United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ 203 epizód

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: news.un.org

Szerző

United Nations

Kategória

News

A podcast weboldala

news.un.org

Legutóbbi epizód

2026. okt. 7.

Hol hallgathatod?

Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio Hamarosan

A podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz

Letöltés a Google Play-ről Telepítsd ingyen Android közel 10 M letöltés · 4,8-as értékelés iOS hamarosan

Epizódok

16 SEPTEMBA 2026 16.09.2026

Hii leo jaridani tunaangazia uokoaji Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi, ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Burundi. • Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hil...

Ukandamizaji unaovuka mipaka na vitisho dhidi ya washirika wake wa masuala ya haki za binadamu 16.09.2026

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho, kulipiza visasi na ufuatiliaji wa kidijitali unaovuka mipaka dhidi ya watu na wadau yanayoshirikiana na mfumo wake unaohusiana na masuala ya haki za binadamu. Kufahamu kwa kina kilichomo kwenye ripoti hyo nimezungumza na Selina Jerobon ambaye amefuatilia kwa kina. Selina Jerobon anaeleza zaidi.

15 SEPTEMBA 2026 15.09.2026

Hii leo tunakuletea mada kwa Kina ambayo leo inaangazia jinsi huduma za afya ya msingi zinavyosogezwa karibu na wananchi katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya. Kupitia msaada wa UNICEF. Pia tunakuletea muhtasari wa habazi kama zifuatazo. • Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2026 kuhusu Hatari za Dunia imebainisha kuwa hofu kuhusu uwezekano wa kutokea kwa vita vikubwa duniani imeongezeka kwa...

IAEA yaangazia hali ya nyuklia Syria, na wasiwasi kuhusu Iran na Ukraine 14.09.2026

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema maendeleo yamepatikana katika kutatua masuala yaliyosalia kuhusu ukaguzi wa nyuklia nchini Syria, huku wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukiendelea kuwa wa dharura. Anold Kayanda amefuatilia kwa kina taarifa hiyo na kuandaa taarifa hii.

Mlo shuleni wabadilisha maisha ya Dieudo na familia yake nchini DR Congo 14.09.2026

Kwa watoto wengi, chakula shuleni si mlo tu, bali ni fursa ya kuhudhuria masomo, kujifunza na kuwa na matumaini ya kutimiza ndoto zao. Huko Kananga, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mwanafunzi Dieudo mwenye umri wa miaka 11 ni mfano thabiti wa jinsi njaa ilivyokuwa ikiathiri wanafunzi kabla ya kuanzishwa kwa mpango wa mlo shuleni unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango...

14 SEPTEMBA 2026 14.09.2026

Hii leo tunaangazia masuala ya mpango wa nyuklia mashariki ya kati, mlo shuleni nchini DR Congo, na ukosefu wa ajira kwa wanafunzi baada ya kuhitimu masomo ya vyuo vikuu Turkana nchini Kenya. • Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema maendeleo yamepatikana katika kutatua masuala yaliyosalia kuhusu ukaguzi wa nyuklia nchini Syria, huku wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran uk...

Ukosefu wa ajira baada ya masomo katika kaunti ya Turkana, Kenya, waelekeza vijana kwenye kilimo 14.09.2026

Duniani kote hivi sasa vijana wanapomaliza masomo hujikuta hawana cha kufanya kwani matarajio ya kupata ajira ili kuanza kujipatia kipato huyeyuka na hivyo kusalia katika sintofahamu. Vivyo hivyo kwa kijana mmoja wa kike huko kaunti ya Turkana nchini Kenya ambaye ndoto zilitwama lakini ujio wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP ulileta tena nuru katika maisha yake. Assum...

Katibu Mkuu awaenzi waathirika wa Septemba 11: “Ni shambulio dhidi ya ubinadamu wenyewe” 11.09.2026

Miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, yaliyotikisa Marekani na dunia nzima, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewaenzi karibu watu elfu tatu waliopoteza maisha, manusura na wahudumu wa huduma ya kwanza waliojitolea kuokoa wengine. Kwa wale waliokuwa New York siku hiyo, kumbukumbu ya mashambulizi hayo bado ni ya hofu, mshikamano na athari ambazo zinaendelea...

Changamoto ndani ya mafanikio ya mradi wa kuongeza kipato na kulinda mazingira Kwale, nchini Kenya 11.09.2026

Nchini Kenya, mradi wa kuboresha mbinu za kipato za wavuvi na kulinda mazingira unaotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia Kamisheni ya Masuala ya Uvuvi kwa Ukanda wa Kusini-Magharibi mwa bahari ya Hindi (SWIOFC) umeanza kuleta nuru kwa jamii za wavuvi kwenye kaunti ya Kwale nchini humo. Kwa sasa kiwango cha uvuvi mathalani dagaa kimeongezeka na kuibua changamoto ndani ya mafanikio.

