RFI Kiswahili
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Makubaliano kati ya Marekani na Iran kuvunjika, maandamano ya mawakili wa Kenya 11.07.2026 20:11
Yaliyojiri wiki hii ni kuvunjika kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran, mazishi ya kiongozi wa kiroho wa Iran A.Khamenei, rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwaonya wanaharakati dhidi ya kuchochea vurugu-wanasiasa wa upinzani, wanahabari pamoja na wanaharakati, Uganda waishi kwa hofu kutokana na vitisho vya mkuu wa majeshi, wapinzani wa jukwaa la C64 DRC walikutana na rais wa Burundi Evariste Ndayi...
DRC yasherehekea miaka 66 ya uhuru, amnesty yalaani vita Sudan, mazishi ya Khamenei huko Iran 04.07.2026 20:12
Makala imeangazia maadhimisho ya miaka 66 ya uhuru wa jamahuri ya kidemokrasia ya Congo, kuanzishwa kwa majaribio ya dawa zizonaweza kuwa tiba ya Ebola aina ya Bundibugyo huko DRC, kufungwa kwa kituo cha televisheni cha NTV na Gazeti la Daily Moniter nchini Uganda, shirika la Amnesty International, layatuhumu mataifa ya nje kwa kuendelea kuchochea mzozo wa Sudan. Polisi nchini Afrika Kusini wazui...
Maandamano ya Gen Z Kenya, ziara ya rais Ndayishimiye DRC,vifo Venezuela vyafikia920 27.06.2026 20:11
Maandamno ya vijana wa Gen Z kuwakumbuka wenzao waliouawa katika maandamano ya mwaka wa 2024 nchini Kenya, kesi ya aliyekuwa meya wa jiji la Kampala Uganda Erias Lukwago, ziara ya rais wa Burundi pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, jijini Kinshasa DRC, Evariste Ndayishimiye, yaliyojiri huko Sudan, Nigeria, Tunisia lakini pia mitetemeko miwili ya ardhi huko Venezuela iliyouwa watu zaidi ya 900, na p...
DRC na kombe la dunia, pia ebola,Gen z kuandamana juni 25 Kenya,hali ya sasa Iran 20.06.2026 20:01
Ni wiki ambayo imegubikwa na michuano ya kombe la dunia 2026 huko Marekani, wiki hii eneo hili la Afrika mashariki na kati lilichangamka baada ya timu ya DRC Leopards kutoka sare na Ureno, virusi vya ebola na juhudi za kikanda kuudhibiti, kukamatwa kwa wakili Erias Lukwago kule Kampala Uganda, lakini pia mashambulio ya kigaidi kwenye uwanja wa ndege wa mjini Niamey huko Niger, na mkutano wa G7 jij...
Michuano ya kombe la dunia, hali ya Ebola kwenye ukanda 13.06.2026 20:15
Ni wiki ambayo imegubikwa na maandamano kadhaa nchini huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, huko Nanyuki nchini Kenya, na watu kutoka nchi kadhaa za Afrika kuihama Afrika Kusini kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya wageni, lakini kubwa kabisa wiki hii lililotikisa ulimwengu ni michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2026 iliyong’oa nanga huko Marekani, Mexico na Canada, bila kuisahau ziara ya Ki...
Ufaransa yazindua mnara wa kumbukumbu ya genocide Rwanda, mgomo wa kitaifa DRC 06.06.2026 20:09
Ufaransa yazindua mnara wa ukumbusho wa mauaji ya kimbari huko Rwanda kwenye jiji la Paris, wapinzani wa DRC juni 03 waliitisha mgomo wa kitaifa, watu zaidi ya kumi waliuawa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa ADF huko Mbau wilaya ya Beni mashariki mwa DRC tunaangazia hotuba ya rais wa Uganda kwa taifa, ziara ya rais wa Tanzania huko Urusi, Afrika kusini kudai kuwa hakuna ubaguzi wala chu...
Wanafunzi 16 wafa katika moto wa shule ya bweni Kenya, mkuu wa WHO azuru DRC 30.05.2026 20:07
Wanafunzi kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Nakuru nchini Kenya, ziara ya mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Uganda kutangaza kuufunga mpaka wake na DRC, hali nchini Sudan, huku Nigeria, kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao, na pia ripoti zinasema Marekani na Iran zakubaliana kuongeza usitishwaji wa vita...
