Goodluck Joseph

Wanangu podcast

Arts EN ↓ 115 episodios

This podcast is hosted by Goodluck Joseph, a curious guy who likes to share all the things he finds interesting in the form of a podcast episode. In other words, this podcast is an extension of his personality and more. Expect to hear topics that range from music, movies, and books to random ideas, all presented in a creative manner.

No dejes de visitar la web del podcast y apoyar a su creador: rss.com

Autor

Goodluck Joseph

Categoría

Arts

Web del podcast

rss.com

Último episodio

2 de nov. de 2026

¿Dónde escuchar?

Podcasts en la app Replaio Radio Muy pronto

Los podcasts llegarán muy pronto a la app. Instálala ahora y sé el primero en descubrir una forma totalmente nueva de vivir los podcasts

Descárgala en Google Play Instálala gratis Android casi 10 M de descargas · valoración de 4,8 iOS muy pronto

Episodios

Episode 115 | Mkono wa Kushoto au Kulia: Nani Aliamua? 02.11.2026

Katika episode hii, tunajadili jambo ambalo wengi wetu hulichukulia kama la kawaida bila kujiuliza maswali mengi: kwa nini baadhi ya watu hutumia mkono wa kulia huku wengine wakipendelea wa kushoto? Je, ni jambo tunalozaliwa nalo, tunalojifunza au kuna sababu za kisayansi zinazoamua mkono tunaoutumia zaidi? Kupitia mjadala huu, tunachunguza sayansi ya "handedness", uhusiano wake na ubongo wa binad...

Episode 114 | Akili Pekee Hazitoshi 26.10.2026

Katika episode hii, Host anajadili kwa nini akili pekee haitoshi kumfikisha mtu mbali kimaisha. Je, ni nani mwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kati ya mtu mwenye akili nyingi anayepanga na kufikiri kwa kina, na mtu anayechukua hatua na kujifunza kupitia uzoefu? Kupitia mjadala huu, tunatafakari uhusiano kati ya kufikiri na kutenda, tukichunguza jinsi ambavyo maarifa bila utekelezaji yanaweza kubaki...

Episode 113 | Tusisahau Kuishi 19.10.2026

Katika harakati za kufikia malengo yetu na kujenga maisha tunayotamani, mara nyingi tunasahau kufurahia maisha tunayoyaishi sasa. Katika episode hii, Host anatafakari umuhimu wa kuthamini safari badala ya kuweka thamani yote kwenye destination, akidadavua namna ambavyo hamu ya kufika tunakotaka inaweza kutufanya tuahirishe furaha yetu, tukiamini kwamba maisha halisi yataanza pale tutakapofanikiwa....

Episode 112 | Hakikisha Upo Mtandaoni! Ft. John Viva. 12.10.2026

Katika episode hii, Host anaungana na mtaalamu wa masuala ya taarifa, Bwana John Viva, kudadavua umuhimu wa kuwa na uwepo mtandaoni katika ulimwengu wa sasa. Kupitia mjadala huu, utapata pia maarifa kuhusu namna ya kujijenga na kufanya vizuri katika ulimwengu huu wa kidigitali.

Episode 111 | Pesa Haitakuwa na Thamani Ifikapo 2036? Ft. Baraka Kambi. 05.10.2026

Pale mtu tajiri zaidi duniani anaposema kuwa pesa huenda isiwe na thamani yoyote ndani ya miaka kumi ijayo, ni kauli inayozua maswali mengi kuliko majibu. Akiungana na mgeni wake, Mr. Baraka Kambi, Host anajaribu kuchambua maana halisi ya kauli hiyo iliyotolewa na Elon Musk katika mahojiano yake na jarida la The Economist, huku wakitafakari mustakabali wa pesa katika ulimwengu unaoelekea kutawaliw...

Episode 110 | Tunafuata Muziki au Tunatafuta Likes? 28.09.2026

Katika episode hii, host anaibua swali: je, kadri tunavyozidi kwenda mbele, mashabiki wanapoteza uhusiano wao wa moja kwa moja na muziki na kuanza kujali zaidi vitu vinavyouzunguka, kama vile ‘likes’ na engagement kwenye majukwaa ya usambazaji wa muziki kama YouTube? Akiendelea kuchunguza sababu zinazoweza kuwa nyuma ya mabadiliko haya, host anarudisha ‘mic’ kwako na kukuuliza: wewe unaonaje kuhus...

Episode 109 | Malengo Yanavyoweza Kukupoteza 21.09.2026

Katika episode hii, Host anatoka nje ya box na kukuletea wazo linalokwenda kinyume na matarajio ya wengi: kwamba kama unataka kufanikiwa zaidi katika unachokifanya, huenda ukahitaji kuacha kuwa na malengo. Akirejea kwenye kitabu kilichomtambulisha wazo hili, Host anaeleza kwa nini mfumo wa maisha unaotufundisha kuweka malengo unaweza kuwa na mapungufu yake. Lakini hoja hapa si kwamba tusiwe na mal...

