Amedeus D. Raphael

Amedeus Live Podcast

Religion SW ↓ 244 episodes

Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,

Author

Amedeus D. Raphael

Category

Religion

Podcast website

amedeuslive.blogspot.com

Latest episode

Apr 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Ongea na Wengine kwa Upole 29.01.2024

Upole ni tunda la Roho, upole ni tabia njema. Upole sio unyonge wala udhaifu. Upole ni kama dawa nzuri. Upole ni tiba njema ya Roho, nafsi na mwili. Waongoze wengine kwa Kristo kupitia Sala ya wokovu mara baada ya episodi hii ya leo.

Jiandae kwa Ajili Yake 29.01.2024

Je, unajua kwamba Yesu anarudi hivi karibuni!? Anarudi kuwachukua wale wanaotazamia ujio wake na waliontayari! Vipi wewe upo tayari!? Kama upo tayari, vipi wengine kwenye ulimwengu wako!? Je, wana taarifa hizi!? Tembelea Rhapsody.tv kupata Habari kemkem za namna ya kuwaanda wengine kwa ajili ya ujio wa mara ya pili wa Bwana Yesu.

Tupo Vitani 29.01.2024

Yeye asiye kusanya na sisi yupo kinyume nasi! Vita hii juu ya nafsi za watu! Mungu hataki hata Mmoja apotee bali wote wafikie toba. Tumia silaha ya maombezi kila mara upajianda kwenda kwenye uinjilisti. Sisi tumeshinda na zaidi ya kushinda. Kama wewe ni teenager Hakikisha unapata biblia hii mahususi kwa ajili yako, itakayo kufanya upende kusoma neno la Mungu kila siku na kuishi katika Nuru yake. U...

Afya ya Akili 27.01.2024

Maombi maalumu kwa ajili ya Uponyaji wa AFYA ya akili kwa wale wote wenye Msongo wa mawazo, hisia za kuchanganyikiwa, kukata tamaa ya kuishi! Bwana anakuta uwe na afya njema, uwe na uzima tele! Uishi maisha ya ushindi na ukuu! Pokea afya yako, kuwa mzima kuanzia leo! Tembea kwenye Uhuru wa Wana wa Mungu.

Chagua uzima 27.01.2024

Kama utakuwa mzima au mgonjwa ni uchaguzi wako! Kama utafanikiwa au utashindwa ni uchaguzi wako. Mungu ametukirimia kila tunachohitaji kwa ajili ya maisha ya ushindi na utauwa, amani na haki, baraka na mafanikio, afya na siha njema. Tembea kwenye kweli hii leo.

Uwe na Nidhamu ya Neno 27.01.2024

Fanya Neno la Mungu liwe kipaumbele chako. Lipe nafasi neno la Mungu maishani Mwako kuliko malighafi nyingine yoyote. Lisha Roho Yako kwa neno kila siku. Neno la Mungu linauwezo wa kukujenga na kukupa urithi wako ndani ya Kristo Yesu.

Haki ya Yesu Kristo 27.01.2024

Tumehasabiwa haki kwa njia ya Imani. Kama umezaliwa mara ya pili unahaki sawa na Bwana Yesu leo kama yeye Alivyo na haki mbele za Mungu.

Angaza kama Mwanga 26.01.2024

Wewe ni Nuru ya Ulimwengu, wewe ni taa ing'aayo sana, inuka na ungaze kwenye ulimwengu wako wote. Ruhusu nuru ya injili ya Kristo idhihirike kipekee kupitia wewe!

Uzima Tele 26.01.2024

Kuna uzima tele kwa ajili yako ndani ya Kristo Yesu. Fanya maungamo haya Imani leo hii, ukiwa umeamini na kusadiki kutoka ndani ya Moyo, na hakika utapokea MUUJIZA WAKO. Uponyaji ni haki Yako na ni hamasa ya Mungu uwe mzima mwenye afya tele.

Umealikwa kwenye Sherehe 26.01.2024

Elewa kwamba unyakuo upo karibu sana kuliko wengi wanavyodhani. Hakikisha unafanya yote yanayopasa ili uwe sehemu ya unyakuo huu wa kwanza! Unyakuo huu ni kwa ajili ya kudhuria Sherehe ya kipekee Sana, bonge la "party", karamu ya kifalme, yenye hadhi ya Kiungu! Natazamia kukuona kwenye karamu hii isiyokuwa ya kawaida.

Kuinuliwa Kwako 26.01.2024

Kupandishwa cheo, hadhi au nyadhifa hakutoki mashariki, au magharibi au kusini, Bali vyatoka kwa Mungu, ambaye kupitia neno lake ametuonyesha namna tunaweza kusabibisha au kuchochea jambo hilo kutokea! Soma mistari maandiko haya na uyatafakari vizuri kabisa: Zaburi 3:3, Zaburi 146:8, Zaburi 27:6

Ilishe Roho Yako. 25.01.2024

Wewe ni Roho, unayo nafsi na unaishi katika mwili! Kama ambavyo unaulisha mwili wako, lisha na roho Yako pia. Jaza kwa wingi neno la Mungu maishani Mwako. Tafakari na ujufunze neno la Mungu kila Siku kupitia rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali.

