Amedeus D. Raphael

Amedeus Live Podcast

Religion SW ↓ 244 episodes

Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,

Author

Amedeus D. Raphael

Category

Religion

Podcast website

amedeuslive.blogspot.com

Latest episode

Apr 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Nini Kimefunuliwa ndani Yako 15.02.2024

Kimjazacho mtu, ndicho kimtokacho. Ndani yako kumejaa nini!? Upendo, amani, haki, upole, hekima, wema!? Au kumejaa chuki, Hasira, ugomvi, husuda! Jaza kwa wingi neno ndani Yako na litaonekana na kuthibitika kwenye kila jambo linahusu maisha Yako.

Jikabidhi kwa Neno na Roho 14.02.2024

Unaweza kuliamini neno la Mungu kukujenga na kuzalisha ndani kile linachosema. Neno ni mwongozo, Neno ni Nuru, Neno ni suluhisho. Litumaini neno na litakupatia urithi katikati ya watakatifu!

Baraka ziko ndani ya Kristo 13.02.2024

Hakuna baraka unayotaka ambayo haipo ndani. Kama upo ndani ya Kristo, elewa kwamba umebarikiwa kwa Baraka zote za rohoni. Wewe ni kifurushi cha baraka ni kinachodhihirika kila Mahali.

Zingatia na Ulitafakari Neno 12.02.2024

Neno la Mungu ni kioo, kinachoweza kubadili muonekano wako, Roho, nafsi na mwili. Kila unapojitizama katika hichi Kuna badiliko linatokea kutoka utukufu hadi utukufu, Imani hadi Imani! Tafakari neno la Mungu kila siku uone badiliko lake maishani Mwako.

Afya Njema ni Haki Yako. 12.02.2024

Tembea kwenye afya njema kila siku kwa kufanya ukiri wa AFYA ya KIUNGU kila mara.

Vitu vyote vipi chini ya Miguu yako 11.02.2024

Je unajua kwamba kama umezaliwa ya pili basi wewe ni kiungo katika mwili wa Kristo na mshirika wa tabia za kiungu na wa-urithi wa watakatifu katika nuru. Hebu gundua kweli hizo leo hii na utembee kwenye hatma yako ndani yake.

Ni nini zaidi Unataka? 11.02.2024

Kila unachotaka umepewa ndani ya Kristo, kama haki, afya njema, uzima wa milele, ubora, mafanikio, ustawi, ulinzi, mamlaka, amani, na mengine mengi. Gundua Kweli hii na Anza kutembea katika uhalisia wake.

Uponyaji kwa ajili yako 07.02.2024

Amini neno la Mungu, lifanyie kazi Hilo neno! Tenda kama neno linavyosema hata kama hisia zako hazikuchochei kufanya hivyo. Afya njema ni haki Yako, idai, isisitize mpaka iwe ni uhalisi wako.

Tiketi ya Kupokea kila Baraka 07.02.2024

Je, unafikiri kuna baraka zimezuiliwa dhidi Yako!? Au unafikiri kuna aina za Baraka ambazo Bwana hajakubariki nazo bado!? Au ni baraka Gani ambayo ungependa kumwomba Bwana akubariki nayo leo!? Jina la Yesu ni tiketi ya Kupokea kila Baraka! Litumie vizuri kuanzia siku ya leo.

Neno ni Silaha Yetu 07.02.2024

Jifunze namna ya kutumia neno la Mungu kama Silaha. Uzima na Mauti vipo kwenye nguvu ya Kinywa. Neno ni upanga mkali ukatao pande mbili. Neno linauwezo wa kuangusha Ngome na kutiisha kila fikra kinzani na injili ya Kristo. Tumia Silaha hiyo kutunza mwili wako na afya Yako kupitia ukiri wa AFYA ya KIUNGU.

Uko juu ya Vyote 06.02.2024

Je, unajua kwamba umeketishwa pamoja na Kristo, mkono wa Kuume wa Mungu Baba. Wewe sio wa hivi hivi, wewe ni kiungo katika mwili wa Kristo. Fahamu sehemu Yako na timiza wajibu wako kama mwana wa Ufalme.

Umehamishwa 06.02.2024

Wewe ni mzao mteule, kuhani wa kifalme. Wewe ni Nuru ya Ulimwengu, ni tawi la mzabibu lizaalo Sana. Fahamu Mahali ulipo sasa ndani ya Ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu. Elewa Kweli hii na tembea katika Nuru yake.

Kuishi katika Jina lake Lisiloshindwa 05.02.2024

Je unajua jina la Yesu ni nyenzo, unayopaswa kuitumia kila siku!? Je, unajua Jina la Yesu ni Ngome na Mnara imara, ambapo kila anayekimbilia hapo anakua salama. Jifunze namna ya kuishi kwa Jina La Yesu kwa kufanya yafuatayo: 1. Tambua uzima wa Mungu uliopo ndani yako. 2. Kataa hofu isiwe na utawala tena dhihi Yako. 3. Kiri neno la Mungu juu Yako na juu ya kila hali za maisha. Fahamu ubora na ukuu...

