SBS
SBS Swahili - SBS Swahili
Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili
Glöm inte att besöka poddens webbplats och stötta skaparen: www.sbs.com.au
Var kan du lyssna?
Poddar i appen Replaio Radio Kommer snartPoddar kommer snart till appen. Installera nu och bli först med att uppleva ett helt nytt sätt att lyssna på poddar
Avsnitt
Yaliyojiri Afrika 21 Novemba 21.11.2025 8:50
Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika
Yaliyojiri Afrika 18 Novemba 21.11.2025 8:44
Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika
Yaliyojiri Afrika 14 Novemba 21.11.2025 6:34
Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika
Yaliyojiri Afrika 11 Novemba 21.11.2025 6:41
Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika
Yaliyojiri Afrika 7 novemba 21.11.2025 7:09
Jason Nyakundi anatujuza yanayojiri Afrika.
Tahadhari kwa wanaohitimu shule 21.11.2025 4:50
Kadri maelfu ya vijana wanaposherehekea kumaliza Mwaka wa 12, wanakumbushwa juu ya hatari zinazokuja na unywaji pombe, hasa nje ya nchi. Wazazi na marafiki wa waathiriwa wa sumu ya methanol, Bianca Jones na Holly Bowles, wamejiunga na juhudi mpya za usalama, wakiwatia moyo wasafiri vijana kuchukua maamuzi salama zaidi.
Programu za kufunza watu wazima kusoma na kuandika 21.11.2025 5:46
Mmoja kati ya Waaustralia watano, au takriban watu wazima milioni tatu, wana kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na kuandika au hesabu - na hii inaweza kuwa na athari kubwa katika jinsi watu wanavyoweza kushiriki maisha ya kila siku. Programu zimewekwa kote nchini kusaidia watu kuboresha ujuzi wao na kufikia malengo yao ya maisha. Ikiwemo moja huko Tasmania, ikiwasaidia watu wazima kuwa tayari k...
Watu wa asili kwenye hatihati ya kutoweka Brazil 18.11.2025 8:18
Shirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.
Uzalishaji wa Net Zero nchini Australia 18.11.2025 8:26
Muungano umeidhinisha rasmi kuondoa lengo la kutofikia uzalishaji wa gesi chafu katika mkutano wa chumba cha chama huko Canberra. Zaidi ya hayo, Liberals na Nationals wamefunua mpango wa kuondoa mabadiliko ya tabianchi kutoka kwenye orodha ya malengo ya mdhibiti wa nishati ya kitaifa, huku wakiapa kuendelea kupunguza uzalishaji kwa kufuatilia maendeleo ya nchi nyingine.
Maumivu ya wanawake kutiliwa maanani zaidi 14.11.2025 8:02
Serikali ya Victoria imetoa ripoti ya mwisho ya uchunguzi kuhusiana na uzoefu wa wanawake katika suala la maumivu - na ni taarifa inayosumbua kusoma. kutokana na uzoefu wa wanawake na wasichana 13,000, ripoti hiyo imebaini mapengo katika huduma za afya kwa jinsia, upendeleo katika matibabu, ubaguzi wa kijinsia, na hisia za kupuuzwa au kutopingwa na wataalamu wa afya zinazoenea katika mfumo wa afya...
Maandamano ya kikundi cha NSN uliwezaje kuruhusiwa kufanyika 14.11.2025 8:52
Maandamano ya neo-Nazi mbele ya bunge la New South Wales yamezua mshtuko katika jamii za Kiyahudi na za tamaduni mbalimbali huko Sydney. Serikali ya jimbo hilo imekashifiwa baada ya kufichuliwa kwamba tukio hilo liliendelea na idhini kutoka kwa Polisi wa New South Wales. Je, ni vipi maandamano haya ya neo-Nazi yalipewa kibali cha kufanyika mwanzoni?
Mazungumzo kuhusu African Youth Summit 2025 14.11.2025 11:17
Mkutano wa kwanza wa African Youth Summit uliandaliwa na kufanyika mwaka huu, na mratibu wa vijana aliyehudhuria anajiunga nasi kuzungumzia mada ya mkutano huo.
Idadi ya watoto wa mataifa ya kwanza gerezani yazua tashwishi 11.11.2025 8:34
Serikali ya majimbo na maeneo nchini Australia zitachunguzwa kama sehemu ya uchunguzi wa bunge kuhusu matokeo na athari za kifungo kwa vijana. Kati ya maswala ya kuzingatia katika uchunguzi huu ni Kuzidishwa kwa kufungwa kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza.
Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kuanzia desemba 11.11.2025 6:40
Mtandao wa Reddit na jukwaa la Kick zitaongezwa kwenye majukwaa yanayohitajika kuzuia watumiaji walio na umri chini ya miaka 16, sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa mwezi Desemba. Marufuku ya Australia ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16, ambayo inajumuisha majukwaa nane kuu, inategemea tathmini zinazoendelea za eSafety ambazo zinaweza kufafanua kati ya huduma za mitandao ya kijam...
Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia 11.11.2025 7:35
Australia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu la...
Mfumo wa utoaji wa mayai ya uzazi Australia huenda ukabadilika 11.11.2025 8:39
Mahitaji ya mayai ya uzazi yanaongezeka nchini Australia kadiri watu wanavyokumbwa na changamoto za uzazi. Lakini mahitaji ya mayai ni makubwa mno kuliko upatikanaji wao na sasa, wataalamu wanapendekeza Australia ifikirie kubadilisha kanuni zinazohusu utoaji mayai.
Afya ya akili:kupata usaidizi kama mhamiaji 10.11.2025 8:03
Wahamiaji wengi wanakumbana na matatizo tofauti wanapojaribu kupata msaada wa afya ya akili. Umoja wa Mataifa unasema kwamba upatikanaji wa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi kwa kila mtu , ikiwemo wahamiaji na wakimbizi. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wahamiaji mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, huzuni, kiwewe na ata upweke kutokana na mazingira...
Jamii ya Sudan walio Australia waendelea kuwa na wasiwasi 10.11.2025 8:13
Jamii ya watu wa Sudan walio nchini Australia wana wasiwasi mkubwa ,wakisubiri habari kutoka kwa familia zao walionaswa katika jiji la Al-Fasher baada ya mlipuko wa ghasia. Jiji hilo lilitekwa na Rapid Support Forces wiki mbili iliyopita, na wataalamu wanaamini kwamba maelfu huenda wameuawa katika mauaji ya kutisha. Kwa kuwa huduma za intaneti na simu zimekatwa, wanaoishi nje ya nchi wanalazimika...
Umaskini wa nishati 10.11.2025 7:17
Maelfu ya kaya za Wenyeji kaskazini mwa Australia wanaishi na mfumo wa kulipa kabla wa umeme, ambapo kukatwa kunaweza kutokea wakati wowote. Ripoti mpya sasa imeonya kwamba bila ulinzi wa kutosha, mfumo huu unaweza kuwa hatari katika joto kali.
Hali ya hewa inawaathiri pinguini 08.11.2025 5:44
Timu ya kimataifa ya wanasayansi imeonya kuwa pIngwini wanaweza kuwa katika hatari kutokana na madhara ya hali mbaya ya hewa. Utafiti mpya unapendekeza kwamba si tukio moja kama vile joto kali inayosababisha hatari kubwa zaidi, bali ni athari zake zilizoungana pamoja katika ardhi na baharini.
Mzio wa karanga kwa watoto upata mwelekeo mpya 04.11.2025 7:28
Miaka kumi baada ya utafiti muhimu kudhibitisha kwamba kuwalisha watoto wachanga bidhaa za karanga inaweza kuendeleza mzio hatari, utafiti mpya umebaini kuwa kuna uwezekano wa kuepuka kuendeleza mizio ya chakula.
Serikali kudhibitisha umuhimu wa wahamiaji kwenye uchumi 04.11.2025 5:42
Waziri wa Mambo ya Ndani, Tony Burke, anasema kwamba serikali inafanya kazi juu ya uwezekano wa kutambua ujuzi wa nje ya nchi. Anasema hii itasaidia kuokoa muda na pesa kwa wahamiaji wenye ujuzi wanaotafuta kuhamia Australia. Katika hotuba yake kwa Klabu ya Waandishi wa Habari huko Canberra, Bw. Burke pia ametangaza mabadiliko kwenye akaunti za benki zisizotumika ili kukabiliana na utakatishaji wa...
Understanding treaty in Australia: What First Nations people want you to know - Mkataba wa amani: Una maana gani na Una manufaa gani 04.11.2025 5:32
Australia is home to the world’s oldest living cultures, yet remains one of the few countries without a national treaty recognising its First Peoples. This means there has never been a broad agreement about sharing the land, resources, or decision-making power - a gap many see as unfinished business. Find out what treaty really means — how it differs from land rights and native title, and why it m...
Taarifa ya Habari 26 Septemba 2025 26.09.2025 14:08
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025 23.09.2025 17:02
Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.
Liknande poddar
Replaio är ingen poddutgivare; programnamn, omslag och ljud tillhör sina upphovspersoner och distribueras via offentliga RSS-flöden