RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

Sports SW ↓ 24 episodes

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.

Author

RFI Kiswahili

Category

Sports

Podcast website

www.rfi.fr

Latest episode

Jul 4, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Kombe La Dunia 2026: Raundi ya 32 yakamilika, Morocco na Misri zafuzu 16 bora 04.07.2026

Tuliyokuandalia leo ni mkusanyiko wa matukio ya raundi ya 32, je ni wakati timu changa kuanza kutamba? Timu mbili tu za Afrika kati ya tisa zafuzu kumi na sita bora, nini kimeiponza Afrika? uchambuzi wa raundi ya 16 bora inaanza leo, kiatu cha dhahabu na mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17. Yanga yashinda ubingwa wa Tanzania kwa mara ya 32 huku DRC ikifuzu raundi ya pili...

Kombe la Dunia 2026: Timu saba za Afrika zafuzu hatua ya muondoano 27.06.2026

Hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia inafikia kilele hii leo, ni timu gani zimefuzu hatua ya mtoano? Wiki ya pili ya michuano hii imeshuhudia rekodi zikiwekwa na kuvunjwa huku mataifa ya Afrika yakiendelea kufanya vizuri zaidi, lakini pia tutakupa uchambuzi wa mechi za kesho asubuhi. Aidha tumeangazia michuano ya Afrika Mashariki mchezo wa Baseball, tetesi za uhamisho na mashindano ya Paris Diam...

Wiki ya kwanza Kombe la Dunia 2026. Matokeo na Matukio yaliyojiri 20.06.2026

Leo tumeangazia kwa undani matukio na matokeo yote ya wiki ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia 2026 - Mbappe, Messi waweka historia wakati Cape Verde na DRC zikihangaisha miamba wa soka wa ulaya, Tunisia yamfuta kazi kocha, uchambuzi wa mechi za leo. Aidha ni mwaka mmoja kuelekea Kombe la Mataifa ya Africa 2027, matokeo ya tenisi kombe la Davis Cup, Police fc ya Rwanda yamfuta kazi kocha wake, ma...

Kombe la Dunia laanza likitatizika kuwasha msisimko Marekani, Mexico na Canada 13.06.2026

Tumeangazia Kombe la Dunia 2026 kuanza kwa vikwazo kadhaa, raia wa Afrika waiunga mkono Mexico dhidi ya Afrika Kusini, uchambuzi wa mechi ya leo Brazili dhidi ya Morocco, DRC wakijiandaa kupambana na Ureno wiki ijayo, maandalizi ya mbio za Kigali Marathon zakamilika, klabu ya Gor Mahia nchini Kenya yaamrishwa kufanya uchaguzi upya, 

Siku Tano tu kuelekea Kombe la Dunia: Mambo muhimu ya kufahamu 06.06.2026

Tuliyokuandalia leo ni mambo muhimu ya kufahamu kuelekea Kombe la Dunia, timu ya Iran na mwamuzi wa Somalia hatimaye wapokea visa zao, namna mataifa ya Afrika yamecheza kwenye mechi za kirafiki kuelekea Kombe la Dunia, Riquelme na Florentino kupambania urais wa Real Madrid, Kenya kuandaa Davis Cup, kocha wa Kenya ajitetea baada ya sare dhidi ya Lesotho, tuzo za Ligi Kuu Kenya, kocha Flaurent Ibeng...

Arsenal yashinda ubingwa wa Uingereza baada ya miaka 22, Fainali za BAL zikianza 23.05.2026

Leo tumeangazia Arsenal kushinda ubingwa wa Ligi Kuu baada ya miaka 22, kocha wa Uingereza Tuchel azomewa kuwaacha nje wachezaji kadhaa, kocha wa DRC Desabre ataja kikosi cha Kombe la Dunia, Aston Villa yashinda Kombe la Europa, Droo ya kufuzu michuano ya AFCON 2027 yakamilika huku AFCON U17 ikiendelea, fainali za BAL zaanza Kigali, Kipchoge kukimbia marathon ya kwanza Afrika, Motsengo Omba ashind...

Michezo kwenye mkutano wa Africa Forward Summit, Ghana yakosolewa mpangilio duni 16.05.2026

Leo tunaangazia baadhi ya matukio ya michezo yaliyozungumziwa kwenye mkutano wa Africa Forward Summit uliokamilika hiki hii, uchambuzi wa Ghana kukosolewa kuandaa mashindano duni ya Afrika ya riadha, Al Hilal ya Sudan yatwaa ubingwa wa soka Rwanda, Motsengo Omba akizindua nguzo zake tano za uongozi wa Fecofa, fainali ya Kombe la Shirikisho, Afcon U17 yaanza huko Morocco, mataifa yaanza kuzindua vi...

