SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 1027 epizód

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: www.sbs.com.au

Szerző

SBS

Kategória

News

A podcast weboldala

www.sbs.com.au

Legutóbbi epizód

2026. okt. 9.

Hol hallgathatod?

Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio Hamarosan

A podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz

Letöltés a Google Play-ről Telepítsd ingyen Android közel 10 M letöltés · 4,8-as értékelés iOS hamarosan

Epizódok

Taarifa ya habari:Nchi za Ulaya zajiandaa kutetea eneo la Denmark 20.01.2026

**Papa waendelea kuwashambulia watu huko Sydney ** Rais Donald Trump aendelea na mchakato wake wa kuchukua Greenland **Soko la Samaki la Sydney sasa limefunguliwa

Makala leo:Mkakati mpya wa usalama wa maji wazinduliwa 19.01.2026

Tangu kuanza kwa kiangazi, watu 33 wamepoteza maisha yao kutokana na kuzama maji huko Australia. Kwa kuwa kuzama maji kunatokea zaidi tangu Janga la COVID-19, Baraza la Usalama wa Maji la Australia limetoa Mkakati Mpya wa Usalama wa Maji wa Australia 2030, ambao unalenga kuimarisha juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya kuzama maji kwa asilimia 50 kufikia mwisho wa muongo huu.

Yaliyojiri Afrika:Upinzani wakataa matokeo ya uchaguzi Uganda 19.01.2026

Mwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Kwa habari ama maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Makala leo:jinsi ya kutambua na kuepuka ulaghai wa AI 16.01.2026

Utafiti mpya unaonyesha kwamba Waustralia wanaamini kupita kiasi juu ya uwezo wao wa kutambua ulaghai wa AI deepfake, hata teknolojia inavyoendelea kuwa ngumu zaidi kugundua. Wataalamu wanatahadharisha kwamba wadanganyifu wanaiba imani na hisia, na wanatoa wito kwa nyinyi kusimama, kuthibitisha na kukataa ujumbe unaotia shaka. Ikiwa mnadhani mngeweza kutambua ulaghai wa deepfake za AI papo hapo, h...

Yaliyojiri Afrika:kura zimeanza kuhesabiwa Uganda licha ya matatizo ya kiufundi hapo awali 16.01.2026

Kwa maelezo au habari zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.su/swahili.

Taarifa ya habari:tume ya kifalme ya kuchunguza hotuba za chuki yakosa uungwaji mkono 16.01.2026

** Kikundi cha Kiyahudi kinatoa wito wa mabadiliko na ucheleweshaji wa marekebisho ya hotuba za chuki za serikali... ** Angalau watu watano wameuawa katika mashambulio ya anga ya Israeli katika Ukanda wa Gaza ** Donald Trump ametishia kutuma wanajeshi kwenda Minneapolis ili kutuliza maandamano yanayoendelea juu ya matendo ya maafisa wa uhamiaji wa shirikisho katika Minnesota.

Taarifa ya habari:Kevin Rudd ajiuzulu kama balozi wa Australia nchini Marekani 13.01.2026

**Kevin Rudd ajiuzulu kama balozi wa Marekani... **Mlipo wa bomu waua maafisa wa polisi kaskazini mwa Pakistan... **Meta yazua shauku kuhusu Australia kuongeza umri wa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa habari ama maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Uganda yajiandaa kwa uchaguzi mkuu Alhamisi 12.01.2026

Mwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili kwa maelezo au habari zaidi.

Makala leo:utafiti unaonyesha miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi,hali inayochangia kaboni 12.01.2026

Utafiti mpya umebaini kuwa miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi kuliko inavyokua, hali ambayo inachangia ongezeko la utoaji wa kaboni. Utafiti huo, unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Western Sydney na kuchapishwa katika jarida la Nature Plants, umebaini kuwa miti katika aina zote za mifumo ya mazingira - kuanzia misitu ya mvua ya tropiki hadi misitu ya eucalypt - inapungua hali ya hewa inavyozidi...

Makala leo:Je,uangalizi wa ndege ni jambo maarufu miongoni mwa vijana sasa hivi? 12.01.2026

Mnapofikiria kutazama ndege, labda mnawazia wastaafu. Lakini kizazi kipya kinaanza kutumia darubini na kujihusisha na burudani hii. Kile kilichokuwa kimbilio kutoka ulimwengu wa mtandaoni sasa kinafufuka tena mtandaoni.

