Kijiwe Nongwa
Kijiwe Nongwa.
Podkasti inayoangazia yanayotokea katika muziki wa bongo fleva kila siku ya Jumanne.
Author
Kijiwe Nongwa
Category
Podcast website
Latest episode
Oct 29, 2024
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Kijiwe Nongwa Ep 24: FLOWER 3 EP | B12 | TMA 23 13.05.2023 1:15:08
Rayvanny ametoa kionjo na orodha ya nyimbo zitakazokuwepo kwenye Ep yake ya tatu ya mfululizo ya Flowers 🌺, tunaizungumzia na jinsi ambavyo Rayvanny anaandika na kuimba kuhusu mapenzi. Usiku wa Tuzo Uko karibu kabisa,tunabashiri washindi na Yale tutayotegemea.
Kijiwe Nongwa Ep 23: LOUI X LEGACY RECORDS | BEBERU TRILOGY | SALU T. 13.05.2023 1:02:26
Tunaangazia kizungumkuti Cha Loui na record label yake ya Legacy. Mengi yamesemwa kuhusiana na BEBERU TRILOGY ya Wakazi tunajaribu kuelewa ni uelekeo gani Wakazi atakwenda na tunamkumbuka Kaka yetu alietutoka SALU T na muziki wake.
Kijiwe Nongwa Ep 22: TUZO ZA TMA 2023 (TULIPOFIKA) | ZIIKI MEDIA. 13.05.2023 1:00:13
Kampuni ya ZIIKI MEDIA imeendelea kuwapa mikataba wasanii wengi wakubwa kwa Tanzania, nini maana Yao na Wana malengo Gani na uwekezaji huu kwa Tanzania? Tunaichambua pia safari kuelekea kilele Cha Tuzo za Muziki Tanzania.
Kijiwe Nongwa Ep 21: LOUI | DAVIDO | UKALI WA MSANII. 13.05.2023 1:04:11
Davido anarudi na album mpya tunaangazia kujua nini tunaweza kujifunza kutoka kwake. Nini haswa kipimo Cha umahiri kimuziki wa mwanamuziki, Hilo nalo tumelizungumzia.
Kijiwe Nongwa Ep 20: PLAYLIST YA VP KAMALA HARISS | MWEZI MTUKUFU | UUZAJI WA MUZIKI 13.05.2023 34:18
Makamu wa Rais wa Marekani Bi Kamala Harris amezitembelea nchi za Ghana, Tanzania na Zambia, na katika safari zake ametoa muziki anaousikiliza katika safari yake, tunazungumza kuhusu Hilo. Mwezi MTUKUFU pia na uhusiano wake na utoaji hafifu wa MUZIKI.
Kijiwe Nongwa Ep 19: WAVE EP (MAONI) | ABIGAIL CHAMS | JOOZEY. 13.05.2023 1:16:13
Joh Makini ametoa Ep mpya ya Wave, tunaichambua. Jinsi ambavyo Abigail Chams anatembea na soko la Tanzania na kama ni njia sahihi sana, tunamaliza na Dj JOOZEY.
Kijiwe Nongwa Ep 18: TOP 20 | MPWT MAONI | SALIMA 13.05.2023 1:06:02
Nini dhana ya Top 20 katika muziki, ni jinsi gani tunaweza kupata chati kwa ufasaha zaidi katika wakati huu wa teknolojia. Nyimbo mpya ya SALIMA kutoka kwa Fredrick Mulla pia tunaizungumzia.
Kijiwe Nongwa Ep 17: WANAWAKE NA MUZIKI | PHINA & ZUCHU | 1.5% COSOTA. 13.05.2023 1:05:29
Siku ya wanawake Iko mbele yetu. Tunaujadili mchango wa wanawake katika muziki wa Tanzania, nafasi Yao na changamoto zinazowakumba.
Kijiwe Nongwa Ep 16: HIP HOP HAIUZI BADO? | PUBLISHING | Q-CHIEF. 13.05.2023 1:00:49
Je, ni kweli bado Hip hop HAIUZI mpaka Sasa? Tunaichambua dhana hii pamoja na kuangalia uchapishaji wa muziki na Q Chief na album yake mpya.
Kijiwe Nongwa Ep 15: TUZO ZA MUZIKI 2023 | ALIKIBA X YOGO BEATS. 13.05.2023 1:02:16
Tunaangalia ukaribu wa ALIKIBA na producer YOGO BEATS na kama wawili hawa wanatengeneza muziki mzuri zaidi wakiwa pamoja.
