SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 1027 epizód

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: www.sbs.com.au

Szerző

SBS

Kategória

News

A podcast weboldala

www.sbs.com.au

Legutóbbi epizód

2026. okt. 9.

Hol hallgathatod?

Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio Hamarosan

A podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz

Letöltés a Google Play-ről Telepítsd ingyen Android közel 10 M letöltés · 4,8-as értékelés iOS hamarosan

Epizódok

Makala Leo: Jacinta Allan akataa kujiuzulu, pambano la uongozi wa chama cha Labor cha Victoria likiongezeka kasi 28.07.2026

Kiongozi wa Jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema atapambana na changamoto ya uongozi inayokuja baada ya viongozi wa mirengo tafuati ndani ya chama cha Labor, kukutana na kukubaliana kwamba amepoteza uungwaji mkono wa wengi katika mkutano wao.

Taarifa ya Habari: Kiongozi wa Victoria asisitiza hajiuzulu! 27.07.2026

Kiongozi wa jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema hatajiuzulu kutoka wadhifa wake, miezi minne kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Yaliyojiri Afrika:Kenya yapokea tani 4.5 zavifaa vya matibabu vya Ebola kutoka India 24.07.2026

Kenya imepokea shehena ya kwanza ya tani 4.5 za vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali ya India, ili kuimarisha uwezo wa nchi kujiandaa kukabiliana na uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Taarifa ya Habari: Hatua ya Marekani kuongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia yazua ukosoaji 24.07.2026

Utawala wa Trump umeongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia kutoka asilimia 10 hadi 12.5, huku kiwango kipya kikianza kutumika alasiri ya leo Ijumaa.

Makala Leo:Nini cha kutarajia kutoka kwa mfumo mpya wa tahadhari ya dharura wa Australia 24.07.2026

Australia inajiandaa kuanzisha mfumo mpya wa kitaifa wa tahadhari ya dharura, ulioundwa kutoa tahadhari muhimu haraka na kwa uhakika zaidi wakati wa majanga.

Makala Leo:China yaambia Australia iache kuzungumzia Bahari ya Kusini mwa China wakati mvutano ukiongezeka katika Mkutano wa ASEAN 24.07.2026

Mkutano wa Kikanda wa ASEAN unakamilika mjini Manila, ambapo Australia imeibua wasiwasi kuhusu hatua za kijeshi za China katika eneo hilo.

Taarifa ya Habari:Waziri Mkuu ataka chama cha Labor, kijitolee kupunguza shinikizo za gharama ya maisha 23.07.2026

Waziri Mkuu Anthony Albanese, amesisitiza kujitolea kwa chama chake kupunguza shinikizo la gharama la maisha katika mkutano wa kitaifa wa chama tawala.

Yaliyojiri Afrika:Kituo chakujitenga cha Ebola nchini Kenya cha wapokea wamarekani 7 kutoka DRC 23.07.2026

Wahudumu7 wamisaada kutoka wamarekani walikuowa wakisaida kupambana na Ebola DRC, wamewekwa katika kituo cha karantini nchini Kenya.

SBS Learn Eng Ep 115 Jinsi yakuzungumza kuhusu kufanya kazi ya ziada 21.07.2026

Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kufanya kazi ya ziada?

Taarifa ya Habari:Waziri Wong aelekea katika kongamano lamawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN kuimarisha uhusiano wa Australia na nchi wanachama 21.07.2026

Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anatarajiwa kwenda Ufilipino kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asia Mashariki na Jukwaa la Kikanda la ASEAN. Tume ya Dhamana na Uwekezaji ya Australia inasema imepata rekodi ya dola milioni 830 katika amri za adhabu za kiraia wakati wa Mwaka wa Fedha wa 2025-2026. Tume hiyo ilianzisha chunguzi zaidi ya 250, ambazo zilisababisha hatia 25 za jinai na...

Australia Yafafanuliwa:Kijana wangu anaweza anza kufanya kazi lini nchini Australia? 21.07.2026

Kuanza kazi ya muda mfupi kunaweza kuwa uzoefu wenye maana kwa kijana, kuongeza kujithamini kwake, kumsaidia kujifunza ujuzi mpya na kupata pesa zake za kwanza.

Makala Leo:Mazoezi muhimu yakimataifa yajeshi yaanza katika Wilaya ya Kaskazini 21.07.2026

Zoezi kubwa zaidi la kimataifa la Jeshi la Anga la Australia, linaendelea katika Eneo la Kaskazini na litafanyika kwa wiki tatu zijazo.

Taarifa ya Habari:Greens wataka makampuni ya mawasiliano nchini kutoa huduma yakuaminika kwa wateja 20.07.2026

Chama cha Greens kinatoa wito wa mageuzi ambayo kisheria yatahitaji kampuni zama wasiliano kama Telstra, Optus na Vodafone kutoa huduma ya kuaminika kwa wateja.

