Amedeus D. Raphael

Amedeus Live Podcast

Religion SW ↓ 244 episodes

Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo. Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,

Author

Amedeus D. Raphael

Category

Religion

Podcast website

amedeuslive.blogspot.com

Latest episode

Apr 1, 2024

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Uwe na Shauku Nae 20.01.2024

Je, jumla ya Shauku Yako ipo kwenye vitu gani!; Ipo kwenye Kazi yako, familia yako, fedha zako, afya yako, kesho yako au kwenye safari yako ya Imani!? Kwa nini unaishi au uishi wa ajili ya nani au kwa ajili nini!? Jaribu kutafakari maswali haya uposikiliza episode hii! Rhapsodi ya Uhakika toleo la Januari 20, 2024.

Jitambue wewe ni Nani Kihalisi 20.01.2024

Taswira halisi ya wewe ni Nani inapatikana katika neno la Mungu. Mungu anataka ujue yote aliyopanga na kuandaa kwa ajili maisha Yako ya ushindi na ukuu! Amekuchagua kipekee kwa ajili ya utukufu wake, wewe ni kazi ya mikono yake! Kazi njema, yenye baraka na thamani mbele zake. Hii ni rhapsodi ya Uhakika toleo la Vijana maarufu kama TeeVo.

God's New Home 18.01.2024

You body is the temple of the holy ghost, don't treat it anyhow. Treat it with respect and care. Have this mindset in you, that you Carrier of Divine presence of God. You are his representative, his ambassador. Let every teenager here this truth and experience it's power and glory. This is Rhapsody of realities - TeeVo.

Neno Kwanza 18.01.2024

Fanya Neno la Mungu kuwa kipaumbele chako, weka umakini wako wote katika nyakati zako za kusoma na kutafakari neno la Mungu. Hii Rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali, umri miaka 6 hadi 12.

Nyumba Mpya ya Mungu 18.01.2024

Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu. Wewe ni maskani yake iliyohai, yenye thamani kubwa mbele zake! Kila unapooenda umebeba uwepo wake na nguvu yake. Hii ni Rhapsodi TeeVo maalumu kabisa kwa ajili ya kila kijana duniani.

Ametupatinisha na Nafsi yake Mwenyewe. 18.01.2024

Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Hakuna wokovu nje ya Kristo Yesu, ulimwengu lazima uje hilo. Tumepewa huduma hii ya upatanisho na lazima tuuambie ulimwengu mzima. Hii na Rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima, Januari 18, 2024.

Kuabudu Kunahusu Nini? 17.01.2024

Elewa maana halisi ya kuabudu kwa vitendo. Kama teenager unapaswa kumwabudu Mungu katika roho na Kweli. Jifunze leo kupitia TeeVo hii na Anza kumwabudu Mungu katika roho na Kweli.

Tunakua na Hatuzeeki 17.01.2024

Fahamu aina ya Uzima na miasha uliyopokea baada Kuzaliwa mara ya pili! Ni maisha ya kiungu, ni uzima wa milele, uzima wa aina ya Mungu! Baada ya kufahamu hili, sasa unaweza kutembea kwenye Kweli hii, kwenye Uhalisi huu na utaona matokeo ya ajabu na kipekee. Hii ni rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima, pata nakala yako Leo kwa rahisi kabisa. Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0736000999.

Moyo Safi 17.01.2024

Safisha moyo wako kwa neno la Mungu! Moyo wako ndio chanzo cha kila kitu katika maisha Yako. Tenga muda kujifunza neno la Mungu kila siku. Rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali, rika la umri kati ya miaka 6 hadi 12.

Hamna Haja Wasiwasi 16.01.2024

Kataa wasiwasi, kataa mashaka! Wasiwasi ni mshale wa moto, tumia ngao yako ya Imani kuuzima! Telekeza wasiwasi na wala usiruhusu ushike fikra au akili zako. Ruhusu amani ya Kristo itawale akili Yako na moyo wako. Hii ni Rhapsodi ya Uhakika toleo la Vijana maarufu kama TeeVo, umri kati miaka 13 hadi 19. #TeeVo #rhapsodiyauhakika

Kuna Taji Inayongojea 16.01.2024

Kazi yako ya upendo kwa ajili ya Bwana Yesu na injili yake na kanisa lake hapa duniani sio ubatili, inathamani kubwa kwa Mungu na utapata Taji ya Haki, yenye thamani kuu kama tuu hautazimia wala kukata tamaa! Hii ni rhapsodi ya Uhakika toleo la watu wazima, Januari 16, 2024. Tafakari nini utafanya mwaka huu kulinda na kutunza Taji Yako.

Asili yako ya Kweli 16.01.2024

Wewe umetokana na Mungu, na neno lake ndio asili yako, kwa sababu neno lake ni fikra zake, mtazamo wake, mapenzi yake. Tambua asili hii na tembea kwenye udhihirisho wa asili hii kila Siku. Hii ni rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali, umri rika kati ya miaka 6 hadi 12.

Alibatilisha Mauti 15.01.2024

Usiruhusu Mauti na madhara yake vitawale maisha yako tena, Yesu Kristo alibatilisha Mauti na kuleta uzima wa milele na kutokuharibika (kutokufa). Tembea kwenye upya wa uzima, ukiwa na afya njema kila siku. Pokea uponyaji na siha njema kwa ajili yako Leo kupitia rhapsodi hii. Mungu ataka uwe na afya njema na uzima tele kila siku na ufurahie uzima huo.

