United Nations

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

News SW ↓ 204 epizód

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mindenképp látogasd meg a podcast oldalát, és támogasd a készítőjét: news.un.org

Szerző

United Nations

Kategória

News

A podcast weboldala

news.un.org

Legutóbbi epizód

2026. okt. 8.

Hol hallgathatod?

Podcastok az alkalmazásban Replaio Radio Hamarosan

A podcastok hamarosan megérkeznek az alkalmazásba. Telepítsd most, és láss elsőként egy teljesen új megközelítést a podcastokhoz

Letöltés a Google Play-ről Telepítsd ingyen Android közel 10 M letöltés · 4,8-as értékelés iOS hamarosan

Epizódok

JIFUNZE KISWAHILI - NENO MZIO 06.08.2026

Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MZIO"

05 AGOSTI 2026 05.08.2026

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Feissal Kirwa akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya amani na usalama, usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama, haki za binadamu na hali ya hewa. MUHTASARI1. Wimbi jipya la mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya raia na majeruhi wengi, limelaaniwa vikali na Mratibu wa Masuala ya Kibinadam...

04 AGOSTI 2026 04.08.2026

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya. Muhtasari wa habari:• Utapiamlo mkali nchini Afghanistan umefikia viwango vya kutisha, huku majimbo 12 yakirekodi kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa cha utapiamlo miongoni mwa watoto wakati huu watu milion...

JIFUNZE KISWAHILI - NENO : KUROA 03.08.2026

Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda Burundi, ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika na mchambuzi wetu ni Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUROWA”. Hiki ni kitenzi kikimaanisha kuvua samaki na nomino yake ni mroaji. Sentensi: Mroaji ameenda ziwa Tanganyika kuangalia iwapo atapata kitoweo cha samak...

03 AGOSTI 2026 03.08.2026

Ili kufahamu ni kwa namna gani Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinawasaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kifedha lakini wana uwezo wa kitaaluma ikiwa ni sehemu ya juhudi za chuo hicho kushiriki katika kuhimiza Malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDG na kuunga mkono utekelezaji wake., Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye alikiwakilisha chuo hicho katika Kongamano la...

31 JULAI 2026 31.07.2026

Hii leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya, katika Kijiji cha Embulbul kilichoko Kaunti ya Kajiado, ambako Shirika lisilo la kiserikali la Tulivu Safe Haven, lililoanzishwa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, linatekeleza hatua mbalimbali za kuwasaidia wanawake. Hii ni pamoja na kuwaokoa na kuwahifadhi manusura wa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia ma...

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, “KUSOROZA.” 30.07.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUSOROZA.”

30 JULAI 2026 30.07.2026

Hii leo tunakuletea mada kwa kina. Mlipuko wa sasa wa ebola ya virusi vya Bundibugyo uliotangazwa rasmi huko DRC mwezi Mei mwaka huu unazidi kuongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida, wamesema maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na waandishi wa habari Karl Skau, Kaimu Mkuu wa WFP, na ndio tunakupeleka nchini humo kufuatilia juhudi za kuudhibiti. • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António...

Mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuingia ng’we nyingine kesho 29.07.2026

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Antonio Guterres anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Je ni nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekuwa anafuatilia mchakato huu na nimezungumza naye angalau atupatie kwa muhtasari.

Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Dkt. wa Ebola DRC 29.07.2026

Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo r...

29 JULAI 2026 29.07.2026

Hii leo jaridani tunaangazia mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa UN, juhudi za mashirika mbalimbali za kuhamazisha wananchi DRC kuhusu udhibiti wa Ebola, na mafunzo ya STEM viziwani Zanzibar zinazolenga kuimarisha kilimo cha mwani.. • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza...

Mafunzo ya STEM yawezesha vijana Zanzibar kuongeza thamani ya zao la mwani 29.07.2026

Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kw...

28 JULAI 2026 28.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Kuna msemo wa kiswahili usemao tahadhari kabla ya hatari na hivyo ndivyo ilivyo kwa ugonjwa wa Homa ya Ini ambapo kama mtu ataenda kufanya uchunguzi mapema anaweza kupata chanjo au matibabu, lakini kama atachelewa basi anaweza kupata hata ugonjwa wa saratani. Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya kuelimisha kuhusu ugonjwa huo Leah Mushi wa Idhaa hii amezungum...

27 JULAI 2026 27.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza simulizi za wananchi kuhusu uhamazishaji wa kudhibiti Ebola. Pia tunakuletea muhtasari wa habari. • Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya mita...

24 JULAI 2026 24.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo v...

23 JULAI 2026 23.07.2026

Mada kwa kina hii inakupeleka Pwani ya Kenya katika Kaunti ya Kilifi ambako mradi wa ‘Tushauriane Tuimarishe Kilimo Biashara’ unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, umewezesha wakulima wa eneo hilo kubadili mtazamo na kufanya kazi kwa pamoja. Ingawa changamoto za kijinsia zimekuwepo kwa muda mrefu, sasa mradi huo umefungua njia inayoleta nuru katika uhus...

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.” 22.07.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”

22 JULAI 2026 22.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini. Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungu...

21 JULAI 2026 21.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Jana katika moja ya viunga vya jiji la Nairobi, wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na raia wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Kenya, ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela walikitembelea Kituo cha Kulelea Watoto ya Yatima kinachofahamika kwa jina Serah’s Vision Children’s Home na walik...

20 JULAI 2026 20.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) yanatambua kuwa kuwawezesha vijana, kulinda mazingira na kuimarisha uhakika wa kupata chakula ni miongoni mwa nguzo muhimu za kujenga jamii zenye ustahimilivu na maendeleo endelevu. Kupitia malengo kama vile la Kutokomeza umaskini, kutokomeza njaa na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , jamii z...

Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO." 17.07.2026

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."

17 JULAI 2026 17.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili. • Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapem...

16 JULAI 2026 16.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Ukanda wa Gaza ambako sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina lililotiwa Saini tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2025 limewezesha wakulima wa eneo hilo kurejea mashambani. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari. • Mashirika mawili ya Umoja Umoja wa Mataifa lile la Uhamiaji, IOM na la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa waliyo...

15 JULAI 2026 15.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana tunamulika jinsi gani vijana waliojiendeleza katika stadi ya akili mnemba au wengine wanaita akili unde, kwa kiingereza Artificial Intelligence au AI, wanarahisisha maisha ya jamii. Na tunamuangazia kijana Kalebu Gwalugano kutoka Tanzania, Muasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Neurotech iliyoanzis...

14 JULAI 2026 14.07.2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendele...

Hallgasd a(z) Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu podcastot a Replaióban

Rádió és podcastok egy alkalmazásban - ingyen és regisztráció nélkül. Telepítsd még ma, és ne maradj le a premierről

Letöltés a Google Play-ről

A Replaio nem podcastkiadó; a műsorok nevei, borítóképei és hanganyagai a szerzőiket illetik, és nyilvános RSS-csatornákon keresztül terjednek.