Taarifa ya habari:Tume ya kifalme yazinduliwa kuchunguza chuki dhidi ya wayahudi 09.01.2026

**WAZIRI MKUU ANTONY ALBANESE AZINDUA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA KESI ZA CHUKI DHIDI YA WAYAHUDI AUSTRALIA. **MAWIO YA MOTO YAWEKWA SEHEMU MBALIMBALI AUSTRALIA HUKU JOTO IKIZIDI KUONGEZEKA ** KIFO CHA MWANAMKE MAREKANI YAZUA UTATA.

Yaliyojiri Afrika:kapteni Ibrahim Traore anusurika jaribio jingine la mapinduzi 08.01.2026

Kwa habari au maelezo zaidi tembelea sbs.com.au/swahili.

Afya:wataalamu waonya dhidi ya madhara ya kuchanganya mipango mbalimbali ya lishe 08.01.2026

Mipango ya lishe kama vile Foodmap, yenye protini nyingi, isiyo na gluten, yenye mafuta kidogo, na kula chakula safi - kuna mipango mingi sana ya lishe, na ushauri unaokinzana. Wataalamu wa Australia wanaonya kwamba kufuata mipango mbalimbali ya lishe kwa wakati mmoja kunaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa.

Makala leo:wazazi wapata afueni baada ya serikali kupunguza gharama za vituo vya malezi ya watoto 08.01.2026

Wazazi wanaopeleka watoto kwenye vituo vya malezi wana uhakika wa kupata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu za wiki, bila kupitia mchakato wowote wa uthibitishaji. Ruzuku hii itagharimu karibu dola milioni 430 kwa kipindi cha miaka minne ijayo, lakini serikali inasema mamia ya maelfu ya familia zitafaidika.

Taarifa ya habari:Maduro na mkewe wakanusha mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha jijini New York 06.01.2026

** Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe walikana hatia katika mahakama ya Marekani. ** Mtu anayedaiwa kuwa mfyatuliwa wa risasi Bondi amehamishwa kwenda gereza la Goulbourn supermax. **Na Denmark yaendelea kuikashaifu Marekani kuhusu manoni yao ya Greenland.

Yaliyojiri Afrika:Ushahidi mpya waonyesha kuwepo kwa jeshi la Rwanda DRC 05.01.2026

Jason anatujuza yanayojiri pande mbali mbali Afrika, Kwa habari zaidi elekea kwa tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Nini kipya mwaka 2026? 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Ukosefu wa maji wawaathiri wakaazi wa Tanzania 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Waasi wa M-23 kujiondoa ili kusaidia juhudi za amani Congo 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Burundi kuanza kusafirisha madini nje ya nchi ili kuimarisha uchumi 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Wanafunzi 300 waachiliwa baada ya kutekwa nyara shuleni Nigeria 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Hatua ya Israel kuitambua Somali Land yazua utata 05.01.2026

Mwanahabari Jason Nyakundi atujuza yaliyojiri Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa mitandao yetu ya kijamii au tovuti yetu sbs.com.au/swahili

Makala leo:YWCA yapewa sifa kwa kuwasaidia wanawake Sydney 05.01.2026

Kukusanya fedha ili kupunguza makazi duni miongoni mwa wanawake ndiyo lengo la hoteli moja mjini Sydney, moja kati ya biashara elfu kumi na mbili ya kijamii nchini Australia zinazochanganya faida na lengo. Likizo za kiangazi ni wakati wenye mafanikio kwa maeneo mengi ya utalii. Lakini hoteli ya Song mjini Sydney inazingatia zaidi ya kutengeneza pesa. Inasaidia miradi ya makazi ya YWCA kwa wanawake...

Makala leo:China yaongeza ushuru kwa bidhaa za nyama ya ng'ombe 05.01.2026

Biashara ya nyama ya ng'ombe ya dola bilioni ya Australia inakabiliwa na mabadiliko makubwa kutokana na hatua ya China kuweka ushuru wa asilimia Hamsini na tano kwa uingizaji wa bidhaa zinazozidi vikomo vya kila mwaka vilivyowekwa kwa ukali. Wakati serikali ya China inadai kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakulima wake dhidi ya usambazaji usiokuwa na kipimo, viongozi wa sekta ya Australia na Upi...

Taarifa ya habari:Marekani yavamia Venezuela na kumkamata rais Maduro na mkewe 05.01.2026

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru shambulio kubwa dhidi ya Venezuela kuwakamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mke wake. Wametuhumiwa na makosa ya dawa za kulevya na silaha huko New York. Hatua hiyo imepongezwa na washirika wa Bw. Trump, lakini imelaaniwa sana na mataifa mengi.

Hallgasd a(z) SBS Swahili - SBS Swahili podcastot a Replaióban

Rádió és podcastok egy alkalmazásban - ingyen és regisztráció nélkül. Telepítsd még ma, és ne maradj le a premierről

Letöltés a Google Play-ről

A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.