United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: news.un.org
Hol hallgathatod?
Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio HamarosanA podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz
Epizódok
07 OKTOBA 2026 07.10.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalumu cha mahojiano yanayozingatia tangazo la jana kutoka serikali ya Kenya ya kwamba mtu mmoja amekufa kwa ugonjwa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo nchini humo. Kufuatia tangazo hilo Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya amezungumza na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani,(WHO) nchini humo Dkt....
Walinda amani wa Umoja wa Matifa nchini DRC wapatiwa Tuzo 06.10.2026 3:20
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC walipatiwa medali za Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu ni Kapteni Hamis Milyango, tuungane naye.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na harakati za kudhibiti Ebola 06.10.2026 3:02
Kufuatia mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nao wanachukua hatua kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauleti changamoto kwenye harakati za ulinzi wa raia. Je wanafanya nini? Tuungane na Private Lazaro Mlyuka kutoka Kikosi cha Tanzania cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kinachohudumu nchini humo.
Mlipuko wa Ebola ukiendelea Ituri na Kivu Kaskazini nchini DRC, maisha ya watoto yaparaganyika 06.10.2026 2:49
Watoto wachanga wawili, mmoja mwenye umri wa miezi 7 na mwingine miezi minane,ni miongoni mwa watoto ambao maisha yao yamebadili baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na sasa Umoja wa Mataifa unataka hatua zichukuliwe kuwalinda wao na wengine wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi.
06 SEPTEMBA 2026 06.10.2026 10:45
Hii leo jaridani tunaangazia Ebola nchini DR Congo na kazi ya walinda amani nchini humo. • Watoto wachanga wawili, mmoja mwenye umri wa miezi 7 na mwingine miezi minane,ni miongoni mwa watoto ambao maisha yao yamebadili baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na sasa Umoja wa Mataifa unataka hatua zichukuliwe kuwalinda wao na wengine wengi. •...
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, MAFAMBA 05.10.2026 0:30
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo Mchambuzi wetu Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili huko Zanzibar, BAKIZA anafafanua maana ya neno, MAFAMBA.
05 OKTOBA 2026 05.10.2026 9:52
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Wiki iliyopita katika Ofisi ya Kenya ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo, KALRO iliyoko jijini Nairobi nchini Kenya, FAO nchini Kenya kwa kushirikiana na serikali walizindua mradi wa SoilFer. Mradi huu unahusisha kuwa na ramani ya aina za udongo za taifa hilo la Afrika Mashariki ili kusaidia wakulima kuongeza tija kwenye kilimo. Je ina maana gani? Na kwa nini...
“Maisha yanaweza kuwa mabaya kwa sababu ya vita, lakini tunaimba tu… na ninapoimba inanifanya kusahau matatizo yote na kuwa katika wakati huo." - Toussaint Chiza 02.10.2026 9:37
Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwenye mada ya leo aliyekimbia vita Jamhuri ya...
02 OKTOBA 2026 02.10.2026 10:46
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwe...
01 OKTOBA 2026 01.10.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Miongoni mwa mikutano iliyochukua nafasi kubwa wakati wa Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , UNGA81 ni kuhusu Akili Mnembaa u AI. Pamoja na changamoto zake lakini AI inauweza mkubwa wa kusaidia jamii kutatua changamoto na hata kuondoa taarifa potofu. Waandishi wa habari hawakuachwa nyuma nao walikuwa na mikut...
30 SEPTEMBA 2026 30.09.2026 11:00
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, tukimsikiliza mmoja wa washiriki wa UNGA81ulioanza tarehe 22 Septemba na kufunga pazia Jumatatu, tarehe 28 Septemba mwaka huu wa 2026 Paul Siniga, ambaye pamoja na wadhifa mwingine alionao ni mchechemuzi wa Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mleta mabadiliko wa watoto kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wato...
29 SEPTEMBA 2026 29.09.2026 9:58
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Dunia hivi sasa imegubikwa na mazingira ya uhalifu yanayozidi kuwa magum ukila uchao. Umoja wa Mataifa unasema kutokana na mazingira hayo huduma, miundombinu na teknolojia vinaweza kutumiwa vibaya na wahalifu. Hii ni pamoja na mienendo mipya inayojulikana kama “uhalifu kama huduma” na “vurugu kama huduma. Ni kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa...