Makala Leo: Mitandao ya teknolojia yaambiwa irekebishe pengo za ulaghai wakujamiana 17.07.2026

Kamishna wa Usalama Mtandaoni wa Australia anatoa tahadhari kuhusu ulaghai wa kingono mtandaoni, baada ya kupokea malalamiko zaidi ya 2,000 katika miezi sita tu.

Taarifa ya Habari:Watoto wa Australia kuanza kuamua katika shule ya msingi kama watafuata taaluma za sayansi na teknolojia kwa msaada wa wazazi 17.07.2026

Utafiti mpya unaonyesha kuwa watoto wa Australia wanaweza kuanza kuamua katika shule ya msingi kama watafuata taaluma za sayansi na teknolojia wanapokuwa wakubwa, huku wazazi wakiwa na ushawishi zaidi kuliko walimu katika maamuzi hayo.

Makala Leo: Argentina na Uhispania zaishi ndoto zakipekee za Kombe la Dunia 17.07.2026

Argentina na Uhispania wanaishi ndoto ya kipekee ya Kombe la Dunia, baada yakutinga fainali ya kombe hilo. Mjini Buenos Aires na Madrid, mashabiki wanachangia jinsi walivyopitia tamthilia, hisia na sherehe.

Taarifa ya Habari:Ombi latolewa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na wakaazi wa Torres Strait 16.07.2026

Kuna wito wa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, huku vikao vikiendelea katika uchunguzi wa ubaguzi wa rangi wa Serikali ya Shirikisho huko Darwin.

Makala Leo:Ufaransa na Uhispania tayari kwa pambano la nusu fainali 14.07.2026

Nusu fainali za Kombe la Dunia zimewadia, Ufaransa na Uhispania zikijiandaa kufufua moja ya ushindani mkubwa wa soka la kimataifa. Tunaangalia kwa karibu habari za hivi punde za timu hizo na kusikia kutoka kwa kambi zote mbili kabla ya pambano kubwa la kesho.

Taarifa ya Habari:Vyuo vikuu kukabiliwa na faini kubwa vikishindwa kupambana na ubaguzi wa rangi 14.07.2026

Serikali ya Shirikisho inasema vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na faini ikiwa vitashindwa kupambana na ubaguzi wa rangi chini ya viwango vipya vilivyoanzishwa Jumatatu 13 Julai 2026.

Makala Leo:Kusini Australia yatoa mpango wakupiga marufuku wahalifu wa vurugu kutoka programu zakuchumbiana 14.07.2026

Jimbo la Kusini Australia limefichua mpango wa kwanza wa kupiga marufuku vurugu za majumbani na wahalifu wa kujamiana kutoka kwa programu za kuchumbiana.

Makala Leo:Mashambulizi mapya yashuhudiwa Iran na Marekani zikibishana kuhusu kufunguliwa kwa Hormuz 14.07.2026

Marekani na Iran zimebadilishana wimbi jingine la mashambulizi, huku mapigano yakiongezeka kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz yakisukuma makubaliano ya kidiplomasia ya mwezi uliopita karibu kuvunjika.

Taarifa ya Habari:Daglo na maafisa wengine wa RSF wahukumiwa adhabu ya kifo 13.07.2026

Mahakama ya Kupambana na Ugaidi na Makosa Dhidi ya Taifa iliyoko mjini Port Sudan nchini Sudan, , imemhukumu kifo kiongozi wa kundi la wanamgambo wa RSF, Mohamed Hamdan Daglo pamoja na maafisa wengine 15 wa RSF.

Yaliyojiri Afrika: Usalama waimarishwa katika mitaa ya Tanzania 10.07.2026

Usalama unaendelea kuimarishwa katika miji mikubwa ya Tanzania, maafisa wa Polisi na Jeshi wenye silaha wakifanya doria.

Mbappé aiweka Ufaransa katika nusu fainali 10.07.2026

Ufaransa imetinga nusu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco. Kylian Mbappé amefunga mabao nane sawa na Lionel Messi, wakati Ousmane Dembélé akikamilisha ushindi huo.

Taarifa ya Habari:Polisi wachunguza kama kifo katika jimbo la Kusini Australia, kina husishwa na kupotea kwa huduma za Telstra Jumatano 10.07.2026

Polisi wanachunguza kama kifo kinahusishwa na kupotezwa kwa huduma ya Telstra kote nchini Jumatano. Wapelelezi wa Kusini Australia wamethibitisha mtu mmoja alifariki katika hospitali ya kanda Jumatano, lakini polisi hawakuwa wamearifiwa kuhusu kifo hicho.

Hallgasd a(z) SBS Swahili - SBS Swahili podcastot a Replaióban

Rádió és podcastok egy alkalmazásban - ingyen és regisztráció nélkül. Telepítsd még ma, és ne maradj le a premierről

Letöltés a Google Play-ről

A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.