Amedeus D. Raphael
Amedeus Live Podcast
Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,
Author
Amedeus D. Raphael
Category
Podcast website
Latest episode
Apr 1, 2024
Where to listen?
Podcasts in the app Replaio Radio Coming soonPodcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts
Episodes
Tumetokana na Mungu 01.04.2024 15:36
Mungu ni chanzo chetu, tumezaliwa neno lake, tumetokana na yeye. Ametuzaa kwa mapenzi yak, sisi na kazi ya mikono yake, limbuko la kwanza la viumbe wake. Tuna uzima wa aina yake, tuna asili yake na tumejazwa kwa Roho wake.
Msingi wa Imani ya Kikristo 01.04.2024 18:09
Kristo ndani yako nfio maana halisi na mjumuisho mzima wa Imani ya Kristo. ukristo sio dini, ni uhalisia uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Ni maisha halisi ya Mungu ndani ya mwanadamu. Ni Uungu katika mwili.
Usijitahidi Kushinda Tena 01.04.2024 12:23
Usijitahidi kuwa kile ambacho tayari upo, tambua wewe ni mshindi, na umezaliwa kwenye mshindi na upaswa kudhihirisha ushindi kila siku. Ni jadi yako, Mila Yako, asili Yako kuishi na kutembea katika ushindi.
Hakuna Baraka zilizosalia Kuomba 01.04.2024 14:40
Umebarikiwa kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa Roho ndani yake Kristo Yesu. Hakuna baraka hata Moja ambayo bado haujapewa. Tembea kwenye uhalisi huu, tembea kwenye kweli hii! Tembea kwenye Nuru hii!
Huburi Maisha ya Ushindi 01.04.2024 15:48
Duniani Mnayo dhiki lakini Jipeni Moyo, mimi Nimeushinda ulimwengu. Yesu ameushinda ulimwengu kwa ajili yako, changamka, kuwa imara. Tembea na ishi maisha ya Ushindi. Ni jadi yako na haki Yako.
Mfunuaji wa Siri za Mungu 30.03.2024 14:19
Mfahamu Roho Mtakatifu kwa undani kabisa kupitia nakala hii! Roho Mtakatifu ni nafsi hai ya Mungu, yeye ni mfariji wetu, rafiki anaye ambatana nasi kwa ukaribu kuliko yoyote yule katika ulimwengu huu! Mjue binafsi na tembea katika ushirika nae kwa viwango vya kipekee.
Uhusiano wa Kiungu 29.03.2024 13:50
Wewe umeungwa na Bwana Yesu, wewe ni kitu kimoja na yeye! Yeye yupo ndani Yako na wewe upo ndani yake. Uzima wake upo ndani Yako leo, wewe umeletwa kwenye daraja la Mungu! Una uzima na asili ya Mungu ndani Yako Leo hii.
Yesu Ndiye Kristo 29.03.2024 14:01
Elewa Kweli hii na tembea katika uhalisi wake, kwamba Yesu ndiye Kristo, ndiye masihi, Mwokozi wa ulimwengu, Neno la Mungu lililofanyika mwili!
Hema Yake Iliyotakaswa 21.03.2024 12:07
Wewe ni makao ya Mungu, maskani yake. Wewe ni mwakilishi wa Mungu katika ulimwengu wako. Dhihirisha ubora na ukuu wake leo, mtangaze Bwana Yesu kila Mahali ulipo au uendapo. Acha ulimwengu umwone Kristo ndani Yako na kupitia wewe kuanzia leo.
Kutembea Ndani Yake 20.03.2024 12:22
Elewa upo ndani ya Kristo kama wewe umezaliwa mara pili. Elewa Kristo ni eneo, ni maskani na upaswa kuenenda ndani yake kupitia neno lake. Neno lake ni Nuru, taa na uhalisi wa maisha yetu ya kila siku.
Haki - Kipawa kwa Wasio Watauwa 20.03.2024 12:03
Je, unajua ni Kipawa na zawadi kutoka kwa Mungu kwa ulimwengu na sio kwa Wakristo! Kipawa hiki kinakuwa asili yako na uhalisi wako pindi tu unapozaliwa mara ya pili. Kipawa hiki kinakufanya mtawala na hodari katika maisha pale kitambua na kutembea katika Nuru yake. Jifunze zaidi kuhusu Kipawa hiki.
Mwenye Furaha kila siku 19.03.2024 12:51
Mara ngapi umejishangaa kwamba unafuraha na haujui kwanini!? Furaha ni tunda la Roho ya mwanadamu iliyoumbwa upya na hivyo unapaswa kudhirisha furaha siku zote. Dhihirisha furaha kila siku! Furaha ni kitu cha Muhimu Sana katika Ufalme wa Mbinguni. Jifunze zaidi kupitia episodi hii.
Jua kile Ulichonacho ndani Yako 18.03.2024 10:40
Kuza tabia ya Mungu iliyo ndani ya roho yako kwa kupitia ufahamu na utambuzi wa sifa na tabia za Kiungu na asili yake iliyoko ndani yako. Soma waraka wa Filemoni 1:6 katika matoleo mbalimbali ya biblia upate kuelewa jinsi utambuzi wa vile ulivyonavyo ndani yako katika Kristo Yesu vinavyoweza kuinua maisha yako katika viwango vya juu sana.
