Yesaya R. Athuman
Yesaya Software Podcast
Ebwana mambo vipi, jina langu ni Yesaya, kila wiki ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuhabarisha, kukuelimisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye upande wa mifumo ya kompyuta.
Author
Yesaya R. Athuman
Category
Podcast website
Latest episode
Jun 13, 2025
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Sikiliza Hamasa kutoka kwa Neema kuhusu Python 08.05.2021 19:53
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Neema Rajabu, Neema ni mhadhili msaidizi yaani assistant lecturer na mbobezi kwenye eneo la Software Engineering. Nilitamani kupata hamasa kutoka kwake kuhusu Python Programming Language. Kuna nini huko, ina wepesi gani na pengine kupata historia yake kidogo. Tuliangazia kwa mapana kuhusu language hii pia frameworks na community support ya Python ikoje...
Wazo la Kidigitali kuwa Bidhaa na Clemence 01.05.2021 24:44
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Clemence Mutalemwa, Clemence ameunda mfumo wa OCApp, ni mfumo unaowawezesha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kufanya clearance baada ya kumaliza masomo yao. Nijadiliana nae kimsingi namna ambayo wazo la kidigitali linazaliwa, hatua katika kutekeleza wazo hilo na hatimae kupata bidhaa ya kidigitali. Mazungumzo yetu yalijikita katika mfumo wa OCApp kama case...
Yesaya Software Update April 25, 2021 25.04.2021 0:52
Hey mambo vipi, Asante sana kwa time yako na kuendelea kusikiliza Yesaya Software Podcast. Nilikuwa kimya lakini nimerudi na mipango mingi kwa ajili yako. Kila jumamosi kutakuwa na episode mpya na tayari nimekwisha kurekodi episode za kutosha kuhakikisha hukosi toleo jipya kila ifikapo jumamosi. Nimeweka pia video kadhaa kule YouTube kuhusu Jetpack Compose, ninafurahi sana na progress yake. Ninadh...
Jetpack Compose toolkit mpya kwenye Android 25.04.2021 1:21
Jetpack Compose ni toolkit ya kisasa kutengeneza native Android UI. Imejikita katika declarative programming model, ambayo inakupa wepesi kwa kusema tuu unataka UI yako ionekanaje, na Compose itafanya mengi kwa ajili yako wakati app inabadili state, na UI yako itajiupdate automatically. Kwa kuwa imetengenezwa na Kotlin, basi inafanya kazi vizuri kabin na Java Programming Language na kutoa direct a...
Adam ametupa Somo na Safari ya Kuilea bidhaa ya Kidigitali 24.04.2021 30:28
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Adam Duma, Mjasiliamali wa kidigitali na kilimo, yeye pamoja na wenzake wameanzia mfumo mahiri wa Smartclass. Nilipenda kufahamu namna walivyoweza kuanzisha wazo lao hili, kulisimamia na pia changamoto wanazopitia? Host: Yesaya R. Athuman
Maandalizi na Uandishi wa CV kwa Developers na Umuhimu wake 28.11.2020 27:43
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Justin Chanda, Senior Software Developer huyu amefanya kazi na kwenye makampuni makubwa hapa Tanzania. Nilipenda kufahamu anapenya penyaje kwenye hizi interview, lakini kubwa anaandika nini kwenye CV yake? Umuhimu wa CV kwa Developer ukoje, na je ni CV moja kwa kazi zote utakazo ziona au kila kazi ya CV yake? Justin amenieleza CV ni muhimu katika ku...
Simeon amechambua mambo mapya ndani PHP 8 21.11.2020 28:52
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Simeon Mugisha Rwegayura mütalaam maridadi na mzoefu huyu kwenye mambo ya programming. Kama unavyofahamu November 26, 2020 toleo jipya ya PHP litatoka na hapa ninamaanisha PHP 8. Nilizungumza na Simeon kutusu nini tunatarajia katika toleo hili, linakuja na mambo gani mambo. Mazungumzo yangu na Simeon yalijikita kwenye feature mpya zilizopo kwenye PHP 8...