Ni kwa nini Young Africans imemfuta kazi kocha Pedro Goncalves? 09.05.2026

Tuliyokuandalia leo ni kufutwa kazi kwa kocha wa Yanga Pedro Goncalves, wawaniaji wengine wawili wajiondoa uchaguzi wa urais DRC, mashindano ya magari ya Africa yangoa nanga nchini Uganda, fainali ya Kombe la Shirikisho mkondo wa kwanza kupigwa leo usiku, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 20, FIFA imetoa orodha ya wasanii wa kutumbuiza mechi za ufunguzi Kombe la Dunia, Ars...

FIFA Series: Kenya ni mwenyeji wa michuano hii ya kwanza kabisa ya kina dada 11.04.2026

Leo tumeangazia mashindano ya kwanza kabisa ya kina dada ya FIFA Series inayoandaliwa nchini Kenya, timu tano zimetinga mchujo wa ligi kuu, ziara ya rais wa CAF Motsepe nchini Senegal, ligi ya mabingwa Afrika yaingia hatua ya nusu fainali, kocha Aliou Cisse atua nchini Angola, michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17, droo ya Afcon U17, michuano ya shule za upili za Afrika...

DR Congo wafuzu Kombe la Dunia, Wanyama astaafu soka, Ghana yafuta kocha 04.04.2026

Leo tumeangazia kufuzu kwa DRC michuano ya kombe la dunia tukiwa na mgeni wetu Felly Mulumba, mchezaji wa soka kutoka DRC, Ghana yamfuta kocha Otto Addo, mageuzi katika kamati andalizi ya AFCON 2027 nchini Kenya, Tigers na Petro de Luanda zafuzu fainali ya BAL, Algeria mabingwa wa basketboli ya vitimagu Afrika, kustaafu kwa Victor Wanyama huku ligi ya Kenya ikilenga kuwa bora Afrika, je De Zerbi a...

Senegal yakataa rufaa rasmi, msimu mpya wa BAL waanza, FIFA Series yashika moto 28.03.2026

Leo kwenye jukwaa tumeangazia rufaa ya Senegal kwa mahakama kuu ya spoti, ripoti ya CAF yasema Afrika Mashariki haipo tayari kuandaa Afcon 2027, Afrika Kusini na Kenya zafuzu Kombe la Dunia la gofu ya chipukizi, ripoti maalum ya FIFA Series mjini Kigali, mashindano ya KipKeino Classic yapata sura mpya, ni kwa nini Djigui Diarra amepigwa marufuku ya mechi tatu nchini Tanzania?, vikwazo vipya vya Ma...

Senegal yavuliwa ubingwa wa Afrika, Kenya na Ufaransa zashirikiana kwenye tenisi 21.03.2026

Leo kwenye kipindi tunaangazia hisia za baada ya Caf kuivua Senegal ubingwa wa Afrika, kwenye tenisi Kenya na Ufaransa zimeingia kwenye ushirikiano, hatma ya Kenya kaundaa Afcon 2027, FIFA yaweka vikwazo kwa Nigeria na DRC, robo fainali ligi ya klabu bingwa Afrika kuanza leo, DRC yashindwa ubingwa wa dunia kwenye basketboli ya vitimagu, ushirikiano wa FIFA na YouTube, Ronaldo kukosa mechi za kiraf...

Mashindano ya dunia ya kukimbiza Magari-Kenya Safari Rally yapamba moto Naivasha 14.03.2026

Mashindano ya dunia ya kukimbiza Magari, Kenya Safari Rally, yanaendelea kushika kasi mjini Naivasha ambapo madereva mbalimbali duniani, wanachuana kutafuta ubingwa. Nani ataibuka bingwa ?

Regragui aondoka Morocco huku CAF ikiahirisha AFCON ya kina dada 07.03.2026

Kwenye kipindi cha leo tumeangazia kuondoka kwa kocha mkuu wa Morocco Walid Regragui, Burkina Fason yapata kocha mpya, athari ya kuahirishwa kwa michuano ya WAFCON, vikwazo vya CAF dhidi ya Al Ahly, Faith Kipyegon aorodheshwa kwa mara ya tatu kuwania tuzo ya dunia ya Laureus. FIFA yatangaza sheria mpya za soka kuelekea Kombe la Dunia. Fred Kerley apigwa marufuku ya miaka miwili. Je, ni suala la mu...

Gofu: Mkenya Njoroge Kibugu afuzu mchujo wa Magical Kenya Open 21.02.2026

Mkenya Njoroge Kibugu alifuzu mchujo wa mashindano ya dunia ya gofu ya Magical Kenya Open wakati mnyarwanda Celestin Nsazuwera akiweka historia, uchambuzi wa droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, mashindano ya wanawake ya COSAFA, wakenya wang'ara katika michuano ya fencing ya Afrika, TFF yafungua zabuni ya haki za kamari katika debi la kariakor, Fifa kufadhili ujenzi wa viwanja vya soka huko Pa...

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 zitafanyika Juni-Julai 14.02.2026

Leo tumeangazia CAF kudhibitisha kuwa AFCON 2027 itaandaliwa Afrika Mashariki licha ya tetesi za kuahirishwa au kuhamishwa, uchambuzi wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi mechi za klabu bingwa, mechi za kufuzu kombe la dunia la wasichana U20, siku ya kwanza ya michuano ya raga ya wachezaji saba kila upande divisheni ya pili ya HSBC, mfumo mpya wa mashindano ya Tour du Rwanda, kiungo wa Ghana Th...

