Amedeus D. Raphael

Amedeus Live Podcast

Religion SW ↓ 244 episodes

Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,

Author

Amedeus D. Raphael

Category

Religion

Podcast website

amedeuslive.blogspot.com

Latest episode

Apr 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Asili ya Kiungu 13.02.2022

Wewe sio wa kawaida, umezaliwa kwa mbegu ya Mungu, wewe ni zaidi ya mwanadamu wa kawaida. Unao uzima wa aina ya Mungu.

Maisha ya Utukufu 12.02.2022

Safari ya Mtu mwenye haki ni kama siku ipambazukayo.... iking'aa na kung'aa mpaka mchana mkamilifu. #mchana #kung'aa #safari #haki

Kutokuzeeka 12.02.2022

Wewe umezaliwa na Neno la Mungu linalodumu na kuishi hata milele. Kataa afya yako isizeeke, kudhoofu au kuathiriwa na Magonjwa.  #kutokuzeeka #umri #uzee #neno

Nastawi Daima 30.01.2022

Mimi ni kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji. Nazalisha matunda mwaka nzima. Maambukizi, viwavi na chochote kinachoharibu hakina nafasi ndani yangu. Maisha yangu ni kusonga mbele na kupanda juu tuu. Hallelujah.

Maisha ya Utukufu 30.01.2022

Tunaishi ndani yake, uzima wake ni uzima wetu! Tumeketishwa pamoja nae katika eneo la mamlaka na ukuu mbali sana na maradhi, magonjwa na mauti. Hallelujah!

Ninaishi kwa Imani 27.01.2022

Kwa maana pasipo imani huwezi kumpendeza Mungu..... Wenye haki wa Mungu wataishi kwa imani na sio kwa kuona, au kuhisi kwa milango ya fahamu ya mwili. 

Imani yangu ndio Ushindi 27.01.2022

1Jn 5:4  Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 

Unabii wa Rhapsodi ya Uhakika mwaka 2022 26.01.2022

Haya ni maneno ya unabii kwa ajili ya usambazaji wa Rhapsodi ya Uhakika (ya Mungu) Tanzania nzima. Bwana ametoa neno lake na jina la Bwana libarikiwe.

Naleta Mabadiliko 23.01.2022

Mimi sio mhanga wa maisha wala wa dunia. Mwili wangu ni Hekalu la Roho Mtakatifu. Ninaishi kwenye afya njema siku zote. Ninatawala na kumiliki katika maisha haya.

Asili yangu ya Kiungu 23.01.2022

Mimi ni wa juu na sio chini! Mimi ni raia wa Sayuni - mji Mtakatifu! Safari ya maisha ni kutoka utukufu hata utukufu.

Sina mahusiano na Mauti 22.01.2022

Mimi ni Roho Mmoja Pamoja na Bwana. Mwili wangu ni makao ya kudumu ya Roho wa Mungu. Mimi ni tawi na yeye ni Shina la Mzabibu.

Uzima wa Mungu ndani Yako 22.01.2022

Wewe una uzima wa aina ya Mungu. Uhai wako unabebwa na aina huu ya uzima. Wewe sio mwanadamu wa kawaida. Wewe ni mwana wa Mungu.

Ninao Uzima wa Mungu 22.01.2022

Tendea kazi neno la Mungu kila Siku. Kataa kuathiriwa au kukwamishwa na Nguvu pinzani. Ukiri wako ni ufunguo wa afya yako.

Twaa Ngao Yako 14.01.2022

Fahamu silaha uliyopewa na Mungu kwa ajili ya kujikinga na mashubulizi ya adui.  Usipojua namna ya kutumia silaha hii utakuwa mhanga katika maisha wakati sio kusudi la Mungu kwa ajili yako. Unaweza kupakua nakala ya rhapsodi hii kwa mwezi mzima kupitia link hii.

Roho Moja Pamoja Naye 10.01.2022

Mimi ni kiungo cha mwili Wake, cha nyama Yake, na cha mifupa Yake! Ninatembea katika ufahamu kwamba niko katika muunganiko na Yesu Kristo. Na kupitia roho, ninaufanya mwili wangu upate utukufu wa mwili Wake uliofufuka. Hakuna ugonjwa, maradhi au udhaifu unaoweza kusitawi katika mwili wangu, kwa sababu nimeunganishwa na Bwana na ni roho moja pamoja Naye. Uungu unafanya kazi ndani yangu. Utukufu kwa...

USISHINDWE NA UOVU 06.12.2020

Rhapsodi ya Uhakika, Dec 6, 2020. Mimi niko kwenye dunia, lakini mimi si wa dunia. Kwa hiyo, ninawaza, ninaongea, na kutenda tofauti na maisha ya dunia yalivyo. Nimetakaswa na Roho Mtakatifu, nikitengwa na Mungu kwa ajili ya kwa ajili ya matumizi matakatifu, yasiyo na mawaa. Ninatawala juu ya dhambi na kazi zake zotemagonjwa, udhaifu, umaskini, kifo nk. Amin.