Wewe Sema Ndiyo Tu 18.03.2024 11:23
Usijaribu kuwa vile ulivyo tayari.... Usijitahidi kupata kile ulichonacho tayari... sema tu, Ndiyo. Mfuate Bwana Yesu na atakufanya kuwa mvuvi wa watu. Jifunze namna ya kufuata kupitia somo na ona badiliko la kipekee katika huduma yako ndani ufalme wa Mungu.
Wajibu wako wa Kiungu 18.03.2024 11:25
Elewa wajibu wako ndani ya Mungu. Umeitwa kuzitangaza fadhili za Mungu kila mahali. Umeitwa kumwakilisha yeye kwenye ulimwengu wako. Huu ni wajibu wako kiiungu.
Kujenga Tabia ya Kiungu Ndani Yako 11.03.2024 16:40
Neno la Mungu linauwezo wa kujenga tabia za kiungu ndani Yako kama utalisikia, utaliamini, Ulitafakari na kulifanya kuwa maisha Yako ya kila siku. Wekeza kwenye neno la Mungu na hakika utakuwa na maisha ya ushindi Daima.
Kuna Kitu cha tofauti kk kuhusu Wewe 09.03.2024 15:02
Wewe ni taifa teule, taifa takatifu, jamii ya Mungu, uzao maalumu. Wewe ni milki ya Mungu, wewe sio ajali wala bahati mbaya. Fahamu wewe ni Nani ndani ya KRISTO na ishi katika uhalisi huu!
Amefanyika kuwa Sisi pale Msalabani 09.03.2024 15:55
Alifanyika dhambi yeye asiyejua dhambi... Alichukua asili yetu na kuwa mbadala wetu ili tuchukue asili yake na kuchukua haki yake... Ametufanya kuwa Wana wa Mungu, wenye asili na uzima wa Mungu... Tafakari Kweli hii na tembea katika Nuru hii.
Kuzaliwa katika Ufalme wa Mwana wa Pendo Lake 06.03.2024 14:03
Kuzaliwa mara ya pili ni kigezo dhahiri. Ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu ni Ufalme halisi uliopo na unaofanya kazi hata sasa. Fahamu namna ya kuenenda na kuishi ndani ya Ufalme huu kupitia episode hii.
Amekupatia Kila Kitu 06.03.2024 13:57
Bwana Yesu ni Kila Kitu. Bwana Yesu ni uzima wa milele, yeye ni Mungu wa Kweli. Mfahamu zaidi Yesu na utembee kwenye uhalisi Kweli ya neno lake na mapenzi yake kwako. Kristo ndani Yako ni tumaini la Utukufu na ushindi mkuu! Jiandae kushiriki mkutano mkubwa wa uponyaji unaitwa "Mito ya Uponyaji".
Haki yake kwa ajili ya asili yako ya dhambi. 04.03.2024 14:30
Haki ni zaidi ya kitendo chema kinacholandana na maadili ya Mungu. Haki ni asili ya Mungu. Haki ni namna ya Mungu anavyoona mambo, anavyosikia, anavyofikiri, anavyoitikia na anahukumu! Kupitia Imani ndani ya Kristo Yesu tumehesabiwa haki mbele za Mungu, tumefutiwa hatia na ile hati ya mashitaka imebatilishwa. Amka kwenye Uhalisia huu, tembea kwenye kweli hii.
Neno lake ni Uthibitisho Unaouhitaji. 04.03.2024 16:25
Neno la Mungu li hai, limevuviwa kwa uweza na nguvu ya Roho Mtakatifu! Linaweza kusabibisha mabadiliko na uhalisia wa kile linachosema. Litafakari na kulitegemea neno kila siku! Neno la Mungu ndio Uthibitisho Pekee unaohitaji!
Nyimbo za Rohoni 02.03.2024 15:15
Jifunze kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli! Panda juu zaidi, katika viwango vikubwa zaidi vya ushirika wako na Bwana Yesu kupitia ibada zako binafsi kusifu na kuabudu. Imba wa Roho, imba kwa akili pia. Sifu kwa Roho, sifu kwa akili pia.
Omba Kwa ajili ya wengine 02.03.2024 12:22
Simama katika nafasi iliyowazi kwa ajili ya familia yako, shule, mji na taifa lako. Unaweza kusabibisha mabadiliko makubwa Sana kupitia Dua, Sala, maombezi na Shukrani kwa ajili ya jamii Yako. Bariki ulimwengu leo kwa kupitia Sala na maombezi.
Umezaliwa kwa ajili ya maisha Mazuri. 01.03.2024 15:18
Wewe haukuumbwa kwa ajili ya shida na tabu, Bali ubora, afya njema na utukufu. Fahamu haki, Stahiki na wajibu wako ndani ya Kristo na Tembea katika halisia za Kweli hizi za ufalme!
Similar podcasts
Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.