Amedeus D. Raphael

Amedeus Live Podcast

Religion SW ↓ 244 episodes

Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,

Author

Amedeus D. Raphael

Category

Religion

Podcast website

amedeuslive.blogspot.com

Latest episode

Apr 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Mafanikio yenye kuongezeka Daima 01.03.2024

Umeitwa katika umilele. Mungu aweka umilele ndani Yako. Wewe ni kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji. Umeunganishwa na mfumo wa Ugavi wa Mungu.... Mafanikio Yako ni dhahiri, halisi na ya kudumu...

Mungu amepangilia maisha Yako kwa Umakini mkuu. 28.02.2024

Wewe ni kazi ya mikono ya Mungu, Mungu alikundalia maisha Bora kwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwepo. Anataka utembee katika ubora, utukufu na ukuu kila siku. Mafanikio, ushindi, afya njema, ustawi na tija ni mpango wake kwa ajili yako.

Mungu anazungumza Kupitia Neno Lake. 27.02.2024

Mungu na Neno lake ni wamoja. Fikra yake, sauti yake, mawazo yake yanawakilishwa katika neno lake! Huwezi kutambua sauti yake kama hautambui neno lake. Jifunze neno lake kila siku.

Ishi kwa ajili ya Kristo 27.02.2024

Maisha kwako yana maana Gani!? Shauku Yako kuu ni nini katika maisha!? Kwanini unaishi!? Mustakhabali wa maisha Yako ni nini au ni upi!? Sikiliza rhapsodi hii na chagua kuishi kwa ajili ya Kristo.

Kuzaliwa mara ya Pili - TeeVo 27.02.2024

Isipokuwa umezaliwa mara ya pili hauwezi kuona wala kuingia katika Ufalme wa Mbinguni... Maisha ni jambo la Kiroho, kilichozaliwa kwa Roho ni Roho na kilichozaliwa kwa mwili ni mwili. Fanya sala ya wokovu mara tuu ya Episode hii na uzaliwe mara ya pili leo hii.

Shahidi wa Kizazi Chako 27.02.2024

Wewe ni shahidi wa Kristo kwa kizazi Chako.... Wewe balozi wa Kristo, shuhuda wa ufalme na Kweli yake... Usikae kimya, usinyamaze, usione haya kwa ajili ya Kristo au injili yake!

Tabia ya Kitauwa 25.02.2024

Kama mtoto wa Mungu unapaswa kuwa na tabia zinamwakilisha Mungu na kumtukuza Mungu wakati wote. Uaminifu, uadili, upole, ukarimu, kiasi, adabu njema, utauwa, ni tabia unazopaswa kuzionyesha wakati wote. Sikiliza podcast hii kila Siku ili ikujenge vema katika tabia za Kitauwa!

Iishi Kweli na Ishi katika Kweli 24.02.2024

Kweli ni neno la Mungu Neno la Mungu ni fikra ya Mungu, hekima yake, haki yake, mawazo yake, makusudi yake, mipango yake iliyowasilishwa kwenye maandishi. Ukiijua Kweli, Kweli itakuweka huru.

Msifu Bwana Hata Iweje 24.02.2024

Mpe Bwana sifa na Shukrani, kwa ukuu wake na ubora, kwa fadhili zake na rehema! Yeye ni Mungu mkuu, muumba wa mbingu na nchi! Anastahili sifa, heshima, utukufu na adhama. Mungu wetu ni Bwana na hakuna kama yeye.

Mtoaji mwenye Furaha 23.02.2024

Toa kwa moyo wa ukunjufu, bila kulazamishwa, malalamiko au kushurutishwa. Ni heri na baraka zaidi kutoa kuliko kupokea.

Fanya Kazi na Roho Mtakatifu 22.02.2024

Huduma yako na utumishi wako ufanye kwa kupitia uvuvio wa Roho Mtakatifu! Yeye ndio anaweza kutakasa kazi yako na kuifanya ikubalike mbele za Mungu. Fauta maelekezo yake naye atakuongoza katika safari ya ushindi na ukuu.

Alikuja kwetu katika Roho Mtakatifu 21.02.2024

Elewa muunganiko wa Bwana wetu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, ni muunganiko wa Ajabu na kipekee. Bwana Yesu ni mfariji aina ile ile kama Roho Mtakatifu, hao wawili ni kitu kimoja. Roho Mtakatifu ni Baba aliyekuwa ndani ya Bwana Yesu, yeye ndiye Bwana Yesu alikuwa akishuhudia kwamba nayatenda yale ninayomwona Baba anatenda! Soma tena na utafakari injili ya Yohana sura ya 14.

Ukiri wangu, Afya yangu 21.02.2024

Uzima, afya njema, amani tele, ustawi na ushindi endelevu ni haki Yako ndani ya Kristo. Tumia Kinywa chako kuthibitisha haki hii kila siku katika kila eneo la Maisha Yako. Jiandikishe leo kushiriki ibada mubashara za uponyaji pamoja na mtumishi wetu wa Mungu Mchungaji Chris Oyakhilome, tarehe 15, 16 na 17 ya mwezi March 2024. Tembelea tovuti hii: www.healingstreams.tv/LHS

Kuna Nguvu ndani ya Neno 21.02.2024

Kama mtoto wa Mungu, wekeza muda wako wa kutosha kusoma na kutafakari neno la Mungu. Hakika litakupa ushindi na ubora kwenye eneo la Maisha Yako.