Episode 108 | Fikra Sahihi Huja Kwa Lugha Asili 07.09.2026

Fuatilia jinsi mstari mmoja wa Nash Mc unavyoweza kuzalisha maswali mengi na yenye kutafakarisha kuhusu uhusiano na kutegemeana kati ya lugha na fikra. Ni kama hadithi ya nani alianza kati ya yai na kuku, lakini safari hii ikiwa katika uwanja wa lugha na utambuzi. Je, lugha ndiyo huchochea namna tunavyofikiri, au fikra ndizo huunda lugha tunayotumia?

Episode 107 | A.k.a Mimi by Ngwair (Uchambuzi) 31.08.2026

Katika episode hii, Host anaichambua album ya kwanza ya Ngwair, A.K.A Mimi , na kueleza mambo aliyogundua baada ya kuisikiliza tena akiwa mtu mzima. Wakati album hii ilipotoka, alikuwa bado mdogo na huenda hakuwa na uwezo wa kuielewa kwa kina kama anavyoweza leo. Safari hii, anaisikiliza kwa mtazamo tofauti; akiunganisha “dots” zilizopo baina ya nyimbo, mambo yanayofanya album hii isimame kama kaz...

Episode 106 | Usiamini Hadithi Moja Tu 24.08.2026

Katika episode hii, tunaangazia tabia ya kuchukua hadithi ya mtu mmoja na kuitumia kama ushahidi wa kuhitimisha jambo kubwa zaidi. Kupitia mifano ya maisha ya kila siku, katika afya, biashara na social media, tunaona jinsi kauli kama “Mimi ninamjua mtu ambaye…” zinavyoweza kutufanya tufanye maamuzi yasiyo sahihi. Episode hii inatukumbusha kwamba stori moja inaweza kuwa ya kweli, lakini isiwe ushah...

Episode 105 | Kampuni Inayouza Rangi Bila Kuuza Rangi! 17.08.2026

Katika Episode hii, tunaangazia historia ya kuvutia ya Pantone , mfumo uliobadilisha namna dunia inavyotambua, kuwasiliana na kutumia rangi. Tutafuatilia jinsi wazo la kuunda mfumo wa kutambua rangi lilivyoanza, namna Pantone ilivyogeuka kutoka kwenye mfumo wa kawaida wa kuchanganua rangi na kuwa sehemu muhimu ya ulimwengu wa ubunifu, mitindo, matangazo na biashara. Karibu!

Filamu ya Afrika Iliyowahamasisha Jay-Z na Beyoncé 10.08.2026

Je, ni nini kinachofanya filamu iliyotengenezwa Afrika zaidi ya miaka 50 iliyopita iendelee kuzungumziwa, kupongezwa na hata kuwavutia mastaa kama Jay-Z na Beyoncé? Katika episode hii, host anasimulia Touki Bouki, mojawapo ya filamu kubwa na zenye ushawishi kuwahi kutokea Afrika. Tunafuatilia safari ya wahusika Mory na Anta, lakini zaidi ya hapo, tunaangalia kile ambacho filamu hii inakisema kuhus...

Episode 103 | Usichokimaliza Hukaa Akilini 03.08.2026

Katika episode hii, Host anaangazia dhana ya kisaikolojia inayojulikana kama ‘ The Zeigarnik Effect’ , inayoeleza kwamba binadamu huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukumbuka kazi au mambo ambayo bado hajayakamilisha kuliko yale ambayo tayari ameyamaliza. Kwa nini hali hii hutokea, na inaathirije maisha yetu ya kila siku? Karibu ufuatilie.

Kupenda Kwangu 'Titles' Kunanigharimu 27.07.2026

Katika episode hii, host anakukaribisha ndani ya mawazo yake na kukuonyesha mchakato halisi anaoupitia kila anapotafuta title ya episode mpya. Ni safari iliyojaa vita ya ndani kati ya kuandika title inayomridhisha yeye kama ‘mbunifu’ na ile inayopewa kipaumbele na mtandao (algorithms) ili kuwafikia watu wengi zaidi. Anaeleza mapenzi yake ya muda mrefu juu ya titles nzuri tangu akiwa mtoto, hadi ch...

Episode 101 | Timamu Kati ya Wasio Timamu 20.07.2026

Katika episode hii, host anachambua utafiti maarufu uliofanywa na Dkt. David Rosenhan mwaka 1973, uliouliza swali muhimu kuhusu uwezo wa wataalamu wa afya ya akili kutofautisha kati ya mtu mwenye ugonjwa wa akili na anayejifanya kuwa nao. Matokeo ya utafiti huo yaliibua mjadala mkubwa na kuonyesha mapungufu yaliyokuwepo katika mfumo wa utambuzi wa magonjwa ya akili, kiasi cha kuwafanya wengi kuhoj...

Episode 100 | Kwanini Iliitwa Wanangu Podcast? 13.07.2026

Host anaadhimisha kwa furaha kufikiwa kwa episode ya 100 ya Wanangu Podcast , akitoa shukrani za dhati kwa kila aliyekuwa sehemu ya safari hii, kuanzia wasikilizaji / watazamaji hadi marafiki waliotoa mawazo, ushauri na mchango wao katika kuiboresha podcast hii. Katika mazungumzo hayo, anasimulia pia chanzo cha jina Wanangu Podcast , sababu zilizomfanya alichague, na anagusia mafunzo makubwa aliyo...

