RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

News SW ↓ 24 episodes

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Author

RFI Kiswahili

Category

News

Podcast website

www.rfi.fr

Latest episode

Jul 8, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Rais Ndayishimiye ataweza kuleta maridhiano kati ya upinzani na serikali nchini DRC ? 08.07.2026

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, wiki hii amekutana  na kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani kutoka muungano wa C64 na viongozi wa Kanisa Katoliki na Kiprotestanti nchini DRC, wanaopinga mchakato wa marekebisho ya katiba unaoungwa mkono na rais Felix Tshisekedi. Je, rais Ndayishimiye, atafanikiwa kuleta maridhiano ?

Kwanini vita vinaendelea mwaka mmoja baada ya DRC na Rwanda kutia saini ya mkataba wa amani ? 01.07.2026

Vita vimeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi na waasi wa M23/AFC wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Rwanda licha ya Kigali na Kinshasa, kutia saini mkataba wa kusitisha vita mwaka mmoja uliopita. Kwanini vita vinaendelea  licha ya kuwepo kwa mkataba huu ? Tunachambua.

Serikali nchini Uganda inatumia Mahakama kuwanyanyasa wapinzani ? 24.06.2026

Nchini Uganda, mwanasiasa wa upinzani na Meya wa zamani wa jiji la Kampala Erias Lukwago anakabiliwa na mashtaka ya uhaini. Alikamatwa nyumbani kwake na wanajeshi kwa agizo la Mkuu wa Majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba na kuzuiwa kabla ya kufikishwa Mahakamani. Wiki hii, mwanasiasa mashuhuri na wakili wa Besigye Martha Karua kutoka nchini Kenya, alizuiwa kuingia nchini Uganda na kufukuzwa nchini...

Kenya kuwalipa fidia waathiriwa wa maandamano ya kisiasa 17.06.2026

Serikali ya Kenya, itaanza kuwalipa fidia watu karibu Elfu Mbili, walioathiriwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kuuawa, kubakwa, kutoweka na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kati ya mwaka 2017 hadi 2025. Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini Kenya, katika ripoti yake, inasema imewatambua waathiriwa wote wanaopaswa kupokea fidia hiyo, ambayo i...

Vijana nchini Kenya wanavyotumia teknolijia kuhamasisha elimu ya kisiasa 10.06.2026

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vijana nchini humo, wanakumbatia teknolojia kuwafikia vijana wengi hasa  wale wa rika la Gen Z, kujiandikisha kama wapiga kura na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Je, hatua hii inaweza kuleta mwamko mpya wa kisiasa nchini Kenya ? Mwanahabari wetu Benson Wakoli alikutana na kuzungumza na vijana hao.

DR Congo: Wanasiasa wachuana kuhusu mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba 03.06.2026

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeundwa miungano miwili ya kisiasa. Kundi la kwanza linaitwa "C4" linalounga mkono mabadiliko ya katiba, chini ya rais Felix Tshisekedi. Nao vigogo wa upinzani wakiongozwa na Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine, wao wameunda C64" vuguvugu linalopinga marekebisho yoyote na kuilinda katiba ya sasa. Nini hatima ya makundi haya ? Tunachambua.

Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027? 28.05.2026

Siasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana na siasa. Tunachambua kauli za viongozi hao wa kisiasa.

Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani 20.05.2026

Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii mpya, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendelez...

Kwanini suala la siasa na usalama, halikupewa nafasi kubwa kwenye mkutano wa Afrika na Ufaransa ? 14.05.2026

Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika, uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kati ya Mei 11 hadi 12, haukutoa kipaumbele suala la siasa na usalama katika mataifa ya Afrika, wakati huu nchi kama DRC, Sudan na yale ya ukanda wa Sahel kama Mali, Niger na Burkina Faso yakishuhudia changamoto kubwa ya kiusalama. Tunachambua kwa kina.

Mpango wa DRC kuwakubali wahamiaji waliofukuzwa Marekani kwazua mjadala 06.05.2026

Hatua ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuingia kwenye makubaliano na Marekani ili kuwapokea wahamiaji haramu waliofukuzwa nchini humo, kumezua mjadala mzito katika nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, hasa maeneo ya Mashariki. Kwanini kuna mvutano ?

Tanzania: Ripoti ya Tume imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa Oktoba 29 ? 29.04.2026

Nchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani ya Shilingi za nchi hiyo Bilioni 125. Je, ripoti hii imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa kilichoto...

Kwanini Ruben Kigame, anataka kuwa rais wa Kenya 2027 ? 22.04.2026

Uchaguzi Mkuu nchini Kenya ni mwezi Agosti mwaka 2027, lakini wanasiasa mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kugombea kiti cha urais. Miongoni mwao ni Ruben Kigame, mwanasiasa, mwanaharakati, mhadhiri, mwandishi wa Habari na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili. Yeye ni mlemavu wa Macho, ameamua kujitosa uwanjani, kutafuta uongozi wa nchi ya Kenya. Nini kimemsukuma ?  Wiki hii anazungumza na mwe...

