Innocent Ngaoh

Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha. Ni podcast ya kipekee ambayo utajifunza mambo mengi ambayo yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku, kila kitu kinachozungumzwa hapa kina uhalisia na siyo nadharia ya kusadikika. Kuwa sehemu ya familia hii na uhakika hautakuwa kama ulivyokuwa mwanzo, podcast ambayo itaboresha na kuongeza thamani ya maisha yako mara 10X au zaidi. Hakikisha unafollow ili uwe wa kwanza kupata episode mpya kila wiki.

Author

Innocent Ngaoh

Category

Education

Podcast website

podcasters.spotify.com

Latest episode

Apr 18, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Maswali Sita (06) Ya Kuepuka Kumuuliza Mtu Ambaye Hujakutana Nae Muda Mrefu...! 10.02.2024

Uungwana ni kuangalia ni maswali gani hupaswi kumuuliza mtu ambaye hujakutana nae muda mrefu, kwa sababu ukiuliza moja maoja unaonakena mtu ambaye hujielewi na hujui nini uzungumze kutoka na eneo ambalo upo.

Jinsi Dada Wa Kazi (House Girl) Alivyoninywesha Sumu Ya Panya Ili Nife...! 07.02.2024

Dada wa kazi alivyotaka kuniua kwa imani za kishirikina kwa kuninywesha sumu ya Panya nikidhani ni dawa. Sikiliza mkasa huu ujifunze kitu kuhusu dada wa kazi na vimbwanga vyao.

Kwanini Ulale Na Diary Kwenye Chumbani Au Kitandani Kwako..! 03.02.2024

Ukiwa chumbani kwako ni sehemu pekee ya kuwa diary 📔 Au daftari ili uweze kuandika ndoto ambazo unaota na mawazo yako ili usiwe kusahau. Sikiliza episode hii ujifunze

Uchambuzi Wa Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE? (Nani Kahamisha Jibini Yangu?) 31.01.2024

Nani kahamisha jibini yangu? Ni kitabu ambacho kinakusaidia kukabaliana na mabadiliko ambayo hukutarajia wala kutegemea kwenye kazi na maisha. Kitabu kipo kwa mfumo wa stori ambao inahusisha wahusika wanne ambao ni 1. Sniff 2. Scurry 3. Hem 4. Hew Ni kitabu ambacho utajifunza namna ya kukabiliana na mabadiliko kwenye maisha. Naamini kupitia uchambuzi wa kitabu hiki utafurahia Sana.

Jinsi Ya Kuachilia Vitu Na Watu Ambao Wamekuumiza Na Hawatambui Thamani Yako...! 27.01.2024

Kuachilia haijawahi kuwa jambo rahisi hasa kwa watu ambao umewathamani na kuamini wangekuwa na wewe maisha yako yote, lakini ghafla wanakuachia maumivu na kukuumiza kiakili, kimwili, kihisia. Inaumiza kuona hawatambui thamani yako na unashindwa kuachikilia na kuishia kuwa na roho ya kutaka kulipa kisasi, uchungu, hasira, msongo wa mawazo na kujichukia. Lakini... Kupitia episode hii utaweza kuachil...

Uchambuzi Wa Kitabu Cha MONEY FORMULA (Kanuni Za Fedha)...! 24.01.2024

Elimu ya fedha isiyofundishwa shuleni wala vyuo vikuu imepelekea kushindwa kupiga hatua kwenye eneo la fedha. Kitabu cha MONEY FORMULA kinakupa mwongozo sahihi ni kwa namna gani unaweza kufanikiwa kifedha kupitia sheria, kanuni na mitazamo sahihi kuhusu fedha. Hakikisha unafanyia kazi ambayo unajifunza.

Uchambuzi Wa Kitabu Cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON (Tajiri Kutoka Babeli) Kwa Lugha Ya Kiswahili.. 21.01.2024

Unataka kufanikiwa kifedha na kuwa tajiri basi kitabu cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON kitakupa mwongozo na sheria za fedha. Uchambuzi wa sura 11 ambazo utapata kwenye episode hii. Hakikisha unaandika pembeni ambayo utajifunza rafiki.

Kwanini Unataka Kuongeza Au Kupunguza Maumbile Ya Mwili Wako...! 15.01.2024

Umekuwa na fikra kuwa ukiongeza au ukipunguza maumbile ya mwili wako basi utakuwa umekamilika na hautakuwa na kasoro hata kidogo si ndiyo? Basi Sikiliza episode hii ujifunze madhara ya kutaka kuongeza au kupunguza maumbile yako.