ATHIRI ULIMWENGU WAKO 05.12.2020

Rhapsodi ya Uhakika, Dec 5, 2020 Mpendwa Baba, ahsante kwa kuniita katika maisha ya athari na kwa kunipa rasilimali kuu kuliko zote—ambayo ni Roho Mtakatifu—ili kunisaidia kutembea katika mapenzi Yako na makusudi Yako kwa ajili ya maisha yangu. Uliniumba katika Kristo Yesu kwa ajili ya kazi njema ambazo uliziandaa tangu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu kwamba nienende katika hizo. Na sasa...

NI KUHUSIANA NA NENO KATIKA KINYWA CHAKO 04.12.2020

RHAPSODI YA UHAKIKA, DEC 4, 2020. UKIRI Kupitia msaada wa Roho, na katika kulitafakari Neno la Mungu daima, ninazungumza kwa uangalifu maneno mazuri, ya kujenga, ya neema, yenye kuhuisha, yenye kuhamasisha, na yenye kutia moyo. Kwa maneno yangu, ninaumba mafanikio, ushindi, afya ya Kiungu na ustawi kutokea ndani, nikisimamisha haki ya Mungu katika ulimwengu wangu, katika Jina la Yesu. Amina.

WEKA SHABAHA YAKO KWA BWANA NA KATIKA UFALME WAKE 03.12.2020

Rhapsodi ya Uhakika: Dec 03, 2020.  Ukiri. Nimehamishwa kutoka katika ulimwengu wa giza na kwenda katika “Ufalme wa Mwana wa pendo Lake.” Ijapokuwa ni ulimwenguni, nina fikra za ufahamu wa Ufalme wa Mbinguni. Hivyo, ninatenda kutoka katika uwanda wa ulimwengu wa roho, na hakuna kitu katika ulimwengu huu wa nyama kwamba ni cha thamani kwangu. Na hakika, kupitia kuenea kwa Injili kusikozuilika,...

ELEWA NA LITAMKE NENO 02.12.2020

Rhapsodi ya Uhakika, Dec 02, 2020.  Kuna Wakristo ambao uzoefu wao katika maisha ni kinyume cha imani yao na Neno la Mungu. Kwa mfano, wanaweza kuwa wanaamini kwamba kama Wakristo, hawapaswi kukandamizwa na Shetani, ila wanapitia uzoefu wa mkandamizo wa kishetani na hila. Wanaamini kuwa hawapaswi kuugua au kuwa na madhoofu katika miili yao, ili hali ni vigumu sana kwao kuwa na uzoefu wa afya...

Changia Kipindi cha Rhapsodi 02.12.2020

Kuwa sehemu ya kupeleka injili katika ulimwengu nzima kwa kuchangia kipindi hichi cha rhapsodi ambacho pia kinaruka hewani kupitia radio za kawaida katika mikoa ya nyanda za juu kusini na katika visiwa vya zanzibar. Wasiliana na nasi katika namba zifuatazo: 0736000999.

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA 01.12.2020

Rhapsodi ya Uhakika - Dec 1, 2020 Ukiri Mimi nimekufa kwa ulimwengu na ulimwengu umekufa kwangu. Hivyo, ninaweka umakini wangu katika Bwana na Ufalme Wake wa milele, nikimpenda Yeye kwa moyo wangu wote. Mambo ya Roho ni ya muhimu sana kwangu kuliko kitu chochote katika ulimwengu huu. Ninaishi kila siku ingali umakini wangu ukiwa katika Injili, kuihubiri na kuieneza kote ulimwenguni kwa uweza wa Ro...

TWALITUKUZA JINA LAKE 30.11.2020

Mungu amejitukuza Mwenyewe ndani yangu; sasa, ninaubeba utukufu huo kila mahali. Hakuna aibu maishani mwangu; ninatembea katika utukufu, na maisha yangu yamejawa utukufu—heshima, nakshi, ukuu, uzuri, upendeleo! Ninatembea kiuendelevu katika afya ya kiungu, ustawi, na kuiathiri dunia yangu kwa utukufu Wake. Asifiwe Mungu!

KUWA NA SHEREHE YA KUSIFU 29.11.2020

Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele (2 Mambo Ya Nyakati 20:21).

UJAZO WAKE NDANI YAKO 28.11.2020

Rhapsodi ya Uhakika - Nov 28, 2020. Mimi ni chombo kimbebacho Mungu; Kristo ndani yangu ni utukufu uliotambulika, ushindi uliohakikishwa, na usitawi uliothibitishwa. Hakuna hofu wala kuchanganyikiwa maishani mwangu. Bila kujali mitihani, majaribu ama changamoto zinazoweza kuja kinyume na mimi, mimi ni mshndi na kinara maishani. Haleluya!

Listen to the Amedeus Live Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.