Tanzania National Parks (TANAPA)

TANAPA PODCAST

Welcome to the official podcast of the Tanzania National Parks (TANAPA).Join us as we explore key conversations on conservation education, tourism, and investment opportunities across Tanzania’s National Parks. Each episode highlights strategies for sustainable conservation and the vital partnerships that help protect our natural resources for current and future generations.

Author

Tanzania National Parks (TANAPA)

Category

Government

Podcast website

www.tanzaniaparks.go.tz

Latest episode

Jul 1, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

TANAPA Podcasts Season II 01.07.2026

TANAPA PODCAST | SEASON II Tumerejea na msimu mpya wenye simulizi, maarifa na mazungumzo yanayokupeleka karibu zaidi na ulimwengu wa uhifadhi, utalii na uwekezaji katika Hifadhi za Taifa 21 za Tanzania . Tegemea vipindi vilivyoboreshwa, maudhui ya kina, wageni mbalimbali na uzoefu mpya wa kusikiliza. TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

TANAPA PODCAST EPISODE 16: MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI. 24.11.2025

Episodi hii inaangazia njia za asili zilizotumika katika utunzaji wa maliasili kwa kufuata taratibu za kitamaduni, mila, desturi na makatazo mbalimbali yaliyosaidia kusimika mizizi imara na kuwa chimbuko la uhifadhi wa kisasa. Hekima za mababu zetu kama vile kuheshimu misitu, kutotumia rasilimali kupita kiasi, na kutambua uhusiano wa binadamu na mazingira vimekuwa dira muhimu inayoongoza mbinu za...

TANAPA PODCAST EPISODE 15: UHIFADHI NI JUKUMU LA KILA MMOJA 17.11.2025

Episodi hii inakuletea uchambuzi wa kina kuhusu Uhifadhi kwa kuzingatia kuwa Uhifadhi wa wanyamapori ni zoezi la kujitolea kulinda na kuhifadhi maliasili kwa maslahi ya Taifa kwa kizazi hiki ma kijacho. Sikiliza Episodi ya 15 upate elimu kutoka kwa Mzee Ibrahimu Kasontola kutoka katika kijiji cha Lukoma wilayani Uvinza - Kigoma aliyejitolea kwa hali na mali kuhifadhi msitu katika eneo la makazi ya...

TANAPA PODCAST EPISODE 14: MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI. 27.10.2025

Episodi hii inaangazia mila, desturi na tamaduni katika uhifadhi wa maliasili, hususan namna jamii ya Wangoni kutoka mkoani Ruvuma ilivyotumia majina na utamaduni wao kulinda Wanyamapori na Misitu  tangu enzi za mababu zetu. Hadithi hii ya kuvutia inaonesha jinsi urithi wa jadi ulivyokuwa chachu ya kulinda rasilimali za Taifa ambazo leo hii zinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya uhifadhi na...

TANAPA PODCAST EPISODE 13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili 20.10.2025

Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katik...

TANAPA PODCAST EPISODE 12 - Zoezi la Uhamishaji Tembo kutoka Misenyi kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato. 16.10.2025

Episodi hii imeangazia zoezi endelevu la kuwahamisha tembo walowezi kutoka maeneo ya karibu na wananchi kwenda hifadhini na zoezi zima la kuwaswaga tembo waliotoka hifadhini kuvamia maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini. Sikiliza Episodi hii kwa taarifa hiyo na mengine mengi kupitia Epsode ya 12. Eneo: Misenyi - Bukoba. Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Guests: Kamishna Ms...

TANAPA PODCAST EPISODE 11 - Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere na Historia ya Taifa letu. 13.10.2025

Kuelekea Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, TANAPA PODCAST tunakueletea uchambuzi kuhusu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Hapa utapata kujifunza mengi kuhusu harakati za Uhuru wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla. Ikumbukwe historia hii imehifadhiwa katika Nyumba ya Kumbukizi ya...

TANAPA PODCAST EPISODE 10 - MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2025 NA PROF. KAMUZORA 09.10.2025

Episodi hii inaangazia mazungumzo ya kina kuhusu zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambapo Profesa Kamuzora anaeleza uzoefu wake katika kupanda mlima kwa muda mrefu. Fahamu faida ya kushiriki kampeni ya “Twenzetu Kileleni katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa Taifa letu, kuhamasisha utalii pamoja na utunzaji wa mazingira. Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena - Mkuu wa Kiten...