Kione na Kitamke 15.01.2024

Jifunze kuona kwa macho ya fikra zako au Moja ya rohoni kile ambacho Mungu akupa tayari katika maandiko, kisha kishikilie na kitamke kwa ujasiri ili kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Hii ndio namna ya kutembelea katika uhalisi wa Baraka zako ndani ya Kristo Yesu.

Uwe Bayana katika Maombi Yako. 15.01.2024

Mungu alituambia tuombe kwa sababu anataka anatujali na anataka kujibu na kutupa haja za mioyo yetu. Bainisha haja yako kila mara unapokuwa unamwomba Baba Mungu kupitia jina la Bwana Yesu. Hii ni Rhapsodi ya Uhakika toleo la wasomaji wa awali, Januari 15, 2024.

Zoezi Letu 13.01.2024

Bwana Yesu alifunua Uungu kwetu kupitia maisha aliyoishi hapa duniani. Alituonyesha fikra ya Mungu Baba, mtazamo wake, mwitikio wake, upendo wake na kila kitu alichofanya kilikuwa ni kudhirisha Haki ya Mungu kwetu. Leo hii tunakapswa kudhihirisha maisha hayo hayo kila siku iitwayo leo. Jifunze zaidi kupitia Rhapsodi hii ya leo!

Imani Moja tu! 13.01.2024

Hakuna wokovu kwa njia nyingine isipokuwa kupitia Yesu Kristo. Hakuna atayeurithi Ufalme wa Mbinguni isipokuwa amempokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Kila kijana (teenager) anapaswa kusikia Habari hizi. Sambaza Ujumbe huu kwa kila kijana katika ulimwengu wako.

Endelea Kutabasamu 13.01.2024

Dhihirisha furaha yako kila siku kwa sababu wewe ni mtoto wa Mungu. Furaha ya Bwana ni nguvu yako. Jifunze zaidi katika rhapsodi ya Uhakika toleo hili la wasomaji wa awali, Januari 13, 2024.

Mamlaka juu ya Giza 12.01.2024

Kila Mkristo ampewa mamlaka ya kisheria (nguvu ya uwakili) ya kutumia jina la Yesu kwenye kila Hali, namna na mahali. Fahamu kile ilichonacho ndani ya Kristo na kitumie ipasavyo kuishi maisha ya ushindi, ubora na ukuu! Hii ni rhapsodi ya Uhakika, toleo la watu wazima, januari 12, 2024.

Haki inakufanya Jasiri 12.01.2024

Je, unajua kwamba wewe ni haki ya Mungu ndani ya Kristo Yesu. Hii ni Moja ya Kweli kubwa sana katika biblia na ufununo injili ya Bwana wetu Yesu Kristo. Jifunze leo namna haki inavyokufanya jasiri na shupavu mbele za Mungu, wanadamu na Dunia nzima. Hii na rhapsodi ya Uhakika toleo la TeeVo, vijana rika la miaka 13 hadi 19, la Januari 12, 2024. Hebu chunya hatua leo kuwajulisha maelfu ya Vijana kwe...

Baraka zake Haziharibiki 12.01.2024

Baraka za Bwana zinatajirisha na hazina majuto, hazileti majuto! Baraka zake ni za milele, za kutegemewa. Hakika unapata nakala yako Leo kwa ajili watoto wako na jamii inayokuzunguka. Nakala moja ni sh.3000 na unaweza kulipia makumi, mamia na maelfu ya nakala kwa ajili ya kuwa kufikiwa watoto wa kitanzania.

Yesu Kristo - Wasifu wa Mungu 11.01.2024

Mgundue Bwana Yesu kwa viwango vya juu zaidi na vipya mbali zaidi ya ulivyokuwa unamdhania au kumfikiria. Yesu ndio wasifu wa halisi wa Mungu. Yesu ndiye taswira ya halisi ya Mungu Baba, ukimwona Yesu umemwona Mungu Baba. Jifunze zaidi katika rhapsodi hii ya leo, toleo ya Watu wazima. Tafakari kweli hii na itabadilisha maisha yako kabisa.

Uchunge Ulimi Wako 11.01.2024

Maisha yako yatachukua uelekeo wa ulimi (kinywa) wako. Anza kuanzia leo kuongea maneno sahihi kuhusiana na maisha yako ya kila siku na kesho au baadae ya maisha yako. Jifunze zaidi katika TeeVo hii namna kuishi kwa ushindi kila siku kwa kutumia ulimi wako kwa usahihi. Waambie wengine kuhusu TeeVo na wasambazie wanafunzi na teenagers wenzako popote pale walipo.

Lulu nzuri na ya Thamani 11.01.2024

Wewe ni mwenye thamani kubwa sana mbele za Bwana Yesu. Yeye anakupenda sana na anataka ujue hivyo na ulimwengu wote ujue kwamba anakupenda na wewe ni kazi ya mikono yake. Jifunze zaidi kwenye nakala hii ya Rhapsodi ya Uhakika toleo la WASOMAJI WA AWALI - rika kati ya miaka 6 hadi 12. Wasambazie wengine kweli hii na leta furaha na tumaini la kweli katika maisha yao.

Wabebaji wa Baraka 10.01.2024

Wewe ni mtoto wa Mungu na umebeba baraka na utukufu wa ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo kila unakoenda dhihirisha baraka, wema na utukufu huu. Kuwa chachu ya mafanikio kwa watoto wenzako na familia kwa ujumla. Kitabu hiki ni mahususi kwa ajili ya watoto wa rika la miaka 6 hadi 12. Kinapatikana kwa lugha za kiingereza na Kiswahili na nyinginezo. Nakaala moja ni sh.3000 tu!

Listen to the Amedeus Live Podcast podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.