SBS
SBS Swahili - SBS Swahili
Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili
Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: www.sbs.com.au
Hol hallgathatod?
Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio HamarosanA podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz
Epizódok
Taarifa ya Habari:Wafanyakazi wa kusambaza vyakula kuongezewa mshahara kuanzia leo 17.08.2026 5:35
Takriban idadi yawa Australia 250,000 wanaosafirisha vyakula kutoka hotelini na dukani kwa ajili ya kujikimu, wanatarajiwa kupokea mshahara wa chini kisheria kwa mara ya kwanza.
Makala Leo:Serikali kuwekeza mamilioni katika nyumba za waathiriwa wa unyanyasaji wa majumbani; lakini je, inatosha? 14.08.2026 11:36
Mgogoro wa makazi ukiendelea, vurugu za kifamilia na majumbani (DFSV) ndio sababu kuu ya wanawake na watoto kuondoka nyumbani kwao na kukosa makazi.
SBS Learn Eng Ep 117 Jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu 14.08.2026 15:27
Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu katika maktaba?
Taarifa ya Habari:Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni 14.08.2026 15:52
Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni leo. Uchunguzi huo ulizinduliwa katika mwezi Mei ili kuchunguza mapendekezo ya Serikali, ya kuokoa karibu dola bilioni 38 kwa kipindi cha miaka minne.
Yaliyojiri Afrika: Uganda na Tanzania za zindua ushirikiano wa nishati 14.08.2026 6:59
Bandari ya Tanga itakuwa kitovu muhimu cha nishati katika jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya ushirikiano mpya wa nishati uliozinduliwa kati ya serikali ya Uganda na Tanzania.
Makala Leo:Sensa imekwisha ila, bado hauja chelewa kama hauja jaza fomu yako 14.08.2026 6:49
Sensa ya 2026 imekwisha na idadi kubwa ya Waaustralia walikamilisha utafiti huo mtandaoni.
Taarifa ya Habari:Serikali yawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama 11.08.2026 13:24
Serikali inawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama, kufuatia visa vya hivi karibuni vya roboti za AI kufanya ujambazi na uvunjaji wa data katika mashirika makubwa.
Yaliyojiri Afrika:Wanariadha wa Uganda watoweka Scotland 11.08.2026 7:58
Mabondia wanne wa timu ya Uganda, wametoweka baada yakufeli kujitokeza kwa safari zao za ndege zakurejea nyumbani, baada ya kushiriki katika michezo ya jumuiya yamadola mjini Glasgow.
Makala Leo: Watetezi wa ulemavu waomba mlinzi nakuonya kuhusu 'athari kubwa' mageuzi yanapokaribia 11.08.2026 9:10
Watetezi wa ulemavu wanaihimiza serikali kufikiria upya mabadiliko ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu unao julikana kama NDIS, kabla ya kura ya bunge inayokaribia kuhusu mageuzi yaliyopendekezwa.
Taarifa ya Habari:Wafanya biashara waomba ushirikiano na serikali kabla ifanye mabadiliko katika uhamiaji 10.08.2026 6:09
Vikundi vya wafanyabiashara vinaihimiza serikali ya shirikisho kushirikiana nao, katika mashauriano kabla ya mabadiliko yoyote makubwa kutangazwa kuhusu sera ya uhamiaji.
Taarifa ya Habari:Ofisi ya takwimu ya Australia yahimiza wanao ishi katika nyumba zenye watu wengi wasiwe na hofu kushiriki katika sensa 07.08.2026 12:52
Usiku wa sensa ukikaribia, maafisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia wanawahimiza watu wanao ishi katika makaazi yenye watu wengi sana, wasiwe na hofu yakushiriki kwa sababu hapatakuwa athari yoyote ya kisheria.
What are my rights if stopped by police in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Haki zangu ni zipi kama nitasimamishwa na polisi nchini Australia? 07.08.2026 13:43
Police officers have a range of operational powers they can exercise under legislation, including to ask questions, give ‘move on’ directions and conduct searches. Here’s what you need to know about your basic rights and obligations in a police interaction. - Maafisa wa jeshi la polisi wana mamlaka mbalimbali ya kiutendaji ambayo wanaweza kuyatumia chini ya sheria, ikiwa ni pamoja na kuuliza maswa...
SBS Learn Eng Ep 116 Jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama 07.08.2026 15:22
Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama?