Yanga yalenga ushindi muhimu kukaribia robo fainali michuano ya klabu bingwa 07.02.2026

Leo tumeangazia mechi za klabu bingwa Afrika, Yanga itachuana na FAR Rabat nayo Azam ikicheza na Maniema, matukio kuelekea michuano ya gofu ya Magical Kenya Open, mechi za kufuzu kombe la dunia la kina dada chini ya miaka ishirini, rais wa soka DR Congo asimamisha shughuli zote katika uwanja wa Tata Raphael, Rais wa FIFA Infantino asema marufuku dhidi yz Urusi hayajasaidia chochote, mzozo kati ya...

Uamuzi wa CAF kwenye fainali ya Afcon 2025: Udhibiti wa Haki au Uharibifu? 31.01.2026

Leo tumeangazia kwa undani hukumu na uamuzi wa Caf kufuatia matukio yaliyoibuka kwenye fainali ya AFCON 2025, Simba inajandaa kwa mechi ya kufa kupona kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, raundi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mechi za Futsal yakamilika, msimu wa sita wa Ligi ya Afrika ya basketboli kumalizia nchini Rwanda, Faith Kipyegon ajenga hospitali huko Kenya, TP Mazembe yapata ko...

CAF: Michuano ya klabu bingwa Afrika imerejea raundi ya tatu ya makundi 24.01.2026

Leo kwenye kipindi tumeangazia uchambuzi wa mashindano ya AFCON 2025, vilabu vya Afrika Mashariki vinatafuta tiketi ya mchujo mechi za klabu bingwa, Kinshasa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Voliboli mwaka huu, wachezaji kadhaa wa ligi ya NBA waonesha nia kuiwakilisha Nigeria kwenye Olimpiki ya 2028, mashindano ya Afrika ya handboli inayoendelea Kigali, Uganda yapata kocha mpya wa basketboli,...

AFCON 2025: Senegal, Morocco zatinga fainali. Je, nusu fainali ziliendaje? 17.01.2026

Leo tumeangazia pakubwa uchambuzi wa matukio na matokeo ya mechi za nusu fainali mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na mechi ya mshindi wa tatu leo usiku, hotuba ya rais wa CAF Patrice Motsepe kabla ya fainali, Droo ya mashindano ya WAFCON ya kina dada ya mwaka huu, Rwanda kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika ya Handboli, Rwanda na Burkina Faso zafuta kazi makocha wao.

AFCON 2025: Mbio za kuwania kufuzu kwa nusu fainali zinazidi kupamba moto 10.01.2026

Leo tutakufahamisha matukio yote kwenye raundi ya 16 bora, uchambuzi wa mechi haswa kuondolewa kwa DRC na Tanzania walivyolakiwa kishujaa nyumbani Dar es Salaam baada ya kutoka Morocco na uchambuzi wa mechi za robo fainali za jana na leo. Morocco na Senegal washajikatia tiketi ya nusu fainali. Algeria dhidi ya Nigeria na Misri dhidi ya Ivory Coast. 

Uchambuzi wa Mada: Je, AFCON 2025 inatoa msisimko kama mashindano yaliyopita? 04.01.2026

Leo tunajadili kwa undani kauli ya kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos kuwa michuano ya mwaka huu haina mvuto na msisimko kama Afcon zilizopita. Uchambuzi wa mechi za jana na leo kwenye hatua ya 16 bora - Tanzania vs Morocco, Afrika Kusini vs Cameroon, DRC vs Algeria. Hatua ya serikali ya Gabon kuvunjilia mbali timu ya Gabon huku marais wa Msumbiji na Benin wakitoa ahadi za pesa kwa timu zao. Moroc...

AFCON 2025: Mtazamo wa hatua ya mtoano, timu 16 zitawania tiketi ya fainali 03.01.2026

Leo tumeangazia kwa undani matokeo na matukio ya hatua ya makundi iliyokamilika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea Morocco, uchambuzi wa hatua ya 16 bora - nani atafuzu robo fainali?, tathmini ya hatua ya serikali ya Gabon kuvunja kabisa timu ya taifa ya Gabon, ahadi za pesa kutoka kwa marais kadhaa Afrika kwa timu zao kuelekea robo fainali, usajili wa Rayon Sport, kwa nini...

AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku 21.12.2025

Leo tunaangazia pakubwa kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025; tunachambua mechi ya ufunguzi kati ya Morocco na Comoros, mjadala kuhusu mageuzi katika michuano hii, namna timu zilivyotua nchini Morocco kwa kuvalia mavazi ya kitamaduni, Morocco wapo kwenye shinikizo ya kunyakua ubingwa kwa kuwa mwenyeji lakini pia ubashiri wa mechi ya ufunguzi na atakayebeba taji la mwaka huu.

Listen to the Jukwaa la Michezo podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.