TANAPA PODCAST EPISODE 09 - YAFAHAMU MAENEO YA MALIKALE YALIYOKASIMISHWA TANAPA 06.10.2025

Episodi hii inaangazia maeneo ya Malikale yanayosimamiwa na TANAPA na faida zake. Maeneo hayo yamebeba historia za kale, biashara ya utumwa, utawala wa machifu, ukoloni na uhuru wa Taifa letu. Sikiiiza TANAPA PODCAST Epsode 09 upate elimu ya kina kuhusu historia ya Taifa letu, asili na umuhimu wa kutunza tamaduni zetu. Eneo: Dar es Salaam. Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena. Gues...

TANAPA PODCAST EPISODE 08 - MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2025 NA CDF (Mst.) GEORGE WAITARA 02.10.2025

Katika Episode hii tunaangaIa mazungumzo ya kuhusu Kampeni ya Twenzetu Kileleni 2015 inayofanyikaga Desemba 09 kila mwaka kukumbuka mashujaa wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika ambapo kwa mwaka huo huo bendera ya Taifa ilipandishwa Mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu kuliko vyote Barani Afrika chenye urefu wa mita “5985 asl” kuangazia nuru ya Uhuru ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Sikiliza...

TANAPA PODCAST EPISODE 07 - Uchambuzi wa maneno yenye mkanganyiko katika Sekta ya Uhifadhi na Utalii 29.09.2025

Episodi hii inaangazia uchambuzi wa kina kuhusu maneno mbalimbali yanayoleta mkanganyiko wa maana na matumizi yake katika jamii. Katika Episode 07 Mtopezi wa lugha ya Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Ndugu Oni Sigala anachambua na  kudadavua maneno kadha wa kadha yenye utata katika sekta ya uhifadhi na utalii. Eneo: Dar es salaam Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Cat...

TANAPA PODCAST EPISODE 06 - Mila, Desturi na Tamaduni katika Uhifadhi wa Maliasili 22.09.2025

Sikiliza Episode 06 uchambuzi wa kina katika mwendelezo wa mada inayoeleza elima ya Uhifadhi ikihusisha Mila, Desturi, Tamaduni na Miiko iliyozuia uharibifu wa Maliasili za Taifa ambapo moja ya maeneo hayo kwa sasa ni Hifadhi za Taifa Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Guest: Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Massana Mwishawa.

TANAPA PODCAST EPISODE 05 - Mila, Desturi na Tamaduni katika Uhifadhi wa Maliasili 15.09.2025

TANAPA Podcast Episode 05 inaangazia mwendelezo wa mada inayoeleza elimu ya Uhifadhi iliyohusisha Mila, Tamaduni, Desturi na Miiko anuwai iliyozuia baadhi ya wanyamapori kuuwawa lengo likiwa ni kuhifadhi maliasili zilizokuwa ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa ambayo baadhi yake kwa sasa ndio Hifadhi za Taifa tunazozishuhudia zikitiririsha nyomi ya watalii nchini. Eneo: Hifadhi ya Taifa Serengeti Mwon...

TANAPA PODCAST EPISODE 04 Mila, Desturi na Tamaduni zilizotumika katika Uhifadhi wa Maliasili 08.09.2025

Episode hii inaangazia mazungumzo kati ya Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena na Mzee Fanuel Mbise, Eliona Miley na Elikesia Akyoo kuhusu elimu ya Uhifadhi kupitia mila, desturi na tamaduni zilizotumika katika kusheshimu na kutunza maliasili zilizokuwa zimehifadhiwa.

TANAPA PODCAST EPISODE 03 Chimbuko la Uhifadhi 25.08.2025

Sikiliza TANAPA Podcast, Episode 03 uelimike kuhusu Chimbuko la Uhifadhi Uanzishaji wa Hifadhi mpya na malengo yake Maeneo matano ya Malikale yaliyokasimishwa TANAPA na Uzalendo katika kutembelea Hifadhi za Taifa. Mgeni maalum: Nakaaya Sumari (Tanzania Safari Channel) Host: ACC Catherine Mbena, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano TANAPA Fuatilia mfululizo huu wa elimu ya uhifadhi, utalii na mir...

TANAPA PODCAST EPISODE 02 - Kazi mbalimbali zinazofanywa na TANAPA 17.08.2025

Katika episode ya pili ya mfululizo huu, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena anaelezea kwa kina kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha maliasili zilizopo ndani ya hifadhi za Taifa zinaendelea kulindwa na kuhifadhiwa kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

TANAPA PODCAST EPISODE 01 Utangulizi kuhusu TANAPA na majukumu yake 11.08.2025

Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa kina kuhusu Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) – kuanzia majukumu yake makuu, muundo wa utendaji kazi, hadi maeneo ya hifadhi yanayosimamiwa chini ya sheria. Ni programu endelevu inayokufahamisha nafasi muhimu ya TANAPA katika kulinda maliasili na kukuza mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

Listen to the TANAPA PODCAST podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.