Majanga ya tabianchi yavuruga masomo ya watoto milioni 171 duniani - UNICEF 11.09.2026

Zaidi ya wanafunzi milioni 171 duniani sawa na mwanafunzi mmoja kati ya kila kumi wa umri wa kusoma shule walikumbwa na usumbufu wa masomo kutokana na majanga ya tabianchi mwaka 2025 kwa mujibu wa uchambuzi mpya uliotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi

11 SEPTEMBA 2026 11.09.2026

Hii leo tunaangazia miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, elimu na athari za mabadiliko ya tabianchi, na mbinu za kipato za wavuvi na ulinzi wa mazingira nchini Kenya. • Miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, yaliyotikisa Marekani na dunia nzima, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewaenzi karibu watu elfu tatu waliopoteza maisha, m...

10 SEPTEMBA 2026 10.09.2026

Mada kwa kina ambayo leo inamulika jinsi Umoja wa Mataifa ulivyobaini umuhimu wa kujumuisha harakati za kutokomeza mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na usaidizi wa chakula kwa wagonjwa, familia zao na wahudumu wa afya. Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP David Stevenson ametanabaisha hayo wakati wa mahojiano yake na Dianne P...

09 SEPTEMBA 2026 09.09.2026

Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia Congo DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MONUSCO kimefanikiwa kurejesha amani katika kijiji cha Sayo kilichopo katika mji wa Beni. jimboni Kivu Kaskazini Tuungane na Private Lazaro Richard Mlyuka aliyetuandalia mada hii kwa kwa kina akieleza juhudi zilizofanyika na wanasa...

08 SEPTEMBA 2026 08.09.2026

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea • Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO linasema kuwa uvutaji sigara una uwezekano mkubwa wa kufanya iwe vigumu kwa mwanamke au mwanaume kupata mtoto likieleza kuwa wanawake wanaovuta sigara wana hatari kwa juu ya asilimia 40 kupata ugumba ikilinganishwa na wasiovuta sigara. • Inakadiriwa kuwa takribani kaya moj...

04 SEPTEMBA 2026 04.09.2026

JP RWEE ni kifupi cha maneno ya lugha ya Kiingereza ambayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Hatua kuelekea Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake wa Vijijini. Huu ni mpango wa kimataifa unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maisha endelevu na kulinda haki za wanawake wa vijijini katika muktadha wa maendeleo endelevu. Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa M...

03 SEPTEMBA 2026 03.09.2026

Dunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya kupung...

Kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5°C: sio sababu ya dunia kukata tamaa 03.09.2026

Dunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya kupung...

02 SEPTEMBA 2026 02.09.2026

Rwanda imepiga hatua kubwa katika kuweka mfumo wa kisheria unaohakikisha wanawake na wanaume wana haki sawa za kurithi. Hata hivyo, katika baadhi ya jamii, imani za kitamaduni, mitazamo ya jadi kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume, pamoja na uelewa mdogo kuhusu sheria, bado vinaweza kuwazuia wanawake kutumia kikamilifu haki hizo. Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Maendeleo kuelekea Uwezeshaji wa K...

01 SEPTEMBA 2026 01.09.2026

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataofa hii leo Anold Kayanda anakuletea • Idadi ya vifo kufuatia mafuriko makubwa Nepal na Cina inaendelea kuongezeka kwa mujibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa sasa Nepal ni 987 na China 16 huku kukiwa na hofu kuhusu wanawake na wasichana • Mashariki ya Kati hali Gaza na Ukingo wa Magharibi bado ni tete kuhusu huduma za afya na upatikanaji wa chakula na mahit...

31 AGOSTI 2026 31.08.2026

Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini Burundi huko ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika anamulika sera za ujumuishi wa watu wenye ulemavu na mchango wake kwenye kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, la kuhakikisha kuna elimu jumuishi, bora na usawa kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Mradi wa maji wa UNICEF waleta nuru kkwa wakaazi wa Garissa Kenya 29.08.2026
UN: Mamia ya maiti wapatikana baada ya mafuriko Nepal 28.08.2026
UNCCD: COP17 yakunja jamvi Mongolia nini kimeafikiwa 28.08.2026
28 AGOSTI 2026 28.08.2026

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Nchini Nepal, warakati za uokoaji zikiendelea kuna hofu inayotanda juu ya uwezekano wa mafuriko mengine zaidi , mamia wamepoteza maisha , wengine kuokolewa na miundombinu kkusambaratishwa UN inafanya kila liwezekanalo kusaidia -Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa katab awa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa...

JIFUNZE KISWAHILI - NENO KIROBEZO 27.08.2026

Na sasa ni wasaa wa kujifunza Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno Kirobezo. Hili linahusu wale wanaopenda kupitapita maeneo ya watu kuvizia mlo.

Hallgasd a(z) Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcastot a Replaióban

Rádió és podcastok egy alkalmazásban - ingyen és regisztráció nélkül. Telepítsd még ma, és ne maradj le a premierről

Letöltés a Google Play-ről

A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.