United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ 204 epizód

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: news.un.org

Szerző

United Nations

Kategória

News

A podcast weboldala

news.un.org

Legutóbbi epizód

2026. okt. 8.

Hol hallgathatod?

Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio Hamarosan

A podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz

Letöltés a Google Play-ről Telepítsd ingyen Android közel 10 M letöltés · 4,8-as értékelés iOS hamarosan

Epizódok

Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 08.06.2026

Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutoa wito wa hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na hali hiyo. Akizungumza kwa njia ya video katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya Bahari inayoadhimishwa kila mwaka Juni 8, Bwana Guterres amesema bahari ni msingi wa maish...

05 JUNI 2026 05.06.2026

Jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo dunia inaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani huku maadhimisho ya kimataifa yakifanyika jijini Baku nchini Azerbaijan. Maudhui ya mwaka huu ni "Sasa kwa ajili ya Tabianchi", yakiweka msisitizo mkubwa wa kuchukua hatua dhidi ya za uhifadhi wa mifumo ya ikolojia na hatua za kukabili tabianchi. Hivi karibuni, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria pamoja na wad...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu” 04.06.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”

04 JUNI 2026 04.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni  kuboresha zao hilo na kuin...

Hifadhi ya Ngorongoro: Ambapo uhifadhi, utamaduni na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu 03.06.2026

Tukilekea Siku ya Mazingira Duniani hapo Juni 5, Leo tunakupeleka katika moyo wa Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamad...

03 JUNI 2026 03.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na...

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “CHOTORA” 02.06.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Mtalaam wetu Onni Sigalla kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA anafafanua maana ya neno “CHOTORA”

02 JUNI 2026 02.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu. Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapem...

01 JUNI 2026 01.06.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo hii leo tutaelekea jijini Kampala nhcini Uganda kuangazia uzunduzi wa awamu ya tatu ya safari ya hija ya “Twende Zetu Butiama”, kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kmabarage Nyerere, rais wa zamani wa Tanzania aliyedumisha amani, msikamano na kupigania maendeleo ambazo ni ajenda zinazopewa kiaumbele cha juu na Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu kati...

29 MEI 2026 29.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo tunamwangazia mmoja wa maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya. Mwisho wa wiki hii, Joyce, raia wa Tanzania ambaye pia amewahi kuhudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNEP na pia Benki ya Dunia anahitimisha utumishi wake katika Umoja wa Mataifa akiwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya...

28 MEI 2026 28.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Taifa la Tanzania na Balozi Togolani Idriss Mavura mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na Flora Nducha kuhusu suala hili muhimu.“Nataka niwe mkweli; hii ni moja ya changamoto zetu kubwa zaidi. Hatu...

Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE." 22.05.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."

22 MEI 2026 22.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililo...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.” 21.05.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”

21 MEI 2026 21.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi. Hadi sasa  Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewa...

20 MEI 2026 20.05.2026

Hii leo kwenye Jarida la Habari tuna Muhtasari na Mada kwa Kina. MUHTASARIOngezeko la idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRCUmuhimu wa kushirikisha jamii kwenye udhibiti wa Ebola Mpango wa Tanzania wa kukabiliana na makazi duniMADA KWA KINAInaangazia uchambuzi wa ripoti ya uanishaji wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania ambapo tumezungumza na Afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Cha...

19 MEI 2026 19.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waa...

18 MEI 2026 18.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mlipuko wa Ebola nchini DRC na Uganda na ujumbe wa Profesa Mohamed Yakub Janabi Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika kuhusu hatua WHO inachukua kudhibiti ugonjwa huo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo..Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa 79 wa...

15 MEI 2026 15.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa s...

14 MEI 2026 14.05.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme ili...

Katibu Mkuu Antonio Guterres aaga Muungano wa Afrika na kutoa tathmni ya ushirikiano wa UN-AU 13.05.2026

Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo  wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.. Assumpta Massoi anafafanua...

13 MEI 2026 13.05.2026

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar. Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa...

UNDPTanzania yajengea uwezo wasaidizi wa kisheria 126 kisiwani Pemba, ili kutatua migogoro kwa njia mbadala 13.05.2026

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. Rashid Malekela na taarifa zaidi.

AfroKids International ni tumaini kwa wanawake wakimbizi barani Ulaya - Farina 13.05.2026

Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nduch...

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “Payapaya.’’ 12.05.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya.’’

Hallgasd a(z) Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcastot a Replaióban

Rádió és podcastok egy alkalmazásban - ingyen és regisztráció nélkül. Telepítsd még ma, és ne maradj le a premierről

Letöltés a Google Play-ről

A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.