skiza maoni ya mskilizaji.
Waziri wa Uingereza kuondoka afisini Septemba 23.06.2026 9:47
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer ametangaza kujiuzulu baada ya shinikizo kutoka ndani ya chama chake na kupungua kwa uungwaji mkono wa raia. Je, viongozi wanapaswa kujiuzulu wanapopoteza uungwaji mkono wa wananchi? Skiza makala ya maoni ya waskilizaji.
Msongo wa mawazo changamoto kwa wanaume 22.06.2026 9:54
Ulimwengu umeadhimisha wiki ya afya ya akili kwa wanaume, wataalamu wanaonya kuwa msongo wa mawazo na matumizi ya dawa za kulevya vinachangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wanaume. Unafikiri kwa nini wanaume wengi huumia kimya bila kutafuta msaada? Skiza maoni ya mskilizaji.
Marekani na Iran zimekubaliana kufikia makubaliano ya kukomesha vita 16.06.2026 9:48
Rais Donald Trump anasema Mlango Bahari wa Hormuz pia utafunguliwa tena hivi karibuni. Mkataba wa amani, unatarajiwa kutiwa saini siku ya Ijumaa, wiki hii nchini Uswizi
Siku ya kimataifa ya watu wanaoishi na Albinism au Ualbino, kuhamasisha haki, usalama na ustawi wao 15.06.2026 10:06
Licha ya jitihada mbalimbali, bado watu wenye ualbino wanabaguliwa kwenye baadhi ya jamii na hata kuuawa kwa imani za kishirikina.
Kipute cha kombe la dunia kinaanza rasmi 11.06.2026 9:54
Kipute cha kombe la dunia kinaanza leo, huku Afrika Kusini ikipambana dhidi ya Mexico mwenyeji. Je, unazungumziaje timu za Afrika zinazoshiriki mashindano ya huu? Skiza makala haya.
Marekani : Yamzuia refa wa Somalia kuingia nchini humo 10.06.2026 9:42
Mwamuzi kutoka nchini Somalia Omar Abdulkadir, amezuiwa kuingia nchini Marekani, alikokuwa ameteuliwa na Shirikisho la soka duniani, FIFA kuchezesha mechi za kombe la dunia, kutokana na kile utawala wa rais Trump umemhusisha na maswala ya ugaidi Skiza makala haya kufahamu maoni ya mskilizaji wetu.
Kenya : Mahakama kuu yaidhinisha uamuzi wa Rigathi kuondolewa afisini 09.06.2026 9:49
Jopo la majaji watatu nchini Kenya limeidhinisha hatua ya bunge la kumuondoa afisini aliyekuwa naibu rais, Rigathi Gachagua kwa kile walichosema, katiba ilifuatwa. Je, unaunga mkono uamuzi wa mahakama kuhusu Rigathi Gachagua na kwa nini? Skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji wetu.
Uchafuzi wa mazingira baharini ni kikwazo 08.06.2026 9:57
Leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Bahari, siku inayolenga kuhamasisha umuhimu wa bahari katika maisha ya binadamu na mazingira. Hata hivyo, bahari zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo uchafuzi wa plastiki, mabadiliko ya tabianchi na uvuvi haramu, katika siku hii tunakuuliza. Unadhani hatua gani zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza uchafuzi wa bahari? Skiza makala haya kufahamu mao...
Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yana umuhimu gani nchini mwako 04.06.2026 10:04
Karibu kwenye kipindi cha habari Rafiki ,mada ikiwa kuhusu maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo yatafanyika Ijumaa,huku kauli mbiu ikiwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Tumekuuliza, serikali ya nchi yako inafanya vya kutosha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ? Na je , sekta binafsi na wananchi wanapaswa kufanya nini sasa,ili kuimarisha mazingira,,karibu tua...
Mada huru kila Ijumaa ndani ya rfi Kiswahili 22.05.2026 10:05
Kila Ijumaa ndani rfi Kiswahili unapata nafasi kuchangia mada yoyote. skiza makala
Kenya : msimamo wa kisiasa yazua balaa 22.05.2026 9:30
Nchini Kenya, msimamo ya kisiasa ya baadhi ya raia kisiasa yazidi kuibua uhasama. Skiza makala
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.