Taarifa ya Habari:Mfanyabiashara afariki mjini Melbourne baada ya tukio linalo shukiwa kutekelezwa na wezi 07.08.2026 5:15
Mfanyabiashara mmoja wa duka mjini Melbourne amefariki baada ya kushambuliwa alipokuwa akijaribu kuzuia kundi la vijana walio kuwa waki iba dukani.
Yaliyojiri Afrika: DRC yaadhimisha GENOCOST 04.08.2026 7:38
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ameongoza kumbukumbuku ya mauaji ya GENOCOST jijini Kinshasa, inayofanyika kila tarehe 2 mwezi Agosti.
Taarifa ya Habari:Mamia ya watu wakimbia mapigano Tigray na kuingia Sudan 04.08.2026 13:24
Mamia yawa Ethiopia kutoka eneo la kaskazini mwa Tigray, wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Sudan katika siku mbili zilizopita, wakikimbia mapigano karibu na mpaka.
Makala Leo:Australia inakabiliwa na 'tsunami ya uharibifu' mkubwa kutokana na mlipuko wa virusi vya homa ya ndege H5 04.08.2026 11:30
Jimbo la Kusini Australia huenda linakabiliwa na tukio la kwanza la vifo vingi vya wanyamapori nchini Australia linalohusishwa na homa ya ndege ya H5N1.
Makala Leo:Benki ya Hifadhi yasema wa Australia wengi hawa elewi jinsi viwango vya riba vinavyofanya kazi 04.08.2026 8:05
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Australia kimepungua, lakini shinikizo la bei la msingi linabaki kuwa juu sana.
Taarifa ya Habari 03.08.2026 5:09
Mdhibiti wa ushindani [[ACCC]] ameombwa na serikali ya shirikisho kufuatilia vituo vya mafuta kwa matukio yoyote ya kupunguzwa kwa bei - sasa kwa kuwa punguzo la muda la ushuru wa mafuta limeisha. Visa 74 vya aina ya H-5 ya homa ya ndege vimethibitishwa nchini Australia. Hiyo inajumuisha uthibitisho wa tukio la kwanza la vifo vingi humu nchini kutokana na virusi hivyo Kusini mwa Australia. Mji wa...
Taarifa ya Habari:Kiongozi wa Victoria, ajiuzulu baada ya siku kadhaa za shinikizo dhidi ya uongozi wake 28.07.2026 14:42
Jacinta Allan amejiuzulu kama Kiongozi wa Victoria, akisema ni uamuzi sahihi kwa Wa-Victoria. Tangazo hilo limekuja nusu saa tu baada ya changamoto inayotarajiwa ya uongozi katika mkutano uliopangwa wa chama cha wabunge, kuashiria kurudi kwa bunge la jimbo.
Australia Yafafanuliwa:Tamasha ya Garma ni nini, na kwa nini ni muhimu? 28.07.2026 10:45
Kila mwaka, maelfu ya watu husafiri kwenda katika jamii ya kijijini kaskazini mashariki mwa Arnhem Land katika Eneo la Kaskazini.
Makala Leo: Jacinta Allan akataa kujiuzulu, pambano la uongozi wa chama cha Labor cha Victoria likiongezeka kasi 28.07.2026 11:00
Kiongozi wa Jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema atapambana na changamoto ya uongozi inayokuja baada ya viongozi wa mirengo tafuati ndani ya chama cha Labor, kukutana na kukubaliana kwamba amepoteza uungwaji mkono wa wengi katika mkutano wao.
Taarifa ya Habari: Kiongozi wa Victoria asisitiza hajiuzulu! 27.07.2026 5:00
Kiongozi wa jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema hatajiuzulu kutoka wadhifa wake, miezi minne kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo.
Yaliyojiri Afrika:Kenya yapokea tani 4.5 zavifaa vya matibabu vya Ebola kutoka India 24.07.2026 7:44
Kenya imepokea shehena ya kwanza ya tani 4.5 za vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali ya India, ili kuimarisha uwezo wa nchi kujiandaa kukabiliana na uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Taarifa ya Habari: Hatua ya Marekani kuongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia yazua ukosoaji 24.07.2026 13:33
Utawala wa Trump umeongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia kutoka asilimia 10 hadi 12.5, huku kiwango kipya kikianza kutumika alasiri ya leo Ijumaa.
Hasonló podcastok
A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.