DRC yashirikiana na WHO, AU kupambana na Ebola, sitisho la mgomo wa madereva Kenya 23.05.2026 20:08
Habari kuu za dunia wiki hii ni pamoja na kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola, DRC na juhudi za kimataifa zinazolenga kupambana na virusi hivyo, mkutano wa Kigali kuhusu nyuklia, mgomo wa madereva wa usafiri wa umma ulivyoathiri wananchi, Kenya, hali nchini Sudan ; lakini pia wahamiaji wasio na vibali wanavyohangaishwa kule Afrika kusini, ziara ya rais wa Urusi kule China ; lakini pia Ma...
Yoweri Museveni aapishwa muhula wa saba Uganda, kongamano la Afrika forward Nairobi 16.05.2026 20:07
Miongoni mwa habari kuu za dunia zilizopewa uzito juma hili ni pamoja na kuapishwa kwa rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa muhula wa saba, kufanyika na kutamatika kwa mkutano wa Afrika na Ufaransa jijini Nairobi nchini Kenya, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame akikosoa vikwazo vya Marekani kuhusu nchi yake, eneo la Afrika magharibi hususan Nigeria, Ghana na Mali, lakini pia Ziara ya rais wa Mareka...
Watu 518 walifariki Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzi, mapigano bado yanaendelea DRC 25.04.2026 20:11
Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita. Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoli...
Kifo tatanishi cha waziri wa habari wa Burundi, Iran na Marekani zatunishiana misuli 18.04.2026 20:08
Makala hii imeangazia kifo cha waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari nchini Burundi Gabby Bugaga, waasi wa AFC/M23 na serikali ya DRC wanaokutana huko Uswis wakubaliana kuhusu kubadilishana na wafungwa, huku Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikisisitizia msimamo wake wa kuitaka Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo la mashariki, ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki nchini Cameroon kabla...
Rwanda yaadhimisha miaka 32, mauaji ya kimbari, Israeli yashambulia Lebanon 11.04.2026 20:15
Maadhimisho ya siku 100 maarufu kama kwibuka kukumbuka mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda, mwanadiplomasia wa Marekani James Swan kuanza kazi kama mkuu wa Monusco huko DRC, mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na waasi wa M23 kufanyika kule Geneva Uswiz chini ya upatanishi wa Qatar, hali ya kisiasa nchini Kenya na Tanzania, na sudan; kampeni za uchaguzi mkuu nchini Benin kutamatishwa kuelekea...
Waasi wa ADF waua 40 mashariki mwa DRC, Iran yapuuzi vitisho vya Trump 04.04.2026 20:15
Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na timu ya taifa ya soka ya DRC Leopards kufuzu kushiriki fainali ya michuano ya kombe la dunia 2026, shambulio la waasi wa ADF laua 30 mashariki mwa DRC, watoto wanne wadungwa kisu hadi kufa katika shule moja nchini Uganda, wapigakura wahamasishwa kujiandikisha nchini Kenya na kupanda kwa bei ya mafuta, kuapishwa kwa rais wa Jamhuri ya af...
UN yasikitishwa na hali mashariki mwa DRC, miili 33 yagunduliwa nchini Kenya 28.03.2026 20:09
Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na baraza la usalama la umoja wa mataifa lataka kufunguliwa upya kwa viwanja vya ndege kwenye miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa DRC, kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine alisema uhuru wake sio mjadala, miili 14 ilipatikana iliyopatikana nchini Kenya kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha vifo. utambuzi wa utumwa kuwa uhalifu dhidi ya haki za ubi...
Bei ya mafuta yapanda duniani, DRC na Rwanda kupunguza uhasama 26.03.2026 20:09
Miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na mwendelezo wa mashambulizi ya Marelkani na Israeli huko Iran, na nchi za Ghuba, huku bei ya mafuta na gesi ikipanda, DRC na Rwanda zilikubaliana kupunguza uhasama wao, rais wa Kenya William Ruto alizindua ujenzi wa reli ya kisasa SGR katika eneo la magharibi mwa nchi yake, hali ya nchini Sudan na Senegal yavuliwa ubingwa AFCON, Morocco ilitangazwa mshindi....
Mashambulio yaendelea mashariki ya kati na mauaji ya mfanyakazi wa UNICEF DRC 14.03.2026 20:06
Makala hii imeangazia pakubwa mashambulio ya Marekani na Israeli huko Iran huku Irani nayo ikijibu mapigo kwa kuishambulia Israeli, na pia kuachiwa huru kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Burundi Alain Bunyoni, shambulio la ndege zisizo na rubani lililowaua watu watatu miongoni mwao, mfanyakazi wa shirika la UNICEF kwenye mji wa Goma, mashariki mwa DRC, siasa za Kenya, Uganda na maeneo mengine ya Afrika...