Mito ya Uponyaji 05.02.2024

Jiandae kwa Ajili ibada mubashara za uponyaji pamoja mtu wetu wa Mungu Mchungaji Chris Oyakhilome. Ibada hizi zitakuwa mubashara Machi 15 hadi 17, unaweza kujisaji kuanzia saa kupitia tuvuti hii; healingstreams.tv Ni haki Yako uwe mzima na mwenye afya njema.

Ieleze Kila Mahali 05.02.2024

Tangaza Habari njema ya Ufalme wa Mungu kila Mahali. Usikae kimya wala kuonea haya injili ya Kristo. Hii ni nguvu ya Mungu iletayo wokovu kwa kila aaminiye! Hawezi kuamini kabla hawajasikia, hawezi kusikia isipokuwa wameambiwa. Dhamini nakala hizi kupitia lipa namba: 8177098.

Umba na Uumbe Upya 03.02.2024

Kama Kristo Alivyo ndivyo na sisi katika ulimwengu huu! Unaweza kuumba upya Hali, vitu, fursa, nafasi ambazo ziliharibika, ulizopoteza au zilitwaliwa kwako bila idhini Yako. Neno la uumbaji lipo kinywani Mwako, chukua hatua.

Anazungumza Lugha ya Roho 03.02.2024

Mungu ni Roho, na anajua namna ya kuwasilisha Ujumbe wake rohoni Mwako katika namna ya kipekee kabisa. Ili kupambanua sauti yake unahitaji kulijua neno lake, Yeye na neno lake ni wamoja! Haongei kinyume na neno lake!

Maisha Bora 03.02.2024

Tumeitiwa maisha ya haki na usawa ndani ya Kristo Yesu. Kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji ndivyo maisha yetu ndani ya Kristo yanapaswa kuwa. Ishi ndani ya neno la Mungu, tembea kati uzuri wa utakatifu.

Uzuri na Utukufu 01.02.2024

Je, ujua mwanadamu ndio limbuko la Kwanza la Viumbe vyote alivyoumba Bwana Mungu. Umeumbwa kwa ajili ya ukuu, ubora na utukufu. Fahamu umuhimu na ufurahie nafasi Yako.

Chochea Upendo wako 01.02.2024

Yesu ndio kila kitu katika maisha haya. Yeye ndio ukamilifu wa maisha, utoshelevu maisha. Ishi kwa ajili yake, mgundue katika namna ya tofauti na ishi katika Nuru ya Kweli hii! Dhihirisha Upendo wako kwake kwa matendo na vitendo.

Maisha ya Shukrani 01.02.2024

Tambua Siri ya kuishi katika afya endelevu, mbali na magonjwa, maradhi na maambukizi! Afya njema ni haki ya kila Mkristo na unapaswa kuishika na kutembea katika afya hii! Moyo wa Shukrani ni kanuni kutembea kwenye afya ya Kiungu. Sikiliza maombezi kwa ajili ya wale wanaosumbuliwa na changamoto za kiafya..

Tembea na Mungu 31.01.2024

Je, unajua maana ya Kutembea na Mungu!? Je, unajua umuhimu wake!? Je unajua mifano ya watu waliotembea na Mungu maishani Mwao na mambo makuu waliyoyafanya!? Chukua uamuzi wa kutembea na Mungu kuanzia leo....

Tamka Kwa Sababu Umeamini 31.01.2024

Mungu anatenda kazi kwa Imani.. Roho ile ile ya Imani aliyonayo ndio tuliyonayo leo! Zungumza sawa na kile alichokisema kuhusu wewe au mji wako. Pasipo Imani haiwezakani kumpendeza Mungu. Achilia neno kila siku kwa Kinywa chako. .

Ukoo wa Ushindi 31.01.2024

Wewe ni mwana familia wa Mungu. Wewe ni mwana ukoo wa wazee wa Imani, wa mitume na manabii! Wewe ni mzao mteule, kuhani na mfalme! Jione kama Mungu anavyokuona! Jione katika ukuu na ubora!

Mito ya Uponyaji 29.01.2024

Ndani Yako itabubujika mito ya Uponyaji....uzima na afya tele! Jiandae kushiriki nasi katika ibada kubwa kabisa ya Uponyaji pamoja na Mchungaji Chris Oyakhilome mwezi March 2024. Haijalishi Hali imekuwa mbaya kiasi Gani, ibada hii ya Uponyaji itakayorushwa mubashara ni maalumu kwa ajili yako. Walisiliana nasi leo kwa taarifa zaidi.

Listen to the Amedeus Live Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.