Clifford Sangai

SportsCast

Sports SW ↓ 63 episodes

Clifford Sangai anaungana na wachambuzi mbalimbali kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.

Author

Clifford Sangai

Category

Sports

Podcast website

www.spreaker.com

Latest episode

Feb 19, 2025

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Makosa ya Makipa katika Ligi Kuu Tanzania Bara 19.02.2025

Katika ulimwengu wa soka, kipa anaweza kuwa shujaa au mhanga wa lawama kwa sekunde chache tu. Goli linaweza kuwa matokeo ya shambulizi lililopangwa kwa ustadi, lakini mara nyingi, kosa la kipa linatosha kuamua hatma ya mchezo. Je, unakumbuka mechi yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kosa la kipa lilibadili mwelekeo wa matokeo?

Washambuliaji wawili, mawinga wenye kasi na namba 10 31.08.2022

Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili. Matumizi ya washambuliaji wawili Timu kuhamia back-four Mawinga wenye speed Singida Big Star Aziz Ki vs Chama Sikiliza episode hii kuyajua yote hayo kisha tupe maoni yako  

Chelsea ya Thomas Tuchel 03.06.2022

Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG. Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina falsafa za raia huyo wa Ujerumani. Miongoni mwa yaliyoongelewa ni kama Tuchel anaweza badili mfumo au atasalia na wa sasa? Kitendawili cha Havertz, Werner na Lukaku bila kusahau...

Mwaka mmoja wa Nabi: Mbinu na Ufundi 06.05.2022

Ni mwaka mmoja sasa tangu Nasreddine Nabi achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga kutoka kwa Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wake. Kuna mambo mengi ameyabadili katika kikosi hicho ambayo Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanayajadili katika episode hii. Kati ya hayo ni kumfanya kiungo Feisal Salum kucheza katika eneo la mbele zaidi kuliko alipokuwa akicheza hapo awali. Swala la muhi...

Taifa Stars ya Kim Poulsen 06.04.2022

Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili hayo yote bila kusahau aina ya wachezaji ambao Kim hapendi kuwakosa kwenye timu. Je ni wachezaji gani hao? Sikiliza Episode hii hadi mwisho

Je, Carlo Ancelottii amebadilika? 22.03.2022

Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo kwa kipindi kirefu? Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadiliana kuhusu falsafa, mbinu na ufundi wa kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real M...

Falsafa ya Marcelo Bielsa 08.03.2022

Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina mbinu na ufundi wa raia huyo wa Argentina. Tumeongelea aina yake ya ukabaji ambayo ni 'MAN TO MAN" tukiangazia kwa kina namna ilivyofaulu na kufeli...

Kwanini kiwango cha Lukaku kimeshuka? 22.02.2022

Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na assists 11 akiwa na klabu ya Inter. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni mifumo ya Chelsea, Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji. Prosper ameenda mbali zai...

Mikimbio ya Washambuliaji wa Simba SC 01.02.2022

Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli? Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kuchambua kwa undani mikimbio ya washambuliaji wa Simba yaani Kagere, Mugalu na Bocco Usisite kushea na marafiki Episode hii Pia unaweza kupakua majarida yetu BURE kuhusu AFCON: https:...

Arsenal: 'Pattern' ya ushambuliaji 11.01.2022

Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka.  Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongeza ili kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji.  Tumegusia pia patnership ya Xhaka na Partey inavyowasaidia katika kufanya mashambulizi. Katika episode hii tumegusia mbinu za Mikel Arte...

Kufeli na kufaulu kwa Viungo wa Simba na Yanga 14.12.2021

Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo. Tumeangazia eneo moja muhimu sana kwa timu zote mbili nalo ni Safu ya Viungo ambapo kila timu imeonesha ubora na madhaifu yake na kama yanaweza kusahihishwa. Unataka kujua madhaifu hayo...

Azam FC: Msimu mpya mambo yale yale 09.12.2021

Msimu mpya huu, unaona mabadiliko yoyote ndani ya kikosi cha Azam FC? Swali hilo ndio limemfanya Clifford Sangai aketi chini pamoja na Prosper Bartalomew kujadili mambo mbalimbali hususani ya kimbinu katika kikosi cha Azam FC. Tumeangazia namna timu inavyojilinda hadi inavyoshambulia huku tukilinganisha na msimu uliopita. Hatujaangazia mechi za Ligi Kuu Tanzania bara tu bali michuano yote ambayo A...

Manchester United Special 29.11.2021

Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina wapi Ole Gunnar Solskjær alikwama kimbinu, tumezichambua kwa kina mbinu za raia huyo wa Norway kwa kuzingatia washindani wake kimbinu. Pia tumegusia mambo ambayo kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameyabadili katika kikosi hicho kwa muda mfupi aliopo. Wakati tunarekodi episode hii dili la Manchester United, Lokomot...

Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 2 07.11.2021

Huu ni mwendelezo wa pale tulipoishia katika episode iliyopita lakini mwendelezo huu ni wa kipekee zaidi. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuchambua mbinu na ufundi katika Ligi Kuu Tanzania Bara maarudu kama NBC Premiere League. Tumeangazia mwenendo wa timu nyingi zinapokutana na Yanga zimekuwa zikijaza wachezaji wengi katika eneo la kiungo (Midfield overload) je kuna faida yoyote i...

Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 1 22.10.2021

Bado unaamini Ligi Kuu Tanzania bara haina mbinu? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu za makocha mbalimbali na ufundi wa wachezaji katika Ligi Kuu ya NBC. Je kocha wa Yanga ameshaonesha mfumo wake rasmi katika kikosi chake? Ipi ni nafasi inayomfaa Bwalya awapo uwanjani? Hayo ni kati ya maswali tuliyojadili bila kusahau ubora wa Chirwa na Lusajo na mabadiliko ya kimfumo k...

Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 2 11.10.2021

Kila siku makocha katika vilabu mbalimbali barani Ulaya wamekuwa wakitafuta kila namna ya kuweka vikosi vyao sawa na kuhakikisha falsafa zao zinaonekana vizuri. Ili kuhakikisha hayo yote yanatimia basi tumekuwa tukishuhudia mbinu mbalimbali za soka na hapo ndipo Clifford Sangai anapoketi na Prosper Bartalomew kuchambua timu mbalimbali pamoja na mwenendo wa timu hizo. Tumeangazia mabadiliko aliyoya...

Martin Ødegaard ni suluhu kwa matatizo ya Arsenal? 23.09.2021

Tuliwahi kuongelea kuhusu kukosekana kwa kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Arsenal kwenye Podcast hii. Sasa Arsenal chini ya Arteta imemsajili kiungo Martin Ødegaard kutoka Real Madrid. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama Ødegaard ataleta ahueni katika eneo la kiungo mshambuliaji. Ødegaard aliweza kuwashawishi mashabiki kipindi yupo kwa mkopo? Takwimu zake zinasemaje...

Tofauti ya Joshua Kimmich na Trent Alexander-Arnold 20.09.2021

"Kwanini umchezeshe beki bora wa kulia duniani katika nafasi ya kiungo?" - Jürgen Klopp Kumeibuka maswali mengi sana tangu kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alipomtumia beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama kiungo katika mechi dhidi ya Andorra huku wengine wakijaribu kumfananisha beki huyo na Joshua Kimmich. Clifford Sangai amekaa chini na Prosper Bartalomew kuch...

Soka Langu: Francis Baraza 13.09.2021

Katika mfululizo huu mpya wa episodes za 'Soka Langu', tutaongelea maswala ya mbinu na aina ya soka la wachezaji pamoja na makocha mbalimbali. Clifford Sangai anakaa chini na Prosper Bartalomew pamoja na Francis Baraza, kocha wa timu ya Kagera Sugar kujadili aina na mbinu za soka ambazo amekuwa akizitumia. Baraza anatupitisha katika safari yake ya ukocha tangu akiwa katika klabu ya Biashara United...

Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 1 04.09.2021

SportsCast imekuandalia uchambuzi wa ligi kuu tano bora barani ulaya tukiangazia hasa mechi za awali kabla ya mapumziko kwa ajili ya timu za taifa (International Break) Kama kawaida Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kudadavua mbinu za makocha mbalimbali na Wachezaji walioonesha viwango katika hatua za awali. Tumegusia mbinu ya Manchester city ilivyofeli katika mechi za mwanzoni kabis...

Je, Tottenham na Manchester City zinaweza kucheza bila mshambuliaji wa kati? 18.08.2021

Pep Guardiola amekuwa na mtindo kwa kucheza bila mshambuliaji wa kati katika mechi nyingi. Nini sababu ya maamuzi hayo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama timu inaweza cheza msimu mzima bila kuwa na mshambuliaji wa kati. Tumetumia klabu ya Tottenham Hotspur na Manchester City kama mfano tukiangazia mbinu za makocha wa klabu hizo. Umuhimu wa Harry Kane kwa Spurs hususani...

Namna Utatu wa PSG utakavyoweza kutimiza ndoto za Klabu hiyo 14.08.2021

Timu zilizopata mafanikio zaidi zimekuwa zikitumia washambuliaji watatu eneo la mbele na mara nyingi mfumo unaotumika 4 3 3. Tumeshuhudia utatu wa BBC (Bale, Benzema na Christiano) katika klabu ya Real Madrid, pia utatu wa MSN (Messi, Suarez na Neymar) wakati wapo Barcelona, bila kusahau utatu wa Liverpool wenye Salah, Firmino na Mane. Lakini je nini siri ya Utatu wa timu hizi kuweza kupata mafani...

Mwenendo wa Usajili katika Ligi Kuu Tanzania Bara 08.08.2021

Kuna madhara au faida gani timu inaposajili wachezaji wengi kutoka katika taifa moja?,Je makocha wana mchango gani wakati wa dirisha la usajili kwenye vilabu vyetu? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Michael Mwebe kuangazia kwa undani mwenendo wa usajili katika Ligi Kuu Tanzania Bara ili kujibu maswali hayo hapo juu na mengine mengi. Tumeangazia kwanini vilabu vyetu vimekuwa...

VPL: Mbinu zilizotawala katika msimu wa 2020/21 24.07.2021

Tumeshuhudia mambo mengi sana katika ligi kuu Tanzania bara lakini sisi SportsCast tumeamua kukuletea uchambuzi wa mbinu zilizotawala katika msimu huu. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu mbalimbali za makocha wa vilabu vya soka katika ligi kuu. Tumeangazia ubora wa wachezaji katika kila nafasi tukianza na magoli kipa hadi washambuliaji wa kati. Tumegusia namna timu mbal...

EURO 2020: Mabadiliko ya kimbinu na athari zake katika mechi ya fainali 12.07.2021

Gareth Southgate alianza mechi ya fainali ya EURO 2020 na mfumo wa mabeki watatu lakini katika dakika ya 70 alibadili kwenda mfumo wa mabeki wanne. Tangu michuano hii ianze Southgate ametumia mifumo miwili tu; 3-4-3 na 4-2-3-1huku kila mmoja ukiwa na faida na hasara zake. Lakini mabadiliko ya kimbinu katika mechi ya fainali dhidi ya Italy yalileta madhara gani katika kikosi cha England? Clifford S...

Listen to the SportsCast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.