Yafumbue Macho Yao 21.02.2024

Injili ndio Nuru ya kufungua macho Yao. Wanavyozidi kuisikia injili ndivyo watakavyozidi kutembea kwenye Nuru na kumfahamu zaidi Mungu na mwanawe Yesu Kristo. Endeleza kampeni ya kusambaza injili kila Mahali, fumbua macho ya teenagers wote Tanzania. Jipatie nakala yako ya Teenagers Devotional Bible kwa gharama ya sh.50,000! Itakubariki sana .

Fanya Imani Yako iwe Hai 20.02.2024

Pasipo Imani haiwezakani kumpendeza Mungu... Imani ni kanuni ya msingi katika Ufalme wa Mungu. Pasipo Imani haiwezakani kunyakuwaliwa.... Chochea Imani Yako leo na Hakikisha ipo hai muda wote....

Wewe ni Makao Makuu ya Mungu 20.02.2024

Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mwili wako ni maskani yake... Moyo wako ni makao yake, dhihirisha tabia yake, ubora wake na hekima yake kila siku.

Kinywa chako - Sheria yako 19.02.2024

Kinywa chako ndio kiunganishi kati ya uhalisia wa maisha yako na yale yote aliyokukirimia Mungu katika maisha maisha Yako. Jifunze namna ya kutumia kiunganishi hichi vizuri kwa ajili ya maisha ya ubora, utukufu na ukuu mwingi.

Ufalme Unaoendeshwa kwa Maneno 19.02.2024

Maneno ni Vitu.... Maneno ni malighafi Muhimu na ya msingi Sana katika Ufalme wa Mbinguni... Maneno yanaweza kuamua hatma yako iwe nzuri au mbaya.... Maneno yanaweza kubadili mustakhabali wa maisha yako kabisa.... Elewa umuhimu wa maneno leo na uyatumie ipasavyo katika Ufalme wa Mbinguni ambamo Leo hii mimi na wewe ni washirika na wazawa.

Kuwa na fikra ya Ufalme 19.02.2024

Elewa kwamba Kanisa la Yesu Kristo hapa duniani ni sehemu ya Ufalme wa Mungu na hivyo linapaswa kufanya kazi zake kama Ufalme zaidi kuliko taasisi. Fahamu kanuni za Ufalme ambao wewe umezaliwa humo na tembea katika ubora na utukufu wa ufalme huu! Fikra na ufahamu wa ufalme ni dhana halisi unayopaswa kutembea ndani yake kila siku.

Zingatia maisha Yajayo 18.02.2024

Kuna maisha zaidi ya haya! Hapo Dunia tunapita, kuna zama za Muda mrefu zaidi ya hizi za wakati na ziko mbioni kuanza. Fahamu Kweli hii na Anza kujipanga kwa ajili ya zama hizi kwa maana halisi na dhahiri! Usiishi kama hapa ndio mwisho, Hakika hapa sio mwisho wa maisha! Tunatarajia kusambaza nakala hizi za rhapsodi pale mji wa moshi wa mbio za marathon, kuwa sehemu ya kampeni hii kubwa moshi nzima...

Utambuzi na Werevu wa Juu 17.02.2024

Je Unataka kuwa mwerevu, mwenye utambuzi wa hali ya juu wa mambo yote ya kiroho na kimweli!? Basi unahitaji kulitafakari neno la Mungu usiku na mchana. Neno la Mungu linauwezo wa kukupa maarifa, Werevu, mtazamo, fikra na uwezo wa ufahamu wa juu sana kuliko malighafi nyingine yoyote duniani. Liendee neno na litabadilisha kabisa maisha yako, katika namna ya ubora na ukuu!

Fuata Ushauri Wake 17.02.2024

Roho Mtakatifu anajua kilichobora kwa ajili yako na kwa ajili ya kila mtu ulimwenguni. Anajua kila kitu, anaweza kukuongoza kwenye kila nyanja ya maisha! Yeye ni Bwana wa mikakati, mshauri wa Ajabu. Maarifa na enzi yote ni Yake...

Hekima ya Mungu 16.02.2024

Hekima ya Mungu ni neno, neno lake limesheni maarifa yake, fikra zake, mtazamo wake, makusudi na mapenzi yake. Tafakari Kweli Yale leo na utembee kwenye hekima ya Kiungu.

Neno katika Mwili 16.02.2024

Vipi siku ukikutana na maneno Yako, utayapenda na kuyafurahia au utayachukia na kuyakimbia! Maneno ni vitu, maneno kielelezo chako, cha mawazo, matarajio na mtazamo wako. Maneno Yako ni wewe mwenyewe! Maneno yako yanabeba utu wako!

Listen to the Amedeus Live Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.