Nimeongea na Mke wangu kuhusu Maisha ya Mahusiano kwa Programmers 14.11.2020 23:14
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Dorah P. Ndazi ana title mbalimbali muhimu kabisa lakini kubwa kabisa ni mke wangu dada huyu na nilipenda kupata mawazo yake kuhusu kuishi na Programmer, changamoto anazopitia na ushauri wake. Niligusigusia tuu kuhusu kulea watoto, kusheherekea mambo mbalimbali kama birthday na vile uko na code inasumbua lakini unafanyaje kutoa muda kuwa na familia. Pi...
Maandalizi ya Devfest November 07 -08, 2020 na Faida ya Kushiriki Event hii ya Developers 24.10.2020 31:07
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na waandaji na washiriki wa Sherehe ya Developers hapa Tanzania yaani Devfest. Devfest ni sherehe za kila mwaka kwa developers, tumekuwa tukienda pale Buni pamoja na yote kuhusu TEHAMA tumekuwa tukila na kujumuika kwa pamoja. Sasa sherehe hizi zimenasimamiwa na community ya Google Developers Group (GDG), kupata update kutoka kwao wafuate pale Twitter @GDG...
Nimefanya Uchambuzi wa Episode Tisa (9) Zilizopita 17.10.2020 20:25
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na … anyways leo mwenyewe na sina mgeni hapa nimeona ni vyema kukafanya mapitio ya matoleo tisa (9) yaliyopita na episode ya 10 imekuwa ni ya kipee kabisa kama milestone muhimu ya kujitafakari na kupata feedback kutoka kwako. Nimefanya uchambuzi wa matoleo tisa (9) yaliyopita, nimekukumbusha machache wasemaji wetu walivyochangia. Ilikuwa wakati mzuri sana...
Anthony ametupa chachu na hamasa kwenye Data Science, Machine Learning and AI kwa nchi zinazoendelea 10.10.2020 33:05
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Anthony Faustine, yeye ni ni Data Scientist na Mtafiti kwenye masuala Machine Learning. Anafanya kazi kwenye kampuni mojawapo huko Ireland akaimplement Data Analytics na Artificial Intelligence Solutions kwenye maeneo mbalimbali. Pia Anthony amejikita kwenye kutumia machine learning, deep learning, data science, na signal processing kutengeneza computa...
Mohamed ametueleza alifikaje Google na namna Maisha yalivyo huko 03.10.2020 30:37
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Mohamed Mnete, yeye ni Software Engineer kule Google. Nilifanya mahojiano naye akiwa huko Texas Marekani. Tunasikia mengi lakini kwa kuwa yupo ndugu yetu huko Google nilipenda yafahamu maisha ya huko Google yakoje, wanafanyaje kazi na kubwa kabisa huyu Mtanzania aliweza pata fursa hii adhimu kabisa. Pia nikagusiagusia kama upo uwezekano wengine kujiung...
Daktari Neema na Siri ya Kupata PhD katika Umri Mdogo 26.09.2020 31:10
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Daktari Neema Mduma, mhadhiri kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela, Arusha. Nilipenda kufahamu aliwezaje fikia ngazi ya PhD katika umri mdogo, safari yake ilikuwaje kufika huko, nilipenda kufahamu kuhusu utafiti wake sababu, matokeo na mapendekezo yake. Nilianza kwa kumuuliza Daktari Neema historia ya elimu yake, mawazo yangu yalikuwa...
Ephraim Katupa somo la Kubaki kwenye Malengo na Ujasiriamali 19.09.2020 21:40
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Ephraim Swila yeye mjasiriamali wa TEHAMA na mkurungezi wa kampuni ya Inets. Nilipenda kufahamu wamewezaje kudumu kwenye ujasiriamali, walianzia wapi na wako wapi sasa. Nilipata wasahaa mzuri zungumza na Ephraim, ni kiongozi wa mfano hakika na nina amini ukifuatilia mazungumzo yetu kuna jambo jema na zuri utajifunza. Ephraim amenijulisha walianza harak...
Billy Ametupa Uzoefu wake Kuongoza Google Developer Student Club 12.09.2020 21:40
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Billy Patrick yeye amehudumu kama Google Developer Student Club Lead katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Nilipenda kufahamu mchakato mzima wa kuomba nafasi hiyo, ushirikiano aliopata kwa uongozi wa chuo na wanafunzi, na vipi kuhusu changamoto alizopitia. Billy amenieleza Google Developer Student Club ni nini, namna inavyofanya kazi pia namna ya kufan...
