Clifford Sangai

SportsCast

Sports SW ↓ 63 episodes

Clifford Sangai anaungana na wachambuzi mbalimbali kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.

Author

Clifford Sangai

Category

Sports

Podcast website

www.spreaker.com

Latest episode

Feb 19, 2025

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

EURO 2020: Namna Viungo walivyoamua mechi za nusu fainali 08.07.2021

Kama ulikuwa ukidhani 'Referee' ndiye mwamuzi pekee wa mechi basi alipata wasaidizi katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya EURO 2020. Wasaidizi hao si washika vibendera bali ni viungo wa timu zote nne; Italy, Spain, England na Denmark. Viungo hao walishiriki kwa sehemu kubwa timu zao kupata matokeo katika nusu fainali. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili ufanisi wa safu z...

EURO 2020: Kwanini timu nyingi zimetumia upande wa kushoto kufanya mashambulizi? 04.07.2021

Hatua ya robo fainali ya michuano hii ya EURO 2020 imekuja na mbinu mpya ambayo baadhi ya timu zimeitumia. Italy, England, Denmark, ni kati ya timu zilizotumia upande wa kushoto kufanya mashambulizi. Ni kwanini timu hizo zimetumia upande huo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujibu swali hilo. Pia tumeangazia mbinu nyingine zilizotumika katika hatua hii ya robo fainali. Tufuate kati...

Namna mabadiliko ya wachezaji yalivyoathiri mifumo ya timu katika raundi ya 16 bora 30.06.2021

Raundi ya 16 bora katika michuano ya EURO 2020 tumeshuhudia namna mabadiliko ya wachezaji yalivyoathiri mifumo ya timu mbalimbali. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia mabadiliko hayo pamoja na athari zake katika timu zote kwenye hatua hii. Tumeangazia mbinu zilizotumika katika mechi zote nane za hatua hii huku tukihusisha na takwimu ili kupima ubora wa nafasi zilizotengenezwa...

EURO 2020: Ubora na ufanisi wa mbinu za Makocha katika raundi ya tatu 24.06.2021

Raundi ya tatu ya michuano ya EURO 2020 imekua ya kuvutia kutokana na baadhi ya timu kusaka matokeo ili zifuzu katika hatua inayofuata. Makocha wametumia ufundi na mbinu zao ili kuhakikisha timu zao zinapata matokeo wanayohitaji. Mabeki wa kulia kutumika upande wa kushoto, mabeki wa pembeni kucheza kama mabeki wa kati ni kati ya mbinu zilizotumika katika raundi hii. Clifford Sangai anaungana na Pr...

EURO 2020: Mbinu gani zimetawala katika raundi ya pili? 20.06.2021

Mbinu mbalimbali za Makocha ndio zimeamua matokeo ya mechi nyingi katika raundi ya pili ya michuano ya EURO 2020. Lakini ubora wa mchezaji mmoja mmoja pia umesaidia kupata matokeo kwa timu fulani kama ambavyo George Job anavyoangazia ubora wa wachezaji katika kikosi cha Italia. Pia tumeungana na Geoffrey Lea kuangazia ubora wa mfumo wa kikosi cha England pamoja na mbinu za mwalimu Southgate. Unapo...

EURO 2020: Tulichojifunza katika mechi za raundi ya kwanza. 16.06.2021

Timu kutumia mfumo wa 3-4-3, mabadiliko ya mifumo, ubora wa Robertson ni kati ya mambo yaliyovutiwa watu wengi katika mechi za ufunguzi wa michuano hii. Lakini si hayo tu ambayo tunaweza kujifunza kutokana na mechi za kwanza kama ambavyo Prosper Bartalomew anavyochambua mechi zote 12 za kwanza. Tumegusia takwimu mbalimbali ili kupima ubora wa nafasi za magoli zilizotengenezwa katia raundi ya kwanz...

Ubora na Mapungufu ya kila kikosi kuelekea EURO 2020 05.06.2021

Vikosi vya timu zinazoshiriki EURO 2020 vimeshathibitishwa na kila kocha ametetea maamuzi yake. Je, unajua ni kwanini makocha wameamua kuita wachezaji fulani na kuwaacha wengine? Tumekuandalia majibu yote hayo. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili ubora wa kila kikosi kuelekea michuano ya EURO 2020. Tumeangazia timu zinazopigiwa upatu kutwaa taji hili kama Ufaransa, Ureno, Ubel...

Champions League: Tutarajie nini katika mechi ya fainali? 25.05.2021

Ikiwa ligi mbalimbali zimefika tamati barani Ulaya mashabiki na wapenzi wengi wa soka wanaisubiri kwa hamu mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Hii ni mara ya tatu kwa Chelsea kutinga katika hatua hii huku Manchester City ikiwa ni mara yao ya kwanza. Lakini tutarajie nini katika mechi hii ya kuvutia? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome kuchambua timu zote mbili zilizotinga...

