SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 930 episodes

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Author

SBS

Category

News

Podcast website

www.sbs.com.au

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Makala leo: Wakristo waadhimisha Pasaka na Jumapili ya Matawi kwa mioyo mizito na furaha 07.04.2026

Waumini wa dini laki kristo walisherehekea Jumapili ya Pasaka, wakiadhimisha tukio hilo wakati vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati vikifunika sehemu kubwa ya dunia.

Makala leo: Waustralia waonywa kupata chanjo dhidi ya aina ya mafua inayo sambaa haraka 07.04.2026

Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza wanahimiza kila mtu apate chanjo ya mafua, kwa ajili ya kujaribu kuzuia kurudia kwa mwaka jana ambapo Australia ilishuhudia idadi kubwa ya vifo vilivyo sababishwa na mafua.

Taarifa ya Habari: Australia yapata usambazaji wa mafuta wa mwezi mwingine 06.04.2026

Serikali ya shirikisho imesema ugavi wa akiba ya mafuta ya Australia sasa umeongezwa hadi Mei, kuanzia katikati ya Aprili.

Taarifa ya Habari: 13 wauawa katika milipuko Burundi 03.04.2026

Ushuru wa petroli unatarajiwa kupunguzwa zaidi, wakati viongozi wa majimbo na wilaya wakikubaliana kuhusu mpango wa kurejesha mapato ya ziada ya ushuru wa bidhaa na huduma kutokana na kupanda kwa bei za mafuta.

Makala leo: 'Acha kutumia miili ya wanawake' kundi la misaada laonya, unyanyasaji wa kingono ukienea Sudan 03.04.2026

Wanawake na wasichana wanaokimbia vita vya Sudan wanaelezea ubakaji, mateso na unyanyasaji, huku wafanyakazi wa misaada wakionya kwamba mateso yanazidi kuwa makubwa kuliko visa vinavyofikia huduma ya matibabu.

Makala leo: Hotuba ya Waziri Mkuu yapokewa kwa hisia mseto 03.04.2026

Hotuba ya kitaifa ya Waziri Mkuu Anthony Albanese kuhusu uchumi unaokabiliwa na matatizo nchini humu, inayosababishwa na mgogoro wa nishati duniani, imepokewa kwa hisia mseto.

Taarifa ya Habari: Milipuko yasababisha mtafaruku Bujumbura 02.04.2026

Waziri wa ulinzi amethibitisha kwamba Australia itajiunga na kundi la mataifa katika mkutano wa dharura kuhusu jinsi ya kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz.

Makala leo: Afueni kwa madereva wanaokabiliwa na matatizo baada ya serikali kupunguza ushuru wa mafuta 31.03.2026

Baada ya wiki kadhaa za shinikizo kuhusu kupanda kwa bei ya petroli, serikali ya shirikisho imepunguza kodi ya mafuta kwa nusu.

Taarifa ya Habari: Serikali yachukua hatua yakupunguza bei ya mafuta nchini baada ya siku kadhaa za shinikizo 31.03.2026

Waziri Mkuu amesema serikali yake imechukua hatua ya kupunguza bei ya mafuta kote nchini, kwa sababu hata kama vita vitaisha mara moja, madhara ya kiuchumi yataendelea.

SBS Learn Eng Ep 104 Makala ya ziada: Jinsi yakuzungumza kuhusu mitihani 31.03.2026

Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu mitihani?

Australia Yafafanuliwa: Pasaka ya Australia:Kuchunguza mila za kijamii na kitamaduni zaidi ya dini 31.03.2026

Pasaka inachukuliwa kuwa likizo muhimu zaidi katika kalenda ya Kikristo.

Taarifa ya Habari: Ongezeko ya bei ya mafuta yalazimisha serikali izingatie hatua zakufanyia kazi nyumbani 30.03.2026

Hatua za kufanyia kazi nyumbani zinaweza wasilishwa lakini mgao wa mafuta hauzingatiwi, na viongozi wanaohudhuria mkutano wa kitaifa wa baraza la mawaziri leo kuhusu mgogoro wa mafuta.

