Tanzania Information Services Department (Idara ya Habari-MAELEZO)

MAELEZO PODCASTS

Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.

Author

Tanzania Information Services Department (Idara ya Habari-MAELEZO)

Category

Government

Podcast website

www.maelezo.go.tz

Latest episode

Jul 10, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android 5M+ downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Fursa kwa Watanzania Kuelekea AFCON 2027 10.07.2026

Send us Fan Mail Kuelekea Michuano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania anatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hii mikubwa Barani Afrika, tumemualika Bw. Allan Allex, Afisa Michezo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Afisa Programu wa Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Nne. Tumezungumza kuhusu fursa zilizopo, zinazoendelea kujitokeza na zin...

Siri ya Tarehe 7 Julai na Historia ya Tanzania Iliyowafanya UNESCO kuichagua kuwa Siku ya Kiswahili Duniani 06.07.2026

Send us Fan Mail Mazungumzo na Profesa Rehema Erasto., Mhadhiri wa Kiswahili kutoka Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu historia ya siku ya Kiswahili Duniani, nafasi ya lugha za kijamii (makabila), makosa kwenye lugha ya kiswahili na namna ya kusahihisha. Mazungumzo haya yanapatikana pia kupitia chaneli ya Youtube ya Maelezo TV. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Kwanini Kongamano la Kiswahili Ufaransa na si kwingine? Majibu ya Msemaji Mkuu wa Serikali 29.06.2026

Send us Fan Mail Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; na Msemaji Mkuu wa Serikali akitoa majibu ya ni kwanini Kongamano la Kiswahili la Pili la Kimataifa limefanyika nchini Ufaransa na si kwingineko. Pia tumezungumzia asili ya makongamano ya kiswahili ya kimataifa, fursa na ushiriki wa wananchi katika makongamano haya. Support the show Msemaji Mkuu wa Serika...

Kuelekea Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa, Paris - Ufaransa 18.06.2026

Send us Fan Mail Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inatarajia kufanya Kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili kati ya Julai 4 - 7, 2026, jijini Paris, Ufaransa. Tumezungumza na Bw. Tito Lulandala, Afisa Utamaduni Mwandamizi, kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha...

Fursa, Ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania: Balozi Matinyi 12.06.2026

Send us Fan Mail Mheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algiers tarehe 10 Juni, 2026.  Balozi Mobhare Matinyi anayeiwakilisha Tanzania nchini Algeria, ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za ushiri...

Balozi Kombo Aeleza Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia katika Kuimarisha Mahusiano ya Tanzania na Urusi 08.06.2026

Send us Fan Mail Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 7 Juni, 2026. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Miaka 10 ya BMH: Jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa Ilivyobadilisha Huduma za Kibingwa Tanzania 04.06.2026

Send us Fan Mail Hospitali ya Benjamin Mkapa ni hospitali ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma, iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa sasa zipo 20 na ubingwa bobezi zipo 17 kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani.  Tangu kuanza kutoa huduma zake, hospitali hiyo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza nchini katika huduma za matibabu ya moyo, f...

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 (Mei 4, 2026) 26.05.2026

Send us Fan Mail Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mei 4, 2026, bungeni, jijini Dodoma. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Hotuba ya Mhe. Rais Samia na Mhe. Rais, Paul Kagame, Mei 03, 2026 24.05.2026

Send us Fan Mail Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania , akizungumza na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu ushirikiano na kukuza uchumi wa pande zote, Mei 3, 2026. Viongozi hawa walikubaliana kuendelea kukuza biashara na uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya kikodi, ili kunufaika na masoko ya kikanda ya...

Hotuba ya Rais, Dkt. Samia Kwenye Kongamano la Biashara Baina ya Tanzania na Kenya, Mei 4, 2026 22.05.2026

Send us Fan Mail Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Kenya (Tanzania & Kenya Business Forum 2026), tarehe 04 Mei, 2026, JNICC, jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hili lilihudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando 25.04.2026

Send us Fan Mail Pata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Elimu kwa umma kuhusu zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI (2022) 15.01.2026

Send us Fan Mail Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Di...

Buriani Benjamin mkapa (Julai 25, 2020) 15.01.2026

Send us Fan Mail Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali

Listen to the MAELEZO PODCASTS podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.