Mambo usiyoyajua katika ligi kuu tano bora barani Ulaya msimu huu (2020/21) 21.05.2021

Timu gani imetengeneza nafasi zenye ubora wa hali ya juu msimu huu? Na ubora wa hizo nafasi unapimwaje? Hayo ni kati ya maswali ambayo wadau wengi wa soka wamekuwa wakijiuliza katika kipindi hiki ambacho takwimu mbalimbali zimekuwa zikitumika katika kupima ubora wa timu mbalimbali. Katika msimu huu wa mwaka 2020/21 timu nyingi barani ulaya zimeweza kuonesha ubora katika nyanja mbalimbali kwenye li...

Namna timu iliyopanda daraja inavyoweza kusalia katika ligi kuu (VPL) 13.05.2021

Tumeshuhudia timu nyingi zinazopanda daraja katika ligi kuu Tanzania bara (VPL) zikitetereka lakini vipi kuhusu timu ambazo hazitetereki katika msimu wa kwanza VPL? timu nyingi zinazopanda daraja katika ligi kuu Tanzania bara (VPL) zikitetereka lakini vipi kuhusu timu ambazo hazitetereki katika msimu wa kwanza VPL? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Thierry Hitimana aliyewah...

Namna umahiri wa Conte ulivyoipaisha Inter Milan 07.05.2021

Mafanikio ambayo klabu ya Inter Milan imeyapata msimu huu yanatokana na mipango ya muda mrefu ya uongozi wa klabu hiyo iliyo chini ya kampuni ya Suning. Kati ya uamuzi bora uliofanywa na klabu hiyo ni kumpa kibarua Antonio Conte cha kukinoa kikosi cha timu hiyo. Conte alianza kibarua hicho huku akipata changamoto mbalimbali za kiufundi kutokana na kukosa wachezaji kadhaa kutoendana na falsafa yake...

Champions League: Tutarajie nini katika mechi za marudiano nusu fainali? 29.04.2021

Nusu fainali ya UEFA imekua ya kusisimua zaidi katika raundi ya kwanza huku ikiacha maswali mengi ya kimbinu. Je, Zidane atarudi kwenye mfumo wake wa 4-3-3 aliouzoea ama atasalia na 3-5-2 dhidi ya Chelsea? Kikosi cha PSG kitakuwa na sura gani kitakapomkosa kiungo Idrissa Gueye katika mechi ya marudiano? Hayo ni kati ya maswali ambayo tumeyajadili kwa kina huku tukijumuisha mbinu za makocha wote wa...

Mbinu anazotumia Solksjaer katika safu yake ya ushambuliaji 22.04.2021

"Ubora wa kocha ni pamoja na kujua mapungufu yako"- Geoffrey Lea Solksjaer ameonekana kuwa katika safari ya mafanikio tangu alipopata kibarua cha kuinoa Manchester United. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Geoffrey Lea kujadili ubora na mapungufu ya safu ya ushambuliaji katika kikosi cha Manchester United. Tumeangazia pia mchango wa mabeki wa pembeni kama Luke Shaw na Wan B...

Siri ya mafanikio ya Simba katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika 14.04.2021

Safari ya Simba SC. kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika imekua yenye mafanikio, lakini nini sababu ya mafanikio hayo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Charles Abel kujadili mbinu zilizotumika na klabu ya Simba Pia tumeangazia mchango wa kimbinu Kocha Didier Da Rosa na namna anavyowatumia wachezaji mbalimbali kikosini. Tumechambua ubora na mapungufu ya safu ya uli...

Sababu zinazopelekea mshambuliaji kupoteza ufanisi mbele ya goli 09.04.2021

"Striker hupimwa kwa magoli" ni msemo uliozoeleka kwa mashabiki wengi wa mpira wa miguu, lakini itakuwaje kama mshambuliaji atapoteza ufanisi mbele ya goli? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa na Klabu ya Yanga Ally Mayay Tembele kujadili sababu zinazopelekea kupungua kwa ufanisi wa washambuliaji. Tumeangazia kwa undani mwenendo wa wachezaji...

Ni Cristiano Ronaldo ama Andrea Pirlo? 30.03.2021

Nani anapaswa kulaumiwa kwa mwenendo wa sasa wa Juventus? Je uamuzi wa kumchagua Andrea Pirlo kukinoa kikosi cha Juve ulikuwa sahihi? Cristiano Ronaldo anafiti kwenye Falsafa za Andrea Pirlo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Mchambuzi George Job kuangazia kwa kina matatizo yanayoisibu klabu ya Juventus. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscastt...