Safari ya Naamini kwenye Android Apps Development 05.09.2020 29:26
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Naamini Yonazi yeye ni Android Developer, pia ameshiriki kwenye makongamano ya Developer mbalimbali kama msemaji (ndani na nje ya nchi) vilevile ameandaa meetup kadhaa za Developers. Nilipenda fahamu safari yake na kufika alipo na je alipitia njia gani? Naamini amenieleza alikuwa na kampani nzuri akiwa chuo ambayo ilimsaidia kufanya mazoezi zaidi kweny...
Jonathan anatueleza kuhusu DevOps 29.08.2020 26:23
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Jonathan Kayumbo yeye ni DevOps and Infrastructure Engineer nchini Sweden, nilitaka kufahanu kuhusu DevOps, ina faida gani, vipi tunaweza itumia hapa Bongo na vipi kuhusu tools zinazohitajika. Jonathan amesoma Tanzania na kuweza kwenda kufanya kazi nchini Sweden, anafanya kazi kama DevOps and Infrastructure Engineer kwenye moja ya kampuni kubwa kule Sw...
Sam aliwezaje Kujiunga na Kufanya Kazi Andela 22.08.2020 19:51
Samwel Charles ni mtanzania na Software Engineer Andela/Cloudflare. Amesoma na kufanya kazi hapa nyumbani Tanzania, lakini aliona fursa kufanya kazi Andela na kwenye toleo hili atatueleza aliwezaje fanikisha hilo. Sam ameeleza hatua alizopitia kutokea mwanzo kabisa namna alivyoona fursa kutoka Andela, namna alivyojisikia baada kufika Andela na namna wanavyofanya kazi huko. Host: Yesaya R. Athuman
Umuhimu wa Kujenga Jamii au Community ya Developers 14.08.2020 19:19
Kwenye toleo hili nimezungumza na Georgia kuhusu umuhimu wa kujenga jamii au community ya Developers hapa nchini. Georgia ni mdau muhimu sana katika kuandaa meetup nyingi za Developers hapa Tanzania na pia anahusika na Google Developer Group (GDG) Dar, Women Tech Makers Dar es Salaam na Facebook Developers Cycle. Host: Yesaya R. Athuman
Tujadili Kotlin Pamoja Julai 27 - #KotlinEverywhere Dar es Salaam 23.06.2019 3:29
Kotlin ndio lugha chagua kwa Google kwa kutengeneza mifumo katika program ya Android. Java huenda isiendee tumika na kupata usaidizi wa moja kwa moja toka Google hapo baadae. Host: Yesaya R. Athuman
Kuwa Mtengeneza Mifumo Tanzania: Changamoto na Fursa 26.05.2019 13:02
Kuwa Mtengeneza Mifumo Tanzania kunaambatana na changamoto na fursa mbalimbali. Katika toleo hili nitakurudisha enzi za zamani nakupata hadhithi za watengeneza mifumo wa zamani. Pia nitakusimulia niliaonza chuo changamoto nilizopitia na kupata kazi. Pia nimeainisha fursa zilizopo sasa kwa watengeza mifumo wa leo. Host: Yesaya R. Athuman
Nitazungumza nini kwenye Mafunzo Mbeya? 24.03.2019 3:40
Fuatilia toleo hili kujua ni nini nitazungumza kwenye mafunzo Mbeya juu ya Computer na namna tunayoweza itumia kama vijana na wanafunzi. Host: Yesaya R. Athuman
Nimefanya nini Wiki Mbili? 24.02.2019 8:24
Ebwana mambo vipi, leo nitakupa taarifa ya kazi nilizofanya kwa wiki mbili. Host: Yesaya R. Athuman
Machine Learning imekuja, Usiachwe Nyuma 04.02.2019 4:36
Ebwana mambo vipi jina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo tutaangalia kwa nini hupaswi acha nyuma na hili joto la Machine Learning na kwa wepesi tuu ni vi...
Tujadili Machine Learning 27.01.2019 4:12
Episode 8 Ebwana mambo vipi jina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo nitakupa chachu kidogo tuu kuhusu Machine Learning, nimejaribu kufuta maana yake kwa K...
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.