Uchambuzi Wa Kitabu Cha "BIRD BY BIRD" 11.01.2024

Ni kitabu mahususi kimeandikwa na Anne Lemmot ambacho utajifunza mambo mengi kuhusu uandishi wa vitabu na kuishi maisha yenye uhuru ndani yake. Hakikisha unaandika pembeni mambo ambayo utajifunza kupitia uchambuzi wa kitabu hiki kizuri cha BIRD BY BIRD yaani NDEGE KWA NDEGE. Katika uchambuzi wa kitabu hiki utajifunza sura tano ambazo mwandishi ametushirikisha kuhusu uandishi wa vitabu na ndani ya...

Sababu 06 Za Kwanini Unaweza Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2024 07.01.2024

Dakika 18 za kubadili kila kitu na uanze kuchukua hatua ili utimize malengo yako kwa kishindo. Utajifunza mambo 06 ili ufanikishe mwaka 2024 kwa matokeo chanya na mafanikip makubwa

Ufanye Nini Unapitia Hali Ya Kutoeleweka Katika Mapambano Au Utafutaji Wako?... 31.12.2023

Usijisikie vibaya kuona watu wa karibu au wa mbali hawaelewi wala hawapo tayari kukuelewa kuhusu mapambano yako. Inaumiza kuona watu ambao unawapenda na kuamini inaweza kuwa, 📌 Wazazi wako, Ulitegemea ndiyo wangekuwa watu wa kwanza kukuelewa na kuamini unachofanya na imekuwa tofauti wanakukosoa na kukalaumu kwanini unafanya hicho. 📌 Marafiki zako, Marafiki ambao umeshindana nao muda mwingi wanak...

Kabla Ya Kuingia Mwaka 2024 Hakikisha Unafanya Haya..! 17.12.2023

Umepanga kufanya maajabu mwaka 2024 na umejipanga vizuri kuanzia kupanga malengo yako, ndoto na maono yako. Lakini kuna vitu unapaswa kuzingatia kufanya leo hii kabla ya kuingia mwaka 2024. Utajifunza mambo 05 ambayo yatakusaidia kujua nini ufanye kabla ya kuingia mwaka 2024.

Jinsi Ya Kupata Nguvu Ya KIBALI Cha Kukubalika Machoni Pa Watu...! 11.12.2023

Unahitaji kukubalika kwenye jambo lolote basi unahitaji sana NGUVU YA KIBALI. Mahali popote hakikisha unaishi vizuri na watu ndiyo maana wahenga wanasema "Mtaji wa mtu ni watu. Ufanye nini upate nguvu ya kibali cha kukubalika machoni pa watu? Sikiliza episode hii mpaka mwisho. Share | Like | Comment | Ask

Namna Rahisi Ya Kujenga Uwezo Wa Kujiamini Na Ujasiri...! 03.12.2023

Zijue mbinu 07 za kuongeza uwezo wako wa kujiamini na mwenye ujasiri mkubwa kwa kushinda hofu, wasiwasi, uoga na kujitilia mashaka. Sikiliza episode hii mpaka mwisho na uwezo kujua mbinu za kuwa mtu mwenye kujiamini

ISHI KAMA KINYONGA....! 26.11.2023

Unajiuliza uishi kama kinyonga ni kwa namna gani si ndiyo? Ni kwamba unahitaji kuwa makini na kuishi kwa tahadhari kama kinyonga na watu wanakuzunguka hasa watu wa karibu yako. Hata wahenga wanasema “Adui hatoki mbali” Sikiliza dakika 9 zenye kukupa mwanga na mabadiliko kwenye Maisha yako. Ushindwe wewe tu rafiki.