Nini suluhu ya matatizo yanayoikumba Yanga? 05.03.2021

Matatizo ya umaliziaji na Timu kukosa muunganiko ni kati ya matatizo makubwa yanayoikumba klabu ya Yanga chini ya kocha Cedric Kaze. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina matatizo hayo na namna ya kuyatatua. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Namna Mbappé na Haaland wanavyojitengenezea ulimwengu wao wa soka 26.02.2021

Wengi wamehusishwa kurithi ufalme wa Lionel Messi na Christiano Ronaldo lakini hawakuweza kufikia kiwango chao. Je, Kylian Mbappé na Erling Braut Haaland wataweza kufikia kiwango cha Messi na Ronaldo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili namna makinda hawa wanavyotengeneza ulimwengu wao wa soka. Tunaangazia zaidi takwimu za mchezo na namna wanavyosaidia timu zao kuweza kupata m...

Je, Diego Simeone amebadili falsafa yake? 19.02.2021

Diego Simeone amezoeleka kwa aina ya soka la kukaba na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ila kwa sasa hali ni tofauti. Ongezeko la asilimia za umiliki wa mpira (Ball Possession) na mabadiliko ya 'formation' ni kati ya vitu vinavyowashangaza wengi kuhusu Atletico Madrid iliyo chini ya Diego Someone. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama kocha Diego Simeone amebadili falsafa...

Matatizo ya kimbinu yanayoikumba Liverpool 11.02.2021

Kukosekana kwa Van Djik kumemfanya Jurgen Klopp kubadili mbinu mbalimbali ili kuweza kukabiliana na pengo hilo. Mabadiliko hayo ya mbinu yamepelekea matatizo mengi kuanzia safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome kujadili matatizo mbalimbali ya kimbinu yanayoikumba Liverpool chini ya Klopp. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sp...

Guardiola amefanya mabadiliko gani baada ya kuanza msimu vibaya? 02.02.2021

"Tulikua hatuchezi vizuri kwa sababu tulikua tunakimbia sana, kwenye mpira unabidi ukimbie kwa kiasi na kwa muda maalum" - Pep Guardiola. Manchester City ya sasa ni tofauti na ile ya mwanzo wa msimu huu wa 2020/21, mengi yamefanywa ili kuweza kupata ubora wa kikosi hicho kwa sasa. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia mabadiliko ambayo Pep Guardiola ameyafanya ili kuirudisha ti...

Namna Stefano Pioli alivyoibadili AC Milan 26.01.2021

Stephano Pioli ameifanya AC Milan kutoa ushindani katika ligi kuu nchini Italia maarufu kama 'Serie A' Uzoefu wake katika ligi hiyo umemuwezesha kuiongoza AC Milan kucheza mechi 29 bila kupoteza mchezo wowote. Tumeangazia mbinu alizotumia kuifanya AC Milan kucheza soka la kasi na lenye kuvutia zaidi. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitte...

Kufeli na kufaulu kwa safu ya viungo wa Chelsea chini ya Lampard 12.01.2021

Chelsea mara nyingi imekua ikipata magoli kwa kutegemea mipira ya krosi ambazo hupigwa na mawinga au mabeki wa pembeni. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew na Barnabas Gwakisa (Mr. Darajani) kujadili kufaulu na kufeli kwa safu ya viungo wa Chelsea chini ya Kocha Frank Lampard. Mfumo wa 4-3-3, nafasi anayopaswa kucheza Ngolo Kante, umuhimu wa Jorginho na ubora wa Kai Havertz ni kati ya...

Nini kinamfanya Meddie Kagere kuwa hatari zaidi mbele ya goli? 05.01.2021

Umri ni namba, shughuli dimbani na Meddie Kagere tangu ametua katika ardhi ya Tanzania ameweza kuonesha shughuli nzito awapo uwanjani. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome pamoja na Michael Mwebe kuchambua kwa kina aina ya soka ambalo Kagere hucheza pamoja na uwezo na mapungfu yake. Tumeenda mbali zaidi kwa kuangazia historia yake, umuhimu wake katika kikosi cha Simba na kulinganisha uwe...

Wachezaji wanaofanya vizuri ligi kuu Tanzania Bara 26.12.2020

Katika mzunguko wa kwanza wa VPL wachezaji mbalimbali wameonesha umaridadi wao katika nafasi mbalimbali wanazocheza uwanjani. SportsCast imekuandalia orodha ya wachezaji watano (5) ambao kwa nafasi zao wameweza kuonyeshe ubora wa kimbinu na kuweza kusaidia katika falsafa za makocha wao. Orodha hii inahusisha wachezaji kama; Prince Dube, Edward Manyama, Adam Adam, Mukoko Tonombe na Clatous Chama. S...

Listen to the SportsCast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.