28 SEPTEMNA 2026 28.09.2026 9:57
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo tunaangazia sekta ya afya barani Afrika na kuzungumzia hilo mwenzangu Leah Mushi amezungumza na Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni Kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi. Suala la kwanza kutaka kufangamu kutoka kwake ni je mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa ulifanyika mwis...
25 SEPTEMBA 2026 25.09.2026 10:16
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo unafanyika mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa na kama nilivyokudokeza kuwa tutakuwa na maoni na ushauri wa baadhi ya wananchi wa Afrika Mashariki kwa viongozi wanaoshiriki mkutano huo, tunaanzia nchini Uganda, kisha tuelekee nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya C...
24 SEPTEMBA 2026 24.09.2026 11:04
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. “Kuwa mkimbizi si chaguo wala hiyari ni shuruti inayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa amani sababu ya vita na kila mtu anaweza kuwa mkimbizi siku moja.” Hiyo ni kauli ya Marry Nyiriak Maker Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kandoni mwa mjadala Mkuu wa Baraz...
23 SEPTEMBA 2026 23.09.2026 12:09
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho Septemba 24 viongozi wa dunia wanaokutana hapa New York, Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa watakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ongezeko la kina cha maji ya bahari duniani. Hatimaye wanatarajiwa kupitisha azimio la kusaidia mataifa yanayokumbwa na madhara yatokanayo na ongezeko hilo. Kutoka Nairobi, Kenya, Assumpta Massoi kwa us...
22 SEPTEMBA 2026 22.09.2026 11:52
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mabadiliko ya tabianchi hayawaathiri watu wote kwa kiwango sawa. Baadhi ya nchi zimejenga uchumi wao kwa miongo kadhaa kupitia matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, huku nyingine zilizochangia kidogo katika uzalishaji wa gesi chafu zikikabiliwa na mafuriko, vimbunga, ukame, ongezeko la kina cha bahari na kupotea kwa njia za kujipatia riziki. Hili ndilo...
Balozi Thigo: Kuwalinda watoto zama za AI na teknolojia ni muhimu sana 21.09.2026 2:17
Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika...
Maandalizi ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA81 21.09.2026 2:41
Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao wenzangu Leah Mushi na Anold Kayanda waafuatilia maandalizi ya mjadala huo.
21 SEPTEMBA 2026 21.09.2026 9:58
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu na vijana kuhusu siku ya amani, ufunguzi wa UNGA81, Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. • Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali ku...
Siku ya amani duniani, vijana wapaza sauti zao 21.09.2026 2:52
Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani.
18 SEPTEMBA 2026 18.09.2026 9:59
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo kufuatilia mapambano dhidi ya ebola ambayo yameanza kupata matumaini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo. • Mlipuko wa sasa wa 17 wa Ebola wa virusi vya Bundibugyo huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umegharimu zaidi wanawake na wasicha kwa kuwa wengi wao wako mstari wa mbele kuhudumia wagonjwa...
17 SEPTEMBA 2026 17.09.2026 11:24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Kenya ambako Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki litakabiliwa El Nino kuanzia mwezi ujao wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu wa 2026. El Nino huweze kusababisha mvua kubwa na kwingineko ukame mkali. Kufuatia onyo hilo, tayari shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula du...
Burundi yazindua chanjo dhidi ya HPV kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 16.09.2026 3:04
Hivi karibuni, Burundi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, pamoja na wadau wengine, imezindua mpango wa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, H mpango unaolenga kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Jengo la makazi laporomoka Gaza, takribani watu 100 wahofiwa kunaswa chini ya vifusi 16.09.2026 2:59
Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hilo wakati lilipoanguka. Operesheni za uokoaji zinaendelea, huku Umoja wa Mataifa ukisema kila dakika ni muhimu katika kujaribu kuokoa maisha. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hasonló podcastok
A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.