SBS

SBS Swahili - SBS Swahili

News SW ↓ 1019 avsnitt

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Glöm inte att besöka poddens webbplats och stötta skaparen: www.sbs.com.au

Skapare

SBS

Kategori

News

Poddens webbplats

www.sbs.com.au

Senaste avsnittet

28 sep 2026

Var kan du lyssna?

Poddar i appen Replaio Radio Kommer snart

Poddar kommer snart till appen. Installera nu och bli först med att uppleva ett helt nytt sätt att lyssna på poddar

Ladda ned på Google Play Installera gratis Android nästan 10 mn nedladdningar · betyg 4,8 iOS snart

Avsnitt

Makala leo:utafiti unaonyesha miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi,hali inayochangia kaboni 12.01.2026

Utafiti mpya umebaini kuwa miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi kuliko inavyokua, hali ambayo inachangia ongezeko la utoaji wa kaboni. Utafiti huo, unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Western Sydney na kuchapishwa katika jarida la Nature Plants, umebaini kuwa miti katika aina zote za mifumo ya mazingira - kuanzia misitu ya mvua ya tropiki hadi misitu ya eucalypt - inapungua hali ya hewa inavyozidi...

Makala leo:Je,uangalizi wa ndege ni jambo maarufu miongoni mwa vijana sasa hivi? 12.01.2026

Mnapofikiria kutazama ndege, labda mnawazia wastaafu. Lakini kizazi kipya kinaanza kutumia darubini na kujihusisha na burudani hii. Kile kilichokuwa kimbilio kutoka ulimwengu wa mtandaoni sasa kinafufuka tena mtandaoni.

Taarifa ya habari:Tume ya kifalme yazinduliwa kuchunguza chuki dhidi ya wayahudi 09.01.2026

**WAZIRI MKUU ANTONY ALBANESE AZINDUA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA KESI ZA CHUKI DHIDI YA WAYAHUDI AUSTRALIA. **MAWIO YA MOTO YAWEKWA SEHEMU MBALIMBALI AUSTRALIA HUKU JOTO IKIZIDI KUONGEZEKA ** KIFO CHA MWANAMKE MAREKANI YAZUA UTATA.

Yaliyojiri Afrika:kapteni Ibrahim Traore anusurika jaribio jingine la mapinduzi 08.01.2026

Kwa habari au maelezo zaidi tembelea sbs.com.au/swahili.

Afya:wataalamu waonya dhidi ya madhara ya kuchanganya mipango mbalimbali ya lishe 08.01.2026

Mipango ya lishe kama vile Foodmap, yenye protini nyingi, isiyo na gluten, yenye mafuta kidogo, na kula chakula safi - kuna mipango mingi sana ya lishe, na ushauri unaokinzana. Wataalamu wa Australia wanaonya kwamba kufuata mipango mbalimbali ya lishe kwa wakati mmoja kunaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa.

Makala leo:wazazi wapata afueni baada ya serikali kupunguza gharama za vituo vya malezi ya watoto 08.01.2026

Wazazi wanaopeleka watoto kwenye vituo vya malezi wana uhakika wa kupata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu za wiki, bila kupitia mchakato wowote wa uthibitishaji. Ruzuku hii itagharimu karibu dola milioni 430 kwa kipindi cha miaka minne ijayo, lakini serikali inasema mamia ya maelfu ya familia zitafaidika.

Taarifa ya habari:Maduro na mkewe wakanusha mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha jijini New York 06.01.2026

** Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe walikana hatia katika mahakama ya Marekani. ** Mtu anayedaiwa kuwa mfyatuliwa wa risasi Bondi amehamishwa kwenda gereza la Goulbourn supermax. **Na Denmark yaendelea kuikashaifu Marekani kuhusu manoni yao ya Greenland.

Yaliyojiri Afrika:Ushahidi mpya waonyesha kuwepo kwa jeshi la Rwanda DRC 05.01.2026

Jason anatujuza yanayojiri pande mbali mbali Afrika, Kwa habari zaidi elekea kwa tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Nini kipya mwaka 2026? 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Ukosefu wa maji wawaathiri wakaazi wa Tanzania 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Waasi wa M-23 kujiondoa ili kusaidia juhudi za amani Congo 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Burundi kuanza kusafirisha madini nje ya nchi ili kuimarisha uchumi 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Wanafunzi 300 waachiliwa baada ya kutekwa nyara shuleni Nigeria 05.01.2026

Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

Yaliyojiri Afrika:Hatua ya Israel kuitambua Somali Land yazua utata 05.01.2026

Mwanahabari Jason Nyakundi atujuza yaliyojiri Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa mitandao yetu ya kijamii au tovuti yetu sbs.com.au/swahili

Makala leo:YWCA yapewa sifa kwa kuwasaidia wanawake Sydney 05.01.2026

Kukusanya fedha ili kupunguza makazi duni miongoni mwa wanawake ndiyo lengo la hoteli moja mjini Sydney, moja kati ya biashara elfu kumi na mbili ya kijamii nchini Australia zinazochanganya faida na lengo. Likizo za kiangazi ni wakati wenye mafanikio kwa maeneo mengi ya utalii. Lakini hoteli ya Song mjini Sydney inazingatia zaidi ya kutengeneza pesa. Inasaidia miradi ya makazi ya YWCA kwa wanawake...