Episode 99 | Tofauti Kati ya Single, EP na Album 06.07.2026

Muziki hutolewa kwa mifumo tofauti kama Single , EP , na Album , lakini je, unafahamu tofauti kati ya aina hizi za utoaji wa muziki na sababu zinazowafanya wasanii kuzitumia? Katika episode hii, tunafafanua kwa kina maana ya Single , EP , na Album , matumizi yake, pamoja na nafasi yake katika tasnia ya muziki. Kama umewahi kusikia maneno haya lakini hukuwahi kuelewa tofauti zake, basi sikiliza epi...

Episode 98 | "Jizime Data Uende Mjini" 29.06.2026

Episode hii inaangazia umuhimu wa kuwa na aibu yenye afya, huku ikihoji: nini kinaweza kuwa mustakabali wa jamii yetu ikiwa sote tutaendelea kuishi kwa falsafa ya “Jizime data uende mjini”?

Episode 97 | Kunawa Mikono Haikuwa Kawaida ya Madaktari 22.06.2026

Episode hii inaangazia maisha na mchango wa Ignaz Semmelweis, daktari wa karne ya 19 aliyegundua kwamba kunawa mikono kabla ya kuwahudumia wagonjwa kulipunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya wanawake waliokuwa wanajifungua. Licha ya ushahidi wake kuokoa maisha mengi, alipingwa na kudharauliwa na jamii ya kitabibu ya wakati wake kwa sababu mawazo yake yalikwenda kinyume na imani zilizokuwepo. Mwisho wa...

Episode 96 | Kwanini Tunahusisha Mateso na Mafanikio? 15.06.2026

Episode hii inaangazia falsafa ya muda mrefu inayodai kuwa mateso na changamoto humjenga mtu kuwa bora, imara, na mwenye uwezo mkubwa wa kufikia mafanikio. Katika mjadala huu, host anachambua na kuunga mkono baadhi ya hoja zinazotolewa na falsafa hiyo, huku pia akitoa tahadhari kuhusu namna inavyoweza kutafsiriwa au kutumiwa vibaya, hasa pale mateso yanapohalalishwa au kuonekana kuwa sharti la maf...

Episode 95 | Kwanini Sauti Yako Iliyorekodiwa Husikika Tofauti? 08.06.2026

Watu wengi hawapendi kusikia sauti zao zilizorekodiwa na hivyo huamini kuwa wana sauti mbaya. Katika episode hii, tunafafanua kwanini sauti yako iliyorekodiwa husikika tofauti na unavyoijua wewe mwenyewe, na tunajadili hatua unazoweza kuchukua ili kuizoea na kuondoa hisia hiyo.

Episode 94 | Mjadala wa Vipimo 01.06.2026

Episode hii inaangazia historia na tofauti za mifumo miwili maarufu ya vipimo duniani Imperial na Metric. Host anafafanua kwa nini baadhi ya nchi hupima kwa maili huku nyingine zikitumia kilomita. Pia tunaangazia matukio halisi ambapo mkanganyiko wa vipimo ulisababisha hasara kubwa, ikiwemo kupotea kwa chombo cha anga cha mamilioni ya dola. Ni simulizi ya kuvutia kuhusu jinsi vipimo vinavyoathiri...

Episode 93 | Fukuto la Ubunifu Feat. Araskies 25.05.2026

Katika episode hii, Host anamkaribisha “mgeni mwenyeji” Araskies, kwa mazungumzo yenye msukumo kuhusu kile anachokiita “Fukuto la Ubunifu” hali ya kutotulia hadi pale unapotekeleza na kukamilisha wazo au ndoto uliyonayo. Ndani ya dakika chache tu, wanagusia mambo mengi yenye kuhamasisha, kukuamsha kutoka kitandani, na kukusukuma kuchukua hatua kuelekea ndoto zako.

Episode 92 | Falsafa za Niccolò Machiavelli (The Prince) 18.05.2026

Katika episode hii, kwa lugha rahisi tunagusia kitabu cha 'The Prince' kilichoandikwa na Niccolò Machiavelli mnamo karne ya 16, kikiwa ni moja ya vitabu vyenye ushawishi mkubwa katika siasa na uongozi duniani. Tunaangazia hoja zake maarufu kama vile 'ni bora kiongozi kuogopwa kuliko kupendwa' na jinsi kilivyoshauri viongozi kulinda tawala zao.

Episode 91 | Gharama ya Kuwa na Fahamu. 04.05.2026

Katika episode hii, host ana-share wazo lililomjia hivi karibuni kuhusu fahamu (consciousness), lililomchochea kuanza kuchunguza kwa kina maana halisi na uhalisia wa dhana hiyo.

Escucha el podcast Wanangu podcast en Replaio

Radio y podcasts en una sola app - gratis y sin registro. Instálala hoy y no te pierdas el estreno

Descárgala en Google Play

Replaio no es editor de podcasts; los nombres de los programas, las portadas y el audio pertenecen a sus autores y se distribuyen a través de canales RSS públicos