Jinsi Kanuni Ya 80/20 Inavyokusaidia Kutoeleza Matatizo Yako Kwa Kila Mtu...! 18.11.2023

Hivi unajua asilimia 80% ya watu unawaeleza matatizo yako hawajali kabisa na asilimia 20% wanafurahi kuona matatizo hayo yanakupata wewe hapo. Kanuni ya 80/20 itakusaidia kuchuja nani wa kuwaeleza matatizo yako na wapi kutowaeleza. Unajiuliza ni kwa namna gani Kanuni hii inafanya kazi si ndiyo? Basi Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze

Sababu 05 Zinazofanya Watu Wakudharau...! 09.11.2023

Hakuna kitu kinaumiza kama watu kukudharau na kubeza uwepo wako si ndiyo? Dharau ina maana kwamba wanachukulia poa jambo au kitu fulani pasipo kukipa thamani inayostahili. Hivi unajua kwanini watu wanakudharau? Ukweli ni kwamba huwezi kuwa mwema na mzuri kwa kila mtu ila inakuwa inaumiza zaidi pale watu ambao umewapa nafasi kubwa kwenye maisha yako halafu wanakudharau. Inaumiza sana si ndiyo? Kuna...

Mambo 05 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kumpenda Mtu Kimahusiano Ya Kimapenzi....! 01.11.2023

Mahusiano siyo jambo la ulazima ila mahusiano ni jambo la utayari. Mapenzi siyo upofu, ila ni mtazamo wako Kuwa ni upofu wakati umepewa macho uone, akili ili uchanganue na hisia ili ujitathimini. Unajua nini uzingatie kabla ya kuingia/kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, basi sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze

Aina 10 Za Ujuzi Ambazo Zitakuingizia PESA (High Income Skills)...! 22.10.2023

Unataka kuingiza pesa na kujikwamua kiuchumi? Kama jibu lako ni ndiyo, basi episode hii inakufaa kwa sababu utaenda kujua aina 10 za Ujuzi ambazo zitakuingizia pesa ni wewe kuchagua Ujuzi mmoja au miwili kisha weka nguvu hapo baada ya mwaka mmoja hadi mitano utaona unaingiza pesa ni uthubutu wako tu. Sikiliza kwa umakini sana

Mjue Leo Mchawi Wa Mafanikio Yako Ndani Ya Dakika 11...! 09.10.2023

Hivi unajua kwamba wewe ni mtabiri wa maisha yako? Wahenga wanasema “Every human is magician” wakiwa na maana kila mtu ni mchawi Unajiuliza ni kwa namna gani? Sikiliza episode hii ujue mchawi wa mafanikio yako.

Ijue Nguvu Ya Mchakato..! 27.09.2023

Ukijua nguvu ya mchakato kwenye maisha yako utapata kuelewa upata kuhusu mafanikio, maendeleo, ukuaji, mabadiliko na kila kitu kinahitaji mchakato. Unataka kujua mchakato haupukeki ni lazima mchakato upitie. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue nguvu ya mchakato.

Mambo 05 Ya Kufanya Ili Ubadili Maisha Yako Kwa Asilimia 100%...! 22.09.2023

Kila mtu anataka kupata mabadiliko chanya ambayo yanafanya anapiga hatua na pengine hata wewe kuna mabadiliko ukifanya utaweza kupiga hatua. Swali la kujiuliza unajua ni mambo gani ufanye ili upate mabadiliko unayoyataka kwenye maisha Yako? Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze.

Kwanini Unahitaji Kusoma Kitabu Cha Sayansi Ya Malengo...! 13.09.2023

Kitabu cha sayansi ya malengo ni kitabu bora ambacho kitakusaidia Kutimiza Malengo yako mara 10X zaidi ya unavyotimiza sasa. Wasiliana na mimi 0674698347 kupata kitabu chako cha Sayansi ya malengo

Jinsi Ya Kuonyesha Kipaji Chako Hadi Kukupa Matokeo Makubwa...! 26.08.2023

Hivi unakijua kipaji chako au kikubwa ni uhai? Pasipo kujali unajua au hujui kipaji chako ila tambua una zawadi ya kipaji ambayo ulipewa na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwako. Kwahiyo... Kuzaliwa kwako Ina maana una kipaji ndani yako. Swali la kujiuliza. Je, unakijua kipaji chako? Hongera kwa kujua kipaji chako cha .... (Taja kimoyomoyo) Ina maana tayari umeshajua kusudi la kuzaliwa kwako. KIPAJI...

Namna Rahisi Ya Kunoa Kipaji Chako Na Kukupa Mafanikio Makubwa...! 18.08.2023

Kipaji ni kama msuli kadiri unavyofanya mazoezi ndiyo msuli unakuwa mkubwa na wenye nguvu si ndiyo? Basi episode hii utajua namna rahisi ya kunoa kipaji chako kiwe kikubwa na kukupa mafanikio makubwa...!

Listen to the Maisha Ni Kuthubutu Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.