Mazungumzo mapya kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya DRC nchini Uswizi 15.04.2026

Awamu ya tisa ya mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalianza siku ya Jumatatu  Aprili 13 nchini Uswizi. Ujumbe wa Qatar ambao ni wasuluhishi, akiwemo mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Massad Boulos, wanashiriki. Nini Ajenda ya mazungumzo haya ? Raia wa DRC wategeme nini ? Tunachambua.

Harakati za watetezi wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC 08.04.2026

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, katika ripoti zao, yamekuwa yakionya kuwa maisha ya wanaharakati wa haki za binadamu, wana habari na viongozi wa mashirika ya kiraia yapo hatarini katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, Mashariki mwa DRC. Wiki hii Ruben Lukumbuka, anazungumza na Jack Sinzaera, mwanaharakati maarufu kutoka Kivu Kaskazini.

Viongozi wa ODM wanaweza kuungana tena baada ya mpasuko wa chama ? 01.04.2026

Chama siasa cha Orange Democratic Movement-ODM kinaendelea kugawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Tangu kufariki dunia kwa Raila Odinga, mwasisi wa chama hicho kikubwa cha upinzani, viongozi waandamizi wa ODM wameshindwa kuelewana kuhusu kuendelea kumuunga mkono rais William Ruto, anayetarajiwa kuwania tena urais kwa muhula wa pili. Nini hatima ya chama hiki ?

DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 25.03.2026

Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 

Nini hatima ya vita vya Marekani na Israeli nchini Iran ? 18.03.2026

Ni wiki ya tatu sasa, baada ya Marekani na Israeli zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran. Mataifa hayo mawili yanasema lengo la mashambulizi hayo ni kuhakikisha kuwa inaharibu kabisa miundo mbinu ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump, anasema vita hivi vitamalizika hivi karibuni, lakini haifahamiki ni lini. Tunachambua.

Kenya: Je, ushirikiano wa serikali kati ya vyama vya ODM na UDA unafanikiwa ? 11.03.2026

Umepita mwaka mmoja tangu chama tawala nchini Kenya UDA na kile cha upinzani ODM, vilipoingia kwenye makubaliano ya kisiasa na kutaja mambo 10 kama vita dhidi ya ufisadi, kupunguza deni la taifa, ujumuishwaji ulio sawa serikalini kama baadhi ya mambo ya kushughulikia baada ya maandamano ya vijana ya mwaka 2024. Je, mwaka mmoja baadaye mambo hayo yametekelezwa kwa kiasi gani ?  Tunachambua.

Nini hatima ya vita vya Israel na Marekani nchini Iran ? 04.03.2026

Dunia inashuhudia vita katika ukanda wa Mashariki ya Kati, baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran, tangu Februari 28. Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wanataka Iran iache kutengeneza silaha za maangamizi, kuyaunga mkono makundi yenye silaha nje ya Iran na kubadilisha utawala. Kongozi wa kiroho Ayatolla Ali Khamenei, ameuawa katika vita hivyo. Nini...

Vita vya miaka minne nchini Ukraine, nini suluhu ? 25.02.2026

Imetia miaka minne, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, katika vita vikubwa tangu vile vya pili vya dunia barani Ulaya. Maelfu ya watu wameuawa, miji na miundo mbinu muhimu imeharibiwa nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelenskyy anasema mwenzake wa Urusi hajatimiza malengo yake ya vita. Kwanini suluhu haijapatikana miaka minne baadaye ?

Kenya: Kwanini chama cha ODM kimegawanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2027 ? 18.02.2026

Joto la kisiasa limeendelea kupanda kwenye chama cha siasa cha ODM nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Chama hicho kilichoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, kimegawanyika kwa makundi mawili. Kundi moja linaongozwa na Oburu Oginga, kaka yake Raila, linamuunga mkono rais William Ruto. Kundi lingine, linangozwa na Edwin Sifuna, Katibu M...

Nini kikwazo cha utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha vita nchini DRC ? 11.02.2026

Wawezeshaji na wasuluhishi wa mzozo wa Mashariki mwa DRC kutoka Umoja wa Afrika, wanataka usitishwaji wa vita na utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Washington na kuheshimu mchakato wa Doha. Ni kwanini inakuwa vigumu kutekeleza mkataba huo  kuheshimu maelewano ya Doha ? Tunachambua.

Mazungumzo ndio suluhu ya changamoto zinazoikabili DRC ? 04.02.2026

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema serikali yake ipo tayari kuongoza mazungumzo kati ya Wakongomani, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo, hasa utovu wa usalama, mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo, Chama cha "Ensemble pour la République, kinachoongozwa na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Moise Katumbi, kinasema mazungumzo hayo yanaweza kufanyik...

Kenya: Nini suluhu ya mzozo wa chama cha ODM ? 28.01.2026

Chama cha ODM kilichoanzishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu  nchini Kenya Hayati Raila Odinga, kinapitia mgawanyiko wa kisiasa kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto kuwania urais kwa muhula wa pili. Viongozi  wa chama hicho wamegawanyika kuhusu mpango huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Mvutano  huu unamaanisha nini ?

Listen to the Wimbi la Siasa podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.