SBS Learn Eng Ep 70 Jinsi yakufanya mazungumzo wakati wa BBQ 30.03.2026

Je, unajua jinsi ya kufanya mazungumzo wakati wa BBQ?

Taarifa ya Habari: Vituo na Wasambazaji kupewa faini ya milioni $100 wakiongeza bei ya mafuta kwa njia bandia 27.03.2026

Vituo vya mafuta na wasambazaji watakaopatikana wakiongeza bei kutokana na vita vya Mashariki ya Kati watakabiliwa na adhabu mpya kali.

Mgogoro wa nishati unaokuja una athari kubwa na kali 27.03.2026

Shirika la Nishati la Kimataifa linaonya viongozi wa dunia huenda hawathamini, kina cha mgogoro wa nishati unaokaribia, huku vita vya Marekani na Iran vikiendelea.

Taarifa ya Habari: Serikali za Australia na Ujerumani za imarisha uhusiano wa usalama 26.03.2026

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani amekutana na mwenzake wa Australia Richard Marles, katika ziara ya kwanza ya mtu aliyehudumu katika nafasi hiyo katika kipindi cha miaka 8.

Australia Yafafanuliwa:Jinsi yakununua sanaa za kiasili kimaadili nchini Australia 25.03.2026

Je, unajua kwamba zawadi tatu kati ya nne zinazouzwa nchini Australia, kama za asili au zilizotengenezwa kwa mtindo wa Asili zimegundulika kuwa si za kweli?

Makala leo: Rhoda Roberts AO: Shujaa wa utamaduni aliyebadilisha taifa 24.03.2026

Salamu za rambirambi zinatolewa kwa Mwanamke aliyekuwa akitoa mwongozo na ushauri katika shirika la habari la SBS kutoka ukoo wa Widjabul Wia-bal, Shangazi Rhoda Roberts, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 66.

Taarifa ya Habari 24 Machi 2026 24.03.2026

Australia inatafuta kupata uhakikisho wa usambazaji wa nishati kutoka kwa washirika wa biashara wakati kukiwa ongezeko la hofu kuwa nchi zitahifadhi mauzo ya nje ya mafuta kwa ajili ya masoko yao ya ndani.

Yaliyojiri Afrika: Kenya na Uganda za zindua upanuzi wa ujenzi wa reli 24.03.2026

Marais wa Kenya na Uganda walikutana mjini Kisumu, kuzindua ujenzi uliocheleweshwa wa upanuzi wa reli yenye thamani ya mabilioni ya dola iliyojengwa na China.

Makala leo: Jinsi vita Mashariki ya Kati vina chochea wasiwasi kuhusu usalama wa chakula 24.03.2026

Vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati, na kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kumesababisha kile ambacho wataalamu wanakielezea kama moja ya migogoro mikubwa zaidi ya nishati katika miongo kadhaa.

Taarifa ya Habari 23 Machi 2026 23.03.2026

Serikali ya shirikisho inaagiza Tathmini ya Kitaifa ya Mnyororo wa Ugavi wa Chakula kwa ajili yakulinda sekta ya kilimo ya nchi dhidi ya usumbufu wa kimataifa.

SBS Learn Eng Ep 106 Kuzungumza kuhusu vyakula vya ajabu 23.03.2026

Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu vyakula vya ajabu?

Taarifa ya Habari:Wakazi wa Kusini Australia wa elekea debeni, je kutakuwa mabadiliko ya serikali? 20.03.2026

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema usambazaji wa mafuta nchini Australia uko salama, lakini anataka Australia iwe tayari kupita kiasi linapokuja suala la kudhibiti uhaba wa mafuta nchini humu.

Makala leo: Waziri Mkuu ateua kikosi kazi chaku kabili maswala yaliyo sababishwa na vita Mashariki ya Kati 20.03.2026

Waziri Mkuu amemteua 'mratibu wa mafuta' kusaidia kushughulikia masuala ya mnyororo wa ugavi yaliyosababishwa na vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati.

Listen to the SBS Swahili - SBS Swahili podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.