Jeshi la Rwanda lawekewa vikwazo, Israeli na Marekani zashambulia Iran 07.03.2026 20:02
Matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya jeshi la Rwanda na maafisa wake wanne wakuu, Sudan iliishtumu Ethiopia kwa kuruhusu ndege zisizokuwa na rubani kuishambulia nchi yake mwezi februari na machi, Macky Sall rais wa zamani wa Senegal miongoni mwa wagombea watatu wanaotafuta ukatibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Marekani na Israel zimeendelea kutekeleza mashambu...
Msemaji wa waasi wa M23 aliuawa, Kenya yazindua dawa mpya ya Lenacapavir 28.02.2026 20:05
Matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na kuuawa kwa msemaji wa kijeshi wa kundi la waasi la M23 Willy Ngoma, serikali ya Kenya ilizindua zoezi la usambazaji wa dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, LENACAPAVIR, UN ulisema taifa la Sudan Kusini, linatoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi elfu 64, watu 25 waliuawa katika jimbo la Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria, pia awamu ya tatu ya maz...
Ndayishimiye ndiye mwenyekiti mpya wa AU, ujumbe wa EU wazuru mashariki ya DRC 23.02.2026 20:07
Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 2026, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya huko DRC, vijana wa Afrika wahadaiwa kupewa kazi nzuri Urusi, na kulazimishwa kupigana vita Ukraine, raia 18 wa Senegal na mmoja kutoka Ufaransa wahukumiwa kwa kuzua fujo wakati wa mechi ya fainali AFCON jijini Rabat. Mkutano wa kimataifa kati ya India na...
Mpasuko ndani ya chama cha ODM, nchini Kenya, huko DRC Monusco kuanza kazi upya 14.02.2026 20:06
Mpasuko kushuhudiwa ndani ya ODM, chama cha aliyekuwa kinara wa upinzani nchini Kenya hayati Raila Odinga, ziara ya kaimu mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Monusco huko Goma mashariki mwa DRC, hali ya nchini Sudan, milio ya risasi kusambaratisha usalama nchini Guinea, Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa Marekan...
Rais Paul Kagame atoa kauli nzito kwa jumuia ya kimataifa, maombi ya rais Tshisekedi 07.02.2026 20:11
Rais wa Rwanda Paul Kagame asema nchi yake haitatizwi na vitisho vya kuwekewa vikwazo na Jumuiya ya Kimataifa, mkutano unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kibishara hasa kwenye sekta ya madini kati ya Marekani na nchi za Afrika wafanyika Washington, tumeangazia siasa za Uganda, yaliyojiri nchini Kenya, hali ya kibinadamu yaendelea kuwa mbaya nchini Sudan, rais wa Nigeria Bola Tinubu aagiza wanajes...
Mwaka mmoja watimia tangu waasi wa M23 waidhibiti Goma na siasa za ukanda huu 31.01.2026 20:08
Makala hii imeangazia kutomia kwa mwaka mmoja tangu waasi wa AFC/M23 waudhibiti mji wa Goma, Rwanda yaishitaki Uingereza kuhusu mkataba unaohusu wakimbizi, mapigano yashuhudiwa huko Sudan, na katika ukanda wa Afrika magharibi tumeangazia shambulio la watu wenye silaha katika uwanja wa ndege wa Niamey, ECOWAS yaiondolea vikwazo nchi ya Guinea, na tishio la Marekani kuishambulia Iran na mengine zaid...
Jeshi la UPDF kuwaua wafuasi 30 wa chama cha NUP, Gavana Purusi arejea Uvira 24.01.2026 20:03
Katika makala utasikia polisi wa Uganda waendelea kuwakamata washirika wa karibu wa mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu baada ya uchaguzi wa wiki iliopita, waasi wa AFC/M23 Kujiondoa kwenye mji wa Uvira mashariki mwa DRCongo, nini kinaendelea? Siasa za Kenya, Tanzania na hali ya sasa nchini Sudan; wanajihadi kuwateka waumini zaidi ya mia moja na sitini wakiwa kanisani kule Nigeria, n...
Watu zaidi ya 10 wauawa katika machafuko Uganda, M23 watangaza kuondoka Uvira 17.01.2026 20:07
Makala hii imeangazia uchaguzi wa nchini Uganda matokeo yakisubiriwa kutolewa leo, mkutano wa Lome nchini Togo kuhusu mustakabali wa amani ya mashariki mwa DR Congo, hali ya nchini Sudan, Somalia, na ugunduzi wa kaburi la pamoja lenye miili ya wahamiaji 21 huko Libya, hotuba ya rais Macron mbele ya maafisa wa jeshi la nchi yake na kauli ya Marekani kuhusu waandamanaji wa Iran
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.