Makala leo:China yaongeza ushuru kwa bidhaa za nyama ya ng'ombe 05.01.2026

Biashara ya nyama ya ng'ombe ya dola bilioni ya Australia inakabiliwa na mabadiliko makubwa kutokana na hatua ya China kuweka ushuru wa asilimia Hamsini na tano kwa uingizaji wa bidhaa zinazozidi vikomo vya kila mwaka vilivyowekwa kwa ukali. Wakati serikali ya China inadai kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakulima wake dhidi ya usambazaji usiokuwa na kipimo, viongozi wa sekta ya Australia na Upi...

Taarifa ya habari:Marekani yavamia Venezuela na kumkamata rais Maduro na mkewe 05.01.2026

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru shambulio kubwa dhidi ya Venezuela kuwakamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mke wake. Wametuhumiwa na makosa ya dawa za kulevya na silaha huko New York. Hatua hiyo imepongezwa na washirika wa Bw. Trump, lakini imelaaniwa sana na mataifa mengi.

Tukio la risasi Sydney:wengi wauawa akiwemo mtoto mmoja, huku wengine wakijeruhiwa. 15.12.2025

Polisi wametangaza shambulio la risasi nyingi huko Bondi Beach Jumapili kama shambulio la kigaidi, baada ya wanaume wawili kufyatua risasi kwa mamia ya watu waliokusanyika kwa ajili ya sherehe ya Hanukkah. Watu wasiopungua 16 wameuawa, pamoja na mtoto, katika shambulio la risasi nyingi lililosababisha vifo vingi zaidi nchini Australia tangu mauaji ya Port Arthur ya mwaka 1996. Tukio hilo limezua s...

Waaustralia wakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha 11.12.2025

Ripoti mpya ya kitaifa imegundua kuwa Waasutralia wanakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha. Ripoti inasema kuwa ingawa teknolojia za matibabu zinakua kwa kasi nje ya nchi, mfumo wa Australia bado uko polepole katika kupitisha na kufadhili teknolojia hizo mpya.

Matokeo ya Cronulla 2005 yakumbukwa kwa hisia mchanganyiko 11.12.2025

Miaka ishirini iliyopita, maelfu walikusanyika kwenye kitongoji cha pwani cha Cronulla huko Sydney, kwa kile kilichogeuka kuwa mkutano wa vurugu dhidi ya uhamiaji kutoka Mashariki ya Kati. Leo hii, wakazi wa Cronulla na baadhi ya Waaustralia wenye asili ya Mashariki ya Kati wanasema mitazamo inabadilika. Lakini wengine wanahofia kuhusu harakati mpya zaidi zilizo na mpangilio wa kupinga uhamiaji.

Wataalamu waonya kuwa msimu wa moto umeanza tunapotarajia joto kuongezeka 11.12.2025

Katika wiki za hivi karibuni, moto wa nyika umesababisha uharibifu wa nyumba na mali katika maeneo ya pwani ya katikati ya kaskazini ya New South Wales, Geraldton huko Magharibi mwa Australia na mashariki mwa Tasmania. Wataalamu wanaonya kuwa huu ni mwanzo tu wa msimu wa moto na nyinyi ambao mnasafiri kwa ajili ya likizo mnahitaji kuwa na ufahamu na maandalizi mkiwa mbali na nyumbani.

Baraza la usalama wa chakula latoa vidokezo jinsi ya kuandaa vyakula kwa usalama ili kuepukana na magonjwa 11.12.2025

Kuna mambo mengi ya kushughulikia wakati huu wa mwaka, na milo yetu inaweza kuja na upande wa magonjwa. Baraza la Habari za Usalama wa Chakula la Australia limetoa vidokezo vyake bora jinsi ya kufurahia msimu kwa usalama - kwa lengo la kupunguza zaidi ya kesi milioni nne na laki tano za sumu ya chakula kila mwaka.

Taarifa ya habari:serikali ya Australia yaomba msamaha rasmi kwa watu wa mataifa ya kwanza leo 09.12.2025

Baadhi ya habari zinazojumuisha taarifa yetu leo, *Victoria inatarajiwa kutoa msamaha kwa watu wa mataifa ya kwanza leo *Serikali ya Northern territory imepinga ziara ya umoja wa mataifa *Australia na marekani waanza mazungumzo kuhusu usalama na pia AUKUS *idadi ya vifo vinaendelea kuongezeka sudan baada ya mashambulio wiki iliyopita Kwa habari na maelezo zaidi tembelea tovuti yetu kwa sbs.com.au/...

Yaliyojiri Afrika:mapigano kati ya waasi wa M-23 na jeshi la DRC yaendelea 08.12.2025

Jason Nyakundi anatujuza kinachoendelea Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa tovuti yetu ya sbs.com.au/swahili.

Wauzaji wajiandaa kwa ongezeko la wizi madukani msimu wa sherehe unapokaribia 08.12.2025

Kadri msimu wa ununuzi wa sherehe unapoanza, wauzaji wanajiandaa kwa ongezeko la wizi madukani. Nchini Australia kote, wizi umefikia kiwango cha juu zaidi katika miaka 21. Wataalamu wanasema kuwa ni sehemu ya mwelekeo mpana zaidi.

Lyssna på podden SBS Swahili - SBS Swahili i Replaio

Radio och poddar i en och samma app - gratis och utan konto. Installera redan idag och missa inte premiären

Ladda ned på Google Play

Replaio är ingen poddutgivare; programnamn, omslag och ljud tillhör sina upphovspersoner och distribueras via offentliga RSS-flöden