Kijiwe Nongwa Ep 14: SINGELI MDUNDO WA TAIFA | LOVE SENTENCE ALBUM | TUZO 13.05.2023 1:01:35
Kwa nini Singeli isiwe mdundo rasmi wa taifa? Tunajibu sintofahamu za mdundo wa TAIFA.
Kijiwe Nongwa Ep 13: MDUNDO WA TAIFA | DIAMOND PLATNUMZ | TUZO ZA MUZIKI. 13.05.2023 1:02:08
Tunalizungumza suala la mdundo wa TAIFA na nini haswa maana yake. Tunaangazia pia Tuzo za muziki wa Tanzania (TMA) kwa mwaka 2023.
Kijiwe Nongwa Ep 12: 13.05.2023 1:00:34
Yaliyotokea wiki hii katika Bongo Fleva.
Kijiwe Nongwa Ep 11: AFRICAN PRINCESS REC LABEL | YAMMI | BONGOFLEVA 2023. 13.05.2023 1:00:07
Nandy amezindua Record Label yake ya African Princess. Tunaangazia maono na dira yake pamoja na changamoto. Pia amemtoa msanii wake wa kwanza Yammi. Tusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 10: WASANII BORA 10 TANZANIA | HATIA V | 2023 13.05.2023 54:37
Tunazungumza wasanii 10 Bora kwa mwaka wa 2022 na ngoma mpya ya Dizasta Vina "HATIA V". Karibu utusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 9: ALBUMS NA EPs KALI ZA 2022. 13.05.2023 1:02:40
Tunazitizama kazi 10 Bora kwa mwaka wa 2022. Karibu utusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 8: TBYK MAONI | PERFORMANCE YA JUX | TOMMY FLAVOR | KONTAWA. 13.05.2023 58:13
Tunaipitia album ya Marioo "The boy You know" na kuitolea maoni. Sambamba na hilo tunaongelea show ya Jux na nyimbo ya Kontawa. Karibu utusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 7: SIO KWA UBAYA | THE SUPERDOME | MAVOKALI. 13.05.2023 52:29
Ukumbi mpya wa The Superdome uko tayari kabisa. Tunazungumza aina ya mapinduzi tunayoyategemea katika show za live kwa hapa nyumbani. Karibu utusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 6: ACCESS & SPOTIFY MASTERCLASS | UJIO WA ASLAY. 13.05.2023 1:01:40
Tulipata nafasi ya kuhudhuria matamasha makubwa kabisa ya muziki ya Access na Spotify,tunayazungumzia hapa pamoja na ujio mpya wa Aslay. Karibu utusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 5: MASTER MANONDO EP (MAONI) | S2KIZZY | ZUCHU. 13.05.2023 1:00:39
Tunaitizama Ep ya mkali Fredrick Mulla pamoja na kuangalia kazi za producer S2kizzy pamoja na Zuchu. Tusikilize.
Kijiwe Nongwa Ep 4: NITONGOZE | PHINA, SUPERWOMAN + HAYA | ALBUM MPYA. 13.05.2023 1:01:25
Tunaizungumzia nyimbo ya Nitongoze ya Rayvanny na Diamond, PHINA na Superwoman na Haya pamoja na album mpya zilizotoka. Tupe sikio.
Kijiwe Nongwa Ep 3: OMMY DIMPOZ DEDICATION REVIEW | VANILLAH + EP 13.05.2023 56:45
Tunaizungumzia album ya Ommy Dimpoz Dedication pamoja na kumuangalia msanii mpya kutoka Kings Music VANILLAH na Ep yake. Tusikilize hapa.
Kijiwe Nongwa Ep 2: VITA YA ALBUMS | KIPI KIPYA | ANACONDA 13.05.2023 1:01:20
Leo tunazungumza kuhusu msururu wa album zilizotoka na ngoma mpya ya Ommy Dimpoz Anaconda. Karibu.
Kijiwe Nongwa Ep 1. MCHUMBA | KWIKWI | SAMPLING | FLIGHTMODE. 13.05.2023 56:45
Karibu kwenye episode ya kwanza ya podcast yetu ya KijiweNongwa. Tusikilize hapa kuhusu Zuchu na SlimSal.
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.