Pokea Uponyaji wa Figo zako 25.01.2024

Uponyaji ni mkate wa watoto. Afya njema ni fungu lako. Yesu Kristo ni yeye yule, leo, Jana na hata milele! Kama aliweza kuponya watu kabla kufa, kufufuka na kupaa, anaweza kukuponya pia Leo hii kupitia makala hii kwa sababu yupo hai ndani yangu na ameivuvia makala hii kwa nguvu yake ya Uponyaji. Pokea uponyaji wako Leo, pokea afya yako leo, pokea Jibu lako katika Jina la Yesu Kristo. https://praye...

Wewe ni wa kiungu kama Yesu Alivyo! 25.01.2024

Hahahah .... Je unafahamu ukweli kwamba wewe umezaliwa na Mungu, umetokana na Yeye! Wewe sio wa ulimwengu huu! Kwamba umeketishwq pamoja na Kristo mkono wa Kuume wa Mungu Baba, katika ulimwengu wa Roho!? Kwamba wewe ni mshirika wa tabia na asili ya Mungu, yaani unashiriki katika Uungu kwa mwana wa Mungu!? Pata nafasi ya kutumia Kinywa chako kuzungumza asili yako ya afya njema na ustawi sawa na kil...

Sauti ya Hekima 25.01.2024

1 Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? 2 Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. 8 Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Igundue sauti ya Hekima, ifuuate, itii na utembee kwenye ustawi, mafanikio, ushindi na ubora tele. Katika toleo la leo Kuna Maombi maalumu kwa yeyote mwenye mgonjwa wa Figo! Pokea uponyaji...

Uonyeshe Ulimwengu Wako Upendo wa Mungu 23.01.2024

Upendo wa Mungu umememiminwa kwa wingi moyoni Mwako, Hakika wewe ni mng'ao wa utukufu wake, dhihirisha upendo huo leo, acha nuru yako iiangaze sana, watu wote waone matendo yako mema, wamtukuze Baba yako wa Mbinguni.

Yeye Yuko Juu ya Yote 23.01.2024

Fahamu vizuri kuhusu ukuu wa Bwana Yesu! Utawala wake, mamlaka yake na enzi yake! Fahamu kuhusu Ufalme wake unafika mbali kiasi gani na katika zama zipi! Maongeo ya enzi yake hayana mwisho, utawala serikali yake ni wa milele. Hii ni rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima, Januari 23, 2024.

Hakuna Kuchanganyikiwa 23.01.2024

Roho Mtakatifu ni msaidizi na mfariji wakipekee maishani! Mpokee Leo hii na mkaribishe ndani yako, atajaza maisha yako kwa Hekima, maarifa na ubora wa kiungu. Atahuisha mwili wako na kufanya uwe na afya njema daima. Roho Mtakatifu ndani yetu ni faida na nguvu yetu ya ushindani!

Afya Stahiki 23.01.2024

Mungu sio chanzo cha magonjwa. Mungu anataka uwe na afya njema, ufurahie maisha na uishi kati Uhuru wenye Haki! Fanya ukiri huu kila mara na tembea kwenye afya njema, bora ambayo ni Stahiki Yako.

Utajiri wa Kristo Usiochunguzika 22.01.2024

Umeitwa kuhuburi utajiri wa Kristo Usiochunguzika, usiopimika, usiohesabika, usioisha. Utajiri ambao marefu yake, mapana, kimo na kina haviwezi kuelezewa kwa ukamilifu kwenye fikra ya kibinadamu. Tafakari mistari hii: Wakolosai 3:8 Warumi 8:17 1 Wakorinto 3:21 Tembea kwenye kweli kila siku kuanzia Leo hii.

Siha Njema 22.01.2024

Ulimi wako unaweza kutunza mwili wako katika siha njema wakati wote. Tamka maneno sahihi kila siku kuhusu ubora wa mwili wako, tamka afya na uzima kila wakati juu ya mwili wako. Siha njema na afya Bora ipo kinywani Mwako.

Mkemee Shetani 21.01.2024

Kataa kuwa mhanga wa shetani na vibaraka wake! Kataa kuishi kwenye kongwa la vifungo vya magonjwa au mashambulizi ya nguvu za Giza! Njoo kwenye Nuru, njoo kwenye Uhuru wa Wana wa Mungu, kwenye Ufalme wa mwana wa pendo lake. Tumia mamlaka uliopewa ndani ya Kristo Yesu na sababisha badiliko katika maisha na ulimwengu wako. Hii Rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima.

Chochea Upako ulionao 20.01.2024

Kuna hazina kubwa sana ya Mungu ndani, usiopotezee!! Ichoche na itumie kuwabariki wengine! Kunena kwa lugha ni Moja na namna ya kuchochea karama hii! Tumia muda Leo kunena kwa lugha na chochea Upako uliopo ndani yako. Bariki ulimwengu leo wa Karama hii iliyowekezwa ndani yako. Rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali.

Unaishi ndani ya Ufamle 20.01.2024

Je, unafahamu kweli hii kwamba Kristo ni eneo na kama umezaliwa mara ya pili upo ndani ya eneo hili. Maisha ni jambo la Kiroho na utambuzi wa Kweli hii utakupa nafasi kutembea kwa ushindi na ukuu kama Mungu anatarajia uishi. Hii ni Rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima, Januari 19, 2024.

Nimebarikiwa 20.01.2024

Uzima na Mauti ipo kwenye nguvu Kinywa chako. Ulimi wako ni lijamu ya mwili wako, unaweza kuongeza siku zako au kuzipunguza kwa kutumia Ulimi huo. Tumia Ulimi huo kutunza afya na siha ya mwili wako kupitia ukiri huu wa AFYA YA KIUNGU.

Listen to the Amedeus Live Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.