RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

Business SW ↓ 34 episodes

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Be sure to visit the podcast's website and support the creator: www.rfi.fr

Author

RFI Kiswahili

Category

Business

Podcast website

www.rfi.fr

Latest episode

Sep 30, 2026

Where to listen?

Podcasts in the app Replaio Radio Coming soon

Podcasts are coming to the app soon. Install now and be the first to see a whole new take on podcasts

Get it on Google Play Install for free Android almost 10M downloads · 4.8 rating iOS soon

Episodes

Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado 07.01.2026

Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.

Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako. 24.12.2025

Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyab...

Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini? 03.12.2025

Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?

Mapinduzi ya Elimu Bondo: Jinsi Teknolojia Inavyowawezesha Wasichana Kuandika Kesho Yao 26.11.2025

Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kita...

Mandale: Kinywaji Cha Asili Kinachowainua Wanawake wa Goma 19.11.2025

Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake. Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.

Nini hatma ya Afrika baada ya kumalizika kwa mkataba wa kibiashara na Marekani ‘AGOA’ 01.10.2025

Mkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia katika viwanda vya nguo nchini Kenya hadi kwa wasafi...

Vijana na ujasiriamali Afrika Mashariki: Nini kifanyike kuwawezesha? 24.09.2025

Msikilizaji katika nchi zote za Afrika Mashariki, kuna wimbi jipya la matamanio kuhusu hali ya biashara, vijana, wakiongozwa na ubunifu na ustahimilivu! Wakigeuza harakati zao kuwa biashara zinazostawi, kubadili changamoto kuwa fursa na ndoto kuwa ukweli. Tutazungumza na Andrew Lukuwi, yeye ni mjasiriamali kijana akiwa nchini Tanzania, pamoja na Dr Onesmo Kyauke mchambuzi wa masuala ya uchumi na s...

Mzunguko haramu wa Fedha: Kizuizi kisichoonekana kwa ustawi wa Afrika 03.09.2025

Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu...

Kuwekeza katika Uchumi wa Bluu: Mkakati wa uhakika au Kamari hatari? 27.08.2025

Leo hii tunatupia jicho uchumi wa bluu, eneo la kiuchumi linalotajwa kama suluhisho jipya la maendeleo endelevu, kukuza ajira na ubunifu, hata hivyo chini ya uso wa maji, maswali magumu yanajitokeza: Je, tunawekeza kimkakati kwa kuzingatia pia jamii zinazozunguka maeneo haya? Tutazungumza na Dr Ponsian Ntui mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini mwanza nchini Tanzania, maaruf...

Listen to the Gurudumu la Uchumi podcast in Replaio

Radio and podcasts in one app - free, with no sign-up. Install today and do not miss the launch

Get it on Google Play

Replaio is not a podcast publisher; show names, artwork and audio belong to their authors and are distributed through public RSS feeds.